"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, March 31, 2008

Uchumba 3


Kabla ya Kuvishana Hako Kapete Kazuri

Hakikisha Umejiuliza Maswali ya Msingi Kwanza
3. JE, KUPENDA KWAKE KUPOJE?
Binadamu wote tumezaliwa tunahitaji kupendwa uwe mtoto, kijana au mzee wote tunahitaji kupendwa uwe tajiri au maskini wote tunahitaji upendo.

Wote tuna asili ya kupendwa na kupendwa ni kutamu, hasa unapoanza kupendwa na mtu ambaye unataka awe na wewe maisha yako yote.

Katika kutafuta mtu wa kuishi na wewe hadi kifo kitakapowatenganisha ni muhimu sana kujiuliza;

Jiulize, Je ni mtu wa kutaka kupendwa tuuu?

Je analalamika sana kwamba hujampigia simu, wakati na yeye ana simu na hakukupigia? Je analalamika sana kwamba wewe hujamtumia email

wakati na yeye email anayo ila hajakutumia?

Je analalamika sana kwamba Mbona hujampelekea zawadi

wakati na yeye hajakuletea zawadi?

Je analalamika kwamba hukumtafuta wakati na yeye mwenyewe wala hakukutafuta,

kujua nini kimetokea kwako?

Je ni mtu wa ku-criticise kila kitu, kulalamika, Kunung’unika?

Ndoa hujengwa kwa kila mmoja kutoa upendo zaidi kuliko kupokea, candidate mzuri wa ndoa ni yule ambaye yeye anakuwa amejiajiri kukupenda tu yaani kutoa upendo kwako bila kujali umefanya nini, anajua wajibu wake ni kutoa upendo kwako siku zote.


Na wote mkiwa hivyo Mbona mambo yanakuwa safi sana!

Ndoa si 50/50 yaani wewe ukinipigia simu basi lazima na wewe unipigie, mimi nikikupa zawadi lazima na wewe unipe zawadi, mimi nikifanya hiki na wewe lazima ufanye kile, siyo hivyo.


Ndoa ni 100/100 yaani unafanya tu bila kutegemea upande mwingine utafanya nini, na ikiwa hivyo automatically na upande mwingine nao utaanza kufanya kwani ni tabia ya upendo kwamba huwezesha kubadilisha hali.

4. JE, UMEKUBALI?
Katika process nzima ya kutafuta mchumba, kuna umuhimu kufahamu kwamba hakuna aliye mkamilifu yaani ukapata kijana wa kiume au wa kike aliye mia kwa mia sawa au sahihi kila kitu unachotaka, huyo atakuwa malaika na utakuwa umepata neema ya ajabu.

Kabla ya Final Decision lazima ujue mambo mazuri na mabaya kuhusu yeye, tabia nzuri na tabia mbaya kuhusu yeye, positive and negative sides kuhusu yeye.

Jiulize je, unaweza kuishi kwa kuvumilia udhaifu wake, mabaya yake unayoyaona au negative sides alizonazo? Je ni wewe tu unayejihisi ndo utaweza kumchukulia udhaifu wake wote.

Je umeridhika na tabia yake ya ubahiri?

Ukali, Kuongea sana kama radio za FM,

Uvivu, Hasira, Ubabe, Ukimya, Kupenda kuongea na watu hata wasiomhusu,

Dharau, Wivu, Kujisikia, kujiona,

Kutokujipenda, Kutojali muda, Uzembe nk
Je umeridhika na kiwango chake cha elimu, kiwango chake cha kiroho, kiwango chake cha ufahamu wa mambo ya uchumi, jamii, dini siasa nk.


Usiseme nitambadilisha baada ya kumuoa, kwa Taarifa yako wewe ndo utabadilika.

5. JE, UMEMUOMBA MUNGU?
Tuna muhitaji Mungu ktk kutoa maamuzi muhimu ktk maisha yetu (important decisions in life) kama kuoa.

Jiulize kama umemuomba Mungu na kuthibitisha kwamba:-


Huu ni wakati wake au wakati sahihi,

Ni mtu sahihi,

Na ni mapenzi ya Mungu.

Mungu anatupenda sana na ana mpango na maisha yetu wakati mwingine tumejichukulia maamuzi bila kumshirikisha Mungu,


Pia Mungu wakati mwingine hutumia watu, Neno lake, mahubiri, radio, TV au watumishi wa Mungu, rafiki zetu, wazazi au mtu yeyote kutuonya hasa kama mtu unayetaka kuoana naye kwako hafai.


Tumeona pia vijana wengi ambao wameweka shingo ngumu na kuendelea na process hadi wakaoana na matokeo yake ndoa zimekuwa mzigo mzito badala ya raha na faraja.Hivyo najua Unamuomba Mungu sana kwa ajili ya hili pia omba Mungu akupe uhakika kwani Mungu akiunganisha hakuna binadamu anayeweza kutenganisha.


Kama una swali unaweza kuuliza au unataka kuchangia unaweza kutuma maoni yako.


Unakaribishwa! ...................................................Uchumba 2

Ms. Sonia (Booked) Haijalishi mtu unayetaka kuoana mmekutana wapi;
hata kama ni kanisani, shuleni, kwenye mkesha wa maombi, kijijini, mjini, hotelini, sokoni, kwenye daladala, barabarani, ofisini, kazini, safarini, kwenye semina au hata kama ni kwenye internet au njia yoyote ile ambayo Mungu anaweza kuitumia maana Mungu hafungwi na njia za kukutanisha watu.
Au Haijalishi ni mzungu, mwarabu, mchina, mwafrika, au awe mnene, mwembamba, mrefu kama Ngongoti, mfupi kama Zakayo,
Awe amesoma au hajasoma, awe mbena au mchaga au mhaya au mgogo au mzigua, au awe anatoka Canada, Kenya, Uganda, Nigeria au Tanzania. Pia haijalisha ktk kukutana naye umeunganishiwa na rafiki yako, au mchungaji wako, au wazazi wako au mtu wako wa karibu.
Kitu cha msingi ni wewe kuwa makini kujiuliza haya maswali matano muhimu.


1. JE, TUNAFANANA? (Compatible)
Ndoa ni kama jengo la nyumba na nyumba ni sharti iwe na msingi (foundation). Msingi imara huwezesha nyumba kuhimili kila aina ya janga linalotokea kama vile mvua, upepo, mafuriko, dhoruba, tetemeko la ardhi nk. Na kuna aina ya material zinazotumika kujengea msingi na hizi aina za material ndizo huelezea aina ya msingi na uimara wake.

Unaweza kujenga ndoa kwa kuvutiwa na umbo la mtu (mvuto wa nje) au urembo tu. Pia sasa hivi kuna uzuri mwingi tu na unauzwa dukani (body shops)
Unavutiwa na kipande kimoja tu cha mwili wake kama vile shingo, matiti, matako, unene, au wembamba, nywele, smile, anavyotembea, miguu, au kifua nk.
this is just physical attraction kuna siku anaweza kubadilika kuna kuugua, kuna ajali, kuna kubadilika mwili nk kwa hiyo ku-base kwenye mwonekano wa nje peke yake lisiwe jibu kwako kuona huyu mtu ananifaa.
Hapo utakuwa umejenga msingi wa nyumba kwa kutumia mabua (straw) au miti hakika nyumba ikishika moto hata majivu tunaweza tusipate.

Ndoa hujengwa ktk misingi 3 muhimu ambayo lazima mfanane au kuwa kitu kimoja. Ni muhimu kusiwe na gap kubwa sana katika mambo haya matatu,
Nayo ni Kimwili,
Kiakili na
Kiroho
(Mind, Body and Soul).
Mara ya kwanza mnapokutana wote (first impression) mmoja anapata kuvutwa na mwingine kwa njia ya tofauti (excitement & attraction) na huko kuvutwa kuna base kwenye mwonekano wa tabia kama vile anavyoongea, anavyotabasamu, anavyopenda na kwa hayo tu huwezi kusema biashara imeisha ananipenda au nimempenda na kukubaliana kuoana.

Unapotumia muda zaidi kuwa naye na kumjua zaidi, uhusiano unakua na unamfahamu zaidi ya ile physical attraction ambayo uliipata kwa mara ya kwanza sasa unaweza kutambua mambo anayopenda,
mawazo yake katika mambo mbalimbali ya kiroho,
kimwili na kiakili,
unaweza kujua talents zake na hobbies zake
hapa ndo inabidi uwe makini kufanya assessment kwani hapo ndo biashara yenyewe kwani ukimpenda na ku fall in love unakuwa blind halafu utaona kila kitu shwari hata watu wakikwambia kuna tatizo utakataa na kuwambia yupo sawa kabisa na bila yeye wewe maisha hayana maana, kumbuka huyo ni mchumba si mke/mume.
Unahitaji kuwa mchunguzi zaidi kuliko kupendwa. Kumbuka hapa unatafuta mchumba hajawa mke so ukiona kuna dalili au tabia ambayo ni hatari inabidi uwe makini.

Upendo wa kweli hauwezi kuwepo bila bonding ya kiroho.
Kutofautiana kiroho na kiimani ni moja ya sababu ya ndoa kuvurugika na hatimaye kuvunjika. Hivyo ni vizuri kupata data kamili kwa kuthibitisha imani yako na yake.

2. JE, UNAKUBALIANA NAYE KTK MAMBO YAKE?
Mtu ambaye kwake pesa na kazi ni namba moja yaani ni kitu cha kwanza, kwake bila hivyo hakuna maisha, yaani muda wake na akili yake ni pesa na kazi kwanza,
Then mambo ya michezo kama soka, au kushabikia tu michezo ni kitu cha pili, familia (mke au mume na watoto) ni kitu cha tatu kwake,
Na mwisho Mungu, yaani Mungu ni kitu cha ziada kwake, akiwa hana cha kufanya ndo anakumbuka mambo ya Mungu, Kama wewe ni dada ukapata kijana wa kiume wa aina hii kuendelea naye fikiria mara mbili.

Au mwanamke ambaye kwake kujiremba, kujisifia au kusifiwa na kuhudhuria sherehe (mama wa shughuli) kwake namba moja, then familia na Mungu baadae.
Kama ni kijana wa kiume binti wa aina hii fikiria mara mbili kabla hujaamua.

Kama ninyi ni Christians kitu cha kwanza ni kila mmoja kuwa na uhusiano na Mungu wake kwanza then familia yaani mke/mume na mtoto then kazi hii ni pamoja na kazi ya Mungu.
Hivi unaweza kwenda kuimba kwaya wakati mke au mume yupo kitandani anaumwa na hakuna mtu mwingine? Mlio kwenye ndoa tusaidie hapo!
Tutaendelea na somo ...............................................

Saturday, March 29, 2008

Mke mwema

Nawatakia weekend njema kwa wimbo kutoka Vijana Kigoma

Thursday, March 27, 2008

Uchumba

Wachumba wakitangazwa na mchungaji mbele ya kanisa
hii ni moja ya safari kuelekea kwenye ndoa katika tamaduni za Kikristo Tanzania
"Apataye Mke Apata Kitu Chema; Naye Ajipatia Kibali Kwa Bwana"
(Mithali 18:22)


Kutokana utafiti ambao umefanywa unaonesha kwamba moja ya mambo ya msingi ambayo kila kijana anahitaji ni Ndoa ya Kudumu ukiacha ongezeko la kufeli kwa ndoa nyingi.

Wakati huohuo moja ya uamuzi (decision) wa maana sana katika maisha ya binadamu ni kuamua nani atakuwa mume wako au mke wako na huu uamuzi ndiyo utakufanya uweze kuishi maisha ya namna gani katika ndoa yako na pia kuathiri kabisa mfumo wa maisha yako kuwa raha au kuwa karaha

Watu wengi katika maisha wamekuwa wakilaumu upande mwingine iwe mke wake au mume wake kwamba ndiye sababu ya kuvunjika kwa uhusiano au ndoa yao.
This is none sense! muhusika mara nyingi ni wewe kwani asilimia 99 ni jinsi ulivyompata huyo mtu ambaye amesababisha ndoa yako au uhusiano kuvunjika.

Mtu anayestahili kupewa lawama zote ni wewe.

Kama hujaolewa au ndio upo kwenye process za kuolewa au kuoa,Fahamu kwamba hakuna jambo muhimu maishani mwako kama huo uamuzi unaotaka kufanya, unaweza kukupa furaha ya maisha au uchungu wa maisha hapa duniani.

Unahitaji kutumia
akili zako zote,
maombi yako yote,
uwezo wako wote na
kila resource ulizonazo
kwani hapa makosa hayana nafasi kabisa

Wala usikubali kumuoa huyo binti au kuolewa na huyo kaka eti kwa sababu:

Watu wanasema Mbona hujaolewa au kuoa!
Au ndugu zako, au mchungaji, au wazazi wako au rafiki zako wamekwambia!
Au kwa sababu umeona muda unakwenda!

Amua mwenyewe na jichunguze kama upo tayari na kama mtu unayetaka kuwa naye anakupa uhakika unaoridhika nao wewe mwenyewe.

Kumbuka it is easy to reshape the mountain siyo mtu, kwa hiyo kama kuna tabia fulani ambayo unaiona kwa mtu unayetaka kuoana naye na hujaridhika nayo Please fikiri zaidi ya mara mbili.
Na kama unaweza give time au fikiri mara nyingi zaidi.

Mara nyingi wanaosema watawabadilisha matokeo yake wao ndo wamebadishwa

Hapa huhitaji kuwa blind kwa sababu ya fall in loves, bado unahitaji kuwa na akili timamu kumfahamu zaidi huyo unataka kuoana naye kabla love haijawafanya kuwa blind au otherwise muwe blind maisha yenu yote.

"Remember any fool can fall in love,
but it takes character for a fool to remain in love"


Kuna maswali matano (5) ya msingi sana kujiuliza kabla hujajikamatisha vizuri kwenye hii kamba ya ndoa

Tutaendelea ………..

Pembe za Ndoa

Asante sana Dada Hellen kwa mchango wako ufuatao:
Kwenye maisha ya ndoa ni pembe tatu. Kuna NDOA, FAMILIA na MSALABA. Na hakuna ndoa bila msalaba wala hakuna familia bila msalaba. Kama tujuavyo ndoa ni agano na kiungo kikubwa kwa ndoa ni uaminifu. Hosea: 1,2. Na kwa kuwa mwenzi ni mshirika wa mambo yote ni kinyume kama humshirikishi mwenzako wa ndoa mipango uliyonayo, matatizo uliyonayo na furaha ulizonazo.
Tusisahau kuwa muwezeshaji wa yote hayo ni KRISTU maana kwake yeye tunapata NGUVU, NEEMA na BARAKA.Ndoa ni sadaka, na sadaka ni kujitoa kwa ajili ya wengine.
Na mafanikio ya ndoa ni Kristu, tusipomuangalia Kristu na kumtegemea yeye basi ndoa zitatushinda.
Familia ni muungano wa mwanaume na mwanamke kwa kuungana kwao wanaweza kupata watoto au wasipate ni mapenzi ya Mungu.
Kwa hiyo twajua kuwa familia ni kanisa dogo la nyumbani, familia ni shule ya imani katika matendo.Watu wa ndoa wanaitwa (maana huo ni wito) si kila mwanamke au mwanaume ni lazima awe kwenye ndoa. Hivyo wanandoa wanaitwa kusihi usafi wa moyo wa ndoa ambao ni uaminifu na kujithamini.
Na tunajua kuwa wito wowote unadai matayarisho ya kipekee na matayarisho kwetu wanandoa ni sala na sadaka.
Kwa nini ndoa ni msalaba?Ndoa inakuwa msalaba pale mmoja asipotimia wajibu wake kwa mwenzake na asipomfanya mwenzake sehemu ya maisha yake. Kuna misalaba ya ndani ya ndoa na ya nje ya ndoa.
Misalaba ya ndani ni:-Kama mwanandoa hatimizi wajibu wake, akiw amvivu, mbinafsi, ana upendeleo, na hata simu za mikononi ni misalaba kama haitumiki vizuri na hasira pia ni msalaba ndani ya ndoa.
Misalaba ya nje ya ndoa ni:Wazazi/walezi, ndugu, marafiki, na shughuli azifanyazo mwanandoa maana mwingine anakuwa yuko busy hata hampi mwenzake nafasi.
Na ndoa za kikristu zinaonekana msalaba kwa kuwa hakuna talaka kuna mlango mmoja tu wa kuingia na hakuna mlango wa kutoka.
Ila kwangu mimi naona ni msalaba mzuri maana tukiubeba vizuri tunavyopaswa basi tutaufikia ufalme wa Mbinguni.

