"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, March 24, 2008

LUGHA SITA MUHIMU ZA HISIA ZA MAPENZI KTK NDOA (Mwendelezo)

Katika jadi nyingi, pete ya ndoa ni ukamilisho wa zawadi zinazotolewa na ni ishara ya kujitoa na kuonesha upendo kwa maharusi. Kuna aina nyingi za pete kama vile uchumba (engagement ring na pete ya Ndoa (wedding ring)
Je utajisikiaje kama ukifanya engagement au wedding bila rings?
2. KUPEANA ZAWADI.
Zawadi ni kitu chochote unachoweza kukishika kwa mikono na kinakupa hisia kwamba aliyenipa zawadi alikuwa ananifikiria na ananipenda.
Kutoa zawadi kulikuwepo miaka mingi iliyopita na tunazidi kurithisha kizazi hadi kizazi na kila mmoja naamini ameshapokea zawadi nyingi ingawa tunatofautiana katika upokeaji huo wa zawadi kwani kuna wengine leo inawezekana hawajapata zawadi, wengine hii wiki, wengine huu mwezi na wapo pia ambao huu mwaka bado hawajapata zawadi yoyote.
Zawadi huelezea upendo, ndiyo maana hata katika uchumba kila upande hujitahidi kutafuta zawadi nzuri kwa ajili ya mpenzi wake.
Wanandoa wengi hupuuza na kuona kwamba zawadi siyo kitu muhimu ktk mapenzi na pia si lazima umnunulie mpenzi wako gari au kumjengea nyumba ndo iwe zawadi, vile vitu vidogo sana kama pipi, Chocolate au maua ni zawadi za msingi sana na zina maana kubwa sana katika kuimarisha mapenzi katika ndoa.
Na kama mpenzi wako kwake zawadi ndo kupendwa basi wewe una kazi nyepesi sana ya kumfikisha pale anataka kwani zawadi ni moja ya vitu rahisi sana kuvifanya.

Zawadi muhimu pia, ni wewe kuwepo au kupatikana pale mke wako au mume wako anakuhitaji anapokuwa na shida, hujasikia mtu anasema nampenda kwa sababu nilipokuwa na shida au matatizo yale alikuwa na mimi muda wote na ni yeye tu, uzoefu iunaonesha zawadi hata za kutoa muda wako hukaa ktk kumbukumbu za mhusika kwa miaka mingi bila kusahau na pia utaongeza level ya mapenzi kwake.
Kwa kuwa unajua zawadi ni nini na kutoa zawadi kitu muhimu hapa basi kitu cha msingi ni matendo si maneno, ni kufanyia kazi sasa hivi ukishamaliza kusoma hapa ebu fikiria jinsi utafanya kuleta mabadiliko katika ndoa yako.
Inawezekana mke wako au mumeo ni watu ambao akipewa zawadi basi yeye ndo kupendwa yaani ndo anaguswa zaidi, moyo wake unaamini ukipewa zawadi ndo unapendwa.
Basi fanya jambo lifuatalo kwa wiki nzima kuanzia sasa hivi,
(i) Mpe zawadi mke wako au mume wako kila siku kwa wiki zima pia andika mahali hizo zawadi unampa, sijasema ukamnunuliea gari ila kama unaweza poa tu. Halafu angalia kama kuna mabadiliko yoyote katika emotions zake kwako katika mapenzi.
Nakuomba ukimaliza tu kusoma hapa nenda kanunue hata maua na ukifika home mpe zawadi mpenzi wako yaani usirudi bila zawadi leo na nakwambia ndoa yako itaanza kuwa na moto wa uhakika na utaanza kuwaka kila sehemu sitting room na mkifika huko bed room acha tu! mimi chichemi!
Ukiona mabadiliko ni makubwa basi fanya kweli kwani hapo utakuwa unagusa maisha yake na unajaza ile sehemu ambayo upendo unatakiwa kujaa.

3. MANENO MATAMU (Kusifia, kutia moyo na kushukuru)
Je ni mara ngapi umesema Asante au kumsifia spouse wako kwa jinsi alivyokurusha vizuri kwenye mahaba na sita kwa sita?
Na je kawaida unapomsifia au ku-appreciate vitu anafanya huwa anajisikiaje?
Hayo maswali ni ya msingi sana mtu kujiuliza hasa kama unataka kujua mke/mume wako kwake maneno matamu ndiyo KUPENDWA
Maneno mazuri au yanayotia moyo au yanayomsifia ambayo ni matamu husababisha mambo yafuatayo kwa mwenzi wako
(a) Huleta upamoja na ukaribu zaidi (intimacy)
(b) Huleta uponyaji kwenye majeraha ya hisia zake kama kuna maumivu moyoni mwake (healing) na kumfariji
(c) Mume wako au mke wako hujisikia kulindwa zaidi na anajisikia yupo katika mikono salama.
Fahamu kwamba wewe ndiye mtu muhimu kuliko mtu yeyote duniani kwake, hivyo maneno unayoongea either yanamjenga au yanambomoa na si kubomoa tu bali na kumuumiza na unampa wakati mgumu. Kwa nini tusibadilike sasa hivi na kuamua kuwa watu wa maneno positive na kufuta kabisa maneno ya amri, ukali, kulaumu, au kuwa mtu wa lawama tu yaani kutaka kila kitu kiwe kama unavyotaka wewe.
Lengo la upendo si kulalamika kwa kile ambacho hupati
bali ni kufanya kile ambacho kitamsaidia yule unayempenda,
yule umechagua uishi naye hadi kifo kitakapowatenganisha.
Mojawapo la hitaji kuu la ndani la mwanadamu ni kuwa appreciated na kile mtu anafanya.
Je umewahi kuwa na boss mkali na mwenye maneno ovyo na mtu wa amri? Huwa unajisikiaje?
Fikiria unaishi na mke au mume wa aina hiyo.
Na kama wewe ni mtu wa ku criticize, kulalamika na kulaumu kila kitu, please jitahidi kubadilika na kuwa mtu wa maneno matamu ili uwe na maisha ya raha ya ndoa yako kwani wewe ndo uliamua kuoa au kuolewa na haipendezi kuwa na ndoa isiyo na mvuto wakati uwezo wa kubadilisha mambo unao.

Jitahidi uwe ni mtu wa maneno ya kutia moyo, maneno ya upole, maneno ya matamu na achana kabisa na maneno ya kulalamika tu kila kitu, au kukaripia tu, au maneno ya ukali kila kitu hadi watoto, mke au mume wanakuogopa hata ukiwepo wanabaki kimya maana kila wanachafanya na kuongea kwako hakifai.

Jizoeshe kumsifia mpenzi wako kwa kila jema analolifanya ama kwa uzuri alokuwa nao, au kwa chakula kizuri unachopika au kazi anavyofanya au jinsi anavyowajibika mkiwa chumbani.
Hapa wanaume tunahitaji kujitahidi zawadi naamini kutokana na mfumo wetu dume wa Kiafrika hata kusema asante au nisamehe au nimekosa inakuwaga kazi, please naomba tubadilike ili ndoa zetu na nyumba zetu ziwe sehemu bora kuishi.

Fanya yafuatayo hii wiki then angalia kama kuna mabadiliko kwa mume au mke wako:
(i) Mwandikie mume au mke wako love letter kwa mkono wako na iache sehemu ambayo ataiona na kitu muhimu mwandikie maneno matamu, ya kusifia, kwa yale yote anafanya.
(ii) Ukiwa na wenzako kama upo naye msifie mbele zao kitu chochote.
(iii) Mpe asante kwa kila kitu hakikisha siku haipiti hajasema asante.
(iv) Msifie mbele ya watoto wako

Naomba Nijibrekishe……… tutaendelea!

2 comments:

Mr Elly 2nyi said...

Kazi njema mzee. Nimeipenda kazi yako naamini itatusaidia hata sisi kina mgendamwene.
Mungu akubariki.

Anonymous said...

Hello Elly, Nashukuru sana kwa maoni yako naamini tutapata muda mzuri wa kujadili mambo haya kwani jamii yatu na hasa in church wengi wanaingia kwa ndoa na wengine wapo kwa ndoa lakini kuna mambo ya msingi ambayo ndo vionjo vya utamu wa ndoa vinakuwa vimewapita mbali. Asante sana kwa maoni yako nakutakia masomo mema na ukipata muda pitia tujadili pamoja.

Lazarus