"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, March 24, 2008

LUGHA SITA MUHIMU ZA HISIA ZA MAPENZI KTK NDOA (lugha ya 4 na 5


4. MGUSO (physical touch)
Kukumbatia, kubusu, kushikana mikono na sex (ktk ndoa) ni njia ya mawasiliano ya hisia za upendo au kupendwa. Watafiti wengi hasa wa maendeleo ya watoto wamethibitisha kwamba kukumbatia, kumbusu na kumshika mtoto kunampa afya njema kihisia.
Kuguswa ni kitu muhimu sana katika mawasiliano ya ndoa hasa linapokuja suala la mahaba, kwa kushikana mikono, kubusu, kukumbatiana na kutekenyana kule kunakonyegesha huleta raha sana kwa mke na mume.
Inawezekana mume wako au mke wako kwake kupendwa ni kukumbatiwa au kupata busu kabla hujaondoka asubuhi na unapokutana naye tena baada ya shughuli za kujenga familia au kutembea mmeshikana naye mikono, pia inawezekana kwako ni jambo gumu na unaona kama ushamba fulani hivi au ulimbukeni, ila fahamu kwamba kila mmoja wetu ana aina ya kujisikia unampenda na ni kitu kidogo lakini kinaweza kufanya ndoa yako kuwa tamu au kuwa chungu.
Kama ni mwanamke unaweza kuwa unatumia muda mwingi sana kupika chakula kitamu, au kununua mizawadi ya gharama kwa ajili yake na lengo ajue unampenda, kumbe yeye kupendwa ni physical touch, inakuwa kama vile unampigia mbuzi gitaa.
Kwa hiyo chunguza mwenzi wako kwake kupendwa ni kufanyiwa nini na kama ni physical touch basi hapa umepatia fanya kweli.
Ktk milango ya mitano Fahamu, kugusa ndo peke yake kunahusisha mwili mzima ingawa kuna sehemu zingine zikiguswa ni balaaa. Kuona tunatumia macho, kusikia tunatumia masikio, lakini kuguswa ni mwili mzima na kitu muhimu katika kuguswa ni kujua unaguswa wapi na unaguswa kwa kutumia nini, je ni mikono au ulimi na ni wapi unaguswa! Kazi kwenu!!
Katika suala zima la physical touch jambo la msingi ni kwamba unatakiwa kugusa pale mume wako au mke wako anapenda umguse siyo kugusa tu, kwani si kweli kwamba sehemu zote ambazo wewe unajisikia raha kuguwa basi na mume wako au mke wako atajisikia raha. pia mwingine anapenda kukumbatiwa kuliko mibusu, na mwingine anapenda sex kuliko kukumbatiwa.
Sex ni physical touch, ndiyo maana kuna wanawake au wanaume bila kumpa sex anaona bado humpendi hata kama utamnunulia gari au kumpeleka vacation Las Vegas.
Mwili ni kwa ajili ya kuguswa,
unaonaje mtu akigoma kukusalimia mikononi?

Naamini utatambua kwamba kuna mushkeli.
Inawezekana mume wako au mke wako kupata mguso wa mwili ni lugha yake ya msingi kuonesha unampenda na anategemea utamgusa mwili wake kila siku kwa kutekenya nywele zake, au kutembea umemshika mkono au kumpa busu na kumkumbatia kila unapoondoka home asubuhi au unaporudi na pia kumpa romance ya uhakika kabla ya sex mkiwa faragha, Fahamu ameacha wazazi wake kuja kwako ili umpe hicho anataka kwa hiyo usituangushe fanya kile mpenzi wako kitampa raha.
HOME WORK KWAKO BAADA YA SOMO:
(i) Jaribu kumshika mkono mnapotembea pamoja
(ii) Unapoondoka asubuhi (amka) hakikisha umempa busu na hug la nguvu likiambatana na maneno matamu yale hujatamka kwa muda mrefu
(iii) Kabla ya kulala omba Mungu pamoja huku mmeshikana mikono
(iv) Pia hakikisha unampa mguso wa uhakika (romance) kabla ya sex mkiwa huko kwenye bustani yenu naamini hiyo chemichemi ya maji itafurika na kiu itapata dawa

5. KUSAIDIANA KAZI AU HUDUMA
Hii ni kufanya vitu ambavyo mke wako au mume wako anatarajia au anategemea ungefanya kuonesha unampenda na kumjali na kuwa wewe ni yeye ni kitu kimoja.