Mafundisho kabla ya ndoa ni Muhimu

Nimepata mchango wa maswali na maelezo kwa email kutoka kwa dada Loveness (Chuo Kikuu cha Tumaini) ambaye naamini si muda mrefu na yeye ataingia kwenye ndoa. Naamini pia kila mmoja wetu anaweza kuwa na mchango wake kuchangia jibu la maswali ktk maoni yake.

Dada Loveness anasema:

"Sijui kama nitakuwa napatia au la. Umesema kuwa swala la kujamiiana(sex) mume na mke ni jambo ambalo vijana au wanandoa wengi ambao wapokanisani au walikulia kanisani wanaona kuwa ni kibaya hasa kutokana na ukweli kwamba sex kbal ya ndoa ni kitu kibaya na hujikuta hawana uzoefu wa mafundisho yanayowawezesha kuwa wana ndoa wazuri kwenye suala zima la mapenzi.Mimi nafikiri pia sio tu kwamba hilo limechangia pia hata jinsi ya kuanza tendo hilo,yaani siku ya kwanza mtu anapoanza kushirikitendo hilo anakutana na nini! hasa hapa nazungumzia binti, kwa sababu unakuta kijana hajapata mafundisho ya
kutosha kuhusu jambo hilo,na unakuta kwa sababu anakuwa na shauku na mwenzake anaweza akasababisha matatizo kwa yule binti kama maumivu n.k.
Sasa huoni kwamaba inakuwa ni sababu ya huyo binti kuona tendohilo kuwa ni baya?Na mara nyingi nakumbuka wale dada zetu walio kwenye ndoa na waliopitia haneymoon huwa wanatuambiaga kuwa nyie msifurahie kwenda honey moon huko kuna kuumwa(yaani maumivu).
Mimi binafsi imekuwa ikinisumbua pia kila nikifikiria juu ya hilo kama kweli ndo hali ni hiyo basi napata mawazo kwamba huko haneymoon nitaumizwa na matokeo yake nakuwa.
So huoni kuwa kweli vijana wa kiume wanaokwenda kufunga ndoa wanahitajimafundisha ya hali ya juu?"
Swali je tuwasaidie vipi vijana wetu ambao hawapati mafundisho mengi juu ya ndoa na pia suala zima la tendo la ndoa?

Enhancing Relationship

Kama watoto wadogo.......


TRUST
Trust is very important factor for all relationships.

When trust is broken, it is the end of the relationship. Lack of trust leads to suspicion, suspicion generates anger, anger causes enmity and enmity may result in separation.

A telephone operator told me that one day she received a phone call. She answered “Public utilities board” there was silence. She repeated “PUB” There was still no answer. When she was going to cut of the line, she heard a lady’s voice, “Oh, so this is PUB. Sorry, I got the number from my husband’s pocket but I do not know whose number it is
Without mutual trust, just imagine what will happen to the couple if the telephone operator answered with just “hello” instead of “PUB”

RIGHT SPEECH
There is a Chinese saying which carries the meaning that “ A speech either prosper or ruin a nation” many relationships break off because of wrong speech. When a couple is too close with each other we always forget mutual respect and courtesy. We may say anything without considering if it would hurt the other party.

A friend and her millionaire husband visited the construction site. A worker who wore a helmet saw her and shouted, “Hi Emily Remember me? We used to date in the secondary school.” On the way home, her millionaire husband teased her, “luckily you married me. Otherwise you will be the wife of a construction worker.” She answered, “You should appreciate that you married me. Otherwise, he will be the millionaire and not you.”

Frequently exchanging these remarks plants the seed for a bad relationship.

It’s like a broken egg – cannot be reversed.

NO OVERPOWERING
Many relationship fail because one party tries to overpower another or demand too much. People in love tend to think that love will conquer all and their spouses will change the bad habits after marriage. Actually this is not the case. There is a Chinese saying which carries the meaning that “It is easier to reshape a mountain or a river than a person’s character.”
It is not easy to change.


Thus, having high expectation on changing the spouse character will cause disappointment and unpleasantness. It would be less painful to change ourselves and lower our expectations

CREATING PERFECT RELATIONSHIP
A person visited the government matchmaker for marriage SDU, and requested, “ I am looking for a spouse. Please help me to find a suitable one. “The SDU officer said, “Your requirement please.”
Oh, good looking, polite, humorous, sporty, knowledgeable, good in singing and dancing. Willing to accompany me the whole day at home during my leisure hour, if don’t go out. Telling me interesting stories when I need companion for conversation and be silent when I want to rest.
The officer listened carefully and replied, I understand you need TELEVISION.”
There is a saying that a perfect match can only be found between a blind wife and a deaf husband because the blind wife cannot see the faults of the husband and the deaf husband cannot hear the nagging of the wife.


Many couples are blind and deaf at the courting stage and dream of perpetual perfect relationship. Unfortunately, when the excitement of love wears off, they make up and discover that marriage is not a bed of roses. The nightmare begins.

NO POINTING FINGERS
A man asked his father in law, “many people praised you for a successful marriage. Could you please share with me your secret?”
The father in law answered is a smile,
“Never criticize your wife for her shortcomings or when she does something wrong.
Always bare in mind that because of her shortcomings and weaknesses,
she could not find a better husband than you.”
We all look forward to be loved and respected. Many people are afraid of losing face. Generally, when a person makes a mistake, he would look around to find a scapegoat to point the finger at, this is the start of war.
We should always remember that when we point one finger at a person the other four fingers are pointing at ourselves.
If we forgive the others, others will ignore our mistakes.

PERSONAL PERCEPTION
Different people have different perception. One man’s meat could be another man’s poison.
A couple bought a donkey from the market. On the way home, a boy commented, “very stupid. Why neither of them rides on the donkey?” Upon hearing that, the husband let the wife ride on the donkey.
He walked besides them. Later, an old man saw it and commented, “The husband is the head of the family. How can the wife ride on the donkey while the husband is on foot?” Hearing this, the wife quickly got down and let the husband ride on the donkey.
Further on the way home, they met an old lady. She commented, “ how can the man ride the donkey but let the wife walk, he is no gentleman.”
The husband thus quickly asked the wife to join him on the donkey. Then, met a young man. He commented, “poor donkey, how can you hold up the weight of two persons, they are cruel to you.” Hearing that, the husband and wife immediately climbed down from the donkey and carried it on the shoulders.
It seems to be the only choice left. Later, on a narrow bridge, the donkey was frightened and struggled. They lost their balance and fell into the river.

You can never everyone praise you, nor will everyone condemn you. Never in the past, not at present, and never will be in the future, thus do not be too bothered by others words if our conscience is clear.

BE PATIENT
This is a true story that happened in the States. A man came out of his home to admire his new truck. To his puzzlement, his three-year-old son was happily hammering dents into the shiny paint of the truck. The man ran to his son, knocked him away, and hammered the little boy’s hand into pulp as punishment. When the father calmed down, he rushed his son to hospital.
Although the doctors tried desperately to save the crushed bones, he finally had to amputate the fingers from both the boy’s hands. When the boy wake up from the surgery and saw his bandaged stubs, he innocently said, “Daddy I am sorry about your truck,” Then he asked, “but when are my fingers going to grow back?” The father went home & committed suicide.

