"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, March 20, 2008

Tofauti ya mwanaume na mwanamke katika maumbile

Mwanaume na mwanamke wanatofauti kubwa katika maumbile, na kufahamu tofauti iliyopo kati ya mwanaume na mwanamke huwezesha pande mbili hizi kuchukuliana na kufahamiana vizuri ili kukamilisha maisha yetu hasa katika suala zima la mahusiano.

Kuna tofauti kubwa sana kati ya mwanaume na mwanamke katika mambo yafuatayo:-
(i) Katika kila seli ya mwanaume na mwanamke kuna tofauti. Tofauti yake (chromosomes) ndiyo husababisha kufanyika kwa mwanaume na mwanamke.
(ii) Imethibitika kwamba Mwanamke anaweza kuishi miaka mingi zaidi kuliko mwanaume [wenye umri mmoja] kwa miaka mitatu hadi minne.
(iii) Mwitikio wa mapenzi (sex) kwa mwanaume ni wa haraka zaidi kuliko mwanamke. Mwanaume huweza kusisimka kwa kuona tu uzuri wa mwanamke wakati mwanamke huathirika zaidi kimapenzi kwa kuguswa na kusikia yale anayosikia kutoka kwa mwanaume. (ndiyo maana wanawake wengi ni waathirika wa kudanganywa na wanaume kwani wapo innocent kuamini kile anaambiwa na wanaume ni mafundi wa kupanga maneno hata ya uongo)
(iv) Kuna tofauti kubwa sana ya maungo (skeleton) kwani kidole cha kwanza cha mwanamke ni kirefu kuliko kidole cha tatu na kwa mwanaume ni kinyume chake.
(v) Mwanamke ana tumbo kubwa, figo kubwa, maini makubwa na mapafu madogo na kwa mwanaume ni kinyume chake. je kuwa na mapafu madogo husababisha wanawake kuchoka haraka?
(vi) Kuna mambo matatu muhimu ambayo yanapatikana kwa mwanamke na hayapatikani kwa mwanaume nayo ni Kupata siku za mwezi, kubeba mimba na Kunyonyesha. Hapa ndipo kwenye siri kubwa ya hisia na saikolojia ya mwanamke.
(vii) Kawaida damu ya mwanamke katika mwili ina maji zaidi kuliko mwanaume na damu yake ina upungufu wa asilimia 20 ya seli nyekundu ambazo husafirisha oxygen sehemu zote za mwili, maana yake mwanamke anakuwa na oxygen kidogo katika mwili kuliko mwanaume ndiyo maana wanawake huweza kuzimia kirahisi na kuchoka.
(viii) Moyo wa mwanamke hupiga haraka zaidi ya mara 80 kwa dakika wakati mwanaume ni mara 72 ingawa mwanamke Blood pressure yake ipo chini kuliko mwanaume na pia mwanamke anauwezo wa kupata high blood pressure kuliko mwanaume.
(ix) Mwanamke hupumua kidogo zaidi kuliko mwanaume
(x) Mwanamke anaweza kuhimili hali ya joto kuliko mwanaume.

Naamini tukifahamu tofauti zetu kimaumbile ndipo tutaweza kuishi pamoja katika ukamilifu wa kuchukuliana na kusaidiana hasa kwa wale waliom katika ndoa.

No comments: