"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, April 30, 2008

Maumivu wakati wa tendo la ndoa - mwisho

Kila mwanamke kwenye uke wake kuna kiwango muhimu cha bacteria, fungus, yeast au protozoa na hawa viumbe hawana madhara yoyote katika mwili hadi hapo kiwango chake kikiathirika na mazingira yake kama matumizi ya antibiotics, kuwa na medication au madawa na uzazi wa mpango na ndipo matatizo hutokea na kupata haya matatizo si kuwa unaumwa magonjwa ya zinaa ni hali ya kawaida kitu muhimu lazima uhakikisha unapata dawa.Leo tumalizie na mambo yanayosababisha kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa kwa mwanamke.
Maambukizo (vaginal infection)
Mwanamke anaweza kupata maambukizi kutokana na bacteria, fungus, yeast na amoeba.
Kawaida kwenye sehemu za siri za mwanamke kuna kiasi kikubwa cha bacteria, fungus, yeast au amoeba ambao hawana madhara yoyote hadi pale uwiano ukiwa tofauti kutokana na sababu mbalimbali kama vile madawa nk
Maambukizi (infections) yanapotokea kawaida kunakuwa na mabadiliko yafuatayo
Kubadilika rangi kwa majimaji yanayotoka sehemu za siri za mwanamke,
Pia kutoa harufu mbaya baada ya tendo la ndoa,
Kuvimba sehemu za siri,
Kusikia maumivu wakati wa haja ndogo,
Kuumia wakati wa tendo la ndoa (maumivu ya kama kuchoma na kuwasha).

Menopause
Upo wakati mwanamke anafikia (miaka 48 - 52) muda ambao hawezi kuzalisha tena homoni za estrogen zinazosababisha kuzalishwa kwa yai kila mwezi.
Kutokuwepo kwa hii homoni husababisha uke wake kuwa mkavu hata wakati wa tendo la ndoa.
Uke kuwa mkavu husababisha kujisikia maumivu wakati wa tendo la ndoa na hasa kama hakuandliwa vizuri.
Zipo sababu zingine kama vile hitilafu katika maumbile ya uke kutokana na operation au kubakwa n.k husababisha mwanamke kujisikia maumivu wakati wa tendo la ndoa.
Je wanaume nao hupata maumivu wakati wa tendo la ndoa?
Ni kweli inawezekana kwa mwanaume kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa ikiwa
Amepata maambukizi ya bacteria, fungus au yeast kutoka kwa partner wake
Kama ameambukizwa magonjwa ya zinaaa
Kama hajatahiriwa na hasa kama ndo anaanza kufanya tendo la ndoa atajisikia maumivu kwa sababu ya gozi (foreskin) kugoma kujivuta nyuma.

Maumivu wakati wa tendo la ndoa -3-

Katika utafiti uliofanywa na kituo cha kuthibiti magonjwa ya zinaa huko Chicago (CDC) Marekani na kutangazwa rasmi kwenye vyombo vya habari tarehe 11/03/2008, inakisiwa kwamba asilimia 26 ya mabinti wenye umri wa miaka 14-19 nchini Marekani wameambukizwa moja ya magonjwa ya zinaa.
Pia kwa mabinti wa kimarekani weusi hali ni mbaya zaidi.
Je, hii inakupa picha gani katika usalama wa afya ya uzazi?
Suala la kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa linasababishwa pia na magonjwa ya zinaa au kwa kimombo Sexual transimitted diseases or infections (STDs & STIs)

Haya ni magonjwa yanayoweza kuambukizwa kwa kufanya mapenzi na mtu ambaye ameathirika tayari na magonjwa ya zinaa.

Je nitajuaje nimeambukizwa magonjwa ya zinaa?
Kama ni mwanamke angalia dalili zifuatazo.
Majimaji ya ukeni ambayo yana harufu isiyo ya kawaida na yenye rangi tofauti na wingi kuliko ilivyo kawaida.
Maumivu au kusikia kama unachomeka au mwasho wakati wa kwenda haja ndogo.
Maumivu na mwasho katika maeneo ya uke.
Maumivu ya ukeni wakati wa tendo la ndoa
Vidonda na malengelenge katika eneo la uke.

Kama ni mwanaume dalili zifuatazo.
Majimaji kutoka uumeni ambayo yana harufu isiyo ya kawaida, au yakiwa mengi.
Kuhisi mwasho ndani ya uume, wakati na baada tu ya kwenda haja ndogo
Vijidonda na sugu ama malengelenge juu au katika sehemu za kiume.
Vipele au uvimbe katika sehemu za siri.
Je, kuna ukweli wowote mwingine kuhusu magonjwa ya zinaa?
Kuambukizwa magonjwa ya zinaa hakumaanishi una wapenzi wengi; ingawa kuwa na wapenzi wengi ndiyo chanzo cha magonjwa ya zinaa, hivyo wana ndoa inabidi kuwa makini kuhusu hilo.
Pia haya magonjwa hakiachwa kutibiwa si kwamba yataleta maumivu wakati wa tendo la ndoa tu, bali pia husababisha madhara ya kudumu kwa afya yako na wakati mwingine kusababisha ugumba au utasa.
Je ni magonjwa yapi ya zinaa ni ya kawaida ukiacha UKIMIWI?
Chlamydia
Husababishwa na viini vya bacteria na waweza kuathiri uke, mrija wa kupitisha mkojo, uume au sehemu ya kupitishia haja kubwa.

Dalili:
Kwa wanawake
Dalili hazionekani kwa urahisi.
Ubaya ni kuwa ugonjwa huo unaweza kuathiri fallopian tubes – yaani mirija ya kupitia mayai kutoka kwa ovari hadi kwenye nyumba ya uzazi hivyo basi kusababisha utasa.
Wakati mwengine dalili hii unaweza kuiona - kutokwa na majimaji ya ukeni yasiyo ya kawaida na kuhisi maumivu wakati wa kukojoa.

Kwa wanaume
Ugonjwa huu huathiri mrija wa kupitishia mkojo, uzuri ni kwamba dalili huonekana wazi, kama vile uume kutokwa na ute na kusikia maumivu wakati wa kukojoa.

Matibabu:
Ni pamoja na kufanyiwa uchunguzi wa mkojo au damu.
Unapotambuliwa daktari hupendekzeza dawa maalum ya kumeza.
Kama umefanya mapenzi hivi karibuni basi yafaa mke au mume wako naye aarifiwe ili nae atibiwe pia.

Kisonono (Gonorrhoea)

Dalili:
Wanawake
Hutokwa na ute mwingi wa njano au kijani kutoka ukeni na kusikia maumivu wakati wa kukojoa.

Kwa wanaume
Uume uliathirika hutoa ute wa njano au kijani, na kupata maumivu wakati wa kukojoa.
Pia kuna uwezekano wa kuwashwa ama kutokwa na maji maji katika sehemu ya kupitishia haja kubwa.
Ingawa baadhi ya watu huwa hawaoni dalili zozote kabisa lakini bado wanaweza kuwambukiza wanaofanya mapenzi nao.
Matibabu:
Iwapo matibabu hayatapatikana kwa haraka kuna hatari ya mirija ya kupitisha mayai (fallopian tubes) kuharibika na hivyo kusababisha utasa.
Kama una kisonono usifanye tena mapenzi hadi utakapofanyiwa uchunguzi na kupewa madawa ya kutibu ugonjwa.
Ni muhimu sana kumfahamisha mpenzio ili nae pia atibiwe.

Herpes
Huu husababishwa na aina fulani ya kirusi, kama kile kinachosababisha mafua na vidonda vya mdomoni.
Mbali na kusambazwa kupitia ngono pia husambazwa kupitia kufanya mapenzi ya kunyonyana sehemu za siri.

Dalili:
Ni Kupata vidonda ukeni au uumeni mfano wa vile vinavyotokea mdomoni wakati wa homa kali ya mafua.

Matibabu:
Sasa kuna dawa na krimu za kupambana na virusi hivi.
Lakini kumbuka hata unapotibiwa virusi vya herpes bado hubaki mwilini mwako na vinaweza kuzusha tena vindonda.
Pia kama umja mzito unaweza kumwambukiza mtoto wako, hivyo basi kama una vijidonda ni vyema kumjulisha mkunga wako ama daktari ili upate matibabu yafaayo.

NSU (Non-specific urethritis)
Ni herufi zinazotumiwa kuelezea magonjwa ya bacteria yanayoathiri mfereji wa kupitisha mkojo yaani urethra.
Magonjwa hayo husambazwa kwa kupitia kufanya mapenzi.
Dalili:
Kwa wanaume dalili kubwa ni kutokwa na ute, kutoka kwenye tundu ya uume na huenda akahisi maumivu wakati wa kukojoa.
Huenda ukasikia maumivu au kuwashwa-washwa.

Matibabu:
Majimaji yakitoka kwenye uume, isipokuwa mkojo au manii, ni lazima uchunguzwe na daktari, au nesi katika kliniki ya afya ya uzazi.
Unaweza kutibiwa kwa kutumia vidonge vya anti biotics

Kaswende (Syphilis)
Ugonjwa huu nao husababishwa na bacteria Treponema Pallidum
Dalili zake hazionekani kwa urahisi.
Huenda ukaanza kwa kijidonda au kipele kwenye uke au uume au sehemu ya kupitishia haja kubwa.
Kidonda hiki kinapopona usidhani ndio mwisho wa maambukizo la! Viini hivyo vinaweza kubaki mwilini kimya kimya kwa miaka mingi!

Matibabu:
Ni bora daktari kufanya uchunguzi wa damu kwani majimaji ya ukeni au uumeni huenda uchunguzi wake usionyeshe viini vya kaswende.
Kaswende ni hatari, kama haitibiwi, inaweza kusababisha utasa au ugumba, na hata kuathiri moyo, mishipa ya damu, ngozi ya mwili, mifupa na hata ubongo na kurukwa na akili.
Hata hivyo matibabu yake ni rahisi – Zipo dawa aina (antibiotics) zinazoweza kutibu kaswende kabisa.
Ili kuzuia kuenea kwa maradhi hayo ni vyema mpenzio nae pia atibiwe.
Tutaendelea na somo letu
WWWWWWWWWWWWWWWWWWWWWWWWWWWWWWW

Tuesday, April 29, 2008

Maumivu wakati wa tendo la ndoa - 2-

Kichwani (brain & mind) ndiyo kiungo kikubwa cha tendo la ndoa, jinsi unavyojiweka kwenye akili zako inaweza kusababisha raha au maumivu ya tendo la ndoa(Picha kwa hisani ya clearingfiles)

Kwa nini ujisikie maumivu.

Maumivu wakati wa tendo la ndoa husababishwa au hutokana na sababu za kihisia na za pia (physical and emotional)
Ili kujua kwa nini maumivu kutokea ni vizuri kujua nini hutokea kwa mwili wa mwanamke wakati wa tendo la ndoa (sex)
Mwili wa mwanamke hupitia hatua nne (4) muhimu kukamilisha tendo la ndoa.

HAMU (dedire)
Hapa mwanamke hujisikia anataka kufanya tendo la ndoa


KUSISIMKA (arousal)
Hapa mwili husisimka kwa sehemu zake za siri (vagina) hutanuka urefu na upana pia hutoa majimaji yanayorahisisha mwanaume kuingia (penis penetration), kisimi hudinda na kuongezeka ukubwa, chuchu husimama na kusisimka, uterus hupanda juu nk


KUFIKA KILELENI (orgasm)
Hapa ni kilele cha mwitikio wa tendo la ndoa, misuli hujikusanya (contradict) na kumpa hisia kubwa za raha na utamu wa tendo lenyewe.


SULUHISHO (resolution)
Viungo vyote vinavyohusika na tendo la ndoa hurudi kwenye hali ya kawaida

Aina za maumivu na sehemu wakati wa tendo la ndoa kwa mwanamke zinaweza kutokea kwenye katika sehemu zifuatazo

Sehemu ya nje ya vagina, yaani vulva na huumia wakati inaguswa au kuwasha hata unapotumia baadhi ya sabuni na wakati mwingine kusababisha makovu au utando unaonesha kuna cheese.

sehemu ya tundu la kuingia kwenye vagina na sehemu ya ndani ya Vagina unayoungan na uterus.

Je ni kawaida mwanamke kupata maumivu hata kama hajaambukizwa magonjwa ya zinaa?
Kawaida kila mwanamke ana aina ya chachu au hamila (yeast) kwenye sehemu za siri zake za siri, na hii yeast ikiongezeka sana inaweza kusababisha kuwasha au maumivu wakati wa kukojoa mkojo wa kawaida na pia husababisha kutoa majimaji meupe mithili ya maziwa na hii hutokea kama mwanamke anatumia antibiotics au medication inayosababisha kuua bacteria wanaofanya hiyo yeast kutoleta madhala yoyote.

Hivyo ni jambo la kawaida kwa mwanamke kujisikia maumivu mara chache wakati wa tendo la ndoa ingawa maumivu yakizidi inabidi uchukue hatua inayotakiwa ili kupata tiba kamili.

Vitu gani vinavyosababisha kuumia wakati wa tendo la ndoa?


Kukaza kwa misuli ya vagina (Vaginismus)

(tamka vaj-uh-niz-muh s)

Ni kukaza kwa misuli ya vagina bila hiari (involuntary) na kusababisha tendo la ndoa kuwa gumu au kutofanyika kabisa.

Mwanamke mwenyewe anaweza asijue kwamba misuli inayozunguka vagina umekaza na kusababisha maumivu wakati mwanaume anaingiza penis.
Hii hali hutokana na hofu na mashaka aliyonayo mwanamke kuhusiana na suala la tendo la ndoa kwamba anaweza kuumia (kisaikolojia).
Pia wanawake wengi wenye vaginismus hawajawahi pata furaha ya tendo la ndoa maishani mwao na wengi ni waoga sana hata kwenda kwa madaktari kuhofia daktari anaweza kuchokonoa vagina zao hivyo kuongeza tatizo zaidi.

Ni nini husababisha hiyo hofu na mashaka?
Malezi aliyofundishwa kwamba tendo la ndoa ni chafu na baya na dhambia na hata akiolewa anafahamu kwamba tendo la ndoa ni chafu na baya.
Malezi aliyolelewa kwa kuambiwa kwamba vagina ni nyembamba sana na hivyo tendo la ndoa husababisha mwanamke kuumia.
Kama amewahi kudhalilishwa kimapenzi kama kubakwa anaweza kuwa na hofu na tendo la ndoa kwa sababu aliumizwa.
Kama amewahi kupata magonjwa ya zinaa yaliyokuwa yanamuumiza sana na kumpa shida pia anaweza kuwa anahisia za kuumia wakati wa tendo la ndoa.
Wanawake wengi wa aina hii hupata raha sana wakati wa foreplay na utamu wa mahaba huwaisha pale tu penetration ikianza.

Kitu cha msingi ni kwamba ili tendo la ndoa liwe tamu na zuri hali ya akili na ubongo ni muhimu sana kwani hisia zote za utamu wa tendo hutafsiriwa kwenye ubongo na ubongo ukipata pollution ya mawazo mabaya basi kila kitu kitaenda kombo.

Tutaendelea na somo kuangalia vitu vingine vinavyosababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa.......

Duniani Kuna Mambo

Huyu ni moja ya akina baba wa ajabu duniani kwa kumfanyia mtoto wake wa kumzaa kitendo cha ajabu (sex assault) tena kwa miaka 24
Josef Fritzl (73) siku ya jumatatu April 28, 2008 amekiri mbele ya Polisi wa mji wa Amstetten nchini Austria kwamba alimufungia mtoto wake wa kumzaa Elizabeth (42) kwenye basement ya nyumba yake tangu mwaka 1984 na kuzaa naye watoto 7 huku yeye (Josef) na mke wake pamoja na watoto wengine 3 wakiishi katika nyumba moja bila wao kufahamu nini kilikuwa kinaendelea.
Elizabeth anasema hajawahi kuona mwanga wa jua pamoja na watoto wake 3 kwa muda wote wa miaka 24 aliyokuwa amewekwa kwenye hiyo jela ambayo baba yake alimuweka.
Pia huyu mzee amekiri kumchoma moja ya watoto aliozaa na binti yake baada ya kuona amekufa.
Pia huyu mzee alikuwa ametengeneza milango inayofunguliwa kwa namba (codes) ambayo mtu mwingine hawezi kufungua.
Pia kelele zote za binti na watoto zilikuwa haziwezi kusikiwa na mtu yeyote kwa sababu alitengeneza aina ya jela ambayo hata ukipiga kelele mtu wa nje hawezi kukusikia.Je huyu mzee amewezaje kuhakikisha huyo mtoto wake anamfungia, anambaka, na kulazimisha kuzaa naye watoto kwenye hiyo jela ya basement kwa miaka yote 24 bila familia kujua, wala majirani kujua, je alikuwa anawapa vipi mahitaji kama chakula na nguo? Na imekuwaje hadi mzee huyu mchafu na wa ajabu kufikia hatua ya kukamatwa na polisi?