Mume wako au mke wako Fahamu kwamba anajua una hekima kubwa kiasi kwamba unafahamu kwamba ngeweza kumsaidia kufanya kitu Fulani so anasubiri kuona je utafanya kwani umesema unampenda.
Inawezekana anategemea ungemsaidia kutandika kitanda, kusafisha nyumba, kupika, kufua nguo, kumsafisha mtoto, kuosha gari, kufyeka majani nk hiyo mnaweza kufanya pamoja na ni njia nzuri ya kueleza kwamba unampenda kwa vitendo.
Tatizo linakuja kutokana na jamii zetu za kitanzania asilimia kubwa ya familia zetu ni extended, hivyo kwa mfano baba akiamka asubuhi na kuanza kufanya usafi wa nyumba au kupika au kufua nguo za wife nahisi hata majirani wataandamana kuuliza kulikoni kwani yawezekana hapo kwako kuna timu ya watu kutoka kijijini au ndugu zako kama dada, kaka, shemeji, wajomba, baba mdogo, ndugu wa shangazi zako au wafanyakazi ulionao kama house girl, house boy na wale wageni waliokuja kutoka kijijini bila kukupa taarifa nahisi watashangaa.

Point hapa ni wewe kumsaidia mwenzi wako so tumia busara na si kuangalia watu maana ndoa ikiwa moto ni wewe.
Yesu mwenyewe aliosha miguu ya wanafunzi wake kuonesha upendo na hii ilikuwa kuwapa practical expression ya jinsi kupendwa kulivyo.
Katika jami yetu ya Kitanzania kwenye hili eneo wanaume ndo tumekuwa wababe na hatukubali na najua kuna wanaume watasema naongea vitu ovyo lakini ukweli ni kwamba kama mke wako lugha ya msingi kwake ni wewe kumsaidia kazi basi unahitaji kubadilika na kufanya ili kunusuru ndoa yako kwani amekuchagua wewe kwa sababu ni wewe tu hapa duniani unayemfaa. Hata kama utampa zawadi kubwa kubwa au unampa sex ya uhakika kama kwake kupendwa ni wewe kumsaidia kazi bado ataona unamtumia tu na humpendi.
Mbona wakati hujamuoa ulikuwa unaenda kwao kusaidia kazi na ulikuwa unajitoa sana kwa hilo na inawezekana ndo sababu alikubali umuoe sasa yupo ndani humsaidii tena na unalalamika kwamba kitandani amepoa ni baridi! Anza wewe kwanza kwa kumpa kila anataka.

Tutaendelea na somo letu......

1 comment:

Hellen said...

Kwenye maisha ya ndoa ni pembe tatu. Kuna NDOA, FAMILIA na MSALABA. na hakuna ndoa bila msalaba wala hakuna familia bila msalaba. Kama tujuavyo ndoa ni agano na kiungo kikubwa kwa ndoa ni uaminifu. Hosea: 1,2. Na kwa kuwa mwenzi ni mshirika wa mambo yote ni kinyume kama humshirikishi mwenzako wa ndoa mipango uliyonayo, matatizo uliyonayo na furaha ulizonazo. Tusisahau kuwa muwezeshaji wa yote hayo ni KRISTU maana kwake yeye tunapata NGUVU, NEEMA na BARAKA.

Ndoa ni sadaka, na sadaka ni kujitoa kwa ajili ya wengine. Na mafanikio ya ndoa ni Kristu, tusipomuangalia Kristu na kumtegemea yeye basi ndoa zitatushinda.

Familia ni muungano wa mwanaume na mwanamke kwa kuungana kwao wanaweza kupata watoto au wasipate ni mapenzi ya Mungu. Kwa hiyo twajua kuwa familia ni kanisa dogo la nyumbani, familia ni shule ya imani katika matendo.

Watu wa ndoa wanaitwa (maana huo ni wito) si kila mwanamke au mwanaume ni lazima awe kwenye ndoa. Hivyo wanandoa wanaitwa kusihi usafi wa moyo wa ndoa ambao ni uaminifu na kujithamini. Na tunajua kuwa wito wowote unadai matayarisho ya kipekee na matayarisho kwetu wanandoa ni sala na sadaka.

Kwa nini ndoa ni msalaba?
Ndoa inakuwa msalaba pale mmoja asipotimia wajibu wake kwa mwenzake na asipomfanya mwenzake sehemu ya maisha yake. kuna misalaba ya ndani ya ndoa na ya nje ya ndoa.

Misalaba ya ndani ni:-
Kama mwanandoa hatimizi wajibu wake, akiw amvivu, mbinafsi, ana upendeleo, na hata simu za mikononi ni misalaba kama haitumiki vizuri na hasira pia ni msalaba ndani ya ndoa.

Misala ya nje ya ndoa ni:
Wazazi/walezi, ndugu, marafiki, na shughuli azifanyazo mwanandoa maana mwingine anakuwa yuko busy hata hampi mwenzake nafasi. Na ndoa za kikristu zinaonekana msalaba kwa kuwa hakuna talaka kuna mlango mmoja tu wa kuingia na hakuna mlango wa kutoka. Ila kwangu mimi naona ni msalaba mzuri maana tukiubeba vizuri tunavyopaswa basi tutaufikia ufalme wa Mbinguni.