Think about this story the next time someone steps in your feet or you wish to take revenge. Think first before you lose your patience with someone you love. Trucks can be repaired. Broken bones and hurt feelings can’t. Too often we fail to recognize the difference between the person and the performance. We forget that forgiveness is greater than revenge.
People make mistakes; we are allowed to make mistakes. But the actions we take in a rage will haunt us forever.
(The author is unknown)

Tuesday, March 25, 2008

LUGHA SITA MUHIMU ZA HISIA ZA MAPENZI KTK NDOA (Sehemu ya mwisho)


6. MUNGU (Christ in me)
Hapo mwanzo Mungu alimuumba mtu, akawaumba mtu mke na mtu mume, kutoka mtu mume akaumba mwanamke (operation ya ubavu). Na kutoka mmoja akatengeneza wawili. Hakuna ambaye anaweza kufanya hivyo isipokuwa ni Mungu peke yake. Then katika ndoa, Mungu akawafanya hao wawili kuwa mmoja na akasema alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganisha, kwani ni Mungu peke yake anayeweza kutengeneza kutoka wawili kuwa mmoja. Alijua hawa wawili wakijua siri za kuridhishana kimapenzi basi ndoa yao itadumu hadi kifo kitakapowatengeanisha. Hapo hakuna swali ni Mungu amesema.

Mungu ni mwanzilishi wa ndoa (author), ndoa ni taasisi ya muda mrefu tangu binadamu anaumbwa na kumekuwa na mabadiliko mengi ya binadamu kiuchumi, kisiasa na kijamii lakini bado asili ya ndoa ipo palepale yaani unapokuwa na uhusiano na Mungu maana yake unaruhusu ndoa yako kuwa imara zaidi.

Kuna mambo makuu mawili ambayo binadamu yeyote inabidi awe makini katika kuamua na hapo unahitaji kuwa genius (akili za tofauti) kwani hapo makosa hayana nafasi
(i) Je baada ya kufa utaenda wapi kutumikia umilele wako
(ii) Mtu utakayeoana naye - uoane na mtu sahihi na maisha yako kuwa ya furaha siku zote au uoane na mtu asiye sahihi uwe kwenye hell (jehanamu ya duniani)
Watu wengi huingia kwenye ndoa wakiwa very lightly, unahitaji kuwa makini kwani ndoa ni zaidi ya makubaliano ni agano (Covenant) kati yako, unayeoana naye na Mungu, na hili agano hudumu hadi kifo kitakapowatenganisha.

Ni pale tu Christ anapokuwa muhimili wa ndoa yako na hapo kila kitu kitakuwa ni furaha amani na upendo unaokupa kuridhika kihisia.

Kwa kuwa Mungu ni mwanzilishi wa ndoa na maana yake pia yeye ni mwanzilishi wa sex, romance, mahaba, mapenzi katika ndoa. Na ndiyo maana alituumba na viungo ambavyo vinatupa raha ya wawili yaani mke na mume wakiwa faragha na si kutupa raha tu bali huvutia hata kwa macho na kuleta ujumbe unaofanya mwili mzima kusisimka na kupata ridhiko la aina yake ni kweli naamini hakuna raha duniani kama raha ya mapenzi.
Mungu ametupa sex kama zawadi kwetu na njia Mojawapo ya kumuabudu yeye kama tunavyofanya ibada zingine kama kuimba na kutoa sadaka. Sex si kwa ajili ya kuzaliana tu bali kutuwezesha Wanandoa kuwa na umoja (oneness, intimacy).
Kama sex ni kazaliana basi Mungu angetuwezesha kupeana mimba hata kwa kusalimiana tu au kwa kuongea tu unatamka na mke anashika mimba, ila alitupa zawadi kuu kwa sababu anatupenda na ni njia ya yeye kutuwezesha kuutambua uumbaji wake.Ametupa hiyo zawadi ili tufurahiane na kupeana raha na zaidi tufurahia kwa kutumia milango mitano ya fahamu yaani Kugusa,
Kuona,
Kuonja,
kusikia na
Kunusa
Kanisa huanzia chumbani hapo ndo kwenye ibada ya kweli tukienda church tunamalizia ibada. Kama chumbani mambo hayaendi vizuri kukutana kwetu church kunakuwa ni unafiki kwani mmoja wetu anakuwa hajaridhishwa kimapenzi ktk ibada kuu kule home ambayo Mungu anaiheshimu pia.

Tunasikia kwamba kuna watu wapo kwenye ndoa zaidi ya miaka 20 lakini mume au mke hajawahi kuona uchi wa mwenzake, Nimesikia kisa kimoja, mwanamke aliwahi kuona kipande cha tako la mumewe siku moja tu, siku ambayo taulo liliteleza na kuanguka na wana watoto 4 na hajawahi kuwa uchi wakafurahi uumbaji wa Mungu.
Mume na mke wote ni mmoja na hakuna raha kama ya kuwa uchi kwa mume na mke chumbani kwenu kwani hiyo ndiyo maana halisi ya Mungu kuwafanya kuwa mwili mmoja kwamba
Mcheze pamoja uchi,
Mlale pamoja uchi,
Muoge pamoja uchi,
pia muifurahie miili yenu pamoja uchi,
Sex ina umuhimu kama kula, chakula, kulala, au kufanya mazoezi. Tatizo ni kwamba jamii zetu zimekuwa na wakati mgumu sana kuongelea masuala ya mapenzi (sex) na matokeo yake ndoa nyingi zimeingia matatizoni.
Ni kweli tunafundishwa kwamba sex kabla ya ndoa ni mbaya na ni kweli ni mbaya kwani kuna raha sana kukutana honeymoon wote hamjui lolote na si kwa sababu ya honeymoon tu bali ni dhambi kabla ya ndoa. Hii imefanya hata Wanandoa wengi waliokulia kanisani kuona kwamba sex ni kitu kibaya na si muhimu katika ndoa, pia kuona kwamba uchi ni kitu kibaya na kitu kichafu kitu ambacho si kweli, hakunakitu muhimu na kisafi kama hivyo viungo tatizo tumfundishwa tangu watoto kuwa huko ni sirini, kunaitwa sirini kwa sababu ndo raha ya duni hapo.
Fahamu umeacha wazazi wako ili kuja kwa huyo mwanaume au mwanamke sababu ya mwili wake na mwili wake ni pamoja na hivyo viungo vyote vya kufanyia mapenzi na kitu cha msingi ni kuridhishana. Pia mmekuwa mmmoja na si wawili tena hivyo furahianeni.
Bila Mungu (Christ in you) bado ndoa itachezewa sana na shetani kuna nguvu moja tu ambayo huweza kurudisha ndoa kwenye asili yake nayo ni maombi.
Kumjua Mungu kusikufanye iwe Tatizo na kuona aibu kufurahia ndoa yako na maisha ya mapenzi kwani Mungu ni mwanzilishi wa romance, sex na wewe kuufurahia mwili wa mke wako au mume wako kwani kama si hivyo basi angetuumba bila viungo vinavyoleta raha ya mapenzi.

