"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, March 31, 2008

Uchumba 3


Kabla ya Kuvishana Hako Kapete Kazuri

Hakikisha Umejiuliza Maswali ya Msingi Kwanza
3. JE, KUPENDA KWAKE KUPOJE?
Binadamu wote tumezaliwa tunahitaji kupendwa uwe mtoto, kijana au mzee wote tunahitaji kupendwa uwe tajiri au maskini wote tunahitaji upendo.

Wote tuna asili ya kupendwa na kupendwa ni kutamu, hasa unapoanza kupendwa na mtu ambaye unataka awe na wewe maisha yako yote.

Katika kutafuta mtu wa kuishi na wewe hadi kifo kitakapowatenganisha ni muhimu sana kujiuliza;

Jiulize, Je ni mtu wa kutaka kupendwa tuuu?

Je analalamika sana kwamba hujampigia simu, wakati na yeye ana simu na hakukupigia? Je analalamika sana kwamba wewe hujamtumia email

wakati na yeye email anayo ila hajakutumia?

Je analalamika sana kwamba Mbona hujampelekea zawadi

wakati na yeye hajakuletea zawadi?

Je analalamika kwamba hukumtafuta wakati na yeye mwenyewe wala hakukutafuta,

kujua nini kimetokea kwako?

Je ni mtu wa ku-criticise kila kitu, kulalamika, Kunung’unika?

Ndoa hujengwa kwa kila mmoja kutoa upendo zaidi kuliko kupokea, candidate mzuri wa ndoa ni yule ambaye yeye anakuwa amejiajiri kukupenda tu yaani kutoa upendo kwako bila kujali umefanya nini, anajua wajibu wake ni kutoa upendo kwako siku zote.


Na wote mkiwa hivyo Mbona mambo yanakuwa safi sana!

Ndoa si 50/50 yaani wewe ukinipigia simu basi lazima na wewe unipigie, mimi nikikupa zawadi lazima na wewe unipe zawadi, mimi nikifanya hiki na wewe lazima ufanye kile, siyo hivyo.


Ndoa ni 100/100 yaani unafanya tu bila kutegemea upande mwingine utafanya nini, na ikiwa hivyo automatically na upande mwingine nao utaanza kufanya kwani ni tabia ya upendo kwamba huwezesha kubadilisha hali.

4. JE, UMEKUBALI?
Katika process nzima ya kutafuta mchumba, kuna umuhimu kufahamu kwamba hakuna aliye mkamilifu yaani ukapata kijana wa kiume au wa kike aliye mia kwa mia sawa au sahihi kila kitu unachotaka, huyo atakuwa malaika na utakuwa umepata neema ya ajabu.

Kabla ya Final Decision lazima ujue mambo mazuri na mabaya kuhusu yeye, tabia nzuri na tabia mbaya kuhusu yeye, positive and negative sides kuhusu yeye.

Jiulize je, unaweza kuishi kwa kuvumilia udhaifu wake, mabaya yake unayoyaona au negative sides alizonazo? Je ni wewe tu unayejihisi ndo utaweza kumchukulia udhaifu wake wote.

Je umeridhika na tabia yake ya ubahiri?

Ukali, Kuongea sana kama radio za FM,

Uvivu, Hasira, Ubabe, Ukimya, Kupenda kuongea na watu hata wasiomhusu,

Dharau, Wivu, Kujisikia, kujiona,

Kutokujipenda, Kutojali muda, Uzembe nk
Je umeridhika na kiwango chake cha elimu, kiwango chake cha kiroho, kiwango chake cha ufahamu wa mambo ya uchumi, jamii, dini siasa nk.


Usiseme nitambadilisha baada ya kumuoa, kwa Taarifa yako wewe ndo utabadilika.

5. JE, UMEMUOMBA MUNGU?
Tuna muhitaji Mungu ktk kutoa maamuzi muhimu ktk maisha yetu (important decisions in life) kama kuoa.

Jiulize kama umemuomba Mungu na kuthibitisha kwamba:-


Huu ni wakati wake au wakati sahihi,

Ni mtu sahihi,

Na ni mapenzi ya Mungu.

Mungu anatupenda sana na ana mpango na maisha yetu wakati mwingine tumejichukulia maamuzi bila kumshirikisha Mungu,


Pia Mungu wakati mwingine hutumia watu, Neno lake, mahubiri, radio, TV au watumishi wa Mungu, rafiki zetu, wazazi au mtu yeyote kutuonya hasa kama mtu unayetaka kuoana naye kwako hafai.


Tumeona pia vijana wengi ambao wameweka shingo ngumu na kuendelea na process hadi wakaoana na matokeo yake ndoa zimekuwa mzigo mzito badala ya raha na faraja.Hivyo najua Unamuomba Mungu sana kwa ajili ya hili pia omba Mungu akupe uhakika kwani Mungu akiunganisha hakuna binadamu anayeweza kutenganisha.


Kama una swali unaweza kuuliza au unataka kuchangia unaweza kutuma maoni yako.


Unakaribishwa! ...................................................No comments: