"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, March 21, 2008

UPENDOUpendo (mapenzi, Kupenda, Love) Ndiyo neno muhimu kuliko maneno yote tuliyonayo katika maisha yetu ya kila siku. Pia ni neno linalotuchanganya sana(confusing), hata kutamani ardhi ipasuke mtu uingia na kuishia.
Kwa watu wote wenye dini na wasio na dini wote tunakubaliana kwamba neno Upendo ni kiungo muhimu sana cha maisha ya mwanadamu.
Pia Bwana Yesu aliagiza kwamba wote wanaomfuata yeye hawana budi kuwa na Upendo kwa kuwa Mungu mwenyewe ni Upendo na hii ndiyo itakuwa tofauti kwao kuonesha ni wafuasi wake halisi.
Paulo Mtume hodari katika Agano jipya anaelezea kwamba katika tabia za msingi wa binadamu yaani Imani, tumaini na Upendo bado Upendo ni namba moja.
Wanasaikolojia wamehitimisha kwamba kupendwa ni hitaji kuu la kwanza la msingi katika maisha ya kihisia (emotions) kwa binadamu yeyote.

Kwa Upendo na Kupenda na mapenzi tunapanda milima, tunavuka bahari hadi bahari, jangwa hadi jangwa, taifa hadi taifa, tunajenga majumba na kununua magari kwa ajili ya wale tunaowapenda pia tunapita katika mambo magumu kwa sababu ya Upendo. Kwa Upendo watu wamekufa na wengine kufanya vitu ambavyo wengine tunawashangaa na kuona akili zao zimewaruka, bado jibu ni Upendo

Upendo ulikuwepo, upo na utakuwepo, utamu wake na machungu yake bado yanatukumba wanadamu na kutupa uzoefu wa maisha kwa njia tofauti.

Wanasaikolojia wamehitimisha kwamba tangu mtoto anapozaliwa anakuwa na nafasi tupu (empty) kwa ajili ya kujaza Upendo na Upendo unavyozidi kujaa katika hiyo nafasi ndipo katika kukua kwake anakuwa imara kihisia (emotionally) na bila kupendwa ataathirika, Angalia watu ambao walikosa Upendo tangu wadogo kutoka jamii waliyozaliwa then utaona tofauti.

Katika moyo wa mwanadamu kuna nafasi hiyo tupu ya hisia (emotional tank, or hole) na kuna hitaji kuu la kupendwa (intimate and to be loved) na mtu mwingine wa jinsi tofauti, Ndoa iliwekwa maalumu kwa ajili ya kukamilisha hilo hitaji.
Kila binadamu bila kujalisha ni maskini, au tajiri, mweusi au mweupe, wa mjini au kijijini mtoto au mzee au kijana wote tunahitaji kuu la kupendwa, kupendwa ni kutamu, ni raha ni kuzuri ni yote katika yote.

Kama umeoa au kuolewa basi fahamu kwamba mwenzi wako (spouse) anahitaji upendo wako, anakuhitaji wewe, kwa hiyo jitahidi kumpenda na kuwa na muda na yeye kuhakikisha hiyo nafasi tupu ya hisia inajaa siku zote (emotional hole or tank is full)

Hapo katika kujaza na kutojaza hiyo nafasi ndipo kwenye matatizo na migogoro ya watu kuanza kutamka kwamba “Naona siku hizi hanipendi” na hapo ndipo kwenye siri kubwa ya nini hutokea baada ya watu kuoana.
Tutaendelea na hatua inayofuata kuelekea kwenye utamu wenyewe………
SES by DegreeAdvantage.com marketing team.

No comments: