"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, March 27, 2008

Pembe za Ndoa

Asante sana Dada Hellen kwa mchango wako ufuatao:
Kwenye maisha ya ndoa ni pembe tatu. Kuna NDOA, FAMILIA na MSALABA. Na hakuna ndoa bila msalaba wala hakuna familia bila msalaba. Kama tujuavyo ndoa ni agano na kiungo kikubwa kwa ndoa ni uaminifu. Hosea: 1,2. Na kwa kuwa mwenzi ni mshirika wa mambo yote ni kinyume kama humshirikishi mwenzako wa ndoa mipango uliyonayo, matatizo uliyonayo na furaha ulizonazo.
Tusisahau kuwa muwezeshaji wa yote hayo ni KRISTU maana kwake yeye tunapata NGUVU, NEEMA na BARAKA.Ndoa ni sadaka, na sadaka ni kujitoa kwa ajili ya wengine.
Na mafanikio ya ndoa ni Kristu, tusipomuangalia Kristu na kumtegemea yeye basi ndoa zitatushinda.
Familia ni muungano wa mwanaume na mwanamke kwa kuungana kwao wanaweza kupata watoto au wasipate ni mapenzi ya Mungu.
Kwa hiyo twajua kuwa familia ni kanisa dogo la nyumbani, familia ni shule ya imani katika matendo.Watu wa ndoa wanaitwa (maana huo ni wito) si kila mwanamke au mwanaume ni lazima awe kwenye ndoa. Hivyo wanandoa wanaitwa kusihi usafi wa moyo wa ndoa ambao ni uaminifu na kujithamini.
Na tunajua kuwa wito wowote unadai matayarisho ya kipekee na matayarisho kwetu wanandoa ni sala na sadaka.
Kwa nini ndoa ni msalaba?Ndoa inakuwa msalaba pale mmoja asipotimia wajibu wake kwa mwenzake na asipomfanya mwenzake sehemu ya maisha yake. Kuna misalaba ya ndani ya ndoa na ya nje ya ndoa.
Misalaba ya ndani ni:-Kama mwanandoa hatimizi wajibu wake, akiw amvivu, mbinafsi, ana upendeleo, na hata simu za mikononi ni misalaba kama haitumiki vizuri na hasira pia ni msalaba ndani ya ndoa.
Misalaba ya nje ya ndoa ni:Wazazi/walezi, ndugu, marafiki, na shughuli azifanyazo mwanandoa maana mwingine anakuwa yuko busy hata hampi mwenzake nafasi.
Na ndoa za kikristu zinaonekana msalaba kwa kuwa hakuna talaka kuna mlango mmoja tu wa kuingia na hakuna mlango wa kutoka.
Ila kwangu mimi naona ni msalaba mzuri maana tukiubeba vizuri tunavyopaswa basi tutaufikia ufalme wa Mbinguni.

No comments: