"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, March 19, 2008

Je mwanamke na mwanaume wanauwezo sawa?

Wanaharakati wengi wa masuala ya jinsia wanaopigania haki za wanawake wanasema kwamba hakuna tofauti kati ya mwanaume na mwanamke likija suala usawa isipokuwa tu kwamba mwanamke anazaa? Kuna masuala mengi kama vile mambo ya emotions, uwezo wa kufanya kazi ngumu nk Je ni sahihi kwamba kweli mwanaume na mwanamke wote ni sawa isipokuwa mwanamke ana beba mimba na kuzaa? Tujadili

4 comments:

Anonymous said...

Mwanamke ni mwanamke na mwanaume ni mwanaume wataendelea kuwa hivi na haitabadilirishwa wala kurekebishwa kwani ndivyo ilivyo na ndivyo inavyo pendeza.Sioni sababau ya kujadili vitu ambavyo havita toa jibu tofauti zaidi ya kufikia ukweli ambao tunaujua.Wanao jitahidi kupoteza muda katika kuviweka hivi viumbe viwili katika usawa ni kazi njema lakini ningependekeza wajibidishe katika kutafuta maarifa ya kufanya hivi viumbe viwili viishi kwa amani ,upendo na maisha bora yaliyo jaa furaha ya kweli.Nafikiri tofauti ni kitu cha muhimu ili kuleta nguvu ya mvutano kati ya mwanaume na mwanamke.Pale mwanaume asipo pawezea basi mwanamke anapawezea,na pale mwanamke asipo pawezea basi mwanaume anapaweea na kila akifanyacho mwingine humfanya mwenzake amwone wa maana kwani pasipo yeye kisinge fanyika.
Lakini sidhani kama kila mwana.. anajua wajibu wake kwa mwana..!!
by Elly

Lazarus Mbilinyi said...

Ni Muhimu tukafahamu tofauti iliyopo kati ya mwanamke na mwanaume kwani ndiyo unayotufanya tukamilishane katika kutegemeana na hapo ndipo kwenye siri kubwa ya kuwa na mapenzi halisi kati ya mwanaume na mwanamke kimaumbile na kisaikolojia

ashura said...

Upo sahihi kabisaaaaaaaaaaa'lkn????????hahaaaaaa, kazi kweli kweli. Upo sahihi brother umechota points zoote. Sina la kuongeza. Big up bra'
Your sis' SONGAMBELE - MEMPHIS

Hellen said...

Mwanamke na mwanaume wako sawa katika utendaji wakazi za kila siku,kwa sasa wanawake tuko mbele kwa kila jambo na hata taifa linaelewa hili. Ila tofauti ndio hiyo kuwa mwanamke anabeba mimba na mwanaume habebi mimba ila kwa mapenzi makubwa mwanamke awapo mjamzito hata mwanaume anakuwa mjamzito. Ila uwezo wa kufikiri, kufanya kazi na uwezo wa maamuzi yote ni sawa kabisa tena kwa wengine wanawake wana uwezo mkubwa zaidi