Kwa bahari zaidi soma hapa
http://www.presstv.ir/detail.aspx?id=53555&sectionid=351020606

http://www.cnn.com/2008/WORLD/europe/04/28/austria.cellar/index.html?iref=mpstoryemail#cnnSTCPhoto

http://www.timesonline.co.uk/tol/news/world/europe/article3835640.ece
Monday, April 28, 2008

Maumivu Wakati wa Tendo la Ndoa

Maumivu wakati wa tendo la ndoa au kuumia wakati mnafanya tendo la ndoa kwa mwanamke hujulikana kama Dyspareunia.
Neno Dyspareunia tamka (dis-pa-roon-ia) linatokana na neno la kigiriki lenye maana ya shida katika kuingiliana wakati wa kufanya tendo la ndoa (difficulty mating au badly mated).
Utafiti unaonesha kwamba kati ya wanawake watatu, wawili wamewahi au hupata maumivu wakati wa tendo la ndoa.
Imefika kwamba baadhi ya ndoa, mwanamke anapata maumivu kiasi cha kutokuwa na hamu tena ya tendo la ndoa na matokeo yake wamekuwa na wakati mgumu linapokuja suala la kufanya mapenzi na pia kila wakirudia kufanya tendo la ndoa, mambo ni yamekuwa ni yaleyale kwa mwanamke kuumia zaidi kuliko mara ya kwanza.
Kawaida huwa haifurahishi kabisa na haina hata ladha kufanya tendo la ndoa huku mmoja kati yenu akiwa anapata maumivu makali au shida hiyo husababisha kutojishughulisha katika kuleta raha ya kweli na hatimaye kuridhishana kimapenzi wakati wa tendo la ndoa.
Tendo la ndoa halikuwekwa ili kukupa shida au maumivu bali kukupa raha, furaha na kuridhishwa.
Moja ya kanuni muhimu sana katika tendo la ndoa ni
Kama unapata maumivu usifanye
Badala yake tafuta nini kimesababisha na tafuta jibu sahihi la kuondoa hiyo hali au muone daktari akusaidie.
Na baada ya kupata tiba na kupona ndiyo unaruhusiwa kuendelea kufanya tendo la ndoa kwa kufurahia na kukupa raha zaidi, vinginevyo itakuwa ni kuleta maangamizi.
Ni kweli kwamba kama moja wapo ya mahitaji ya msingi ya kihisia (emotions) kama hili la tendo la ndoa halipatikani katika ndoa linaweza kusababisha mmoja ya wanandoa kutokuwa mwaminifu kwa mwenzake na kutoka nje kwenda kutafuta mtu wa kumridhisha zaidi, hata hivyo kwa mwanamke kufanya tendo la ndoa huku anapata maumivu au kuumia kwa kuogopa kwamba asipompa Mume wake haki yake basi anaweza kutoka nje na kutokuwa mwaminifu hilo si sahihi kwani ni kutojiamini na kutojali si afya yako tu bali haki yako ya msingi ya kufanya tyendo la ndoa kwa kupata raha.
Mnahitaji kujulishana na kuelezana ukweli ili muweze kupata dawa na hatimaye kurudi kwenye raha upya badala ya kuumizana.
Kuna mambo mengi yanayosababisha mwanamke au hata mwanaume kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa na inaweza kuwa ni wakati mwanaume anapoingia (penetrate) au wakati wa kitendo chenyewe au baada ya kitendo chenyewe.
Inaweza kuwa ni maumivu makali sana au inaweza kuwa ni kuwashwa au inaweza kuwa ni maumivu wakati wa kukojoa mkojo wa kawaida au inaweza kuwa ni maumivu ambayo unasikia kama moto unawaka vile ndani yako wakati wa tendo la ndoa.

Naamini kufika mwisho wa hili soma utakuwa umefahamu si nini kinasababisha bali utafahamu jibu la hili Tatizo.Saturday, April 26, 2008

Honeymoon (Fungate) - Mwisho

Ni vizuri kumkubali mwenzako kama alivyo kwa maana kwamba wewe tu peke yako hapa duniani ndiye unayeweza kuvumilia na kuchukulia udhaifu wake wote alionao, vinginevyo kila mtu akijiona bora kuliko mwenzako mnaweza kufanya honeymoon kuwa uwanja wa masumbwi.
Mambo ambayo yanaweza kuharibu honeymoon:
1. Usitegemee mwenzako afanye kama wewe unavyotaka.
Kumbuka mmekutana watu wa malezi tofauti na aina tofauti ya maisha, hivyo usitegemee sana kila unachotaka wewe mwenzio atafanya na kutimiza.
Hapo mnakutana ili tofauti zenu zianze kuunganishwa na kuwa kitu kimoja kinachofanana hivyo mnahitaji muda na uvumilivu ili kuijenga familia mpya iliyozaliwa.
Kutakuwa na tofauti kubwa katika kufikiria mambo na kufanya mambo hivyo mnahitaji kuvumiliana.
Mwingine akilala usiku amezoa kuzima taa na pia atapenda wakati wa kufanya mapenzi taa ziwe zinawaka na inaweza kuwa mwenzako ni kinyume chake yaani anaona aibu na anapenda taa zizimwe, msipokuwa na Hekima mnaweza kufikishana mbali na mkaumia.
2. Kutegemea mwenzako akupe furaha wewe.
Furaha ni kitu ambacho kipo ya ndani ya mtu, huwezi kukigusa kwa mikono, na huwezi kuchukua furaha kwenye bakuli na kuijaza kwenye moyo wa mtu mwingine, bali ni wewe mwenyewe kwanza kuwa mtu mwenye furaha bila kutegemea mwenzako awe chanzo cha furaha.
Kila mmoja akiwa na furaha automatically wote mtakuwa na furaha.
Otherwise mtangulize mwenzako kuliko kujitanguliza wewe kwa kila jambo.

3. Angalia maneno unayotamka.
Maneno unayotamka wakati huu ni muhimu sana unaweza kujenga au kubomoa, unaweza kufurahisha au kuhuzunisha, unaweza kubariki au kulaani unaweza kuongeza moto wa mapenzi au kuzima moto wa mapenzi.
Kuna wanandoa ambao wakati wapo honeymoon mwanamke alimwambia mwanaume "lakini wewe ni mzee sana hivi kwa nini ulichelewa kuoa?" mwanaume alikasirika sana na tangu siku hiyo ndoa imeingia zogo la aina yake.
Sentensi moja tu imemfanya mwanaume ajisikie anadharauliwa na mke wake tena siku ya kwanza honeymoon na sasa ndoa imeingia katika mgogoro na wanaishi tu bila mapenzi ya kweli.
Hivyo inabidi uwe makini na maneno au kauli unazotoa iwe utani au kawaida, fikiria kwanza kwani bado hamjazoeana tabia bado.
Pia usiwe mtu wa kulalamika na kulaumu kila kitu kwa kujilinda au kujiona wewe upo sahihi zaidi kuliko mwenzako.
Kumbuka kuna maneno huumiza kuliko kupigwa makofi na mangumi.

4. Usiweke kumbukumbu ya vitu mwenzio anakosea.
Jitahidi kusahau kila kitu ambacho mwenzako unaona anakosea.
Uliyempenda ni mpenzi wako sasa ila si mtu aliyekamilika hivyo kukosea ni sehemu ya maisha yake.
Isitokee akifanya kosa tena unakumbushia na kosa la nyuma, huko ni kumuumiza zaidi na atakumia zaidi kuliko kawaida.
Pia jitahidi kuahidi kitu ambacho unauwezo nacho (hasa wanaume) kwani kuna watu (hasa wanawake) wanakumbukumbu sana kwa kila ahadi huwa hawasahau kiasi kwamba ahadi yoyote isipotimizwa inakuwa nongwa.
Naamini kwa somo lote hili utakuwa na swali au maoni unkaribishwa tuweze kujadiliana zaidi.
Mungu akubariki sana.

Friday, April 25, 2008

Honeymoon (Fungate) -4-

Mara ya kwana kufanya mapenzi (Tendo la Ndoa)

Ni jambo lisilopingika na ni dhahiri kwamba kitendo cha kufanya mapenzi (sex) ndicho kitendo chenye utamu (feelings) kuliko kitu chochote duniani.
Pia hakuna mtu anaweza kukufundisha kufanya mapenzi kwani kufanya mapenzi ni kitu mtu anazaliwa anajua.
Hapa ni katika kupeana uzoefu, hivyo kama wewe ni mara yako ya kwanza kufanya mapenzi usiwaze sana na kujiuliza itakuwaje.

Kama mmekutana wote mna uzoefu wa kufanya mapenzi hamhitaji maelezo sana, kitu cha msingi ni kujimwaga kitandani na kuanza kazi.
Kama mmoja wenu ana uzoefu wa kufanya mapenzi ni vizuri awe wazi ili kumuelekeza mwenzake na hatimaye mambo yawe mazuri, usipoteze muda kujifanya hujui huo ni unafiki na kutojiamini kwani mmeshaoana tayari, sasa unaficha nini.
Na kama kweli wote ni mabikira na ni mara yenu ya kwanza kufanya mapenzi basi kitu cha msingi ni kuwa tayari na pia kupata idea zifuatazo ili ziwasaidia kuimarisha utamu wa hiyo siku mnayoisubiri kwa hamu duniani na hiyo siku ipo inakuja.