Marriage is C3
Commitment
Communication
Christ

Monday, March 24, 2008

LUGHA SITA MUHIMU ZA HISIA ZA MAPENZI KTK NDOA (lugha ya 4 na 5


4. MGUSO (physical touch)
Kukumbatia, kubusu, kushikana mikono na sex (ktk ndoa) ni njia ya mawasiliano ya hisia za upendo au kupendwa. Watafiti wengi hasa wa maendeleo ya watoto wamethibitisha kwamba kukumbatia, kumbusu na kumshika mtoto kunampa afya njema kihisia.
Kuguswa ni kitu muhimu sana katika mawasiliano ya ndoa hasa linapokuja suala la mahaba, kwa kushikana mikono, kubusu, kukumbatiana na kutekenyana kule kunakonyegesha huleta raha sana kwa mke na mume.
Inawezekana mume wako au mke wako kwake kupendwa ni kukumbatiwa au kupata busu kabla hujaondoka asubuhi na unapokutana naye tena baada ya shughuli za kujenga familia au kutembea mmeshikana naye mikono, pia inawezekana kwako ni jambo gumu na unaona kama ushamba fulani hivi au ulimbukeni, ila fahamu kwamba kila mmoja wetu ana aina ya kujisikia unampenda na ni kitu kidogo lakini kinaweza kufanya ndoa yako kuwa tamu au kuwa chungu.
Kama ni mwanamke unaweza kuwa unatumia muda mwingi sana kupika chakula kitamu, au kununua mizawadi ya gharama kwa ajili yake na lengo ajue unampenda, kumbe yeye kupendwa ni physical touch, inakuwa kama vile unampigia mbuzi gitaa.
Kwa hiyo chunguza mwenzi wako kwake kupendwa ni kufanyiwa nini na kama ni physical touch basi hapa umepatia fanya kweli.
Ktk milango ya mitano Fahamu, kugusa ndo peke yake kunahusisha mwili mzima ingawa kuna sehemu zingine zikiguswa ni balaaa. Kuona tunatumia macho, kusikia tunatumia masikio, lakini kuguswa ni mwili mzima na kitu muhimu katika kuguswa ni kujua unaguswa wapi na unaguswa kwa kutumia nini, je ni mikono au ulimi na ni wapi unaguswa! Kazi kwenu!!
Katika suala zima la physical touch jambo la msingi ni kwamba unatakiwa kugusa pale mume wako au mke wako anapenda umguse siyo kugusa tu, kwani si kweli kwamba sehemu zote ambazo wewe unajisikia raha kuguwa basi na mume wako au mke wako atajisikia raha. pia mwingine anapenda kukumbatiwa kuliko mibusu, na mwingine anapenda sex kuliko kukumbatiwa.
Sex ni physical touch, ndiyo maana kuna wanawake au wanaume bila kumpa sex anaona bado humpendi hata kama utamnunulia gari au kumpeleka vacation Las Vegas.
Mwili ni kwa ajili ya kuguswa,
unaonaje mtu akigoma kukusalimia mikononi?

Naamini utatambua kwamba kuna mushkeli.
Inawezekana mume wako au mke wako kupata mguso wa mwili ni lugha yake ya msingi kuonesha unampenda na anategemea utamgusa mwili wake kila siku kwa kutekenya nywele zake, au kutembea umemshika mkono au kumpa busu na kumkumbatia kila unapoondoka home asubuhi au unaporudi na pia kumpa romance ya uhakika kabla ya sex mkiwa faragha, Fahamu ameacha wazazi wake kuja kwako ili umpe hicho anataka kwa hiyo usituangushe fanya kile mpenzi wako kitampa raha.
HOME WORK KWAKO BAADA YA SOMO:
(i) Jaribu kumshika mkono mnapotembea pamoja
(ii) Unapoondoka asubuhi (amka) hakikisha umempa busu na hug la nguvu likiambatana na maneno matamu yale hujatamka kwa muda mrefu
(iii) Kabla ya kulala omba Mungu pamoja huku mmeshikana mikono
(iv) Pia hakikisha unampa mguso wa uhakika (romance) kabla ya sex mkiwa huko kwenye bustani yenu naamini hiyo chemichemi ya maji itafurika na kiu itapata dawa

5. KUSAIDIANA KAZI AU HUDUMA
Hii ni kufanya vitu ambavyo mke wako au mume wako anatarajia au anategemea ungefanya kuonesha unampenda na kumjali na kuwa wewe ni yeye ni kitu kimoja.

Mume wako au mke wako Fahamu kwamba anajua una hekima kubwa kiasi kwamba unafahamu kwamba ngeweza kumsaidia kufanya kitu Fulani so anasubiri kuona je utafanya kwani umesema unampenda.
Inawezekana anategemea ungemsaidia kutandika kitanda, kusafisha nyumba, kupika, kufua nguo, kumsafisha mtoto, kuosha gari, kufyeka majani nk hiyo mnaweza kufanya pamoja na ni njia nzuri ya kueleza kwamba unampenda kwa vitendo.
Tatizo linakuja kutokana na jamii zetu za kitanzania asilimia kubwa ya familia zetu ni extended, hivyo kwa mfano baba akiamka asubuhi na kuanza kufanya usafi wa nyumba au kupika au kufua nguo za wife nahisi hata majirani wataandamana kuuliza kulikoni kwani yawezekana hapo kwako kuna timu ya watu kutoka kijijini au ndugu zako kama dada, kaka, shemeji, wajomba, baba mdogo, ndugu wa shangazi zako au wafanyakazi ulionao kama house girl, house boy na wale wageni waliokuja kutoka kijijini bila kukupa taarifa nahisi watashangaa.

Point hapa ni wewe kumsaidia mwenzi wako so tumia busara na si kuangalia watu maana ndoa ikiwa moto ni wewe.
Yesu mwenyewe aliosha miguu ya wanafunzi wake kuonesha upendo na hii ilikuwa kuwapa practical expression ya jinsi kupendwa kulivyo.
Katika jami yetu ya Kitanzania kwenye hili eneo wanaume ndo tumekuwa wababe na hatukubali na najua kuna wanaume watasema naongea vitu ovyo lakini ukweli ni kwamba kama mke wako lugha ya msingi kwake ni wewe kumsaidia kazi basi unahitaji kubadilika na kufanya ili kunusuru ndoa yako kwani amekuchagua wewe kwa sababu ni wewe tu hapa duniani unayemfaa. Hata kama utampa zawadi kubwa kubwa au unampa sex ya uhakika kama kwake kupendwa ni wewe kumsaidia kazi bado ataona unamtumia tu na humpendi.
Mbona wakati hujamuoa ulikuwa unaenda kwao kusaidia kazi na ulikuwa unajitoa sana kwa hilo na inawezekana ndo sababu alikubali umuoe sasa yupo ndani humsaidii tena na unalalamika kwamba kitandani amepoa ni baridi! Anza wewe kwanza kwa kumpa kila anataka.

Tutaendelea na somo letu......

LUGHA SITA MUHIMU ZA HISIA ZA MAPENZI KTK NDOA (Mwendelezo)

Katika jadi nyingi, pete ya ndoa ni ukamilisho wa zawadi zinazotolewa na ni ishara ya kujitoa na kuonesha upendo kwa maharusi. Kuna aina nyingi za pete kama vile uchumba (engagement ring na pete ya Ndoa (wedding ring)
Je utajisikiaje kama ukifanya engagement au wedding bila rings?
2. KUPEANA ZAWADI.
Zawadi ni kitu chochote unachoweza kukishika kwa mikono na kinakupa hisia kwamba aliyenipa zawadi alikuwa ananifikiria na ananipenda.
Kutoa zawadi kulikuwepo miaka mingi iliyopita na tunazidi kurithisha kizazi hadi kizazi na kila mmoja naamini ameshapokea zawadi nyingi ingawa tunatofautiana katika upokeaji huo wa zawadi kwani kuna wengine leo inawezekana hawajapata zawadi, wengine hii wiki, wengine huu mwezi na wapo pia ambao huu mwaka bado hawajapata zawadi yoyote.
Zawadi huelezea upendo, ndiyo maana hata katika uchumba kila upande hujitahidi kutafuta zawadi nzuri kwa ajili ya mpenzi wake.
Wanandoa wengi hupuuza na kuona kwamba zawadi siyo kitu muhimu ktk mapenzi na pia si lazima umnunulie mpenzi wako gari au kumjengea nyumba ndo iwe zawadi, vile vitu vidogo sana kama pipi, Chocolate au maua ni zawadi za msingi sana na zina maana kubwa sana katika kuimarisha mapenzi katika ndoa.
Na kama mpenzi wako kwake zawadi ndo kupendwa basi wewe una kazi nyepesi sana ya kumfikisha pale anataka kwani zawadi ni moja ya vitu rahisi sana kuvifanya.

Zawadi muhimu pia, ni wewe kuwepo au kupatikana pale mke wako au mume wako anakuhitaji anapokuwa na shida, hujasikia mtu anasema nampenda kwa sababu nilipokuwa na shida au matatizo yale alikuwa na mimi muda wote na ni yeye tu, uzoefu iunaonesha zawadi hata za kutoa muda wako hukaa ktk kumbukumbu za mhusika kwa miaka mingi bila kusahau na pia utaongeza level ya mapenzi kwake.
Kwa kuwa unajua zawadi ni nini na kutoa zawadi kitu muhimu hapa basi kitu cha msingi ni matendo si maneno, ni kufanyia kazi sasa hivi ukishamaliza kusoma hapa ebu fikiria jinsi utafanya kuleta mabadiliko katika ndoa yako.
Inawezekana mke wako au mumeo ni watu ambao akipewa zawadi basi yeye ndo kupendwa yaani ndo anaguswa zaidi, moyo wake unaamini ukipewa zawadi ndo unapendwa.
Basi fanya jambo lifuatalo kwa wiki nzima kuanzia sasa hivi,
(i) Mpe zawadi mke wako au mume wako kila siku kwa wiki zima pia andika mahali hizo zawadi unampa, sijasema ukamnunuliea gari ila kama unaweza poa tu. Halafu angalia kama kuna mabadiliko yoyote katika emotions zake kwako katika mapenzi.
Nakuomba ukimaliza tu kusoma hapa nenda kanunue hata maua na ukifika home mpe zawadi mpenzi wako yaani usirudi bila zawadi leo na nakwambia ndoa yako itaanza kuwa na moto wa uhakika na utaanza kuwaka kila sehemu sitting room na mkifika huko bed room acha tu! mimi chichemi!
Ukiona mabadiliko ni makubwa basi fanya kweli kwani hapo utakuwa unagusa maisha yake na unajaza ile sehemu ambayo upendo unatakiwa kujaa.

3. MANENO MATAMU (Kusifia, kutia moyo na kushukuru)
Je ni mara ngapi umesema Asante au kumsifia spouse wako kwa jinsi alivyokurusha vizuri kwenye mahaba na sita kwa sita?
Na je kawaida unapomsifia au ku-appreciate vitu anafanya huwa anajisikiaje?
Hayo maswali ni ya msingi sana mtu kujiuliza hasa kama unataka kujua mke/mume wako kwake maneno matamu ndiyo KUPENDWA
Maneno mazuri au yanayotia moyo au yanayomsifia ambayo ni matamu husababisha mambo yafuatayo kwa mwenzi wako
(a) Huleta upamoja na ukaribu zaidi (intimacy)
(b) Huleta uponyaji kwenye majeraha ya hisia zake kama kuna maumivu moyoni mwake (healing) na kumfariji
(c) Mume wako au mke wako hujisikia kulindwa zaidi na anajisikia yupo katika mikono salama.
Fahamu kwamba wewe ndiye mtu muhimu kuliko mtu yeyote duniani kwake, hivyo maneno unayoongea either yanamjenga au yanambomoa na si kubomoa tu bali na kumuumiza na unampa wakati mgumu. Kwa nini tusibadilike sasa hivi na kuamua kuwa watu wa maneno positive na kufuta kabisa maneno ya amri, ukali, kulaumu, au kuwa mtu wa lawama tu yaani kutaka kila kitu kiwe kama unavyotaka wewe.
Lengo la upendo si kulalamika kwa kile ambacho hupati
bali ni kufanya kile ambacho kitamsaidia yule unayempenda,
yule umechagua uishi naye hadi kifo kitakapowatenganisha.
Mojawapo la hitaji kuu la ndani la mwanadamu ni kuwa appreciated na kile mtu anafanya.
Je umewahi kuwa na boss mkali na mwenye maneno ovyo na mtu wa amri? Huwa unajisikiaje?
Fikiria unaishi na mke au mume wa aina hiyo.
Na kama wewe ni mtu wa ku criticize, kulalamika na kulaumu kila kitu, please jitahidi kubadilika na kuwa mtu wa maneno matamu ili uwe na maisha ya raha ya ndoa yako kwani wewe ndo uliamua kuoa au kuolewa na haipendezi kuwa na ndoa isiyo na mvuto wakati uwezo wa kubadilisha mambo unao.

Jitahidi uwe ni mtu wa maneno ya kutia moyo, maneno ya upole, maneno ya matamu na achana kabisa na maneno ya kulalamika tu kila kitu, au kukaripia tu, au maneno ya ukali kila kitu hadi watoto, mke au mume wanakuogopa hata ukiwepo wanabaki kimya maana kila wanachafanya na kuongea kwako hakifai.

Jizoeshe kumsifia mpenzi wako kwa kila jema analolifanya ama kwa uzuri alokuwa nao, au kwa chakula kizuri unachopika au kazi anavyofanya au jinsi anavyowajibika mkiwa chumbani.
Hapa wanaume tunahitaji kujitahidi zawadi naamini kutokana na mfumo wetu dume wa Kiafrika hata kusema asante au nisamehe au nimekosa inakuwaga kazi, please naomba tubadilike ili ndoa zetu na nyumba zetu ziwe sehemu bora kuishi.

Fanya yafuatayo hii wiki then angalia kama kuna mabadiliko kwa mume au mke wako:
(i) Mwandikie mume au mke wako love letter kwa mkono wako na iache sehemu ambayo ataiona na kitu muhimu mwandikie maneno matamu, ya kusifia, kwa yale yote anafanya.
(ii) Ukiwa na wenzako kama upo naye msifie mbele zao kitu chochote.
(iii) Mpe asante kwa kila kitu hakikisha siku haipiti hajasema asante.
(iv) Msifie mbele ya watoto wako

Naomba Nijibrekishe……… tutaendelea!

Saturday, March 22, 2008

LUGHA SITA MUHIMU ZA HISIA ZA MAPENZI ZA KUZINGATIA KWENYE NDOA

Ndoa ni kama Kamba, siyo kamba ya kukunyonga, bali kamba inayounganisha (kuwafunga) wawili kuwa mmoja. Kamba ya ndoa umetengenezwa kwa kuunganisha nyuzinyuzi za upendo wa ahadi nne za yaani mawasiliano, kujitoa, kumwelewa mwenzako na kumsamehe.

Wakati mwenzi (Spouse) wako anajisikia kuridhishwa kimapenzi (emotionally/romantically) hujiona (feel) salama kihisia na hujiona ulimwengu unampa vyote na atajitoa zaidi kuhakikisha anajitoa katika kiwango cha juu kwao kuimarisha upendo na mahusiano.

Na anapojisikia kutoridhishwa kabisa kimapenzi, hujisikia ni kama vile anatumika au unamtumia tu kufanikisha hitaji lako la mapenzi bila kupendwa na kwake ulimwengu unageuka kuwa mahali hatari kwake na husababisha hata vitu vingine ulivyompa kama nyumba, gari, fedha nk kuwa havina maana katika uhalisia wa maisha.

Mapenzi yana lugha kama zilivyo lugha za mawasiliano, utamu wa lugha ni pale unapoifahamu kuisikia na kuiongea, pia utamu wa mapenzi katika ndoa ni pale unapofahamu lugha ya mapenzi kusikia na kuongea.

Raha ya Kiswahili ni pale unapoongea Kiswahili na mswahili mwenzako, na kuongea vile vimaneno vitamu vinavyofanya ufurahi na kucheka na kujiona kweli Kiswahili kitamu. Je inakuwaje unapoongea Kiswahili na mtu anayeongea Kichina, Unamuomba maji anakuletea jiwe na anajifanya anajua kile umemuomba, naamini hamtaelewana kama nakudanganya Nenda mashariki ya mbali waulize wale jamaa waliotaka kujenga mnara ufike hadi mbinguni ambako Mungu yupo, then Mungu akawageuzia kibao akawachanganya lugha, Guess what? Hawakufanikiwa maana mtu akitumwa mchanga alikuwa analeta sululu.

Kuna watalamu na washauri ya mambo ya ndoa na mapenzi wameandika sababu nyingi sana zinazoelezea lugha halisi za mapenzi, real emotional love languages, wengine wanasema zipo 5, wengine 10, wengine 50, wengine 100 Mimi naona zipo sita ila moja (ile ya sita) ni muhimu kwa wote na ni msingi halisi wa ndoa na ni asili yake na kuizembea hiyo naamini inaharibu mtiririko wa lugha zote za hisia za mapenzi. Kuzijua hizi lugha sita na kufahamu ni zipi (ipi) mke wako au mume wako yupo basi ndoa inakuwa tamu kwelikweli, utamu halisi usio na hila, na utakiri kwamba kweli ndoa ni tamu.

Lugha za msingi za kuelewana katika ndoa kwa hisia za mapenzi ni kama ifuatavyo:-
1. Kuwa na muda na mwenzi wako
2. Kupeana zawadi
3. Kusaidia kazi/huduma
4. kumpa maneno ya kumsifia, kushukuru na kumtia moyo kwa kile anafanya
5. Mguso wa kimwili (wale wa mabusu na ma-hug kazi kwenu)
6. Mungu (Christ in You) Muhimu kuliko zote

Leo tutaongelea namba Moja

1. KUWA NA MUDA NA MWENZI WAKO (Quality time)
Msingi wa kuwa na muda na mwenzi wako ni upamoja (togetherness) pamoja na kuwa kimawazo, kimwili na kiakili (focused attention)

Kuwa na muda na mwenzi wako hatumaanishi kukaa pamoja kwenye sofa au makochi kuangalia TV; au movie hapo mnaipa time au muda wa pamoja TV au movie mnayoitazama siyo mwenzi wako.
Kuwa na muda na mwenzi wako ni kukaa pamoja na kumpa attention yote, anaongea na wewe unamsikiliza tena ninyi wawili tu, kutembea pamoja yaani mmeamua kwenda kutembea kwa ajili ya kwenda kutembea wewe na yeye tu si kwa sababu mnaenda kanisani au mnaenda kazini, kupeana muda wa pamoja ni kama vile kwenda kula pamoja (outing) ninyi wawili na mkifika hapo kwenye hoteli mnaongea kwa kuangaliana ninyi romantically.

Ukienda kwenye hoteli au sehemu yoyote watu wanaenda unaweza kula chakula au huduma zingine (outing) utajua tu wapenzi walio kwenye ndoa na wale ambao bado wachumba au dating couples, Guess what? Wachumba utakuta wanaongea kwa kuangaliana tena kwa karibu na vikolombwezo kibao na wanatamani wabaki hapo, tuje walio kwenye ndoa wanakula na kunywa kila mtu anaangalia kwake, wanaangalia kuta na watu na unajua wameenda kula na si kuwa na muda pamoja, halafu wana haraka sana, kidogo tu waaondoka kama vile wamelazimishwa kwenda outing.
Tuwe romantic jamani, tutaendelea kujadili zaidi huko mbele safari ya somo letu.

Ni kweli kila mtu anahitaji muda na mwenzi wake, lakini maajabu ni kwamba si kila mwanandoa ukimpa muda au kuwa naye kwake ndo anajisikia na kujiona unampenda kwani kwake kuwa na muda naye hakumgusi kama ukiwa unamletea zawadi, au unapo mpa maneno ya kumsifu kwa kitu amefanya, au kumshukuru na kumpa affirmation kwa kila anachofanya.

Kitu cha msingi ni wewe kuchunguza je mpenzi wangu anajisikiaje kwa kila mambo 5 ni lipi linamgusa sana na kujiona kwake ndo la msingi kuliko yote. Kama ni Kumpa muda ndo anajisia unampenda basi fanya makeke your baby ajipe raha.

Mbona tunapo date tunakuwa na muda pamoja huko tumepanga kukutana? Kwa nini baada ya kuoana watupeani time hata kama tunalala pamoja issue hapa ni kumpa muda ambayo katika masaa 24 hata kama ni dakika 20 tu mpe mpenzi wako na kama lugha yake ya mapenzi ni kuwa na muda na wewe basi utampatia sana na kama hufanyi ndo yale yale unampa zawadi ya gharama lakini bado anasema humpendi na love tank inazidi kuwa empty Hebu jaribu kufanya kweli uone kama mwenzi wako hajakwambia baba Fulani au mama Fulani siku hizi unanipenda sana, yaani umebadilika, acha kusema upo busy, gharama ya kusuruhisha ndoa unayoenda ICU ni mbaya sana kuliko huo ubusy.

Fanya yafuatayo katika suala zima la kumpa mwenzi wako muda wa pamoja hasa kama kwake kumpa muda ndo anajisikia unampenda
(a) Mwangalie usoni wakati anaongea (eye contact) atajua unamsikiliza
(b) Usimsikilize huku unafanya kazi nyingine, kama huwezi muombe akupe muda kidogo then utamsikiliza anachosema kuliko kuendelea kufanya kile unafanya huku unamsikiliza, utamuumiza sana
(c) Onyesha hisia kwa kile anakwambia, kama unahisia amekatishwa tamaa mwambia ukweli kwamba nahisi unajisikia umeumizwa au kukata tamaa, basi nitafanya hivi na hivi, changia kupata solution
(d) Hakikisha unajua anaongelea nini na anajisikiaje (body language)
(e) Usimkatishe anapoongea, sikiliza maana wengi huwa tunadhani tunajua hata alichokuwa anataka kusema hata kabla hajasema, eti nilikuwa najua utasema hicho tu

Unakaribishwa kutoa maoni, maswali na naomba niwahi mwaliko wa Pasaka then Tutaendelea …………………..

Friday, March 21, 2008

UPENDOUpendo (mapenzi, Kupenda, Love) Ndiyo neno muhimu kuliko maneno yote tuliyonayo katika maisha yetu ya kila siku. Pia ni neno linalotuchanganya sana(confusing), hata kutamani ardhi ipasuke mtu uingia na kuishia.
Kwa watu wote wenye dini na wasio na dini wote tunakubaliana kwamba neno Upendo ni kiungo muhimu sana cha maisha ya mwanadamu.
Pia Bwana Yesu aliagiza kwamba wote wanaomfuata yeye hawana budi kuwa na Upendo kwa kuwa Mungu mwenyewe ni Upendo na hii ndiyo itakuwa tofauti kwao kuonesha ni wafuasi wake halisi.
Paulo Mtume hodari katika Agano jipya anaelezea kwamba katika tabia za msingi wa binadamu yaani Imani, tumaini na Upendo bado Upendo ni namba moja.
Wanasaikolojia wamehitimisha kwamba kupendwa ni hitaji kuu la kwanza la msingi katika maisha ya kihisia (emotions) kwa binadamu yeyote.

Kwa Upendo na Kupenda na mapenzi tunapanda milima, tunavuka bahari hadi bahari, jangwa hadi jangwa, taifa hadi taifa, tunajenga majumba na kununua magari kwa ajili ya wale tunaowapenda pia tunapita katika mambo magumu kwa sababu ya Upendo. Kwa Upendo watu wamekufa na wengine kufanya vitu ambavyo wengine tunawashangaa na kuona akili zao zimewaruka, bado jibu ni Upendo

Upendo ulikuwepo, upo na utakuwepo, utamu wake na machungu yake bado yanatukumba wanadamu na kutupa uzoefu wa maisha kwa njia tofauti.

Wanasaikolojia wamehitimisha kwamba tangu mtoto anapozaliwa anakuwa na nafasi tupu (empty) kwa ajili ya kujaza Upendo na Upendo unavyozidi kujaa katika hiyo nafasi ndipo katika kukua kwake anakuwa imara kihisia (emotionally) na bila kupendwa ataathirika, Angalia watu ambao walikosa Upendo tangu wadogo kutoka jamii waliyozaliwa then utaona tofauti.

Katika moyo wa mwanadamu kuna nafasi hiyo tupu ya hisia (emotional tank, or hole) na kuna hitaji kuu la kupendwa (intimate and to be loved) na mtu mwingine wa jinsi tofauti, Ndoa iliwekwa maalumu kwa ajili ya kukamilisha hilo hitaji.
Kila binadamu bila kujalisha ni maskini, au tajiri, mweusi au mweupe, wa mjini au kijijini mtoto au mzee au kijana wote tunahitaji kuu la kupendwa, kupendwa ni kutamu, ni raha ni kuzuri ni yote katika yote.

