"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, March 25, 2008

LUGHA SITA MUHIMU ZA HISIA ZA MAPENZI KTK NDOA (Sehemu ya mwisho)


6. MUNGU (Christ in me)
Hapo mwanzo Mungu alimuumba mtu, akawaumba mtu mke na mtu mume, kutoka mtu mume akaumba mwanamke (operation ya ubavu). Na kutoka mmoja akatengeneza wawili. Hakuna ambaye anaweza kufanya hivyo isipokuwa ni Mungu peke yake. Then katika ndoa, Mungu akawafanya hao wawili kuwa mmoja na akasema alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganisha, kwani ni Mungu peke yake anayeweza kutengeneza kutoka wawili kuwa mmoja. Alijua hawa wawili wakijua siri za kuridhishana kimapenzi basi ndoa yao itadumu hadi kifo kitakapowatengeanisha. Hapo hakuna swali ni Mungu amesema.

Mungu ni mwanzilishi wa ndoa (author), ndoa ni taasisi ya muda mrefu tangu binadamu anaumbwa na kumekuwa na mabadiliko mengi ya binadamu kiuchumi, kisiasa na kijamii lakini bado asili ya ndoa ipo palepale yaani unapokuwa na uhusiano na Mungu maana yake unaruhusu ndoa yako kuwa imara zaidi.

Kuna mambo makuu mawili ambayo binadamu yeyote inabidi awe makini katika kuamua na hapo unahitaji kuwa genius (akili za tofauti) kwani hapo makosa hayana nafasi
(i) Je baada ya kufa utaenda wapi kutumikia umilele wako
(ii) Mtu utakayeoana naye - uoane na mtu sahihi na maisha yako kuwa ya furaha siku zote au uoane na mtu asiye sahihi uwe kwenye hell (jehanamu ya duniani)
Watu wengi huingia kwenye ndoa wakiwa very lightly, unahitaji kuwa makini kwani ndoa ni zaidi ya makubaliano ni agano (Covenant) kati yako, unayeoana naye na Mungu, na hili agano hudumu hadi kifo kitakapowatenganisha.

Ni pale tu Christ anapokuwa muhimili wa ndoa yako na hapo kila kitu kitakuwa ni furaha amani na upendo unaokupa kuridhika kihisia.

Kwa kuwa Mungu ni mwanzilishi wa ndoa na maana yake pia yeye ni mwanzilishi wa sex, romance, mahaba, mapenzi katika ndoa. Na ndiyo maana alituumba na viungo ambavyo vinatupa raha ya wawili yaani mke na mume wakiwa faragha na si kutupa raha tu bali huvutia hata kwa macho na kuleta ujumbe unaofanya mwili mzima kusisimka na kupata ridhiko la aina yake ni kweli naamini hakuna raha duniani kama raha ya mapenzi.
Mungu ametupa sex kama zawadi kwetu na njia Mojawapo ya kumuabudu yeye kama tunavyofanya ibada zingine kama kuimba na kutoa sadaka. Sex si kwa ajili ya kuzaliana tu bali kutuwezesha Wanandoa kuwa na umoja (oneness, intimacy).
Kama sex ni kazaliana basi Mungu angetuwezesha kupeana mimba hata kwa kusalimiana tu au kwa kuongea tu unatamka na mke anashika mimba, ila alitupa zawadi kuu kwa sababu anatupenda na ni njia ya yeye kutuwezesha kuutambua uumbaji wake.Ametupa hiyo zawadi ili tufurahiane na kupeana raha na zaidi tufurahia kwa kutumia milango mitano ya fahamu yaani Kugusa,
Kuona,
Kuonja,
kusikia na
Kunusa
Kanisa huanzia chumbani hapo ndo kwenye ibada ya kweli tukienda church tunamalizia ibada. Kama chumbani mambo hayaendi vizuri kukutana kwetu church kunakuwa ni unafiki kwani mmoja wetu anakuwa hajaridhishwa kimapenzi ktk ibada kuu kule home ambayo Mungu anaiheshimu pia.