Siyo lazima au sheria kwamba lazima tendo la ndoa lifanywe usiku ule wa harusi.
Mnaweza kusubiri muda wowote mkiwa tayari kwani maharusi wengi huwa wamechoka nyang’anyang’a na hizo sherehe za harusi.
Mnaweza kuishia kuchezeana miili tu na kusubiri muda muafaka wakati mpo tayari, ingawa kwa nini kusubiri kesho wakati leo inawezekana?
Kufanya mapenzi kwa mara ya kwanza huleta hofu sana, kwanza ukifikiria tu kitendo cha kuwa uchi (naked) mbele ya mwanamke au mwanaume kwa mara ya kwanza tangu umekuwa mtu mzima na kuonesha sehemu za siri; hakika si jambo dogo unaweza ku-panic, ukawa nervious, unaweza kuanza kutoa jasho bila mpangilio pia unaweza kukosa hata maneno ya kuongea.


Ufunguo
Ufunguo wa mambo yote ni kwanza kufurahia kwamba siku au muda muafaka uliokuwa unasubiri kwa hamu duniani umefika hivyo jiweke katika hali ya kufurahi na kushangilia.
Baada ya wasimamizi kuwaaga na kuwaacha ninyi wawili ingia kwenye hicho chumba (cha honeymoon), oga vizuri wengine huoga pamoja ila kama ni mara ya kwanza kuwa na mwanamume au mwanamke si rahisi, labda sana sana baada ya siku mbili au tatu au wiki au mwezi na si sheria bali hiari.
Mkishakuwa tayari relax, pigeni story za mambo mengi tu huku mkishikana na kuongea maneno matamu na kujipongeza lengo ni kutengeneza mazingira ya kuondoa tension, stress, au kuwa nervous na issue iliyo mbele yenu.
Kila mmoja aondoe aibu na kama una aibu hapo si mahali pake jitahidi kuhakikisha una participate kwenye shughuli nzima.

Mawasiliano ndiyo msingi wa kuhakikisha kila kitu kinaenda vizuri mwanaume na mwanamke wote kwa pamoja zungumzeni kila kitu unachopenda kama umechoka, sema nimechoka kama unataka mkaoge wote sema tukaoge, just be free free free free free huyo ni wako.


Hakikisha chumba chenu mlango umefungwa locked, wanawake wapo sensitive sana na mwingiliano wa kitu chochote wanapenda sana kuhakikisha kuna usalama na privacy ya hali ya juu.
Pia Kumbuka kwamba; kwa mara ya kwanza hakuna mtu amewahi kukosea kufanya mapenzi kwani jinsi siku zinavyokwenda ndivyo mtazidi kuwa wataalamu.
Na hakuna mtu amewahi kuwa mtaalamu wa kufanya mapenzi siku ya kwanza, hivyo vyovyote vile kitu cha msingi relax na furahia.


Mwanaume:
Wewe ndiye nahodha wa kuhakikisha hiyo meli yako (penis) inatia nanga bandarini (penetrate kwenye vagina) salama na kama unaona huwezi kutia nanga hiyo siku usiwe na haraka kwani umeshafika karibu kabisa na bandari na umeruhusiwa kutia nanga hivyo uwe na saikolojia kubwa kusoma mazingira ya bandari na nchi yenyewe inayomiliki hiyo Bandari kwamba ipo tayari kuipokea meli yako kutia nanga hahahaha hapo pametulia (tafsida).

Kama amekubali kwamba leo unaruhusiwa kutia nanga bandarini basi kitu cha msingi hakikisha umetengeneza mazingira ya mwenzi wako kuwa na hakikisha yupo huru na hana hofu wala mashaka, akili na mawazo yake yametulia na yupo relaxed.

Anza kwa kumuandaa, uwe mbunifu kuanzisha mazungumzo ambayo yatamwezesha kuwa huru kwa mfano unaweza kuanza kuongelea mafanikio ya harusi, jinsi unavyompenda, jinsi alivyo mzuri na alivyokuwa anapendeza huku unamsogelea ili kumpa mgusu na maneno matamu na mazuri then romance hadi awe amesisimuka vya kutosha.
(kumbusu, kumpa mgusu wa kimahaba sehemu zote ambazo yeye atakuelekeza kwamba anafurahia kama vile lips, shingo, chuchu,
na sehemu zote za mwili na sehemu yoyote yeye atayokuelekeza)

Huruhusiwi kuingiza meli yako kutia nanga bandarini kama hajawa aroused/full stimulated and moist (unaweza kujua kwa kupeleka kidole huko kwenye bandari yake).
Hakuna muda maalumu wa kumuandaa hadi awe tayari; hapo inatokana na ninyi wenyewe mambo yanavyoenda na jinsi mnavyojua kuchezea viungo vyenu, ila muda wa wastani kawaida ni kuanzia dakika 15 hadi 30
Ukiona yupo tayari au yeye anaweza kukwambia yupo tayari, ingiza meli polepole bandarini anaweza kukuelekeza yeye mwenyewe inatokana na uzoefu na jinsi alivyojifunza.
Hakikisha unawasiliana naye vizuri kujua anaumia sana au la kwani njia yake bado ni ndogo.


Mwanamke:
Kwanza lazima ufahamu kwamba kuna raha ya ajabu na utamu wa ajabu kwa hiyo meli kutia nanga kwenye hiyo bandari yako.
Wakati mmekaribiana na kuanza kujiandaa kwa kitendo hakikisha unausoma vizuri mwili wako, unahitaji kumwelekeza mwenzi wako sehemu zote ambazo unaona unajisikia raha na kunyegeka zaidi kama
ni kubusiwa,
kunyonywa
au kuchezewa chuchu, kisimi nk.
Mwanamke una nafasi kubwa kuhakikisha suala zima linaenda vizuri siyo suala la kumuachia mwanaume kila kitu afanye na wewe kulala tu kama gogo, elekeza, sema chochote na tia moyo kama unapata raha, sema na kama unapata shida sema, mwambie vipi unajisikia kwani mawasiliano ni muhimu.
Kama huwezi kuongea chukua mkono wake na weka pale unataka yeye aguse au achezee, hapa mnajenga msingi wa raha ambayo utakuwa unaipata kila siku.
Kama hata baada ya foreplay kwa muda mrefu unaona bado upo dry kwenye bandari yako kiasi kwamba meli haiwezi kuitia nanga, maana yake hujawa tayari hivyo mwambie mumeo kwamba you need more time ni vizuri msifanye kuliko kulazimisha ukaumia na baadae ukaathirika kisaikolojia na kuona sex ni kitu kibaya wakati ni kitu kitamu kuliko kitu chochote.

Ukishajisikia upo aroused na stimulated vya kutosha na upo wet/moist kiasi cha kutosha na upo tayari kuruhusu meli kutia nanga kwa mara ya kwanza mwambie nahodha afanye makeke kwani hiyo ndo raha yenyewe.
Ukiona wakati anaingia unapata maumivu unaweza tumia mafuta ya kulainisha (KY Jelly yanapatikana kwenye maduka ya madawa)

Mikao
Kuna mikao mingi kwa ajili ya kufanya mapenzi ila kwa wanandoa wapya tena kwa mara ya kwanza mkao unaotakiwa ni ule wa mwanaume juu na mwanamke chini (missionary position) hii ni rahisi na huwezesha meli kutia nanga bandarini kwa mara ya kwanza vizuri na bila matatizo makubwa ya kiufundi.
Muhimu ni kwamba jinsi siku zinavyozidi kwenda ndipo mtajua mikao mingi na kujua upi unafaa na kuwapa raha zaidi.

Je, mwanaume akishindwa kusimamisha?
Huwa inatokea, hata kama hiyo meli ulikuwa una uhakika nayo kuhusu utendaji wake kuna wakati huwa zinagoma kwa mara ya kwanza kutia nanga sababu ya stress, woga au ku-panic. Omba Mungu kuhakikisha meli inatia nanga bandarini si utani kama wewe ni nahonda kwa mawa ya kwanza.
Muhimu tulia mambo yatarudi na kuwa safi kabisa.
Au wewe mwanaume mwambie mpenzi wako akutajia kwa sauti bila aibu viungo vyote vya kwenye mwili ambavyo anapenda umbusu, umnyonye, na kumchezea, nina uhakika kuna viungo akitaja tu mood itabadilika na umeme utawaka tena.

Maumivu na kutoka damu je?
Kama ni bikira na bado hymen ipo, bila shaka katika harakati za meli kutia nanga bandarini lazima hymen itatifuliwa na kusababisha maumivu ya muda mfupi na uwezekano wa damu kidogo kutoka.
Hakikisha mnafanya maandalizi ya kutosha kabla ya meli kutia nanga.
Tumia vilainisho kama KY jelly na pia muwe na bed sheets zenu au taulo, msichafue mashuka ya watu.

Je, ikitoke amemaliza bada ya dakika 1 au 3?
Kwa mara ya kwanza inaweza kutokea kwa mwanaume kumaliza (kufika kileleni) baada ya dakika 1 au 3, na kaisha fika kileleni meli inaishiwa nguvu kabisa kwenda kutia nanga.
Usijali wala kuogopa kitu cha msingi tuliza akili na endelea na romance na ukiona imeshindikana relax na tafuta muda tena na mweleze mwenzi wako kwani hapo ndo unaanza kupata uzoefu wa hii shughuli.