Kama umeoa au kuolewa basi fahamu kwamba mwenzi wako (spouse) anahitaji upendo wako, anakuhitaji wewe, kwa hiyo jitahidi kumpenda na kuwa na muda na yeye kuhakikisha hiyo nafasi tupu ya hisia inajaa siku zote (emotional hole or tank is full)

Hapo katika kujaza na kutojaza hiyo nafasi ndipo kwenye matatizo na migogoro ya watu kuanza kutamka kwamba “Naona siku hizi hanipendi” na hapo ndipo kwenye siri kubwa ya nini hutokea baada ya watu kuoana.
Tutaendelea na hatua inayofuata kuelekea kwenye utamu wenyewe………
SES by DegreeAdvantage.com marketing team.

Thursday, March 20, 2008

NINI HUTOKEA KWENYE MAPENZI BAADA YA KUOANA?


"Nilidhani tunapendana sana lakini baada ya honeymoon ndoa imekuwa maafa"


Tume Date kwa miezi sita na tulijiona duniani ni sisi tu kwa moto wa mapenzi/mahaba, lakini baada ya kuoana nyumba yetu imekuwa uwanja wa vita kwa kutokuelewana, Why?


Hili swali na mengine mengi yanayofanana na hilo huulizwa na maelfu ya watu ambao wameoa haijalishi mmeishi miaka mingapi, na wengine wamepeana talaka na kuoa na kuolewa mara nyingi zaidi na bado maswali kama hayo yapo.

Wengine wamewauliza wazazi wao, viongozi wao wa dini na pia washauri wao, lakini wakirudi nyumbani baada ya kupewa ushauri na majibu bado hali ni ile ile ni kama vile kutibu cancer kwa kutumia Asprini au ni kama kitendo cha mende kuangusha kabati.

Inakuwa raha sana kabla ya kuoana/uchumba na baada ya kuoana hali inakuwa tofauti kabisa na wengine wanajuta kwa nini waliolewa na kuoa.

Pamoja na kuwa na TV, radio, magazeti, vitabu vyenye topic nzuri za kuimarisha ndoa zetu na semina mbali mbali, lakini bado mapenzi baada ya ndoa yanazidi kuwa kitendawili.

Ni ndoa chache kwa sasa ambazo zimebarikiwa kufahamu siri hii kubwa ya mapenzi baada ya kuoana na kutokana na kufahamu siri hiyo hao wanandoa wanaweza kukuthibitishia kwamba hakuna kitu kizuri duniani kama kuwa na mke au mume. Ndoa ni tamu, ndoa ni mpango wa Mungu kumkamilisha binadamu, ndoa ni msingi wa familia na taifa.
Je Siri ni nini?
Tuanze somo letu kwa kuangalia msingi kabisa wa mambo ya mahusiano ya kimapenzi hatua kwa hatua na leo napenda kukuletea utangulizi wa somo letu wakati tunaelekea kuchambua hili suala.


Mapenzi yana lugha kama zilivyo lugha za kawaida yaani Kiswahili, Kingereza au Kichina. Wengi tumezaliwa tunaongea lugha tulizafundishwa na wazazi wetu au ndugu zetu na kutokana na kuzifahamu vizuri zimekuwa lugha mama yaani Primary. Tunajisikia raha kutumia hizo lugha na pia tunajisikia raha kusikia kwani tunaelewa kuliko lugha zingine.


Katika mapenzi kuna lugha pia (emotional love languages) kwa hiyo mwanaume anaweza kuwa ana lugha yake na mwanamke ana lugha yake katika kuitikia mapenzi au kujisikia kwamba anapendwa. Kutokujua lugha ya mwenzake ni sawa na watu wawili (wanandoa) kuishi pamoja na kuwasiliana kwa kutumia kichina na kiswahili na kudhani wataelewana. Haitawezekana kamwe!

Hujasikia mwanaume analalamika kwamba "Mke wangu nimepa kila kitu, nimemjengea nyumba nzuri, nimemnunulia gari zuri, fedha za matumizi nampa nk, lakini analalamika kwamba simpendi, hiyo ni kudhihirisha kwamba huyo mwanaume kwa kumpa nyumba nzuri na gari zuri mke wake kwake ni lugha ya kuonesha anampenda mwanamke, wakati mwanamke kupewa gari na nyumba kwake bado si kupendwa yawezekana kusikilizwa na kuwa na muda pamoja (quality time) kwani ni lugha inayoeleweka kuonesha anapendwa.


Tutaendelea kujadili .........................................

Tofauti ya mwanaume na mwanamke katika maumbile

Mwanaume na mwanamke wanatofauti kubwa katika maumbile, na kufahamu tofauti iliyopo kati ya mwanaume na mwanamke huwezesha pande mbili hizi kuchukuliana na kufahamiana vizuri ili kukamilisha maisha yetu hasa katika suala zima la mahusiano.

Kuna tofauti kubwa sana kati ya mwanaume na mwanamke katika mambo yafuatayo:-
(i) Katika kila seli ya mwanaume na mwanamke kuna tofauti. Tofauti yake (chromosomes) ndiyo husababisha kufanyika kwa mwanaume na mwanamke.
(ii) Imethibitika kwamba Mwanamke anaweza kuishi miaka mingi zaidi kuliko mwanaume [wenye umri mmoja] kwa miaka mitatu hadi minne.
(iii) Mwitikio wa mapenzi (sex) kwa mwanaume ni wa haraka zaidi kuliko mwanamke. Mwanaume huweza kusisimka kwa kuona tu uzuri wa mwanamke wakati mwanamke huathirika zaidi kimapenzi kwa kuguswa na kusikia yale anayosikia kutoka kwa mwanaume. (ndiyo maana wanawake wengi ni waathirika wa kudanganywa na wanaume kwani wapo innocent kuamini kile anaambiwa na wanaume ni mafundi wa kupanga maneno hata ya uongo)
(iv) Kuna tofauti kubwa sana ya maungo (skeleton) kwani kidole cha kwanza cha mwanamke ni kirefu kuliko kidole cha tatu na kwa mwanaume ni kinyume chake.
(v) Mwanamke ana tumbo kubwa, figo kubwa, maini makubwa na mapafu madogo na kwa mwanaume ni kinyume chake. je kuwa na mapafu madogo husababisha wanawake kuchoka haraka?
(vi) Kuna mambo matatu muhimu ambayo yanapatikana kwa mwanamke na hayapatikani kwa mwanaume nayo ni Kupata siku za mwezi, kubeba mimba na Kunyonyesha. Hapa ndipo kwenye siri kubwa ya hisia na saikolojia ya mwanamke.
(vii) Kawaida damu ya mwanamke katika mwili ina maji zaidi kuliko mwanaume na damu yake ina upungufu wa asilimia 20 ya seli nyekundu ambazo husafirisha oxygen sehemu zote za mwili, maana yake mwanamke anakuwa na oxygen kidogo katika mwili kuliko mwanaume ndiyo maana wanawake huweza kuzimia kirahisi na kuchoka.
(viii) Moyo wa mwanamke hupiga haraka zaidi ya mara 80 kwa dakika wakati mwanaume ni mara 72 ingawa mwanamke Blood pressure yake ipo chini kuliko mwanaume na pia mwanamke anauwezo wa kupata high blood pressure kuliko mwanaume.
(ix) Mwanamke hupumua kidogo zaidi kuliko mwanaume
(x) Mwanamke anaweza kuhimili hali ya joto kuliko mwanaume.

Naamini tukifahamu tofauti zetu kimaumbile ndipo tutaweza kuishi pamoja katika ukamilifu wa kuchukuliana na kusaidiana hasa kwa wale waliom katika ndoa.

Wednesday, March 19, 2008

Je wanawake mpo sawa na wanaume?Kuzaa Watoto ni Moja ya Tofauti ya Mwanaume na Mwanamke

Je mwanamke na mwanaume wanauwezo sawa?

Wanaharakati wengi wa masuala ya jinsia wanaopigania haki za wanawake wanasema kwamba hakuna tofauti kati ya mwanaume na mwanamke likija suala usawa isipokuwa tu kwamba mwanamke anazaa? Kuna masuala mengi kama vile mambo ya emotions, uwezo wa kufanya kazi ngumu nk Je ni sahihi kwamba kweli mwanaume na mwanamke wote ni sawa isipokuwa mwanamke ana beba mimba na kuzaa? Tujadili