Thursday, November 26, 2009
Wednesday, November 25, 2009
Je, ni Muhimu Kiasi gani?
Je, sex ni muhimu katika ndoa kiasi gani?Wanandoa wengi wana struggle sana ili kuhakikisha ndoa yao inakuwa ya kuridhisha ingawa ni kweli ndoa yoyote imara huhitaji efforts kwa mke na mume ili mambo kila siku yawe mazuri na vicheko vya hapa na pale.
Swali la leo ni kwamba Je, baada ya ndoa kutokuwa na sex ni kitu gani kingine kinaweza kuwafanya wanandoa kushikana au kubaki na bond strong?
Je, ni familia yaani watoto na kule kujisikia ni mke na mume au ni urafiki wa kubaki kuishi kama dada na kaka walioamua kuishi pamoja?
Je, unaweza kuishi kwa kuridhika katika ndoa ambayo hakuna sex kwa hiari yaani si ugonjwa au tatizo ambalo daktari amethibitisha bali wanandoa wameamua tu?
Kila mmoja ana majibu yake ambayo anayo kichwani, mwingine atasema ndiyo na mwingine atasema hapana haiwezekani kuishi bila hiyo huduma.
Hata hivyo ni kweli sex ni muhimu sana katika ndoa, na ukishaingia kwenye ndoa ina maana kwamba umeingia mahali sahihi ambapo sex ni kitu cha bure na si dhambi, kwani sex ni mali ya ndoa, nje ya ndoa ni uchafu na laana kama si dhambi na kuwa na hatia.
Hii ina maana kama ni mwanandoa usipopata sex ndani ya ndoa huna sehemu nyingine ambayo unaweza kupata hiyo huduma.
Hii ina maana kwamba unayokazi ya kuhakikisha ndoa inakupa ridhiko na kuridhika huanza kwa kupata huduma muhimu kama sex.
Kitu kilicho muhimu kwetu ambao tumeoa na kuolewa ni kwamba sex ni haki yetu na tunahitaji kuwa wazi kueleza matarajio yetu, mahitaji yetu, interest zetu na vile tunajisikia au tunapenda wapenzi watu watufanyie.
Ndoa yenye furaha na bora ni ile ambayo ina balance mizani katika vitu vitatu yaani
Kwanza ni mwili,
Pili ni nafsi na
Tatu ni roho.
Kimoja kikikosekana tu basi kasheshe huanza na tofauti huendelea kutafuna ndoa kisirisiri kama mchwa.
Inawezekana mume wako au mke wako ana hasira, ukali, majibu ya mkato, kuwa mbali na wewe, kutumia muda na rafiki zake au kufanya vitu vingine badala ya kukaa na wewe si kwa sababu ya makosa unafanya bali kutopenda kwako sex.
Sex si hitaji la mwili tu katika ndoa bali ni kuonesha (approval) kwamba mume au mke wangu ananipenda, ananihitaji, ananijali, ninamvutia na napendeza na zaidi kuwa connected.
Frustrations nyingi za wanandoa huanza kwa masuala ya kitandani kuwa baridi.
Kwa maelezo zaidi soma hapa.
Take good care!
Tuesday, November 24, 2009
Una ripoti ya ukaguzi?
"Mpenzi …………,nionyeshe uso wako, na niisikie sauti yako, kwa maana sauti yako ni tamu, na uso wako unapendeza.Tukamatie mbweha, mbweha wadogo wale wanaoharibu mashamba ya mizabibu, mashamba yetu ya mizabibu yalichanua".
Ukisoma kitabu cha Wimbo ulio bora katika Agano la kale sura ya 2 kuanzia mstari wa 1 hadi ule wa 14 unakutana na maneno ya wapenzi wawili (wanandoa) ambao wana wakati mzuri na wanaongea lugha ya kimahaba, wapo faragaha kimapenzi (intimacy) wapo deep in tender affection na it is romantic.
hata hivyo kufika mstari wa 15 maneno yanabadilika na wanatangaza kuwa na tahadhari na kuonya kwamba kuna mbweha wadogo wanaoharibu shamba lao la mizabibu iliyochanua na wawakamate.
pamoja na kuwa na mapenzi matamu, mapenzi yanayokua na kuongezekan kuwapa raha bado wanafahamu kwamba kuna mbweha wadogo wanaweza kuharibu ndoa yao.
Kinachofurahisha ni kwamba wapo very concerned na hao mbweha wadogo na kila mmoja anaonekana ni inspector mzuri wa mahusiano yao.
Pamoja na uzuri wote wa mapenzi bado mmoja wao amechukua hatua ya kuwa inspector na kuomba hao mbweha wadogo wakamatwe na kuondolewa.
Hili ni somo zuri kwa mwanandoa yeyote kuwa makini na mbweha wadogo ambao wanaweza kuharibu ndoa ikawa chungu kama limau.
Ni muhimu sana kukagua mahusiano yako wewe mke na mume kuangalia kama kuna mbweha wadogo na inawezekana ndoa yako isiwe na mbweha wadogo bali wadudu wadodgo kama mchwa ambao wanaweza kuvamia ndoa yako na kuodondosha ghafla bila kutegemea.
Katika sehemu ambazo kuna mchwa ni rahisi sana nyumba zilizojengwa kwa miti na mbao kutekekea kwa mchwa kuliko moto.
Mchwa ni wadogo na huwa kimya hata hivyo ni industrious zaidi kuharibu nyumba kuliko moto ambao hata media nyingi huzipa nafasi zaidi.
Kumbuka, ni vitu vidogovidogo sana ambavyo kwenye ndoa ndivyo vyenye umuhimu iwe kujenga au kubomoa na mara nyingi hasa sisi wanaume (si wote) huwa tunaamini vitu vidogovidogo (kama vile kumwambia mke nakupenda, au kumbusu, au kumkumbatia au kumsifia pale amefanya kitu kizuri au pale amependeza nk) havina nafasi sana katika kujenga ndoa au kubomoa ndoa, ukweli ni kwamba vina maana sana.
Matukio kama kupoteza kazi, Ugonjwa wa ghafla, kifo cha motto nk mara nyingi huimarisha ndoa kuliko vitu vidogo.
Hivyo kama mwanandoa hakikisha unafanya ukaguzi mara kwa mara kama kuna mchwa unakula ndoa yako au wale mbweha wadogo ambao wanapenda kuvamia shamba lenu la mizabibu iliyochanua.
Ubarikiwe na Bwana!
Monday, November 23, 2009
"Too late to catch the bus"
Mara nyingi hobbies husababisha wanandoa kuwa na mawasiliano mazuri, kuongea pamoja, kuwa na kicheko na kufanya vitu kwa pamoja.Inakuwa ngumu sana kuwa na mawasiliano mazuri pale inapotokea wawili walioamua kuishi pamoja hadi kifo kitakapowatenganisha kila mmoja kuwa na hobyy yake kiasi kila mmoja anachukukia kile mwenzake anapenda.
Kuna hii story kwamba kuna mwanamke mmoja katika nchi fulani isiyo na jina ambaye aliamua kuwekeza kwa watoto wake na akamsahau mume.
Hawa wanandoa wawili walioana na wakawa na wakati mzuri sana pamoja kabla ya kupata watoto.
Baada ya kupata mtoto wa kwanza mke akawa anatumia muda wote kwa ajili ya mtoto hakuwa na muda tena kwa ajili ya mume wake.
Baada ya miaka 3 mtoto wa pili akazaliwa na sasa mama akawa too much occupied na watoto hivyo mume kuwekwa pembeni kwani kila kitu sasa ni “Watoto kwanza”.
Mume kuona hivyo akaamua kuwa na maisha yake yaani kuwa na marafiki wengine ambao anaweza kuongea nao, akatafuta masikio mengine ya kike ya kumsikiliza feelings zake, si unajua mwanaume huhitaji masikio ya mwanamke wakati fulani kati maisha yake ili kuongea kile anaamini kinamfanya yeye kujiona ni mwanaume.
Lazima tukubali kwamba kila mmoja aliumbwa na uhitaji wa jinsia nyingine hata kama hakuna sex bali sharing ya siri, mafanikio na matatizo ya maisha haya au masumbufu ya maisha haya.
Mwanaume akawa na watu wapya ambao aliunganisha feelings zake iwe ni hobbies au interest ilimradi maisha yawe na ladha, jambo la msingi ni kwamba alifahamu kwamba mke wake yupo na watoto na anahitaji kuwa na maisha yake.
Maisha yakawa yanaenda kama kawaida huku mke na watoto wake na mume na kazi na maisha yake mwenyewe.
Wale watoto wakakua na wakafika wakati wa kwenda college, na wakawa sasa wanarudi wakati wa likizo tu, ndipo mke akaanza kujisikia upweke na kuanza kujitahidi kujiunganisha kwa mume wake ambaye miaka 25 iliyopita waliacha connection kama mke na mume kuongea pamoja na sharing ya mambo mbaliombali ya maisha.
Sasa mwanamke anajigonga kwa mume waanze kuongea, waanza kuwasiliana, waanze kuenjoy intimacy, waanza kufurahia maisha kama mke na mume hata hivyo mume anamwambia mke
Hata hivyo kibaya zaidi sasa watoto wameolewa na mama akitaka kwenda kwao au kuongea nao wanamwambia lazima atoe taarifa kwani wanapenda sana kutumia muda wao na wapenzi wao na si mama tena.
Sasa mke anaishi kwa upweke ingawa mume anaye.
Upweke (loneliness) ni kitu kinachohuzunisha sana bila kujali upo umri gani, hata hivyo kuwa mpweke na uzee maumivu ni makali zaidi.
Kumbuka kuna wanaume wengi ambao baada ya watoto kuzaliwa wamejikuta katika upweke uliokithiri.
Na baada ya kupita kwa muda wa miaka mingi barabara hii ya upweke hufika mahali ambapo hata siku mke akitaka waanze upya mawasiliano huwa too late to catch the bus.
Hivyo kama wewe ni mwanamke ni muhimu sana kuwa na busara na hekima ya kuhakikisha mume unampa nafasi katika maisha yako hata kama unajiona una wajibu mkubwa kwa mtoto au watoto ulionao na muhimu weka priorities kwa mume kwanza maana watoto hawawi watoto milele.
Unaweza kuwa mama na mke kwa wakati mmoja na mwanamke mwenye busara huanza kama mke na kumaliza kama mke.
Ubarikiwe
Sunday, November 22, 2009
Nimempa kile anapenda!
Siri kubwaKuna usemi wa msingi sana kuhusiana na ndoa hasa linapokuja suala la interests na hobbies kati ya mume na mke.
Jambo la msingi kwa mke ni kukumbuka kwamba kuna progress zingine katika ndoa huja polepole sana, na kama utakuwa mvumilivu na caring vya kutosha ipo siku utaona mambo yanalipa.
Ni muhimu sana kwa mke kujifunza kitu chochote hata kama ni kidogo sana kuhusiana na taaluma ya mume wake na hiyo itakuwa moja ya siri kubwa ya kuondoa upweke na kusaidia kuwa kitu kimoja kuliko kubaki kimya na kukiri kwamba that is his stuff.
The man who can do anything he feels like doing with a woman, is more likely to say everything he feels like saying.
Nina rafiki yangu ambaye ni dereva wa magari na anapenda sana masuala ya magari na mnaweza kuongea habari za magari usiku kucha na hakuna kitu anapenda kama kazi ya kuendesha magari.
Mke wake ana busara sana, anajua ugonjwa wa mume wake ni magari na kitu chochote kinahusu magari, usipopenda magari kama mke ina maana ni upweke.
Anachofanya mke wake ni kwanza siku za Birthday parties anamnunulia vitu vinavyohusu magari anayopenda mumewe kama Tshirt na kofia zenye majina ya makampuni ya magari na zaidi mke hununua movies mbalimbali zinazohusu magari na yeye na mumewe huangalia na kuwa na muda mzuri.
Ni kweli kugundua kile mume wako anakipenda kama hobbies zake au interest zake ni siri na silaha muhimu sana kwa mwanamke yeyote anayetaka mume awe anaongea lugha moja na yeye.
Inawezekana mume wako anapenda sana kuimba kwaya, au kusoma bible au kusoma vitabu au kupanda maua au kupanda miti au kucheza gitaa au vyovyote vile, siri kubwa ni kwamba ukitaka mume wako aende extra mile jiingize kwenye interest zake kama si zile za kutenda dhambi.
Nimejiunga naye.... Amebadilika!