Je, lazima mwanaume awe kiongozi wa hii shughuli?
Si lazima hapa ni kuelekezana na lengo ni kuanza safari hivyo mawasiliano na kushirikiana bila aibu ndo msingi wa mafanikio ya tendo zima.

Kufika kileleni
Uzoefu unaonesha wanaume ndo hufika kileleni kwa kufanya mapenzi siku ya kwanza na wanawake wao ni mara chache sana labda awe mzoefu na hii shughuli.
Hivyo mwanamke anahitaji kuwa mvumilivu kwani asipofika pale alitegemea bado muda upo na safari imeanza.

Usitegemee mambo makubwa sana
Sex kwa mara ya kwanza ni kichekesho zaidi kuliko utamu hasa kama mmekutana wote washamba kwa maana kwamba hamna uzoefu.
Utamu wa tendo la ndoa unahitaji uzoefu na uzoefu huja baada ya kufanya mara kwa mara hivyo ridhika na chochote kitakachotokea mara ya kwanza.

Na je mwanaume akishindwa kabisa muda wote wa honeymoon?
Kama mwanaume ameshindwa kabisa kuhakikisha meli yake ina penetrate na kutia nanga muda wote wa honeymoon, asi-panic muda anao maana si lazima kila kitu kiwezekane huko honeymoon.
Pia kana kuna Tatizo awaone wasimamizi wa harusi wawasaidia maana si rahisi na huwa haitokei watu kushindwa kufanya mapenzi.
Litakuwa ni Tatizo kubwa sana.
Otherwise labda honeymoon yenyewe ilikuwa ni usiku mmoja na pia kuna sababu za msingi kama vile kuepuka mimba na mambo ya red card.
Tutaendelea na sehemu ya mwisho..........................

Thursday, April 24, 2008

Honeymoon (Fungate) -3-

(Sasa safari imeiva kwenda honeymoon) Vitu Muhimu Kubeba unapoenda Honeymoon:
Kujua ni vitu gani utavibeba kwenda navyo honeymoon ni hatua muhimu sana na inabidi uwe makini ili ukifika huko usiwe na muda wa kulalamika kwamba, kuna kitu ulipaswa kuwa nacho lakini umekisahau.
Pia inabidi uwe makini, maana unaweza kubeba vitu ambavyo hata hutavitumia.
Kitu cha msingi ni kuangalia kwanza yale mambo utaenda kufanya ukiwa huko, aina ya hali ya hewa, je ni sehemu za baridi au sehemu za joto?
pia muda utakaotumia kukaa huko na huyo mpenzi wako.
Unaweza pia kufuatilia kuona je sehemu mtakayo tumia (hotel) kwa honeymoon yenu inatoa vitu gani kwenye huduma zao ili msije beba vitu ambavyo nao wanatoa pia.
Suala la nini kinafaa kuchukua, ni muhimu kujadiliana pamoja na mwenzi wako ili kupunguza vile vitu ambavyo mnaweza kuvibeba wote na kuongeza mzigo wa bure.
Ifuatayo ni Orodha ya vitu Muhimu Kuvibeba kwa Ajili ya Honeymoon.
Begi (Luggage)
Ni vizuri kubeba begi ambalo si kubwa sana hadi linachosha kubeba.
Usichukue begi kubwa au mizigo mikubwa sana, zingatia kwamba mnaenda kupumzika (relax) baada ya hekaheka nyingi za harusi na pia kuanza maisha mapya na yule anayetimiza ndoto zako hapa duniani.
Haina umuhimu kubeba nguo zote na kujaza kwenye begi, kitu cha msingi unaweza kubeba zile nguo za kawaida (casual wear) nguo za kuvaa mchana, nguo za kuvaa usiku, nguo za kuvaa chumbani na nguo za ndani (inner wear).
Nyaraka Muhimu (Documents)
Vitambulisho, ATM cards (pesa), orodha ya namba za simu muhimu, ticket, passport nk.
Pia inategemea umesafiri kwenda sehemu gani kwa ajili ya honeymoon, lolote linaweza kutokea, iwe ajali au dharura hivyo unahitaji kuwa na nyaraka muhimu ili kikitokea kitu chochote inakuwa rahisi kupata solution hata kuomba msaaada.
Nguo
Mwanaume
Mwanaume usisahau vitu vifuatavyo, Mkanda (hiari), Mashati, Viatu, Sandals, Kofia (fun), Jacket au koti (kama kuna baridi sana), Tshirts, bukta (shorts), Nguo za ndani za kutosha, socks na nguo za sports na vingine unavyooona wewe vitakufaa

Mwanamke
Mwanamke usisahau vitu vifuatavyo Bras, Kofia, Jacket au koti (kama kuna baridi), Vito kama herein nk, Nguo za ndani za kutosha na zenye style tofauti na rangi tofauti, Sandals, Skirts na tops pia nguo zingine ambazo wewe unaona zitakufaa.
Camera, CD player, Laptop, memory card, Simu (mobile)
Hakikisha kama umebeba simu unachukua na chaja yake.
Kupiga picha ni muhimu sana hasa kutokana na wakati muhimu kama huo wa ku-relax na mwenzi wako na kutengeneza kumbukumbu muhimu za maisha mapya na msingi wa maisha pia.
Pia mnaweza kusikiliza mziki mzuri mnaopenda wakati mnajipumzisha chumbani au wakati wa mambo fulani fulani hapo kitandani.
Kuna hotel zina wireless connection ya internet hivyo mnaweza kutumia laptop yenu kuweza kujua nini kinaendelea duniani.
Siyo lazima uwe na vitu vyote nimevitaja hapo juu ni uamuzi na pia kama mnavyo.
Pia ni muhimu kuwa na simu hasa ikitokea dharura.
Pia mnaweza kubeba dawa za kutulia maumivu kama kichwa nk, kalamu na karatasi na miwani .
Afya, usafi na kuoga (Bathroom)
Mwanaume
Ni muhimu kubeba vitu vifuatavyo, dawa ya kusukutua (mouthwash), dawa ya meno(toothpaste), mswaki, Shampoo, nyembe za kunyolea (razar) na shaving cream, kitana, Deodorant, na taulo la kuogea pia mints na vitu vingine unavyovifahamu.
Mwanamke
Ni muhimu kubeba vitu ambavyo mume wako havitumii kwani wewe na yeye ni kitu kimoja kwa hiyo unahitaji kubeba vitu vile ambavyo ni kwa ajili yako kama vile Pads and tampons, mswaki, tissue, taulo na vipodozi vyote unavyoona vinakufaa.
Mahaba (Romance)
Kwa kuwa mnaenda kufanya mapenzi kwa mara ya kwanza (kama ni mabikira) ni muhimu kujiandaa vizuri na kama ni mara ya kwanza kwa mwanamke kufanya tendo la ndoa hii ni kudhihirisha kwamba atahitaji lubricants kwa ajili ya kulainisha (njia) ili kupunguza maumivu kwa mara ya kwanza.
Na kama hamuhitaji kupata mtoto mapema, naamini inabidi mfikirie mtaenda na kifaa gani au njia gani ya birthcontrol (kuzuia mimba) au Njia ya asili (muwe mmepanga tarehe vizuri)
Pia ni muhimu kuwa na sabuni zinazozuia bacteria na fungus kwani tendo la ndoa kwa mara ya kwanza husababisha maambukizi ya fungus na bacteria kwenye viungo vya uzazi vya mwanamke.
(Tutaangalia kwa upana zaidi kwenye somo la Lubricants kwa ajili ya mwanamke bikira)
Tutaendelea na somo.............................................................
Tuesday, April 22, 2008

Honeymoon (Fungate) - 2-

Wana ndoa wapya wakiwa honeymoon {wakitembea beach}.
(Picha kwa Hisani ya Black Magazine)
Mambo ya Msingi Kuamua kuhusu Honeymoon
Honeymoon ni muda ambao wanandoa wengi huusubiria kwa hamu kubwa, ni kweli kuna raha yake kwani unatimiza moja ya ndoto kubwa duniana za kupata ubavu wako.
Kama ni kijana wa kiume naamini una subiri kwa hamu sana kwa sababu kuna nguvu katika hisia zako inakuongoza kuisubiri kwa shauku hiyo siku.
Na kama ni binti naamini unajiuliza sijui itakuwaje na kutokana na mengi unayosikia kuhusu siku ya kwanza naamini kuna wakati unahuzunika na kuna wakati unafurahi pia.

