"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, March 27, 2008

Mafundisho kabla ya ndoa ni Muhimu

Nimepata mchango wa maswali na maelezo kwa email kutoka kwa dada Loveness (Chuo Kikuu cha Tumaini) ambaye naamini si muda mrefu na yeye ataingia kwenye ndoa. Naamini pia kila mmoja wetu anaweza kuwa na mchango wake kuchangia jibu la maswali ktk maoni yake.

Dada Loveness anasema:

"Sijui kama nitakuwa napatia au la. Umesema kuwa swala la kujamiiana(sex) mume na mke ni jambo ambalo vijana au wanandoa wengi ambao wapokanisani au walikulia kanisani wanaona kuwa ni kibaya hasa kutokana na ukweli kwamba sex kbal ya ndoa ni kitu kibaya na hujikuta hawana uzoefu wa mafundisho yanayowawezesha kuwa wana ndoa wazuri kwenye suala zima la mapenzi.Mimi nafikiri pia sio tu kwamba hilo limechangia pia hata jinsi ya kuanza tendo hilo,yaani siku ya kwanza mtu anapoanza kushirikitendo hilo anakutana na nini! hasa hapa nazungumzia binti, kwa sababu unakuta kijana hajapata mafundisho ya
kutosha kuhusu jambo hilo,na unakuta kwa sababu anakuwa na shauku na mwenzake anaweza akasababisha matatizo kwa yule binti kama maumivu n.k.
Sasa huoni kwamaba inakuwa ni sababu ya huyo binti kuona tendohilo kuwa ni baya?Na mara nyingi nakumbuka wale dada zetu walio kwenye ndoa na waliopitia haneymoon huwa wanatuambiaga kuwa nyie msifurahie kwenda honey moon huko kuna kuumwa(yaani maumivu).
Mimi binafsi imekuwa ikinisumbua pia kila nikifikiria juu ya hilo kama kweli ndo hali ni hiyo basi napata mawazo kwamba huko haneymoon nitaumizwa na matokeo yake nakuwa.
So huoni kuwa kweli vijana wa kiume wanaokwenda kufunga ndoa wanahitajimafundisha ya hali ya juu?"
Swali je tuwasaidie vipi vijana wetu ambao hawapati mafundisho mengi juu ya ndoa na pia suala zima la tendo la ndoa?

3 comments:

Anonymous said...

Nakupongeza dada lovelyness kwa mchango mzuri na ni kweli kwani kama kitu kinaongelewa ni muhimu jamii kuchukua hatua za msingi.

Ogonvi mwingi na watu kuto ona umuhimu wa ndoa nafikiri moja ya sababu inaweza kuwa ni hii.Lakini toka wajuane na kuanza uchumba na wanajua wataoana kwanini wasizungumzie mambo ya msingi moja wapo likiwa ni hili.Wanapiga porojo za maisha na kusahau kile kilicho wafanya wawe pamoja. Pengine ukimya na woga wa mabinti nao unachangia kwa kiasi chake!
Nakubaliana kuwa wanaume hatuja funzwa vizuri na jamii haioni umuhimu wa kuwafundisha vijana wakiume juu ya hili,lakini naamini wanaume ni wasikivu hasa kwa wale wanao wazunguka mmoja wapo akiwa ni yule anayetegemewa kuolewa.mimi nafikiri wasichana nao waache aibu kuwaambie ukweli wachumba wao hata kama hawajaoana. wasiogope kuachwa kwa kuzungumza mambo ya msingi kama haya,na kama yupo kijana wa kiume atakaye mwacha binti kwa sababu ameelekezwa kitu kama hiki basi sidhani kama angekuwa mume mwema.
Lakini pia ukimya uliopo makanisani juu ya suala hili unatakiwa ufutwe na watu waone ni jambo la kawaida. mwisho naomba wachumba waache kuoneana aibu kama inawezekana zungumzeni haya pia ,najua mwanzoni itakuwa vigumu lakini baadaye mtafurahia matunda.
Kumbuka kuwa binadamu yoyote anajali sana kile akipendacho ,hivyo si rahisi sana kukifanyia ubaya kwa makusudi.
Mungu awabariki.
Elly
INI Algiers

Lazarus Mbilinyi said...

Nashukuru sana Bwana Elly,

Ni kweli vijana makanisani tunatakiwa kuwa wawazi na wenye malengo kuzungumza kitu sahihi kwa wakati sahihi na kutoa maamuzi sahihi, kwanza lazima kama ni kijana wa kiume unayetaka kuoa ktk hatua yako ya uchumba lazima uwe makini kuhakikisha unafahamu mambo ya msingi kabla ya kukabithiwa mke kwani wakati wa uchumba wengi hujisahahu hasa kutokana na utamu wa kupendwa matokeo yake unaanza kzungumza na mchumba wako habari za kupendana na kama kusifiana, zawadi nk ni vizuri kusifiana na kupeana zawadi lakini hapa ufahamu kitu cha msingi ni kumchunguza mtu ili ujue detail zake na wakati huohuo kupata mafundisho sahhihi ya nini kifanyike honeymoon na hata baada ya harusi mnapoanza maisha na tunaomba vijana wenye uzoefu makanisani wawafundishe vijana wenzao ambao wanahitaji mafundisho na zaidi sana kushirikiana nao.

Mr. Elly Twivulunge said...

Thanks Mr mbilinyi kwa maoni mazuri.Japo sijawahi fika huko honeymoon na sinampango wa kwenda huko karibuni kwa kutokuwa na nauli yakutosha ,naomba ungewaandalia walau kakurasa kamoja kwa ajili yao walio tayari kwenda huko mwezini kama pocket money wakiwa huko. Hata wasio tayari watafurahia kuyajua ili wakati ukifika wasichanganyikiwe kwa kukosa msaada. Nafikiri itakuwa rahisi mtu kusoma akiwa pekeyake kwenye blog hii kuliko akikalishwa chini aambiwe na mtu kwani hata yule atakaye mfundisha kwa kuona aibu anaweza asimwambie yote. Hivo naamini kama kuna mtu anajua gharama za matumizi ya kawaida huko
honeymoon basi asisite kutuletea hapa the hill of wealth ili watu warudi wakicheka na sio wakilia kama ndugu yetu anavyo twambia.

Kazi njema Mr Mbilinyi.