James ni mwanaume anayependa sana soka si kuangalia kwenye Tv tu bali hata kuhudhuria mechi mbalimbali kuanzia uwanja wa taifa jijini Dar es salaam hadi mechi ndogondogo mitaani na wakati mwingine kukiwa na mjadala wowote kuhusu soka basi hapo ni ugonjwa wake yaani anajisikia raha na anajisikia yupo nyumbani.Mke wake Jane tangu wameoana amekuwa hapendi kabisa kusikia habari za mchezo wa soka na amekuwa analalamika (kefyakefya) kwa tabia ya mumewe James kupenda soka kiasi hicho kwani wakati mwingine huondoka nyumbani kwenda kuangalia mechi za ligi kuu ya Uingereza na kurudi usiku sana.
James ni shabiki wa kutupwa wa timu ya Asernal Uingereza na timu ya Yanga jijini Dar Es Salaam.
Baada ya kusemana sana na kuzozana sana, ilifika siku Jane akaamini kwamba ni kweli mumewe hawezi kubadilika kuhusu kuacha kuwa shibiki na mwanaume mpenda soka kupindukia na zaidi kila anavyozidi kumsema na kumlalamikia ndivyo James anazidi kujiweka mbali na kupenda soka na kutumia muda zaidi kuangalia TV au kwenda kwa wenzake kuangalia na kuchelewa kurudi nyumbani.
Jane anasema kwamba
“Tangu nilipogundua kwamba sasa mume wangu hawezi kubadilika nimeamua kujiunga naye (if u cant fight them join them) hivyo siku hizi namuuliza hii weekend kuna mechi ya nani na nani ili tuwe wote na kama kuna mechi kwenye Tv basi tunakaa wote tunaangalia na ikifika break time nampa snacks na tunaendelea kuangalia.
Unaweza kustaafu mpweke!
Kustaafu kazi huwa maisha ya upweke sana kwa wanandoa kama waliishi maisha yakukuwa bila mawasiliano kwa miaka mingi.Wanandoa wawili ambao mume alikuwa anapenda sana kucheza Golf walikuwa na kwaida ya kwenda vacation katika kisiwa Fulani huko Amerika ya kusini.
Huyu mwanaume alikuwa ni mwanaume mwenye mafanikio makubwa na hawakubahatika kuwa na watoto hivyo alipanga kwamba akistaafu kazi atahamia kwenye hicho kisiwa ili amalizie maisha yake kwa kucheza golf kwani kwa kucheza golf kutamsaidia kuweka mwili wake fit ukiacha kwamba golf ilikuwa interest yake na moja ya hobby muhimu sana kwake.
Swali lilikuwa na mke wake mpenzi ambaye kwake Golf ilikuwa ni kitu kigeni na kitu ambacho hapendi si kusikia tu bali kuona mume wake mwenyewe anapenda.
Je, nitaishi maisha gani kama mwenzangu kila siku itakuwa ni golf tu na mimi na upweke wangu?
Si nitakuwa mjane wakati mume bado ninaye?
Je, ni raha ilioje kama wote kwa pamoja tutakuwa na wakati mzuri pamoja kucheza golf kila siku?
Je, nitaanzeje wakati hata golf sijui?
Kwa kuwa walikuwa wamebakiza miaka miwili tu na kuhamia moja kwa moja kwenye kisiwa maarufu cha golf huyu mwanamke alifanya uamuzi wa kuanza kujifunza kucheza golf kwa nguvu zote na uwezo wote.
mara nyingi tunakubali hatuwezi au hatutaki kwa sababu tumeamua kwamba hatuwezi na hatatuki na huo ndio mtazamo wetu hata hivyo mwenzetu aliamini kwamba bado anaweza kujifunza na kuwa mcheza golf mzuri.
Alijifunza kwa miaka miwili na kuficha hiyo siri kwa mumewe hata hivyo baada ya kuhamia kwenye hicho kisiwa ikawa golf na wao na wao na golf na ikawa furaha ilioje kwa mume kuona mke wake nae kwenye golf wamo.
Hii ni moja ya success story ya kumfanya mume awe anaongea na wewe mwanamke.
Kumbuka unachokifanya sasa ni muhimu sana kwa ajili ya maisha yako ya uzeeni kama wanandoa.
Kama hamuwezi kuwasiliana leo, usitegemee kesho mtaweza kuwasiliana ghafla.
Mke wa Professor!
Linda akafika mahali akajiuliza itakuwaje maisha kama haya ambayo mke na mume hawana kitu cha kuongea pamoja?
Linda akaenda kununua vitabu vinavyohusu ndege, na akamuomba mumewe wahudhurie semina na kitu chochote kinachohusu ndege na ikajibu kwani hata mumewe akawa anapenda sana kuhusu ndege na wamekuwa sasa wanafanya hata vacation mahali ambapo wanaweza kwenda kuangalia ndege (bird watching)
Ni miaka 20 sasa wanafanya kitu kimoja na kufurahi pamoja. Linda hajui lectures ambazo mumme wake hutoa chuo na pia hajui kozi gani anafundisha ila anajua kitu kimoja tu kwamba yeye na mumewe linapokuja suala la ndege huongea pamoja na kuwaunganisha pamoja kama wanandoa.
Inawezekana mumeo ana interest na kitu fulani na kupitia hicho kitu ukiungana naye unaweza kumleta karibu zaidi katika maisha yako kuliko unavyopingana naye.
Kama mumeo ni mlevi wa kutupwa kuungana naye ni kujimaliza mwenyewe!
Wednesday, November 18, 2009
Usiumie!
Hello rafiki Jane,
Asante kwa barua yako ambayo niliipata jana usiku.
Pia pole sana kwa wasiwasi na hofu hata mashaka kutokana na yale unakutana nayo kuhusu mumeo kupata secretary mpya ambaye unahisi anaweza kumteka mumeo.
Kwanza mdogo wangu naomba usipaniki, wala kuwa na hofu na mashaka, usioni ndoa yetu na John imefika umri wa miaka 30 kwani kuna milima na mabonde tumevuka pamoja na moja ya milima ni kama huo wa kwako kujipa wasiwasi kwamba mumeo atachukuliwa na mwanamke anayeshinda naye kazini.
Ni Adamu na Hawa ambao hawakuwa na maisha ya wasiwasi wa mume au mke kuchukuliwa na mwingine kwani wao ndo walikuwa wanandoa wa kwanza duniani hata hivyo kabla ya kuanza kuwa na hofu na mashaka naomba jiangalie kwanza kwenye kioo (sina maana uchukue kioo) nina maana jiangalie mwenyewe kwanza je unampenda mumeo kiasi ambacho unaamini mtu mwingine haweza kuchukua nafasi, maana kuna wakati sisi wenyewe wanawake tunajisahau mno kwenye ndoa zetu.
Nakumbuka nilipokutana na tatizo kama hilo la kwako ilinipasa niende kwa dada wa jirani hapa ambaye ni nyumba ndogo ya kigogo mmoja hapa mjini nikamuuliza inakuwaje au anafanya vipi kuhakikisha mume wa mtu anabaki kwake muda wote hadi anasahau familia yake.
Yule dada alinijibu kwamba anachofanya ni kumpa uhuru huyo mwanaume kusema na kufanya kile ambacho kwa mke wake hapati nafasi, hii ina maana kwamba mwanaume akifika kwake anakuwa huru kusema chochote anataka na kufanya chochote anataka kuanzia jikoni hadi chumbani.
Ile mume wa mtu akifika tu mlango anampokea kwa mabusu na hugs.
Swali je wewe unafanya hayo?
Unampa James nafasi na uhuru kiasi hicho au kila unachofanya unafanya just for granted?
Ukifanya kila kitu kwa kadri ya upendo wako wote kwake basi haina haja kuwa na hofu na huyo secretary labda awe ni mwanaume ovyo.
Tutawasiliana zaidi na pia nitakupigia simu baadae saa mbili usiku tuongee zaidi na nitakushauri zaidi mdogo wangu.
Ni mimi Neema
Tuesday, November 17, 2009
Inaniuma sana!
Hello Neema,
Naamini wewe na mumeo John mnaendelea vema.
Mimi na mume wangu James tunaendelea vizuri ingawa kuna tatizo kidogo.
Ni mwezi sasa mume wangu amepata secretary mpya ofisini kwake na nimesikia huyo secretary bado ni msichana mbichi kabisa na mume wangu amekuwa akimtajataja na kilichonistua zaidi ni kwamba sasa mume wangu amekuwa na tabia ya kuchelewa kurudi nyumbani tofauti na ilivyokuwa kabla ya huyo secretary wake mpya, kibaya zaidi jana amerudi saa sita usiku eti walikuwa na Board meeting.
Ninajaribu kujisahaulisha nisiwaze kuhusu mume wangu na secretary wake kitucha ajabu ni kwamba ndiyo nawaza zaidi na ninavyowaza zaidi natamani kuchukua hatua kubwa zaidi kuhusiana na hili jambo.
Nahisi mume wangu anaweza kutekwa na huyu secretary mpya maana mabinti wa siku hizi hawaaminiki kabisa na mume wangu anavyojua kutoa pesa hapa nina homa ya jiji.
Kilichonistua zaidi ni kwamba jirani ameniambia kwamba eti secretary ni mke wa boss ofisini yaani hapa inaniumia sana, sijui ni wivu au hasira au sijiamini acha tu!
Nishauri nifanyeje?
Ni mimi Jane
Monday, November 16, 2009
Wanaume wengine Ovyo!
Umemfanyia vitu vyote ambavyo mwanaume anastahili kupata wa mke wake hapa duniani. Naamini jibu ni ndiyo, wapo wengi tu iwe mjini au vijijini hali ni sawa.
Mwanaume ovyo ni yule ambaye hataki mabadiliko, na mojawapo ya mifano ya wanaume ovyo ni kama ifuatavyo:-
1. MWANAUME MLEVI (alcoholic)
Ni mwanaume mzuri sana (wonderful) akiwa hajalewa, tatizo ni kwamba si rahisi kumkuta hajalewa.
Anautwika siku nzima, tangu akitokea kazini kwenda nyumbani anakuwa tayari amelewa, anaporudi nyumbani huanza kufungua mlango wa nyumba kwa kelele tangu mita mia kabla ya kuufikia, akifika nyumbani anaanza kuangalia TV na anaenda kulala hapohapo kwenye kiti chake na siku zingine na haja ndogo hapohapo.
Kila siku au muda mwingine ananukia breweries na hii mke hujikuta yupo turned off completely idara zote.
2. MWANAUME ASIYEMWAMINIFU
ndani yake kuna kitu kinamuambia bila mwanamke mwingine yeye si mwanaume tena, hata mke wake ampe zawadi ya mwili kila siku bado akimuona mwanamke mwingine akili zake zinamruka na anachanganyikiwa bila kujali kinachoelea ni dhahabu au maluweluwe.
3. MWANAUME WA PESA, MALI NA MAFANIKIO
Ahadi yake ni kwamba siku tukipata milioni tutaanza kufurahia maisha, baada ya kupata hiyo milioni sasa anasema tukipata milioni 2 ndo tutaanza maisha, baada ya kupata milioni 2 sasa anasema tukipata milioni tatu ndipo tutaanza kufurahia maisha, inaendelea na kuendelea hadi uzeeni.
Ukweli huu ni ugonjwa ila hataki kukubali kwamba ni ugonjwa na kwamba anaumwa.
Eti atacheza na watoto akipata milioni 5, kumbuka watoto hawabaki watoto bali ipi siku wanakuwa watu wazima na kuondoka zao.
Hataki tufurahie tendo la ndoa eti yupo busy kutafuta hizo milioni, hajui miili ikizeeka inaishi kwa medication na hakuna nguvu tena za ku-enjoy sex kama wanandoa.
4. MWANAUME KATARI , JAMII YA AKINA HITLLER
unajua ilivyongumu kuishi na mwanaume mwenye mtazamo kwamba kila kitu unafanya fanya kama ninavyokuelekeza au in my way na anaamini huo ndio ushirikiana wa wanandoa.
Ni kama anajitahidi kufidia yale mama yake alikuwa anamfanyia na ni kweli kwake mwanamke ni kifaa fulani si mtu, si kiumbe sibinadamu.
5. MWANAUME BARIDI
Pole sana, huyu Ukitaka suala la sex amekufa, hana hamu, havutiwi na anaweza kukaa na mke miezi sita bila kufanya mapenzi na akaona ni kawaida.
Anaogopa kuongea na Daktari au mtu yeyote ili kupata msaada wa ushauri.
Ni kama anamlazimisha mke kuwa na maamuzi ambayo mke hapendi na hakutegemea kama yangempata kwenye ndoa yao.
6. MWANAUME MWENYE WIVU WA KUPINDUKIA
Humuamsha mke wake usiku wa manane ajibu maswali yake ya nani aliongea naye mchana, ilikuwaje akawa ana smile alipokutana na James, nani alikuwa anaongea naye kwenye siku nk.
Mke huchoka kwa visa vya kutiliwa mashaka na kujiona mtumwa au yupo jela ndani ya ndoa yake.
Hii orodha ya wanaume hopeless huendelea hadi 7, 8, 9 hadi 116
Hizi ni ndoa ambazo kama ni daraja basi upande mmoja limevunjika na mmoja amegoma kufanya repair kwa ule upande umeharibika.
Katika ndoa za aina hii kuna mambo mawili yanaweza kutokea nayo ni
(a) Mwanamke huweza kuchukua kile tu anaona anakipata na kuamua kuishi katika uhusiano huu na zaidi mke hujijengea aina ya maisha yake anayayajua ndani ya ndoa aina hii na kuendelea kama vile hakuna matatizo yoyote
(b) Mwanamke huamua kuanza mbele (check out)
Na kama mwanamke ameamua kuchukua uamuzi (b) basi kuna maswali magumu na mazito yanahitaji majibu.
Utafanya nini kuhusiano na kipato,
“Divorce doesn’t help a person prone to excessive anxiety and emotional upset”.
Wapo watu huendelea na safari kutoka kushindwa ndoa moja hadi nyingine au kutoka ya kwanza kwenda ya pili na kushindwa na kuendelea na tatu na kushindwa hadi nne, tano na nk, hadi pale wakibadili tabia na mitazamo yao.
Wanasaikolojia wanaita hii tabia ni symbiotics kwa maana kwamba kawaida tatizo hutafuta tatizo lingine (problems looking for matching problem) na hutokea ndiyo maana mara nyingi mwanamke anayemuacha mwanaume hopeless huenda kumpata mwanaume hopeless mwingine mwenye matatizo mapya kabisa.
NB:
Kumbuka kuna matumaini kwa mwanaume yeyote ambaye yupo ovyo au hopeless katika ndoa yako.
Hivyo basi ukimwamini Mungu ndoa yako inaweza kurudia katika matumaini mapya bila kujalisha ipo katika hali tete kiasi gani.
Sunday, November 15, 2009
Uangavu
Kama kuna neno moja la msingi ambalo ni msingi wa ndoa yoyote neon hili ni Uangavu (transparency).uangavu katika ndoa ni mwanaume au mwanamke kuweza kusoma sms na kupokea simu za mwenzake bila mashaka wala wasiwasi, kusoma emails zilizomo kwenye inbox yake bila wasiwasi wala hofu, Kufahamu akaunti yake benki ina kiasi gani, kuongea siri zako kwake bila mashaka na zaidi kuwa huru kuhakikisha mwenzako anajisikia vizuri kihisia.
Unachonga sana!
Je kuna njia yoyote ambayo mwanamke anaweza kufanya mume wake aongee kama hataki kuongea naye?
Ukweli siku zote ukitaka kuleta mabadiliko ni wewe mwenyewe kuanza kujiangalia kwenye kioo (yaani kwa kujiangalia mwenyewe).
Na jambo la msingi ni mwanamke mwenyewe kujiuliza je unaongea sana, je unachonga sana.
Wakati mwingine tunaweza kumasaidia mtu mwingine kuongea hasa kwa sisi wenyewe kupiga zip kwenye midomo yetu.
Wapo wanawake huongea kama kasuku muda wote na hii ni mbaya sana kwa mwanaume yeyote.
Kama hujajua kama wewe ni mwongeaji kuliko kawaida ukitaka kujichunguza basi angalia ukiwa na rafiki zako au ukiwa na mumeo unaongea asilimia ngapi ya maongezi kama ni asilimia 51 basi ina maana you talk too much.
Jambo la pili ni kuangalia unaongelea topic gani au ni topic zipi huwa zinatawala maongezi yako? Na je maongezi yako ni kuhusu wewe mwenyewe tu, au maongezi yako ni nyimbo ambazo mumeo hazipendi.
Jambo la tatu je unaongea topic za wanawake tu?
Hakuna mwanaume ambaye atavumilia kusikiliza women stuff muda wote au feminine stuff all the time.
Hivyo ni muhimu kuangalia subject na muda unaotumia kuongea.
Jambo lingine la msingi ni wewe mwanamke kujifunza vitu ambavyo huweza ku turn off mwanaume na asiongee na wewe.
Kwa maelezo zaidi soma hapa
Mmmmm.................
Mara nyingi tunaamini kile mtu anaongea sisi tunafahamu zaidi hata kabla hajamaliza na zaidi tunawakatisha kuendelea kuongea na kuwasaidia kumalizia kile walikuwa wanaongea.Hatusubiri hadi wamalize kile wanaongea huku tukiwasilikiza ili waongee chote walitaka kuongea.
Sasa jawabu ni nini?
Wanasaikolojia wanasema kwamba jibu la hili tatizo ni pale tu watu tutakapoamua kusikiliza kwa kutumia sikio la tatu.
Hii ni sanaa, hivyo unaweza kuwa na aina fulani ya signal kuonesha unaelewa kile anaongea.
Na signal nzuri kwenye ndoa ni uwezo wa kuitikia “Mmmmmmmm…. Na maana yake ni kwamba unavutiwa na kile anaongea na kwamba anatakiwa kukueleza zaidi au kuongea zaidi kwani upo tayari kusikiliza.
Wanaume nao........
Wanaume hufa mapema zaidi kuliko wanawake:Kuna wazo ambalo kampuni nyingi za Bima zinalitamka wazi kwamba wanawake wengi wazee watakuwa wajane miaka 7 hadi 11 baada ya mume kufa.
Hii ina maana kwamba wanaume hufa miaka 7 hadi 11 kabla ya wake zao.
Sasa swali ni kwa nini wanaume hufa mapema zaidi ya wake zao.
Wanaume wengi hawako honest kwa wake zao kuhusu kitu chochote katika maisha.
Wanakuwa na maisha yaliyofungwa (boxed) zaidi kuliko wake zao.
Hii ina maana kwamba wanaume wengi huficha true feelings walizonazo, na kila wanapoficha hisia zao hupunguza life span yao.
Ni mmoja tu au wawili duniani!
Kila mwanandoa isipokuwa mmoja au wawili tu duniani hatakuwa na matatizo yanayohusu tendo la ndoa na wengi wanaokwambia hawana matatizo yoyote watakuwa wanakudanganya na unatakiwa kuwa makini kuwasilikiliza kwa sikio lako la tatu.
Kila mwanaume tangu siku akioa lazima atakutana na tatizo lolote iwe kukojoa mapema (pre ejaculation), kutosimamisha (kudindisha), kukosa uzazi nk. Vyote ni sehemu za changamoto ya kuendelea kujifunza.
Habari njema ni kwamba kuna njia ya kuondoa haya matatizo ukianza na moja hadi jingine na njia sahihi ni kukubali kwamba kuna tatizo na kuanza kupambana nayo hadi unapata jibu na si kutumia muda mwingi kufikiria tu bali fanyia kazi.
Friday, November 13, 2009
Kucheza kimapenzi
Katika moja ya misingi ya kujenga mahusiano kati ya mke na mume ni pamoja na mke na mume kuwa na muda wa kucheza pamoja.Tuache kucheza michezo mingine tuangalie kucheza kimapenzi.
Kwanza, lazima muwe ninyi wawili tu.
Pili, mnahakikisha kuna kuheshimiana katika kuchagua mchezo mnaotaka kucheza.
Tatu, mchezo wenu hauwezi kusababisha maumivu kimwili, hisia na kukwazana kiroho.
Na tano hakuna kuingiliana kimapenzi (no genital union)
Tumegundua Siri (majibu)
Hata hivyo baada ya kuingia chumbani na kuanza kuomba jambo moja limejitokeza nalo ni namna gani tuombe kwani kuna aina fulani ya vizuizi ambavyo vimejitokeza ngoja nikueleze vizuri hapa chini naamini utaweza kutushauri pia.
Mimi ninafahamu jinsi ya kuomba (kuongea) na Mungu mwenyewe na nimezoea hivyo bila mtu mwingine kunisikiliza na huwa nakuwa wazi sana kueleza kila kitu kwa Mungu bila kumficha, nipo wazi (transparency).
Tunaomba msaada wako iweje kwani tumeamua kuwa na maombi kabla ya kuwa mwili mmoja kila siku tukiwa faragha.
Usichoke kutushauri na Mungu akubariki sana na msalimie mumeo mpenzi John.
Jane (Mrs James)
Wednesday, November 11, 2009
Tumegundua Siri!
Kuna siri moja ambayo tumeigundua na mimi na mume wangu ni watu wa vitendo na si maneno, tuliamua kwamba kama kweli kufanya hili jambo kabla ya kuwa mwili mmoja lina maana na huleta matokeo tuliamua kufanyia kazi kwa nguvu zote.
“Great prayers are the way to great sex”
Pia tumegundua kwamba:-
“Sex at its best is spiritual”
Ni kweli tumegundua kwamba miili huunganika vizuri pale roho zinapounganika zaidi na njia nzuri ni maombi ya pamoja hivyo kabla ya tendo la ndoa tunaanza kwa maombi, kuombeana na pia kuomba Mungu atusaidie ili tunapopeana zawadi ya mwili kila mmoja apate raha nk.
Sasa hivi nikimsikia mume wangu John ananiambia twende chumbani kuomba mwili mzima unanisisimka na najua sasa raha inakuja na kuridhika kumewadia acha tu…….
Pia tumegundua kwamba kila kitendo cha kuomba pamoja (mara nyingi tukiwa tumekumbatiana) na kuwa karibu kiroho na kimwili hutusaidia kufanya discovery ya qualities za ndani na nje ambazo bila maombi tusingeweza kuziona na hivyo kupendana zaidi, ni kama kila siku namuona mume wangu ni mpya na anang'aa zaidi katika tabaia na u-handsome wake, eti naye anasema siku hizi nimekuwa mrembo ya uhakika na pia tabia yangu ni nzuri sana, naamini ni kwa sababu ya maombi.
“Ninamuona special na yeye ananiona mimi ni special”
Waingereza wanasema
Hivyo dada Jane kama unataka wewe na mumeo james mambo yawe sawa usisahau hii siri ya kuomba pamoja kabla ya kuwa mwili mmoja.
Kumbuka:-
“Jinsi Mume na Mke wanavyoweka urafiki pamoja na Mungu kwa njia ya maombi, ndivyo Mungu anavyoidi kuimarisha urafiki kati ya mke na mume”
Ni mimi rafiki yako
Tuesday, November 10, 2009
Kuna aina tofauti!
Aina za tendo la ndoaKuna wakati wanandoa hujikuta wanahitaji kuwa na tendo la ndoa ambalo ni perfect, kama tetemeko la ardhi, kama fireworks na kufika kileleni kwa mpigo na raha ya ajabu.
Utakuwa umepiga hatua kubwa sana au umefanikiwa sana katika ndoa kama utafahamu kuwa kuna aina mbalimbali za sex na wakati mwingine haitajalisha kama utafika kileleni au la kwani lengo ni kuhakikisha mke wako au mume wako yupo connected katika feelings zake na wewe.
Saturday, November 7, 2009
Usitanie ni mali yenu!
Mzuri kitandani?Tunapooana kama wanandoa tunakubaliana kwamba tutakuwa tunafanya tendo la ndoa sisi wawili tu maisha yetu yote (monopoly) haijalishi tunafanya kwa kufikiria, au kwa kutofikiria, au tunafanya bora liende au kwa ufanisi, tunfanya kwa kupenda au kulazimishwa, tunafanya kwa ubunifu au kwa uchoyo au kwa kubania au kwa hiari au vyovyote vile kitabu kimefungwa na lazima kila mmoja apate kile mwenzake anampa iwe nusu au kitu kizima au kunyimwa kabisa au kupewa kila ukihitaji.
Ukweli wengi wetu huwa tunachukua kila kitu for granted, hakuna efforts zozote tunaweza kuziwekeza kuhakikisha mwenzako anapata the best kutoka kwako hasa linapokuja suala la tendo la ndoa kwani ni wewe tu ndiye mwanamke au mwanaume duniani ambaye amekubali kuishi na wewe na kushirikiana kupeana hiyo zawadi ya mwili ambayo ni mali ya ndoa yenu na sivinginevyo.
Je, una hamu ya kumpa kitu cha uhakika (mapenzi, mahaba) kwa sababu ya jinsi anavyokupenda, anavyokujali na jinsi alivyoshirikiana na wewe hadi hapa mmefika?
Au umefika mahali umechoka, huna hamu tena ya kuhakikisha mume wako anapata kila mlikubaliana wakati mnaoana?
Je, kwa nini huweki juhudi yoyote kuhakikisha kitanda chenu kinakuwa mahali bora kukimbilia kama mke na mume?
Sex ni mali ya ndoa na ndivyo Mungu alivyo design, hivyo kama upo kwenye ndoa ina maana suala la tendo la ndo lisichukuliwa just for granted, panga, andaa na wekeza kwa uwezo wako wote kuhakikisha mke wako au mume wako anaridhika na wewe na utendaji wako.
Kumbuka Bibilia inasema:
“Ndoa na iheshimiwe na watu wote, nayo malazi yawe safi, kwa kuwa Mungu atawahukumu wazinzi na waasherati wote.
Waebrania 13:4
Ndoa haibadilishi jiko.....................
Jiko la mkaa na MicrowaveMwanaume huweza kusisimka ndani ya dakika 2 au 2 na wakati mwingine sekunde 30, Lakini mwanaume huchukua zaidi ya mara 10 ya mwanaume kusisimka hii ina maana ni dakika 20 kwenda 30 kwa mwanaume kuwa amesisimka kiwango cha kutosha.
Biblia inasema:-
Upendo hauna kiburi.
Haukosi kuwa na adabu.
Upendo hautafuti mambo yake, haukasiriki upesi, hauweki kumbukumbu ya mabaya.
Upendo haufurahii mabaya bali hufurahi pamoja na kweli.
Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote.
(1Wakorintho 13)
Kwa maelezo zaidi soma hapa
Kulala vizuri ni kuwa sexy!
PumzikaWanawake ambao hujimyima usingizi hawapo sexy, hivyo kabla ya kufikiria kuwa na maisha mazuri ya kimapenzi na mke wako au mume wako zingatia kwanza kuwa na muda mzuri wa kupumzika.
Eti Sivutiwi!
Wakati mwingine Inashangaza sana jinsi wanawake wanavyowawekea kiwango cha chini wanaume kuhusiana na hamu yao ya tendo la ndoa.Ni kubusu tu!
Kwa maelezo zaidi soma hapa
Kileleni kwa mpigo!
Kuna imani potofu kwamba mke na mume huweza kusisimka kwa wakati mmoja na kufika kilele kwa wakati mmoja na hii kufanya tendo la ndoa kuwa la kuridhisha zaidi.Usiwe bubu wa ishara
Kutoa IsharaKuonesha ishara (positive) wakati mke na mume wapo kitandani huweza kusaidia ufanisi na kila mmoja kujisikia vizuri hata hivyo lawama au kukosoana au upekuzi au kumlalamikia au kusutana na mwenzako kwa kile anakufanyia (criticism) kamwe havichangamani na kusisimuana kimapenzi.
Kama unahisi unahitaji kumrekebisha kile anafanya ni vizuri kutoa comments zako zikiwa positive kuliko zikiwa negative.
Badala ya kusema kwa sauti ya juu na hasira
“Wewe vipi mbona unanikandamiza kwa nguvu niache”
kwa nini usiseme kwa kumnong’oneza
“Mpenzi polepole nitajisikia vizuri zaidi na asante”
Pia ni vizuri kufahamu kwamba mkiwa kitandani kuna lugha ya alama (Non verbal cues) ambapo mnaweza kuwasiliana vizuri bila kuongea kwa maneno.
Baada ya kila mmoja kufahamu hii lugha ya alama mnaweza kuwa na enjoyment zaidi katika faragha yenu.
Kama vile kila mmoja kuupeleka mkono wa mwenzake pale anaona kuna njaa ya kuguswa.
Pia unaweza kupeleka au elekeza mwili wako au kiungo chako sawa sawa na stimulation unayotaka.
Pia ni muhimu kuwa wabunifu.
Husisimka sawa
Mwanaume na kuongezeka Umri.Mwanaume anavyozidi kuongezeka umri huhitaji direct stimulation ya stick yake kuwa tayari kwa ajili ya sex kuliko kuitikia kwa kuona kama kawaida ya wanaume.
Hata hivyo kitendo hiki kuimarisha tendo zima la ndoa kati ya wanandoa kwani mke na mume wanavyozidi kuongezeka umri sasa wote huhitaji kuchezeana viungo vyao ili kuwa aroused na tayari kwa kupeana zawadi yao ya tendo la ndoa.
Zaidi soma hapa
Kupanga
Inashangaza sana mke huwa na mipango kamili na kuwekeza jitihada kubwa kwa ajili ya maandalizi ya mlo wa kawaida iwe chakula cha mchana au usiku au kifungua kinywa.Lakini tunaamini kwamba tendo la ndoa linatakiwa kuwa ghafla kama vile kwenda jikoni na kuanza kupanga sahani za chakula na kusema leo tutakuwa na mlo wa ghalfa, naamini mlo wa aina hiyo haupo kwani inabidi kupanga kwanza.
Hata tendo la ndoa ni the same, ingawa hatufanyi hivyo hatuna planning, bila kupanga, maandalizi, makusudi, maazimio au kuwa na jitihada tunaweza kujikuta tumechoka na hakuna kuridhishana.
Kama tunahitaji tendo la ndoa linaloridhisha kupanga ni muhimu na kuwasiliana kati ya mke na mume kuhusiana na tendo hili takatifu ndani ya ndoa ni muhimu sana.
Pia tunahitaji kuweka kipaumbele kwa ajili ya tendo la ndoa kama tunavyoweka kipaumbele vitu vingine kama vile kulipa bills, kuhakikisha watoto wanapata chakula, ni rahisi sana kufikiria kwamba mbona hata kesho ipo hata hivyo wakati mwingine tunahitahitaji kuzipa hisia zetu kile zinataka.
Zaidi soma hapa
Kuponya Maumivi ya Kuachana (7)
HATUA YA NNE NI KUSEMA KWA HERIHii ni hatua ngumu sana kukutana nayo kwani ni hatua ambayo unakubali na kumwambia kwa heri Yule amekuacha.
Hapa ni hatua ambayo unakubali kwamba ni kweli mahusiano yamefika mwisho.
Hapa una admit kwamba huyu mtu hayupo tena katika maisha yangu na sasa natakiwa kuendelea mwenyewe.
Kumbuka ukitaka kuwa mtu huru na uweze kuendelea mbele jambo la msingi katika hatu hii ni wewe KUMSAMEHE.
Andika kwenye karatasi yale unaamini mpenzi wako amekukosea na yasome na kuomba Mugu akusamehe na yeye pia umsamehe.
Bila kusaheme inakuwa ni sababu muhimu sana ya kuzuia Baraka zako kwwa mahusiano yajayo na mahusiano yako wewe na Mungu.
Tunaweza kusaheme kwa sababu Mungu anatusamehe.
Inawezekana wakati upon a mpenzi wako kulikuwa na maeneo muhimu ambayo mlikuwa mnaenda pamoja inaweza kuwa ni kanisa, hotel, viwanja na sehemu za vacation na tangu mmeachana ukizikumbuka hizo sehemu unajisikia uchungu sana.
Kama unapotembelea hizo sehemu unajisikia hofu na uchungu kitu cha msingi kufanya ni wewe kwenda na rafiki zako/yako na ziombee kwa Jina la Yesu.
Mungu atakupa amani na utajisikia raha kuwepo hizo sehemu tena.
HATUA YA TANO NA SITA KUJIJENGA NA MATUMAINI MAPYA
Kwenye hatua hizi mbili sasa unaweza kuiongelea future huku ukiwa na matumaini mapya.
Hata hivyo tunatakiwa kukumbuka kwamba kukiwa na tukio la kuachana huwa kunakuwa na matokeo ya aina tatu kwa aliyeathirika.
Kuponya Maumivu ya Kuachana (6)
HATUA YA TATU NI KULALAMIKAHisia za lawama huweza kukupata na ukazielekeza kwa yule amekuacha au hata wewe mwenyewe.
Tabia yako na matendo yako huweza kubadilika na wewe mwenyewe ukajishangaa, unaweza kujiingiza katika Ulevi wa pombe kupindukia, kutembea (sex) na wanaume/wanawake tofauti na huko nyuma.
Hofu ya kukataliwa, upweke (isolation) na kujiona hujakamilika huweza kusababisha uwe na tabia ambazo ni tofauti na values zako mwenyewe.
Ukiwa kwenye hatua hii unaweza kujiingiza kwenye makosa ambayo yanaweza kusababisha kushindwa kupona maumivu ya kuachwa kwani unaweza kujikuta unakuwa na mawazo ya jumla kuhusiana na maisha na jinsi unavyowaona wengine (wanawake na wanaume) unaweza kuamini kwamba:-
“Wanawake wote hufuata wanaume kwa sababu ya pesa”
Wanaume ni viumbe wa sex kama wanyama hakuna mapenzi”
“Wanawake wote wamejaa emotions na hawawezi kufikiria mambo”
Pia katika hatua kama hii unaweza kujikuta unajipa utabiri wako mwenyewe na utabiri ambao siku zote si kweli kama vile:-
“Sitaolewa tena au sitaoa tena kwani sioni kama kuna mtu atanipenda tena”
“Nitabaki single maisha yangu yote kwani najiona nimeshajizeekea nani atanioa”
Utabiri potofu wa aina hii huweza kukufanya kuwa kipofu kuona uwezekana na Baraka zilizo mbele yako.
Mtazamo kama huu hukufanya uwe defeated mapema kabisa.
Utabiri wako potofu unakwambia mahali ulikotoka badala ya mahali unapotakiwa kwenda.
Utabiri kama huu badala ya kujenga husaidia kuwa kilema wa relation inayofuata.
Kosa lingine kubwa ambalo linaweza kukupata katika hatua hii ni kuwa na matarajio yasiyowezekana.
Unaweka matarajio kwa ajili yako na wengine kama vile:-
“Lazima niwe perfect ili nipendwe”
“Kama sijatimiza mahitaji yake anaweza asinipende”
“Kama akiniuliza kuhusu mahusiano yangu ya zamani basi atakuwa hanipendi”
Kuwaza hivyo na kuwa na matarajio ya aina hiyo ni kujiweka katika mtego ambao ukinasa unaweza kujiharibia mahusiano yanayofuata.
Kosa lingine la kawaida ambalo unaweza kulifanya katika hatua hii ni kulipa kisasi (revenge loving).
Kwanza unajiangiza kwenye mahusiano mapya ili aliyekuacha au uliyemuacha apate wivu.
Unafanya kila njia na juhudi kuhakikisha aliyekuacha au ulimuacha anafahamu na kukuona na mpenzi mpya.
Pili ukiwa na mpenzi mpya unakuwa na tabia ya kumpa suluba kama ulizokuwa unapewa, kama ulikuwa unateswa au kutukanwa unatumia the same weapon kwa mpenzi wako mpya.
Tatu unaamua kum-control mpenzi mpya idara zote kuogopa na yeye asijeakakuacha na kukuumuza tena.
Tatizo lingine kubwa ambalo unaweza kukutana nalo kwenye hii hatua ni kuwaza kuwa na mpenzi mpya ambaye kwa viwango vya duniani hayupo kwa maana kwamba unaweka qualification za juu kuliko binadamu yeyote.
Kosa lingine ni kwamba unaweza kujikuta unaangukia kwa mwanaume wa aina ile ile tena au mwanamke wa aina ile ile tena kitu kinachodhihirisha kwamba matatizo yaliyokuwepo mara ya kwanza badala ya kuyatatua mliamua kulaluana wenyewe.
Thursday, November 5, 2009
Kuponya Maumivu ya Kuachana (5)
HATUA SITA AMBAZO ALIYEACHWA HUPITIA ILI KUPONYA MAUMIVU.Kama kuugulia tunakopata kutokana na mtu kufa, hatua unazoweza kupitia baada ya kuachwa katika mahusiano zinajulikana na huwa na makali mfano wa kifo.
Hizi hatua zinaelezea hali ya kawaida na afya katika kukurejesha katika hali ya kawaida baada ya kuachwa.
Kama uponyaji (healing) umetokea kutokana na maumivu ya kuachwa bado utabakiwa na kovu (emotional scar) na si kidonda na lengo ya kuachambua hizi hatua ni ili wewe ufikie kuwa na kovu na si kubaki na kidonda miaka nenda rudi.
Watu ambao wameshindwa kumaliza hatua zote zinazotakiwa wamejikuta wakiwa katika maumivu na vidonda kutopona (hubaki vidonda ndugu) hadi zaidi ya miaka 15. Inahuzunisha sana!
Jambo la msingi ni kukumbuka kwamba hizi hatua ambazo unapitia hutofautiana urefu na makali kutokana na namna ulivyodumu kwenye mahusiano na jinsi mlivyopendana.
Kuna hatua sita ambazo unaweza kupitia ukiachwa na yule ulikuwa unampenda, maumivu huwa makali sana katika hatua tatu za kwanza na unavyozidi kuendelea maumivu huendelea kupungua hadi hatua ya mwisho na wewe kurudi katika hali yako ya kawaida.
Jinsi unavyoendelea kutika hatua moja hadi nyingine hofu na mashaka huendelea kupungua.
Jambo la hatari ni pale unapokwama kwenye hatua moja bila kusonga mbele au kuendelea hatua nyingine.
HATUA YA KWANZA NI MSHITUKO
Unapoachwa na mtu unayempenda duniani utajisikia kutelekezwa, kutishwa, na kupata mshituko wa kutisha (total shock).
Hata kama kuachana kulikuwa kumetegemewa au ulikuwa unajua mapema siku ya kuachana kikwelikweli ni mshituko wa ajabu.
Ukweli hili jambo ni tofauti kwani wengi hushindwa kuendelea na kazi au shughuli zao za kila siku kama vile kushindwa kula, kulala, kwenda kazini.
Unakuwa mtu wa machozi, ni kulala na kushinda unalia kulikotawaliwa na upweke na hofu ya watu watakuonaje, watasemaje na zaidi your future.
Badala ya kuishi kama kawaida unaanza kuishi kwa feelings, na feelings huwa na nguvu kuliko wewe (nafsi)
Hata hivyo unahitaji kuwa na feelings za aina hii ili uweze kupokea healing na hili tukio.
Katika hatua kama hii unahitaji kuwa na watu wa karibu kukutia moyo kwani uwepo wao hukusaidia kuondoa upweke.
HATUA YA PILI NI MAJONZI/HUZUNI AU MASIKITIKO
Hii hatua huweza kuwa ndefu kutokana na kuugulia au kusononeka au kuomboleza mambo mazuri ulikuwa unafanya naye, umepanga naye na kuahidiana naye na zaidi yale ambazo mlipanga na hamjatimiza bado.
Bahati mbaya ni kwamba wote umelekeza hasira zako wanaweza wasiwe na taarifa kwamba umewakasirikia.
Katika hatua hii unakuwa na mawazo ambayo ni potofu wewe na kuachwa kwa mfano unaweza kuwaza na kujisemea kwamba:-
“Hakuna anayefahamu uchungu na maumivu niliyonayo”
“Afadhari nife kuliko aibu kama hii”
“Kila mtu ananiongelea mimi na kuachwa kwangu”
“Kila ninakopita wananinyoshea vidole kunisema na kunicheka”
“Hata rafiki zangu wananikwepa”
Wanajua na kufahamu feelings za kuachwa, wanafahamu jinsi kisu cha maumivu kinavyokata hadi kukosa usingizi, kula na kwenda kazini.
Unaweza kujawa na mawazo kwamba kila mtu anakuchukia na pia unaweza kuwaza kwamba Mungu amekuchukia hata hivyo inawezekana wengine wanakwepa kuongea na wewe kwa kuhofia kushindwa nini waongea (kama umepata talaka) pia kumbuka Mungu anachukia kupeana talaka hata hivyo Mungu anampenda mtu yeyote aliyepewa talaka.
Pili soma haya maandiko kwa sauti
Isaya 26:3
Efeso: 4:23
Wakolosai 3:1,2
2Wakorintho 10:5
Wafilipi 4:6-9
Wednesday, November 4, 2009
Kuponya Maumivu ya Kuachana (4)
Kuvunjika moyo, kukatishwa tamaa, upweke, nk ni maneno yanayoelezea feelings za uzoefu ambao binadamu hupitia pale mahusiano yanapovunjika iwe urafiki wa kawaida, uchumba au ndoa.Kila survivor wa kuvunjika kwa mahusiano huendelea kuwindwa na mabaki ya hofu na mashaka ya mahusiano yatakayofuata.
Wapo ambao baada ya mahusiano kuvunjika huanza mahusiano mapya ambayo huvunja moyo tena kama mara ya kwanza na hawakati tamaa na hujifunza kwa kuondoa hofu na mashaka na kujenga trust upya na kuendelea kufurahia mahusiano mapya tena.
Wengine huruhusu vidonda (emotional) kuendelea kuwatawala na wanakuja wamejifungia (locked) kutoruhusu kupenda na kupendwa upya.
Jambo la msingi ni kwamba maumivu ya kupotelewa au kuachwa na mtu unayempenda ni moja ya maumivu makali sana na baada ya kuachwa kupenda tena huwa ni moja na hofu kubwa sana mtu anapitia katika maisha yake kwani wengi hujikutana wanakutana na walewale.
Unapompenda mtu kwa moyo wako wote na hisia zako zote na kwa mapenzi yako yote, mahusiano yanapovunjika maisha hubadilika na kuathiriwa kiasi cha kusimama ghafla.
Kuna usemi kwamba
“Usually the first love lost is the most painful”
Na wakati mwingine hufikiria mbali zaidi kwa kuamua kufanya kitu chochote kuhakikisha wanarudiana kibaya zaidi partners wao huwa walishafanya maamuzi na hawawezi kurudi tena.
Pia unapoachwa na mpenzi feelings zako hujigawa pande mbili, upande wa kwanza unakwambia unaweza kuanza mahusiano mapya sasa na upande mwingine unakwambia usifanye na ukifanya au jiingiza kwenye kupenda tena utaishia kuumizwa kama mwanzo.
Pia kuacha au kuachwa hujenga kujisia hatia (guilt) bila kujalisha wewe ni uliyeachwa au uliyeacha, rejected au rejecting, dumped au dumper wote huwa na hisia za kujiona ni failure.
Kujisikia hatia hujenga hali ya kujisikia kutojiamini na kutojiamini huzaa hofu ambayo huendelea kukuwinda kila mara unapokumbuka mahusiano yalivyovunjika.
Hiyo hofu huingia akilini na kugonga kama nyundo kukumbushia machungu na makali ya kuachwa hadi unafikia hali unajikuta kuchanganyikiwa kama si kupaniki.
Vilevile hofu hii huweza kupooza hatua yoyote unayotaka kuchukua ili kuanza mahusiano mapya na unajikuta huwezi kuwekeza tena kwenye kupenda na kupendwa upya, unakuwa mwoga kupenda upya na unaogopa pia kukaa mwenyewe bila mtu wa kukupenda, ni kizunguzungu tu.
Jambo la kujiuliza kwa nini unajisikia hatia je, ni kweli ni wewe uliyesababisha mahusiano kuvunjika au ni illusions tu?
Je, ni kweli ulivunja kiapo (vow/covenant) ulichoahidiana na mpenzi wako?
Je, ni kweli hukuwa responsible kwenye mahusiano hadi hajavunjika?
Kama si kweli basi unajichukulia lawama ambazo hustahili.
Je, ni hatua ngapi mtu aliyeachwa anaweza kutumia ili kuponya maumivu yake na kurudi kwenye maisha ya kawaida?
Kuponya Maumivu ya Kuachana (3)
Kuachwa (na mpenzi) ni tukio gumu na zito na huja na mabadiliko tofauti na kumpa mtu uzoefu wa aina yake, ni ngumu na inaumiza sana, lakini watu hujifunza kukua, hupata mitazamo mipya kimaisha, uelewa mpya, na uchujaji wa mambo upya na matumaini mapya ingawa huwa ngumu sana kuona mbali au mbele baada ya kukutana na hii patashika.Hakuna anayependa kuachwa, kwani ukiachwa unajiona umefeli na tumefundishwa katika maisha jambo la msingi ni kuwa washindi si kufeli au kuwa failrues. (winners not losers).
Inaumiza sana kwa sababu hatujafundishwa kutegemea kushindwa na pia hatujafundishwa tukishindwa tufanye namna gani (how to handle).
Mtu yeyote anapokutana na kushindwa wengine huanza kumlaumu na kumtamkia maneno kama vile:-
“Angekuwa mke mwema wala asingeachwa na mume wake”
“Wazazi wake wangekuwa makini mtoto wao asingejiunga na wavuta bangi”
“Asingekuwa anajifanya mjuaji asingefukuzwa kazi”
“Wangekuwa wanaishi Kikristo haya yote (mabaya) yasingetokea”
Je, umewahi kuwa na mawazo ya namna hiyo kwa wanaoshindwa?
Naamini umewahi na ndivyo binadamu tulivyo.
Yohana 9:1-3
Yesu alipokuwa akipita, akamwona mtu aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa. Wanafunzi Wake wakamwuliza,
Mungu anachukia wanandoa kuachana, anachukia talaka na talaka si mpango wa Mungu bali mwanadamu, hata hivyo Mungu anawapenda walioachwa na waliacha, Mungu anawapenda walipewa talaka na bado ana mpango na maisha yao ingawa sisi binadamu huweza kuwakwepa walioachwa na kutalikiwa na kuwaona ni watu wenye hitilafu katika maisha.
Tuesday, November 3, 2009
Kuponya Maumivu ya Kuachana (2)
Kwa nini maumivu ya talaka au kuachwa na mpenzi huwa machungu zaidi ya kifo?Kawaida inapotokea kifo jamii nzima huhusika kwa kuwa ni suala la jamii nzima yaani msiba, watu wote wanakuja kulia na wewe, kuimba na wewe, kukuliwaza na zaidi hata kutoa michango mbalimbali kuhakikisha unakuwa na maisha.
Unapoachana na mpenzi wako au kupewa talaka hakuna mtu wa kuwa na wewe ni wewe peke yako (no shoulder to cry).
Unapoachana na mpenzi wako ni shida yako mwenyewe (lonely hell)
Pia unapoachwa na mpenzi au talaka ukienda mtaani siku moja utakutana na yule alikuacha au achana naye na kama una hasira naye hali huwa mbaya zaidi ila kama ni kifo hutaonana naye.
Unapoachwa hisia zako hujigawa pande mbili ile inayosema unaweza kuwa na mahusiano mapya na ile inasema ukiwa na mahusiano mapya utaishia kuachwa kama mwanzo.
Sunday, November 1, 2009
Kuponya Maumivu ya Kuachana (1)
Kawaida mahusiano yoyote ya mapenzi yanapofika kwenye mzozo mkali (battlefields) huwa na matukio matatu tu.Kwanza mmoja huamua kuondoka zake na kuanza mbele au pili wote au mmoja huamua kuendelea kuishi katika mahusiano ambayo hata hayaridhishi/bora liende au tatu wote au mmoja huamua kuanza kupenda upya katika hali zote kuhakikisha mahusiano yanarudi kwenye mstari.
Hata hivyo inakuwaje pale mmoja anaamua kuanza mbele na kumuacha mwenzake kwenye mataa?
Mara nyingi mahusiano yanapokatika iwe uchumba au iwe ndoa au iwe urafiki a kawaida unaweza kujikuta umechanganyikiwa bila kujali ni wewe uliyeamua kumuacha mwenzako au wewe uliyeachwa (The Dumper and The Dumped).
Bahati mbaya ni kwamba si wote wenye uwezo na nguvu za kujikusanya na kuendelea na maisha kama kawaida kwani wengine hudhoofishwa na kufikia mahali wanaona maisha hayana maana tena.
Kila mahusiano lazima yatakufikisha mahali ambapo utajifunza na kukua haijalishi yanaendelea au yamefeli. Hata hivyo mahusiano yanayoshindwa hufundisha zaidi na hutoa uzoefu mkubwa kwani mafanikio huja si kwa kurudia makosa yale tumefanya au kuchukulia vitu for granted bali kuepuka yale tulifeli mara ya kwanza.
Nimewahi sikia mtu mmoja muhimu sana akiongea maneno haya:
“Nisingeweza kufikia mafanikio yote haya kama si kuwa na mtazamo mpya na kuongeza juhudi kujenga taaluma yangu baada ya kuachwa na mchumba wangu wa mwanzo na hatimaye kumpata mume bora niliyenaye sasa”
Tutaendelea kesho............................
Saturday, October 31, 2009
Umri ni namba tu!
Mamia ya watu walihudhuria sherehe za harusi ya mzee Ahmed Muhamed Dore mwenye miaka 112 akiaoana na binti aitwaye Safia Adulleh mwenye miaka 17.“Leo Mungu ameniwezesha kufikia ndoto yangu” alisema mzee Ahmed Muhamed Dore baada ya kuoana na binti mbichi kabisa kutoka maeneo ya Galguud huko katikati ya Somalia.
Mambo yanayovutia kuhusu hii ndoa
Wanafamilia wa binti wanasema binti yao amefurahi kupata mume.