Ingawa harusi mara nyingi hushikirikisha ndugu, jamaa na marafiki katika maamuzi mengi, suala la honeymoon ni la mke na mume mtarajiwa kuamua ni wapi na kwa muda gani.
Hivyo suala la kuongelea jinsi harusi itakavyokuwa linatakiwa kwenda sambamba na jinsi honeymoon itakavyokuwa, mkizembea haitakuwepo sijui mtamlaumu nani.
Wanandoa wengi hujisahau kuzungumzia suala la honeymoon na matokeo yake hujikuta fedha zote zimeishia kwenye maandalizi ya harusi na kubakia weupe bila pesa na hivyo kusababisha kukaa honeymoon kwa siku moja au mbili tena sehemu ambayo hawaipendi.Mambo ya msingi kuamua kuhusu haneymoon yenu:
Bajeti
Ni muhimu kujua ni sehemu (hotel) gani mtaenda na bei yake itakuwaje na zaidi mnataka kukaa siku ngapi au kutumia siku ngapi kwa ajili ya honeymoon.
Kiwango cha chini kabisa ni siku mbili, ingawa wapo wamekaa honeymoon kwa siku moja naamini tatizo ni bajeti kwani wengi hujisahau.
Wengi sana hutumia siku 5 au 6 hasa kutokana na majukumu ya kazi na maisha kwa ujumla. Wapo hukaa mwezi mzima honeymoon.
Kitu cha msingi ni kukubaliana ninyi wenyewe ni muda gani mnahitaji kuwa pamoja kwa kuangalia bajeti mliyonayo.
Wapo wengi hutegemea wasimamizi wao kuwapa pesa za honeymoon, kama ni hivyo ongea nao mapema ususibiri siku ya harusi ndiyo uanze kuwauliza honeymoon itakuwa wapi.
Pia wengine husubiri fedha za zawadi ndo ziwasaidie kulipia honeymoon, uwe makini kwani unaweza kupewa zawadi za vitu bila pesa sijui utauza vitu?
Pia ni muhimu kuwa na pesa ya ziada zaidi ya bajeti kwa ajili ya dharura.

Wazo Kamili
Wengi hudhani honeymoon ni kwa ajili ya kufanya tendo la ndoa kwa mara ya kwanza; na kuelekeza akili zote kwenye hicho kitendo tu.
Kumbuka, sasa ninyi mtaishi pamoja wawili kuliko muda wote mlivyoishi na wazazi wenu hivyo haina haraka kuhakikisha kwamba lazima hiyo siku ya kwanza utimizi kila kitu.
Pia huyo ni mume wako au mke wako haraka ya nini wakati ni mali yako,
Polepole ndiyo mwendo na haraka haina baraka.
Honeymoon ni mahali ambapo unaenda kupumzisha akili baada ya mikikimikiki ya maandalizi ya harusi, unaenda kukaa nakutumia muda wako maalumu na yule unampenda na kuanza uzoefu mpya wa maisha pamoja huku mkifurahia uumbaji wa Mungu.
Fikiria ni kitu gani mtakifanya zaidi ya kula na kulala.
Je, kuna mchezo wowote mtacheza kama kuogelea.
Andika vitu vile mtapenda kufanya pamoja mkiwa honeymoon vitakavyowafanya muwe kitu kimoja na zaidi sana kuwaweka karibu kujuana zaidi.
Pia Fahamu kwamba mnapoongelea suala la namna honeymoon mnataka iwe, tayari mnapata uzoefu wa maisha ya ndoa kwani kuna vitu mtakubaliana na vingine vitahitaji muda.
Chagua Sehemu
Chagua sehemu kufatana na bajeti yenu, msisubiri mpaka kila kitu cha harusi kikamilike.
Nenda sehemu mnapenda kuitumia kwa ajili ya honeymoon na fahamu bei yake fanya booking na zaidi angalia kama wanafanya punguzo kwa ajili ya honeymoon.
Kama ninyi hamna muda tumia wasimamizi wa harusi yenu au marafiki mnaowaamini ili kuhakikisha suala zima la honeymoon limekamilika kabla ya siku ya harusi yenyewe.
Visa na Passport
Kama mnaenda nje ya nchi kwa ajili ya honeymoon ni vizuri kuhakikisha passport yako haijaisha muda na pia unapata visa mapema iwezekanavyo.
Hii inatokana na kwamba baadhi ya nchi ili kupata visa unahitaji muda mwingi zaidi hasa nchi za Ulaya na Amerika hawakubari kirahisi inabidi uombe visa miezi mitatu hadi minne kabla.
Kuwa na Siri
Unahitaji kutunza siri ya wapi unaenda kwa ajili ya honeymoon.
Honeymoon ni kwa ajili yenu wawili tu si rafiki wala ndugu.
Hivyo jitahidi sana kuhakikisha kuna kuwa na siri kweli.
Hutakiwi kuwaambia rafiki zako au ndugu zako mtakuwa wapi isipokuwa wale unaoamini tu, kwani kuna marafiki hawana dogo wanaweza kuharibu honeymoon yenu kwa simu moja tu, kama unaweza zima kabisa simu za mkononi na wape muda maalumu watu muhimu kwamba wakupigie saa ngapi au muda gani.
Mawasiliano na Ratiba
Ni vizuri kuwa na ratiba kamili inayowawezesha kuwapa uzoefu wa utendaji ambao hauna utaratibu, ni muhimu kupanga jinsi mtakavyoitumia siku ya pili yake kabla ya kulala usiku, ili kila mtu ajue siku inayofuata mtaitumia vipi na pia itawapa uzoefu kama wanandoa wapya.
Unaweza kupanga muda kwamba hatafanya chochote bali kufurahi tu.
Pia ni muhimu sana kuhakikisha kila mmoja anakuwa na mawasiliano mazuri na mwenzake, kwani kabla ya hapo kila mtu aliishi mwenyewe na sasa mnakuwa kitu kimoja hivyo ni vizuri kumweleza mwenzako kila kitu unataka kufanya.
Uwepo Kwenye Honeymoon
Unatakiwa kuwepo kwenye honeymoon kimawazo, kiakili na kimwili pia.
Lazima umtangulize mwenzio kwa kila kitu hakikisha wewe unajitahidi kumfurahisha mwenzako kwa kadri unavyoweza na si kusubiri yeye akufurahishe wewe.
Sema naye, cheza naye, ongea naye na fanya vitu vingi na yeye, tumia muda wako pamoja na wewe na si kusoma vitabu, au vitu vingine.

Tutaendelea.........

Monday, April 21, 2008

Honeymoon (Fungate) - Utangulizi

Hicho kitanda kione tu! kama ulipitia hapo una hadithi ya kuongea na kama bado, kuna hadithi nzuri sana inakusubiri, utamu ni pale wote mkiwa zero (bikira) na hata siku moja hujawahi kuona nini sijui..... halafu unaambiwa twende tukaoge pamoja then mrudi hapo hapo kwenye hako kakitanda!
Honeymoon ni nini?
Ni wakati ambapo wanandoa wapya huenda sehemu mbali na mahali wanapoishi (holiday) baada ya siku ya harusi yao, kwa ajili ya kupata uzoefu mpya wa maisha mapya ya mahusiano ya kimapenzi katika ndoa.
Pia wanandoa wapya huenda sehemu ambayo ndugu na marafiki hawawezi kuwaingilia na shughuli yao hiyo yakufahamiana kimwili na kiroho na kupeana uzoefu mpya wa kuanza kuishi pamoja.
Pia ni wakati mzuri kwa wana ndoa kupumzika baada ya shughuli nzito ya harusi.
Pia ni mwezi mzima wa maisha ya ndoa tangu kuoana.

Kwa nini Honeymoon na si jina lingine?
Simulizi za kwanza kabisa kwenye karne ya 16 hasa huko kaskazini mwa Ulaya, kulikuwa na tabia ya kijana wa kiume kumteka binti (kidnap) anayetaka kumuoa na kuingia naye mitini hadi mwezi upite huku ndugu wa binti wakimtafuta.
Huo mwezi mzima ambayo kijana wa kiume alikuwa na binti a huku anaendelea na uhusuano wa mapenzi ulikuwa unaitwa ni honeymoon na haikuwa kesi.
Muhimu ilikuwa lazima ujitokeze baada ya mwezi na pia ndugu wa binti walikuwa wanakonyezwa na ndugu wa kijana kwamba binti yao ni salama so wasubiri mwezi.
(Pia kuna makabila ya kiafrika hii system ilikuwepo)

Pia simulizi nyingi za kale huko misri na baadhi ya nchi za Scandinavia zinaonesha kwamba wana ndoa wapya walikuwa wanapewa kinywaji kinachotokana na asali (Mead) kunywa kila siku kikombe kimoja kwa mwezi mzima.
Ndiyo wakaita honeymoon.
Na Pia ulikuwa ni mwezi wa kwanza kwao kwa ajili ya kuhakikisha wanafanya kweli ili kupata mtoto kwa sababu waliamini hiki kinywaji kilikuwa kinawapa viini muhimu kwa ajili ya kuhakikisha uzazi na afya njema kwa wanandoa wapya.

Pia kuna simulizi zinazofananisha maisha ya ndoa kama asali kwa maana kwamba mwezi wa kwanza tangu kuoana ni mtamu kama asali kuliko miezi mingine,hivyo kuitwa honeymoon.
Utamaduni wa honeymoon unahusiana sana na wanandoa ambao ni mabikira (mwanaume na mwanamke).
Kuna watu wanaenda honeymoon wakati wanajuana kimwili tayari (sex) na wengine walishaishi pamoja tayari, hiyo haitaitwa honeymoon bali vacation tu ya kawaida kama zingine.