Tunasikia kwamba kuna watu wapo kwenye ndoa zaidi ya miaka 20 lakini mume au mke hajawahi kuona uchi wa mwenzake, Nimesikia kisa kimoja, mwanamke aliwahi kuona kipande cha tako la mumewe siku moja tu, siku ambayo taulo liliteleza na kuanguka na wana watoto 4 na hajawahi kuwa uchi wakafurahi uumbaji wa Mungu.
Mume na mke wote ni mmoja na hakuna raha kama ya kuwa uchi kwa mume na mke chumbani kwenu kwani hiyo ndiyo maana halisi ya Mungu kuwafanya kuwa mwili mmoja kwamba
Mcheze pamoja uchi,
Mlale pamoja uchi,
Muoge pamoja uchi,
pia muifurahie miili yenu pamoja uchi,
Sex ina umuhimu kama kula, chakula, kulala, au kufanya mazoezi. Tatizo ni kwamba jamii zetu zimekuwa na wakati mgumu sana kuongelea masuala ya mapenzi (sex) na matokeo yake ndoa nyingi zimeingia matatizoni.
Ni kweli tunafundishwa kwamba sex kabla ya ndoa ni mbaya na ni kweli ni mbaya kwani kuna raha sana kukutana honeymoon wote hamjui lolote na si kwa sababu ya honeymoon tu bali ni dhambi kabla ya ndoa. Hii imefanya hata Wanandoa wengi waliokulia kanisani kuona kwamba sex ni kitu kibaya na si muhimu katika ndoa, pia kuona kwamba uchi ni kitu kibaya na kitu kichafu kitu ambacho si kweli, hakunakitu muhimu na kisafi kama hivyo viungo tatizo tumfundishwa tangu watoto kuwa huko ni sirini, kunaitwa sirini kwa sababu ndo raha ya duni hapo.
Fahamu umeacha wazazi wako ili kuja kwa huyo mwanaume au mwanamke sababu ya mwili wake na mwili wake ni pamoja na hivyo viungo vyote vya kufanyia mapenzi na kitu cha msingi ni kuridhishana. Pia mmekuwa mmmoja na si wawili tena hivyo furahianeni.
Bila Mungu (Christ in you) bado ndoa itachezewa sana na shetani kuna nguvu moja tu ambayo huweza kurudisha ndoa kwenye asili yake nayo ni maombi.
Kumjua Mungu kusikufanye iwe Tatizo na kuona aibu kufurahia ndoa yako na maisha ya mapenzi kwani Mungu ni mwanzilishi wa romance, sex na wewe kuufurahia mwili wa mke wako au mume wako kwani kama si hivyo basi angetuumba bila viungo vinavyoleta raha ya mapenzi.

Marriage is C3
Commitment
Communication
Christ

2 comments:

Hellen said...

Makuzi yetu ya kiafrika ndio yatufanyayo tuoneane aibu kwa suala la mapenzi hata kama ni mtu na mwenzi wake. Pamoja na hayo kwa kuwa tumekuzwa hivyo utakuta mwanamke anaona haya na hawezi kumuanza mwenzake kwa suala la mapenzi au kama anataka kubadilisha style ya mapenzi maana ataulizwa amejifunza wapi? amefundishwa na nani? na maswali kama hayo. Na sisi waafrika mwanaume ndio kila kitu mwanamke anatumika kama chombo cha starehe tu na wala hana thamani na hilo ndio tatizo kubwa sasa unakuta mwanamke anakuwa hayuko huru kwa mwenzi wake na hii inapelekea watu kutembea nje ya ndoa zao kwa kuwa wanakuwa wamechagua visivyo na kujikuta wako kwenye jehanamu ya dunia na hawajui raha ya ndoa na wanaona ndoa ni mateso tu

Lazarus Mbilinyi said...

Hellen,
Nashukuru sana kwa maoni yako mazuri, ni kweli malezi yatu na utamaduni wetu kiafrika umesababisha wakati mwingine kutengeneza ukuta kuzuia kuingia kwenye raha yenyewe ya ndoa, kitu cha msingi kila kila mwana ndoa kuamua kuwa wazi na kubadilika na haina haja kuulizana hiki mwenzangu umepata wapi au ulijifunza wapi kwani lengo liwe kuimarisha ndoa zetu.
Utafiti unaonesha kwamba wana ndoa wengi wanaotoka nje, huko nje wanakoenda wanakuwa huru sana kufanya yale ambayo hawafanyi na wake zao au waume zao vyumbani mwao, Kwa hiyo tunahitaji wanawake kwa wanaume kubadilika sasa ni information society so mtu unajifunza mahali popote si lazima uwe ulifanya na mtu na lengo ni kuimarisha ndoa zetu.