Bwana harusi alikuwa anasubiri kwa karibu zaidi binti aendelea kukua hadi amshauri waoane bila kumlazimisha bali kumvutia kwa upendo ili waoane.
Ni ndoa ya aina yake kwenye eneo ya Horn of Africa kwa babu miaka 112 kuoana na binti wa miaka 17.
Wapo watu ambao hawaridhiki na tofauti ya umri ingawa katika sheria za kiislamu inaruhusiwa.
Wapo waliofurahi na kukiri kwamba umri si kizuizi linapokuja suala la ndoa na kupendana.
Bwana harusi tayari ana watoto na wajukuu 114 huku motto wake wa kwanza akiwa na miaka 80.
Bado anaamini huyu mke mpya ataendelea kumzalia watoto.
Zaidi anakiri kwamba ni Baraka sana kuwa na mtu unayempenda na akaendelea kukutunza.
Kwa maelezo zaidi soma hapa
Friday, October 30, 2009
Utaumia!
Tafadhari chukua glass ya maji mkononi, usisome tu naomba kama unaweza chukua glass jaza maji na ishike mkononi.Ndivyo mahusiano ya ndoa yanavyofanya kazi wakati mwingine.
Kuishi wawili ni sharing ya mambo mbalimbali na kuna wakati mwenzako anaweza kukwaza, kukuumiza, kukusema vibaya, kufanya vibaya, kukutukana, kukudanganya nk na kila kitu unafanya kwake au wewe unafanyiwa kina uzito mkubwa au mdogo sana moyoni kwa partner wako.
Inawezekana chanzo cha hasira zako au uchungu ulionao au maumivu uliyonayo nk ni matokeo ya vitu ambavyo uliweka moyoni mwako miaka 5 au 10 au 25 iliyopita katika ndoa yako.
Kubwa zaidi hukufanya juhudi yoyote kuhakikisha unaongea bayana na wazi kwa mke wako au mume wako na kutokana na hiyo tabia leo umefika hapa baada ya hayo mambo kujijenga kwenye moyo wako kwa miaka zaidi ya 5 nk.
Huku mwenzi wako akiwa amesahau hayo mambo, wewe umeendelea kuyashika ndani ya moyo wako na ni wewe unayeumia kwani mwenzio hajui kama bado yapo moyoni mwako.
Hata ukimwambia leo anaweza kuwa shocked kusikia kwamba bado ulikuwa umeweka jambo au mambo kama hayo moyoni.
Unajisikia humpendi tena mume wako au mke wako.
Na kidonda kinazidi kuliwa na wadudu na damu kutoka bila wewe kujua.
Jifunze kuwa wazi na kuongea kwa mpenzi wako kama amekukosea mwambie na msahemeane na kusahau yaliyopita.
Thursday, October 29, 2009
Nani ana Hasira Zaidi?
Je, wanaume hukasirika zaidi kuliko wanawake?Wengi huwaona wanawake ni viumbe ambavyo vipo emotional na very affectionate wakati wanaume ni aggressive na wakati huohuo very courageous.
Tafiti nyingi hazioneshi kwamba wanaume hukasirika haraka kuliko wanawake bali zinaonesha tofauti iliyopo hasa namna ya kuonesha (express) hizo hasira.
Ukweli ni kwamba wanaume na wanawake wote huwa na mawazo sawa ya kukasirika, ingawa wanawake huonesha intensity kubwa ya hasira na kwa muda mrefu na hupenda kutoa hasira zao kwa njia ambayo ni submissive zaidi ya wanaume.
Kwa upande mwingine mwanaume akikasirika anachukua direct approach ili kupambana na mtu amesababisha akasirike.
Wednesday, October 28, 2009
Hataki kuongea!
Mimi ni mwanamke ambaye nipo kwenye ndoa sasa mwaka wa 8 nimekuwa nikitatizika sana na tabi ya mume wangu kushindwa kuongea na mimi, kila nikitaka kuongea chochote anaonesha hali ya ku-ignore kile nataka kumwambia.
Kinachoshanga zaidi ni kwamba tunapoenda kazini wote tunatumia gari moja hata hivyo zaidi ya Km 8 zote tunakuwa mabubu hadi kila mmoja anaenda kazini kwake na ni kama vile tumekuwa watu wawili tofauti.
Nifanyeje ili mume wangu awe anaongea na mimi tena kama wakati wa uchumba na miaka ya kwanza ya ndoa yetu.
Jibu
Dada mwenye mume bubu!
Asante sana kwa swali zuri ambalo naamini si wewe tu ambaye unakutana na hali kama hiyo wapo wanawake wengi tu hawasemi au wanaume wengi tu ambao wamejikuta kila mmoja hana hamu ya kuongea na mwenzake tena, kinachoshangaza ni kwamba wameapa kwamba wataishi pamoja hadi kifo kitakapowatenganisha.
Kabla hatujaanza kujibu swali vizuri jambo la msingi unatakiwa kutambua kwamba ndoa hupitia hatua mbalimbali na kwamba unapokutana na hali kama hiyo unatakiwa kuwa makini zaidi ili kuhakikisha unairudisha kwenye mstari au badala ya kuweka maji kwenye moto wewe unaongeza petrol.
Inawezekana unapokumbuka mume wako alivyokuwa anaongea na wewe kwa simu au text messages au email au kukutana tu na kuwa na hamu na wewe kabla ya kuoana na leo hii, hisia zako zinaumia sana kwani inawezekana alikuwa anakesha na si kuongea na wewe tu bali kuhakikisha anaongea vitu ambavyo vinakufanya uwe au ujisikia happy na kwamba una mume anayejua kupenda na ni yeye tu duniani, leo umeoana mambo ni kinyume.
Wanandoa wengi hujisahau (wanaume na wanawake) kwamba wanahitaji kuendeleza romance na surprises hata baada ya kuoana.
Kama wanandoa wawili wamefika mahali hawawezi kuongea tena hii ina maana kwamba mmoja wao hajisikii kuvutiwa (hisia) kuweza kuongea na mwenzake, anajisikia unam-bore, humvutii tena.
Inaweza kuwa ni wewe mwenyewe umesababisha mume wako awe disconnected na wewe au ni yeye amepata mwingine ambaye anamvutia zaidi na kumfanya anapoongea ajisikia vizuri.
Kabla ya kuamini kwamba ni yeye labda ni vizuri kuanza kuisafisha nyumba yako moyoni mwako kwanza yawezekana ndo itakuwa dawa kamili.
Je, bado upo attractive kama ulivyo kuwa enzi zako zile za uchumba, honeymoon na miaka ya kwanza ya ndoa yenu?
Je, unamheshimu mume wako kama wakati wa uchumba au mwanzo wa ndoa yenu?
Je, unaongea tu, na kumkefyakefya (nagging) kwa kila kitu hata kitu kisicho na maana hadi yeye kujikuta hana majibu na jibu sahihi ni kujibakia kimya?
Je, umakuwa unalalamika kwa kila kitu hata yeye kutoongea na wewe?
Je, mahusiano yako kimapenzi ni mazuri na yeye (yaani kuna enjoyment ya kuridhisha linapokuja suala la sex)?
Kuna msemo kwamba “People take things for granted when married” kwa sababu wanaamini wanaishi kwenye mapenzi tayari hivyo wanakuwa jeuri kwa wapenzi wao.
Dawa ya kuweza kuongea na yeye ni wewe kuwa na bonding mpya na mume wako yaani ajisikie yupo connected na attracted na wewe na hii haiwezi kutokea overnight kuna kazi unahitaji kufanya.
Unaweza kuanza kufanya vitu vile yeye anapenda kufanya, kama vile michezo, project, business hata mambo anayopenda kuongea, hapo atajisikia vizuri kwani unagusa maeneo yake.
Wanaume hufanya bond haraka kwa kufanya activities pamoja na si kwa kukaa na kupiga soga kama wanawake, hivyo ukitaka mumeo aongee mfuate kwenye shughuliza zake binafsi anazopenda kufanya.
Kama kuna kazi amefanya au kitu amefanya jitahidi kuhakikisha unampa credit au praise, kumsifu kwa vitu anavyofanya kunampa feelings kwamba unatambua mchango wake na kwamba yupo respected na wewe pia atafahamu unatambua juhudi zake katika familia hivyo ataanza kuongea na wewe.
Pia inawezekana kutokana na yeye kushindwa kuongea na wewe umeamua kuwa rough yaani humpi respect nah ii imeathiri ego yake na anakuona hakuna lolote, hivyo geuza kibao kwa kumpa respect kwanza.
Pia unaweza kujipa kalikizo kadogo kwenda mbali kidogo ili ujenge hamu ya kukutaka au wewe kutokuwepo kuna kujisikia Fulani ambalo kwa wawili wanaoishi pamoja lazima itajenga hamu ya kukuhitaji tena.
Pia kumbuka approach ya maisha na mapenzi kwa ujumla kwa mwanamke na mwanaume ni tofauti hivyo unatakiwa kuwa makini na namna unavyoongea na mume wako kwani sasa mnaishi kwenye ndoa ni maisha halisi ni kitu halisi.
Pia inawezekana sasa hakuna fun zozote, hakuna kucheza wala kutaniana wala kufurahishana, wote mmejikita kwenye kazi na responsibilities na matokeo yake hakuna kicheko na mnakuwa disconnected, jiulize wewe na mume wako mmecheza mchezo wowote lini?
Kama unaweza basi kuanzia leo jifanye ni mchumba na act kama mchumba uone kama hataongea.
Usipende kuongeea naye eti kwa kuwa kuna issue muhimu ya kuongea, ongea naye hata wakati hakuna issue sensitive, just for fun.
Haina haja kuongea (kuchonga) ili kutaka mume wako aongee na kujibu kila swali unalomuuliza au kuzunguka kutoa maelezo mengi badala ya kuongea point ndipo wanaume wengi hujisikia wanawake hawaeleweki na too much na wakati mwingine mume amechoka wewe unataka kuongea na maswali kibao.
Uwe na hekima, wakati mwingine wanaume anahitaji kwenda pangoni.
Hata kama hatulipii kuongea haina maana tuongee ovyo na kuuliza maswali yote, ni vizuri kuwa makini na jinsi tunavyoongea na si kila wakati ni wakati wa kuongea.
Tuesday, October 27, 2009
Kutojiamini - 2
Kuwa na staha ya chini au kutojiamini ni ugonjwa ambao unawakumba wanawake siku za leo kuliko nyakati zote katika historia ya dunia.Siku za leo mwanamke ambaye anaamua kukaa nyumbani hana respect yoyote, hakuna status yoyote. Mama wa nyumbani (house wife) sasa anataniwa na kupewa jina kwamba yeye ni supermom.
Hapa hatukatai kwamba mwanamke hatakiwi kufanya kazi zingine au kusaidia kuingia kipato bali tunazungumzia mwanamke kutojiamini au kuwa na staha ya chini (low self esteem)
Ushahidi wa kisayansi unathibitisha kwamba hakuna tofauti yoyote kati ya mwanamke na mwanaume linapokuja suala la akili au intelligence, ingawa kuna maeneo ambayo kila gender huwa imara zaidi kama vile wanaume ni wazuri kwenye mahesabu (abstract reasoning) na wakawake ni wazuri kwenye Lugha (verbal skills).
Matokeo yake wanaume hujiona ni muhimu kuwa na akili au kuonekana ana akili kuliko mwonekano mzuri, hata wanawake huangalia mwanaume mwenye akili kuliko urembo wakati mwingine (yaani mwanaume hata akiwa anafanana na sokwe mtu kama ana akili na mipesa bado huwa ni sumaku ya uhakika kuvuta wanawake.
Monday, October 26, 2009
Eti Kulala Pamoja si Afya!
Tafiti za karibuni zinaonesha kwamba wanandoa kulala kitanda kimoja si afya
Kitendo cha wanandoa kulala kitanda kimoja kilianza wakati wa mapinduzi ya viwanda (industrial revolution) kitu kilichosababisha watu kuhamia katika miji na kujikuta wanakosa accommodation na kulazimika mke na mume kulala kitanda kimoja.
hali hiyo imeendelea hadi leo na kuwa kama mfumo ambao watu wakioana tu huamua kulala kitanda kimoja.
Pia bado baadhi ya jamii zinazoishi vijijini mke na mume huendelea kulala kila mmoja kitanda chake hadi leo.
Wanandoa kulala pamoja huweza kusababisha kusumbuana na hatimaye kusababisha magonjwa
Pia historia inaonesha kwamba kitandani hakukuwa mahali pa kulala wanandoa bali ilikuwa sehemu muhimu (maalumu) ya wanandoa kukutana pamoja kwa ajili ya kuwa mwili mmoja (tendo la ndoa) na si wanandoa kulala pamoja.
Daktari wa sociology kutoka chuo kikuu cha Surrrey Dr. Robert Meadows anasema kwamba watu hujisikia vizuri wakilala kitanda kimoja na wapenzi wao hata hivyo ushahidi ni kwamba kulala kitandani kimoja si afya.
Je, unaonaje suala Hili la kulala kila mwanandoa kitanda chake mwenyewe?
Saturday, October 24, 2009
Mchumba asiye mwaminifu huwa mwenye ndoa asiyemwaminifu!
Mimi ni binti mwenye umri wa miaka 29, nilikuwa na relation ya kwanza ambayo ilidumu kwa miaka mitatu lakini kikubwa kilichotufanya tusaparete ni dini yeye muislam mie mkristu.
But baada ya muda kupita nikapata mvulana mwingine kwa kweli nilifurahi toka siku ya kwanza kwa kuwa wote ni wakristu na nilimuona kwamba anampenda Mungu kwa matendo yake lakini kadri tulivyoendelea na relation nikagundua ana affair na wasichana wengine.
Maswali
Je, Ni kweli mwanaume wa hivi anarekebishika kweli?
Je, kwa nini anakuwa na wasichana tofauti tofauti?
Na nikajaribu kupeleleza kwao nikaambiwa ni mimi peke yangu nilipelekwa kutambulishwa.
Je, kweli anafaa kuwa mume?
Maana sihitaji kuwa nabadilisha wanaume kila siku nahitaji kupata ushauri wa kuwa kama anabadilishika bora nitulie nae kuliko kufuata mwingine na kila siku kuwa na wanaume tofautitofauti.
Kweli nampenda kwasababu familia yao ipo katika misingi ya dini imara.
Nimeelemewa na mawazo.
MAJIBU YA SWALI LAKO
Pole sana dada Yamenikuta!
Kama mmoja ya watu ambao hupokea maswali mengi yanayohusiana na ndoa na uchumba au mahusiano kwa ujumla, ukweli kumekuwa na mijadala mingi sana kuhusiana na suala la wanandoa kuoa wrong partner, na kinachoshangaza zaidi ni kwamba wengi wa hawa ambao wameoana na wanaume/wanawake wasiofaa wanakiri kwamba walikuwa wanajua na kufahamu fika kwamba wachumba zao walikuwa na tatizo hata kabla ya kuoana, kwa kuwa walikuwa wamependa (fall in love) au pendana kwa muda mrefu au muda wa kuoa ulikuwa umefika waliamua kwa hiari zao kuendelea na mahusiano wakitegemea kwamba siku moja watabadilika.
Je, tunaweza kujifunza kitu gani kutoka kwa hawa watu?
Hivyo basi dada Yamenikuta, ni jambo la busara na hekima kubwa kuwa makini na maamuzi unayofanya hasa baada ya kukutana na mwanaume ambaye ameshindwa kutembea katika ahadi kamili za msingi wa mahusiano yenu na kutegemea kuwa na ndoa yenye baraka.
Usikubali kuoana naye kwa sababu eti unampenda sana na umekuwa naye kwa muda mrefu katika mahusiano kabla ya kuoana.
Urefu wa mnahusiano kabla ya kuoana (uchumba) au wewe kumpenda na kujioana huwezi kuishi bila yeye hauna uhusiano wowote na afya ya ndoa yako baadae kama huyo mchumba wako ameshindwa kuwa mwaminifu kabla ya kuoana.
Tabia alizonazo kabla ya kuoana haziwezi kubadilika ghafla baada ya kuoana.
Mwanaume asiyemwaminifu kabla ya kuoana hatakuwa mwaminifu baada ya kuoana pia.
Ndoa huwa haibadilishi mtu kiburi chake, hasira zake, umalaya wake, wizi wake, tabia zake chafu sana sana ndoa hufunua hizi tabia na kuziweka mezani uzione.
Usijidanganye mwenyewe na kujipa moyo, utaangukia pua!
Kile unachoona sasa ndicho utakachopata ukioana naye.
Si kweli kwamba huyo mwanaume anampenda Mungu kwa matendo kama ulivyosema na sijajua ulitumie vigezo gani kwani kutembea na wanawake wengine ni uthibitisho kwamba dini yake ni ovyo.
Pia yeye kukupeleka kwa wazazi wake (baada ya wewe kumlazimisha kama uthibitisho kwamba anakupenda) kukutambulisha si jambo kubwa sana ambalo linaweza kumfanya mwanaume mhuni asiwe mhuni bali ni taratibu tu za kuwaambia wazazi kwamba huyu ni mtarajiwa (siyo mke) hii ina maana hata kesho anaweza kuamka na kumtambulisha mwingine.
Pia wazazi wake kuwa wanadini wazuri haina maana mtoto wao naye atakuwa na dini nzuri na kukuhakikishia maisha safi ya ndoa, hata hivyo dini nzuri kwa maana ipi ? kwenda kanisani au kuona wagonjwa au jinsi wanavyoishi?
Ni kweli kama wewe upo makini na dini yako uamuzi wa kuchangua mume ambaye dini zinafanana ni wa busara sana unaweza kusoma hapa
Sasa tuje kujibu maswali yako.
Mwanaume wa aina hiyo huwa harekebiki na Mungu anakupenda sana kwamba amekuondoa kwenye shimo ambalo ungeingia kutoka ingekuwa kazi ya ziada, hivyo furahi na amini kwamba Mungu anaweza yote na shukuru kwa kukuonesha kwamba huyo mwanaume hafai.
Ni ngumu sana kukubali kwamba mwanaume huyo hafai kwani inaonesha ulimkabithi moyo wako wote hata bila kuchunguza vizuri ni wapi moyo wako unaweka.
Suala la kwa nini anakuwa na wasichana wengi naamini yeye ndiye anajua hata hivyo inaonesha kwamba hata kama anakupenda ana tabia mbaya ya uhuni kiasi kwamba hawezi kuwa na wewe tu bila hao wanawake wengine.
Na je anafaa kuwa mume, ukweli ni kwama hafai na kimbia na mwogope (kama njaa) kwa maelezo zaidi kuhusu kujua anafaa au hafai au ni yeye au si yeye wa kuoana naye soma hapa
Usijifariji kwamba eti afadhari ubaki naye yeye ili usionekane unabadilisha wanaume, ukweli huyo hafai na pia kama wewe umezoea kuwa na mwanaume na kumpa mwili wako ni kweli hisia zako zitakuwa zimeumia zaidi, wakati mwingine ukipata mchumba hakikisha humpi mwili wako kwanza hadi ndoa.
Kwa maelezo zaidi soma hapa Soma hapa
Ladies, you don't need a man that drives an X6, M3, Land Rover, Mercedes or Hummer to feel special!!The happiest people don't necessarily have the best of everything;
They just make the best of everything they have.
Source: Mtandao
Thursday, October 22, 2009
Kujiamini!
Nini maana ya kujiamini au staha?Kujiamini au Staha (self esteem) ni jinsi unavyojiona mwenyewe, ni image yako mwenyewe, kama una staha ya juu (high self esteem) maana yake unajiona mzuri kila eneo na kama una staha ya chini maana yake unajiona mbaya katika maeneo yote ya maisha yako.
Kuwa na staha ya chini (low self esteem, low self image) ni ugonjwa unaowasumbua wanawake wengi sana katika jamii yetu ya sasa kuliko wakati wowote katika historia ya dunia.
Tunaposema mwanamke fulani ana low self esteem au low self image tuna maana gani?
Hii ina maana kwamba mwanamke anakaa mwenyewe na kuanza kujishangaa kwa nini hana marafiki wa kweli.
Anakuwa na hamu ya kuongea na mtu ana kwa ana na anajua huyo mtu hayupo.
Ni mwanamke anayejisikia kwamba wengine hawawezi kumpenda wakigundua kwamba ni yeye halisi so anajitahidi kujifanya fulani ili watu wampende.
Ni mwanamke anayeogopa kuongeea na wanawake wenzake wa rika moja kwa maana kwamba yeye hayupo smart kama wao.
Ni mwanamke anayeamini wafanyakazi wa kike wa ofisini kwa mume wake ni wazuri zaidi kuliko yeye hivyo kila siku mume akirudi anaonywa na kwamba ajihadhari na hao wanawake.
Ni mwanamke anayejisikia mjinga fulani au maskini fulani au failure fulani hasa akiwa nyumbani kwake peke yake akifikiria maisha.
Ni kujishangaa kwa nini watu wengine wana uwezo na talents nyingi kuliko yeye.
Ni mwanamke anayejisikia hapendezi na havutii tena kimapenzi (sexually unattractive).
Ni mwanamke kujisikia ameshindwa kuwa mke na mama.
Ni mwanamke ambaye hapendi kitu chochote kuhusu yeye na kutamani ingekuwa vile na vile kama wengine.
Ni mwanamke kutamani muda wote angekuwa Fulani au angekuwa mtu mwingine.
Ni mwanamke anayejisikia hapendwi na hapendi mtu na matokeo yake anafunikwa na huzuni na upweke.
Ni mwanamke anayejisikia moyoni yupo empty hasa kwa kukosa upendo wa kweli.
Ni mwanamke ambaye anahisi wanawake ambao mume wake anaongea nao ni wazuri kuliko yeye hivyo wanaweza kumchukua au kutembea naye.
Ni mwanamke anayesubiri kuwe kweusi aanze kutoa machozi mazito kwa kujihurumia kwa hali aliyonayo na amefunikwa na msongo wa mawazo.
Ni mwanamke anayejiangalia kwenye kioo na kujiona hafai na kutamani sura yake ingekuwa kama ya fulani au angekuwa kijana zaidi.
Je, low self esteem huwapata wanawake tu?
Kuwa na staha ya chini au ndogo si kwa wanawake tu bali huwapata zaidi wanawake.
Hili dubwana huweza kummeza mtu yeyote pale tu akianza kujisikia hayupo respected na mwingine.
Asilimia 90 ya wazo la low self esteem au low self image hyujengwa kwa kuwaza kuhusu wengine wanavyowaza kuhusu wewe.
Kawaida huwa inakuwa ngumu sana kujiamini mwenyewe kama the rest of the world wanaamini wewe ni dumb, ugly, mvivu, boring, uncreative, undesirable nk.
“No one can stand the awful knowledge that he/she is not needed”
Tutaendelea
Wednesday, October 21, 2009
Tuesday, October 20, 2009
Usisahau kutaja jina lake!
Tendo la ndoa ni sanaa kama sanaa zingine na hakuna mtu anaweza kukufundisha kwamba unapotaka kuwa mwili mmoja na mke wako au mume wako kitu cha kufanya ni hivi na hivi kwani kila mwanamke ni tofauti na hata huyo mwanamke mmoja anatofautiana kwa siku kadhaa katika mwezi mmoja kutokana na mzunguko wake.Kwanza kabla ya mambo yote ni jambo la msingi sana wewe mwanaume kuwa clean na umeoga vizuri na unanukia version nzuri inayovutia, hii inatasaidia yeye kuwa na focus zaidi kwa sex kuliko harufu ya ajabu ambayo inatoka kwako, hapa haijalishi una sexual skills au sexual techniques za juu kiasi gani kwani kuwa mchafu na harufu chafu ya mwili ni total turn off.
jambo lingine muhimu ambalo kila mmoja hufahamu na kulipenda ingawa wakati wa foreplay au sexual act husahauliwa ni kukumbuka kumnong’oneza jina lake ukirudiarudia ikiendana sambamba na unavyopumua na huku ukimbusu shingo yake na sehemu zingine ambazozinamsisimua.
Onyo:
Mwisho haijalishi anafurahia kiasi gani utaalamu wako na ufundi wako jambo lingine muhimu ni kuhakikisha kunakuwa hakuna routine na inabidi ubadilishe mambo mara kwa mara, chumba kilekile, kitanda kilekile, mwelekeo uleule, saa ile ile, mwanga au giza lilelile, muziki uleule, mlalo uleule huwa inasumbua baada ya muda na inaweza kuzima kabisa moto wako kitandani.
Sunday, October 18, 2009
Mwanaume anahitaji zaidi!
Je, wanaume wanawahitaji wanawake zaidi kuliko wanawake wanavyowahitaji wanaume?Hili ni swali ambalo si gumu wala si rahisi ila inatokana na mtazamo wa jinsi kila mmoja anavyozifahamu hizi gender mbili.
Wanawake mara nyingi huonekana wanawategemea sana wanaume kuliko wanaume wanavyowategemea sana wanawake.
Na pia mwanamke huonesha kwa uwazi zaidi kwamba anamilikiwa na mwanaume kuliko mwanaume kuonesha mwanamke ndiye anayemmiliki.
Wanawake hupanda kuelekea mafanikio hasa kutokana na kusifiwa (praise) na kutiwa moyo wanakopewa na wale wanaowazunguka.
Wanawake huwa na interest na watu na hupenda kutegemea watu (mwanaume) wakati wanaume huwa na interest na vitu na pia hupenda kujitegemea au kutegemewa.
Mke mara nyingi huhitaji approval kutoka kwa mume, upendo kutoka kwa mume, kutiwa moyo kutoka kwa mume na kupewa attention kutoka kwa mume wakati mwanaume hupenda competition na kwamba kufanikiwa katika kazi au business ndicho kitu kinachompa approval na kujisikia kweli naye ni mwanaume wa uhakika.
Kwa haraka haraka unaweza kufikia conclusion kwamba ni kweli mwanamke anamuhitaji mwanaume zaidi kuliko mwanaume anavyomuhitaji mwanamke?
Je, mwanaume ambaye yupo umri ambao alitakiwa kuwa na mke na familia na anaishi mwenyewe anafaa (fit) katika jamii kuliko mwanamke ambaye alitakiwa kuwa na mume au familia na ainaishi mwenyewe?
Mwanaume na mwanamke waliumbwa kila mmoja kumuhitaji mwenzake na kwamba kila mmoja akiwa mwenyewe hujisikia hajakamilika.
Hata hivyo wanawake hufanya vizuri zaidi bila kuwa na mume kuliko mwanaume kuwa mwenyewe bila mke.
Ingawa hii huonekana ni kinyume kidogo na mtazamo wa jamii nyingi kwani mtazamo wa wengi ni kwamba mwanamke ambaye hajaolewa au anayeishi mwenyewe (single) huonekana ni mtu miserable katika jamii na hafai kitu ambacho si kweli kwani mwanamke single ana mambo mazuri mengi ukilinganisha na mwanaume single.
Ni mara nyingi sana kukuta mwanaume ambaye yupo mwenyewe bila mke wala familia anakuwa mlevi wa kupindukia, anaweza kutumia drugs, anaweza kujihusisha na uhalifu, hata Landlord’s wengi huwa hawapendi kupangisha nyumba kwa mwanaume asiye na mke, hata baadhi ya insurance hugoma.
Wanaume wasio na mke wala familia wengi huendesha magari kwa speed au fujo, wana hasira, pia wanakuwa na risk kubwa ya antisocial behavior na wakati mwingine kipato chao huwa kidogo kwa sababu wanajiona hawana responsibilities na wanaweza kuruka kutoka kazi moja hadi nyingine, who cares? hahahaha!
Pia mwanamke asiye na mume huwa tofauti kutokana na nguvu ya uzazi aliyonayo (uwezo wa kuumba mtoto ambao wanao ndani yao) huwawezesha kuwa tofauti na wanaume linapokuja suala la watoto bila kujali awe mtoto wake wa kuzaa au hapana na hii huwapa uwezo wa kuwa mtu tofauti katika jamii tofauti na mwanaume ambaye anachojua sana ni kusubiri siku bunduki yake itoe askari wake a marine na mtoto azaliwe.
Mwanamke akiolewa na mwanaume kile anafanya ni kuitumia nguvu ya mwanaume (sexual energy) ambayo alikuwa nayo na anaitumia kuunda kupata mtoto na mwanaume hujikuta anakuwa na responsibilities na pia anawajibika katika kulinda na kuipa familia kila inachohitaji na mabadiliko ya aina hii ni muhimu sana kwa jamii na tamaduni zozote ambazo kuna mwanaume na mwanamke.
Ni kweli wanawake wanawahitaji wanaume lakini si kama wanaume wanavyowahitaji wanawake ili dunia iwe mahali bora kuishi.
“One of the saddest creatures on earth is a man without a woman”
Wewe unasemaje?
Saturday, October 17, 2009
Upendeleo kwa mtoto mmoja
Swali:Nataka kujua zaidi katika malezi ya watoto kuna kitu inaitwa parental favouratism.
Iwapo mtoto mmoja anajisikia kutopendwa sana kama mwenzake au wenzake na wazazi ,inaweza ikamletea athari gani baadae?
Na kwanini wazazi wengine wanakuwa na upendo zaidi kwa mtoto fulani.
Utakuta mwingine mtoto wa baba, mwingine yupo tu.
Jibu
Mzazi mwenzangu asante sana kwa swali zuri.
Ni kweli tabia ya kumpendelea mtoto mmoja au kila mzazi kuwa na mtoto wake ambaye anagusa zaidi moyo wake ipo sana katika familia zetu.
Kuna msemo wa waingereza unaosema “The elephant is in the living room” kwa maana kwamba wengi huwa kulitaja au kuliongelea kwa undani ingawa ni kweli familia nyingi zitakiri kwamba hili ni tatizo sugu na pia inawezekana wewe ni mmoja ya watoto waliopendwa au ambao hawakupendwa na moja ya wazazi wenu.
Kwa nini upendeleo hutokea kwa mtoto mmoja?
Inawezekana tabia ya huyo mtoto ni njema zaidi kuliko wengine, wakipewa kazi mmoja anafanya na mwingine hafanyi mara zote, anayetii hujikuta anapendwa zaidi.
Inawezekana tabia ya huyo mtoto ni rahisi na mwenzake au wenzake ni ngumu.
Inawezekana mtoto anafanana na mzazi zaidi kuliko wengine (tabia na mwonekano).
Inawezekana huyo mtoto anafanikisha matarajio ya wazazi wake au mzazi mmoja.
Inawezekana kwa sababu ni mvulana peke yake au msichana peke yake mzazi hujikuta anampenda zaidi.
Pia inawezekana talents zake au vipaji vyake vinafanana na vile mzazi anataka mtoto awe au inawezekana ndiyo values za familia.
Pia inawezekana mtoto asiyependwa ni mtoto ambaye ni mbishi au ni mtoa hamasa (challenge authority) kuliko mwenzake au wenzake. Mtoto ana njia zake au mitazamo yake kuhusu maisha na vitu hivyo wazazi au mzazi hujikutana wanabishana kila kitu.
Pia kuna mazingira ya kuzaliwa ambayo hufanya mtoto kupendelewa zaidi ya wenzake kama vile mtoto kuzaliwa siku au wakati (huohuo) ambao mzazi wa baba au mama (babu au bibi) yake anafariki, ingawa haina ushahidi wa kisayansi ila matukio mengi huonesha kwamba mtoto wa aina hii huonekana wa thamani kuliko wengine na ni kama vile roho ya babu au bibi huenda kwa mtoto anayezaliwa na wazazi kujikuta wanampenda kuliko kawaida.
Au inaweza kuwa ngumu sana mzazi kuweka bond na huyo mtoto kutokana na huzuni, stress na depression mzazi alipata wakati anazaa na wakati huohuo mzazi wake mwenyewe (baba au mama) naye anafariki.
Mtoto kuzaliwa bila kutegemea hasa baada ya wazazi kudhani wamemaliza kuzaa.
Mtoto kuwa na matatizo ya afya hivyo wazazi kutumia muda mwingi kwake na wengine kujiona mwenzao anapendelewa.
Wakati mwingine inatokea tu mzazi hujikuta anampenda mtoto fulani katika familia kuliko wengine.
Nini mojawapo ya Dalili za mtoto kupendelewa?
Kununuliwa zawadi zaidi ya wenzake.
Kutoa adhabu rahisi kuliko wenzake kwa kosa moja, wenzake wanakula fimbo yeye anaonywa tu.
Sherehe au sikukuu zake kuwa tofauti na wenzake kwa jinsi zinavyoandaliwa nk.
Wenzake wakiomba kitu hichohicho wanakataliwa lakini yeye anapewa au kuruhusiwa.
Mzazi kutumia jina lake kumaanisha watoto wake wote kama vile baba anarudi kazini na watoto hawapo na mtoto anayempenda anaitwa James na badala ya kuuliza watoto wapo wapi yeye anauliza “akina James wako wapi?”
Tumia muda mwingi na mtoto mmoja.
Kuonesha upendo wa dhahiri kwa mtoto mmoja nk nk nk.
Mtoto anakuwa na wakati mgumu sana kujikubali na kujipenda mwenyewe kwa kuwa anaamini mzazi/wazazi hawampendi na anaweza kuwa na tatizo sugu la kutojiamini (chronic low self-esteem)
Mtoto hujiona duniani hakuna haki na kwa kuwa hatendewi haki nay eye anaweza kuanza kutowatendea haki wengine kwani “unfairness begets unfairness”
Je, mtoto anayependwa anaweza kupata madhara yoyote?
Kwa kuwa anapendwa basi atajitahidi kufanya zaidi kwani anaamini asipofanya kila kitu juu anaweza kupoteza kuendelea kupata upendeleo hivyo kama ni shule atajitahidi kupata grades za juu, kama ni tabia atajitahidi asikasirike nk na matokeo yake atakuwa hajiamini na anaweza kupota msongo mawazo.
Mtoto anayependelewa anaweza kuwa si mzuri sana linapokuja suala la wenzake wa rika moja au walimu au watu wengine kwenye maisha kwani kile kitendo cha kujiona anapendelewa na wazazi au mzazi humpa kakiburi Fulani.
Mtoto anayependwa hujiona yeye ndo mzuri na huwa hakosei hata hivyo maisha hayako hivyo na matokeo yake atakuwa na wakati mgumu mbele ya maisha hasa llikija suala la kupambana na matatizo.
Hasara ya kumpendelea mtoto mmoja huendelea hadi kwa wajukuu na inaweza kuleta matatizo na migogoro kwa kuwa wajukuu wa watoto wote huanza kuzozana kwa kuwa mmoja wa wazazi wao alikuwa anapendwa zaidi na babu au bibi.
Je, kwa mume na mke ni tatizo?
Ndiyo kunaweza kutokea mgogoro kati ya mke na mume hasa kwa mtoto mmoja kupendelewa na mzazi mmoja, kwa mfano baba anampa fedha nyingi zaidi mtoto mmoja anayempenda bila kujali ni mdogo kuliko wenzake, mama akiona au kusikia naye huja juuu kitendo ambacho kitafanya ndoa iwe katika mzozo.
Je, unaweza kuepuka vipi kumpendelea mtoto mmoja?
Kwanza wewe mzazi jikubali kwamba wewe ni binadamu na kwamba katika watoto wako mmoja anakubalika kwako zaidi kuliko wengine.
Wasikilize watoto wengine ambao wanakwambia unampendelea mwenzao na usijilinde, wasikilize na anza kufanyia kazi yale wanasema (kuacha kumpendelea mmoja)
Gundua utofauti wa kila mtoto na kile anapenda kufanya (characteristics, skills, interest) na mhudumie kutokana na vile anavipenda.
Usiwalinganishe au kumsema mmoja kwa sababu ya mwingine kwani kila mtoto yupo tofauti, sentensi kama “mwenzako James akirudi shule anafanya homework yake vizuri na animalize wewe hadi ulazimishwe!”
Kama unanunua zawadi ni vizuri kununua zawadi zinazolingana siyo mmoja unanunua zawadi ya Tsh. 100,000 na mwingine Tsh. 20,000
Tumia muda vizuri na sawa kwa watoto wote.
Kumbuka jinsi unavyozidi kuwa na watoto wengi ndivyo utakuwa na kibarua kigumu zaidi, kwani unahitaji kutafuta muda maalumu kwa kila mtoto na kugundua kipaji chake na kuhakikisha unakiendeleza sawa na watoto wengine.
Jambo la msingi ni kila mzazi kumpa (treat) kila mtoto sawa katika hali zote na juhudi za ziada zinahitaji katika mazingira ya nyumbani kuhakikisha watoto wote wanalelewa sawa na kila mmoja kujiona ana thamani sawa kwa wazazi mmoja mmoja na kwa pamoja.
Thursday, October 15, 2009
Tunatofautiana muda!
Kama tulivyoangalia huko nyuma, mwanamke na mwanaume wana system tofauti linapokuja suala la sex na mapenzi kwa ujumla.
Haina maana kwamba mwanaume akiwa tayari maana yake mwanamke naye yupo tayari na hili ni tatizo moja kubwa sana ambalo wanaume wengi huwa hawalioni.
Hata kama kuna direct route ambayo mwanamke akiandaliwa vizuri anaweza kuwa tayari hadi kufika kileleni bado anahitaji dakika 20 wakati mwanaume huhitaji dakika 2 tu.
Maandalizi kwa ajili ya tendo la ndoa kwa mwanamke si luxury bali ni hitaji muhimu (need/necessity)