Honeymoon ni mahali pa kujenga msingi wa nyumba
Honeymoon si tu kuwa mbali na marafiki na ndugu ni mahali ambapo unaenda kujenga msingi wa ndoa yako na huyo mume na mke mpya.
Ni wakati ambapo unaenda kuyafukia maisha yako ya zamani na kuanza maisha mapya ukiwa na mtu mwingine kabisa mpya.

Siku ya ndoa mnakuwa mmeunganisha physically tu, lakini mkiwa honeymoon mnaunganika katika mambo yote kimwili, kihisia, kiroho na kuhakikisha ndoa inakuwa ndoa kisheria.
Honeymoon ni wakati wa kujenga sura mpya ya maisha ya pamoja mtakayokuwa nayo hadi kifo kitakapowatenganisha.
Unapopanga jinsi harusi itakavyokuwa usiweke nguvu nyingi kwenye harusi ukasahau kwamba unahitaji muda mzuri wa kuwa honeymoon na mke/mume mpya kwa ajili ya kujenga msingi mpya.
Ndoa nyingi zogo huanzia kwenye honeymoon so unahitaji kuwa mwangalifu na makini zaidi kuhakikisha hii likizo yako ya honeymoon inakuwa honeymoon na si vinginevyo.
Tutaendelea na mambo ya msingi ya kuzingatia huko kwenye huo mwezi mtamu kama asali............

Kumbe Salary inatokana na neno Salt

This term is taken from the early English word band, which means a fastening. The word bond implies that one is "bound" to repay an obligation.
The word borrow derives from the Old English word borg, which means "pledge".
In the Middle Ages, French merchants carried their money in a bougette, or "little bag". The word borrows from the Latin word bulga, meaning "a leather bag". Within the bag, one's monetary resources were kept.
Business originally applied to a person suspected of taking part in mischievous activity. Eventually, it related to any type of activity, and later still to a type of vocation.
This word comes ultimately from the Latin word for "head". The words capital and cattle come from this same root. Cattle were and are a source of wealth, and are typically measured in terms of how many "head of cattle".
This word originates with the Latin word charta, which means "paper" and led to the English word for chart. Initially, the word referred to a written challenge to a fight. Later, it changed its meaning and referred to a libelous written statement. By the 1600s, it became an agreement associated with prisoner of war exchanges. Eventually, the word came to take on its current meaning, "an agreement in restraint of trade".
This word stems from the Latin word for "box", cassa. Originally, the French used this term to refer to the "moneybox" holding any cash, but later the term applied to the cash itself.
The word coin comes originally from the Latin word cuneus, meaning "wedge". The term came to apply to the wedge-shaped die that made these small pieces of money. Later, the word coin was applied to the stamped image on the money, but eventually referred to the money itself.
This word is a combination of two Latin words: com, meaning "together"; and merx, meaning "goods".
This is a term developed by Karl Marx from the Old French word for "common" and based upon the Latin word communis, or "essential goods". It was thought that essential goods should be owned in common and thus shared.
The Latin words cum, "with", and panis, "bread", combine to form the source of the word company. Initially, the word was relational, corresponding with the word companion. Eventually, it came to exist within a business context as well.
The Latin term consumo means "eat up completely", which understandably led to our current use of the term consumer.
Deposit is created by putting together two Latin words: de, a relatively common prefix that means "away"; and positus, meaning "placed".
This important word is taken from the Greek word oikonomia, which means "house management". It originally applied to persons who were good administrators within a community, business or home.
Finance derives from the Latin and Old French word for fine, which originally meant "end". The French word for finance came to mean both "payment" and "ending", but in the 18th century the English adapted it to mean "the management of money".
This word comes from the Latin word laborare, which means "to be tired". Beginning with the Reformation, labor supposedly came to be regarded as a duty.
The word manager comes from the Italian word maneggiare, "to train horses", which derives from their word mano, meaning "hand".
The Roman word for "plunge" or "sink" is mergo.
One of the responsibilities of the Roman goddess Juno was to warn the Romans of impending danger. In this capacity, she was called Juno Moneta, where the name Moneta derives from a Latin word meaning "warn". As a tribute to Juno, the Romans built a temple in her honor on Capitoline Hill, which later became the place where coinage was kept. Becoming known also as the guardian of finances, the name Moneta would evolve into our word money.
In Greek, the word monopolion means "the right to exclusive sale".
The word revenue was created by combining the Latin words: re, which means "back"; and venio, which means "come".
The Latin word salarium, meaning "salt allowance", is the origin of the word salary. A necessary part of one's diet, Roman soldiers were supposedly given an allowance to buy salt as part of their income. In time, this word applied more generally to one's wages.
The Latin words se and cura combine to form this word. Translated literally, these words mean "without care".
This term originates with the Latin word socius, which had the basic meaning of "sharing", but was also used to refer to a comrade, a sharer or an ally.
Stocks originates from the Old English word stocc, a word for tree trunk. It implied that something was solid, or even safe.
The word comes from two related French words: sur, which means "over"; and plus, which means "more".
This word comes from an ancient Arabic term, tarrif, which means "notification".
Trade.When suppliers were less mobile, they walked between places where their goods were sold.
The Old English word for "tread" is trod, and the root of the word trade.

Sunday, April 20, 2008

Mambo 6 Muhimu Kuhusu Fedha Katika Ndoa

Zipo Ndoa ambazo mke na mume wanaishi tu kwa sababu ya watoto, au kuogopa kupoteza nyumba, au mali kwani utamu na raha ya Ndoa imetoweka, hata hivyo kila kitu kina chanzo na ni muhimu kujua chanzo ili uweze kutatua tatizo kabla halijakumaliza na kujikuta umechelewa.
wahenga walisema
"Heri Kinga Kuliko Kuponya". Unahisi huyo mwanamke anamwambia nini Mume wake hapo kwenye picha?

Tafiti nyingi zinaonesha kwamba migogoro mingi ya wanandoa hutokana na mambo yanayohusu pesa.
Pia mfumo wetu dume katika jamii umeongeza tatizo kuwa kubwa zaidi kwani suala la pesa ameachiwa mume bila mke kuwajibika, kujua au kuchangia lolote, hata wanawake wenyewe wengi wamejiweka katika kundi la kuwaachia wanaume kuwajibika kwa kila kitu kinachohusu pesa katika na kutoa maamuzi yote yanayohusu pesa katika ndoa.
Na kuna maamuzi mengine yameangamiza familia kwa sababu ni mtu mmoja tu katika ndoa ndo hutoa maamuzi linapokuja suala la pesa yaani baba au mume.

Sasa ulimwengu umebadilika wanawake nao wana uwezo, wanafanya kazi, wanaingiza pato katika familia na ndoa.
Pia kuna familia ambazo mke ndiye mwenye kipato kikubwa kuliko mume, na kuna ndoa ambazo kila mmoja akipata pesa hutumia anavyotaka yeye bila kukaa pamoja na kupanga nini kifanyike na matokeo yake kumekuwa na migogoro ya hapa na pale na kusuguana kwa hapa na pale.
mambo yafuatayo ni muhimu sana kuwekwa wazi kwa wanandoa kwa ajili ya kuimarisha ndoa hasa linapokuja suala la fedha.

Kuwa na Account Moja:
Kitu kikubwa ambacho wana ndoa wapya hukupamba nacho mara wakishaanza maisha pamoja ni jinsi ya kupangilia matumizi ya pesa.
Kama wote mnafanya kazi, je ni muhimu kuwa na account moja ya pesa? au kila mmoja kuwa na account yake then wote kuwa na account ya tatu ya pamoja?

Asilimia kubwa ya wanandoa wapya hufungua Account ya pamoja wakishaoana .

Kitu cha msingi ni kuhakikisha mmekuwa kitu kimoja si katika mwili mmoja tu, bali hata katika pesa.
Kuwa na account moja ni sawa, pia kuwa na account tofauti ni sawa.
Kitu cha msingi ni kuwaelewana juu mapato na matumizi ya pesa zenu na pia malengo ya kiuchumi ya muda mrefu na muda mfupi, kama kuwekeza na akiba kwa pamoja.
Pia kujua aina ya matumizi ya pesa kwa kila mmoja kwani kama mmoja ni mtumiaji na mwingine ni mtu wa kuweka akiba, mnahitaji kujuana ili kusiwe na kinyongo kwa mmoja.

Pia kama mmoja wenu ameingia kwenye ndoa huku anadaiwa na Bank ni vizuri kumjuulisha mwenzake kwani kuoana ni pamoja na hilo deni mnakuwa kitu kimoja.
Kuna wengine wanaingia kwenye ndoa huku tayari walishawekeza kwa ajili ya mke/mume na watoto aliokuwa anatarajia.
Kitu muhimu ni kuwa wazi kuhakikisha mke wako au mume wako anajua.

Jinsi ya Kupambana na Madeni
Katika mambo yote ya pesa katika ndoa, madeni ni jambo linaloongoza kuleta zogo mwenye ndoa na kama hamjafahamishana vizuri inaweza kuleta maafa.
Pia mara nyingi wana ndoa huwa wanatofautiana katika mtazamo kujua lipi ni deni kubwa au dogo hasa kutokana na elimu ya fedha ya kila mmoja.

Hilo ni deni lenu wote hivyo lazima muweke mikakati ya kuondokana nalo kwa pamoja.
Mara nyingi wengi hujiingiza katika deni bila upande mwingine kujua hali ikiwa mbaya ndiyo mtu anaanza kutoa taarifa kwamba ilikuwa hivi na vile huku nyumba inataka kuuzwa au kufukuzwa kazi.
Hapo ndiyo zogo huanza na ndoa huanza kuyumba kwani upande mwingine hujiona hauthaminiwi.

Mmoja kuwa Mtumiaji wa Pesa zaidi ya Mwenzake.
Wanandoa wengi hulaumiana kwamba "wewe ni mtumiaji mbaya kuliko mimi" au kumtuhumu mwenzake kwamba anatumia pesa katika kununua vitu visivyo muhimu katika maisha.

Jinsi ya kutumia pesa huleta maneno katika ndoa nyingi, wapo wanaume akipata pesa tu ni kwenda kununua TV kubwa, Music System na vitu vingi vya starehe wakati mke anataka Pesa ya kununua kiwanja amechoka kukaa nyumba ya kupanga, au mwanamke yeye ni kununua nguo za fasheni mpya iliyoingia mjini hata kama ni gharama kubwa wakati mtoto anahitaji ada ya shule.
Kitu cha msingi ni kuwa na malengo ya muda mrefu na muda mfupi na kwamba kuwa na uelewano wa kujua nini kinunuliwe (bajeti).
Kuvaa ni muhimu na pia kuwa na vitu vya starehe ndani ya nyumba ni muhimu ila kupanga malengo na kuwa na mawasiliano mazuri hilo ndiyo jambo la kwanza.
Kaa pamoja, panga vitu vya msingi,
Tununue nini na kwa nini?
Tuwekeze wapi? na kwa nini?
Tuweke akiba kiasi gani kila mwezi na kwa nini?

Panga pamoja kila mmoja aelewe kwa nini hiki kinafanywa Badala ya hiki.

Kuwekeza kwa Busara na Hekima:
Mustakhabali wa maisha yenu ya miaka 5, 10, 20. 30, 50 ijayo ni sasa na jinsi mnavyotimia pesa na kupanga malengo.
Kuwekeza pesa katika business mara nyingi huwa na risk na risk ikitokea mara nyingi mmoja huanza kumlaumu mwenzake kwamba wewe ndo ulilazimisha tufanye hivyo.

Ni muhimu kushirikiana katika kuweka uamuzi wa pamoja mnapowekeza pesa kwenye miradi au business pamoja.
na piakukubaliana risk yoyote ikitokea pamoja kwani kama ni faida ni yenu wote na kama hasara ni yenu wote.
Katika hali ya kawaida katika ndoa inaonesha kwamba wanaume ndo wanaongoza kwa kujitosa kufanya kitu chochote (business) hata kama kuna risk kubwa baadae na wanawake huogopa sana kuwekeza katika kitu ambacho hawana uhakika.

Kitu cha msingi ukitaka kufanikiwa katika business au maisha lazima uwe risk taker kwani ukifanikiwa unaweza kubadilisha uwezo wa kifehda wa familia yako, ingawa unahitaji kufanya utafiti mkubwa kabla ya kuwekeza pesa zako na uwe na njia ya kupunguza risk inapotokea au Usibebe mayai yote kwenye kikapu kimoja kwani kikidondoka umeumia.

Kutunza Siri zinazohusu pesa
Wengine wanaamini siri za pesa walizonazo bila mume au mke kujuahazina ubaya sana kwenye ndoa.
Ukweli ni kwamba unahatarisha sana ndoa yako kwa kuficha siri za pesa ulizonazo au business unazofanya bila mke au mume kujua.
Wengine wameficha wake au waume fedha walizonazo katika Account walizonazo
Wengine hata wakinunua vitu hudanganya bei waliyonunulia vitu.
Na wengine hujiingiza katika business ambazo mke au mume hajui na huko ikitokea hasara au tatizo ndo hurudi kusema kwa mke au mume, hapo ndo zogo linaanza.

Wengine huwapa ndugu zao au marafiki zao pesa nyingi bila mke au mume kujua na siku mke au mume akijua kwamba mmoja alitoa pesa bila kuambiwa hapo tena moto unalipuka.
Ni muhimu kutoficha siri zozote kwa mke au mume wako kwani lolote linaweza kutokea wakati mwingine hata kifo, utatesa watoto bure kwa kuficha siri muhimu kama hizo ambazo si siri bali jambo muhimu kwa mke au mume wako.

Kupanga kwa ajili ya fedha ya dharura
Wengi hudhani haina haja kuwa na pesa ya dharura
Na wengine hupanga fedha ya dharura kwani chochote kinaweza kutokea, anaweza mtoto kuugua au ninyi wenyewe mmoja kuugua ghafla pia kunaweza kutokea mchango wa dharura bila kujua.
Hata kama una kazi nzuri kama hujajipanga vizuri kwa ajili ya mambo ya dharura unaweza kushangaza mke au mume kwani lolote laweza kutokea.

Matatizo hayataisha hadi tuwe tumekufa, kupangilia vizuri masuala ya pesa kutawezesha ndoa yako kuwa yenye afya na imara.

(1 Timotheo 6:10)

Saturday, April 19, 2008

Asante sana


Hii ni kuhitimisha mwezi mmoja tangu blog hii ianzishwe.
Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wote waliochangia mawazo, walio toa ushauri na wote waliopitia kusoma posts mbalimbali.
Mungu awabariki sana

Friday, April 18, 2008

Weekend Njema

Nakutakia weekend njema kwa kuangalia hii movie www.dashpoemmovie.com

Tunatofautiana Kimwitikio

Kama vile wanapigilia misumari!
Kuna tofauti kubwa sana ya maana na mwitikio wa mapenzi kati ya mwanaume na mwanamke.

Wanaume kawaida wanauwezo wa kutenganisha mwili na moyo
(Body and Heart)
Kwa upande wa wanawake tunaweza kusema wao wamekomaa kimapenzi kuliko wanaume kwa sababu kwao kutenganisha mwili na moyo inakuwa vigumu na wakati mwingine haiwezekani.
Mwanamke anapompenda mwanaume huanza na hisia za ndani za moyo wake moyo wake then hisia za nje za mwili wake;
wakati mwanaume anapompenda mwanamke huanza kupenda kuanzia hisia za mwilini mwake kwenda then hisia za moyo wake.
Ni rahisi mwanaume kukwambia anakupenda kumbe hakupendi anakutamani tu na wanawake wamekuwa wanaumizwa sana na wanawake kutokana na hii style yao ya kupenda kwa kumuweka mtu moja kwa moja kwenye moyo wake.
Utafiti mwingi unaonesha kwamba wanawake wengi huwa hawafurahii kufanya mapenzi na mwanaume asiyempenda;
wakati wanaume wanaweza kufurahia na kupata raha ya mapenzi (kufika kileleni) hata kwa mwanamke asiyempenda.
Ndiyo maana mwanaume anaweza kutembea na mwanamke yeyote hata kama ni mbaya kila idara ukilinganisha na mke wake.
Ndiyo maana matukio mengi ya ubakaji hufanywa na wanaume.
Wanaume wanaweza kutenganisha upendo na kufanya mapenzi (love and sex)
Wanawake hutazama kufanya sex ni kitendo cha ziada baada ya upendo wa kweli na wakati mwingine hufanya mapenzi ili kuimarisha mapenzi kwa mwanaume, wakati wanaume sex ni kwa ajili ya kufurahia tu siyo lazima awe anampenda mwaname anataka kufanya naye sex.Kwa mwanaume kufanya sex ni kitu kinachofanywa nje ya mwili (out-of-body experience) kwa sababu viungo vyake vya kufanyia vya sex vipo nje na anapofanya mapenzi anakuwa anafanya kitu kwa mtu mwingine (mwanamke) kama vile kupigilia msumari kwenye ukuta;
Kwa upande wa wanawake viungo vya sex vipo ndani ya mwili na kwao kufanya mapenzi ni kama kumkaribisha mtu ndani ya nafasi ya ndani yake, hivyo inakuwa ngumu kutenganisha mwili, moyo na hisia zake.
Kama ilivyo kwa watu wote kwamba mtu mgeni akiingia nyumbani kwako hutajisikia raha kwanza au hutajisikia salama hadi ufahamiane, ndivyo wanawake walivyo.
Kwa mwanamke kufanya mapenzi na mwanaume asiyemfahamu au mgeni au asiyempenda ni sawa na mtu anayeingilia mipaka ya shamba la mtu, (trespace)
Kumvamia mwanamke bila kuonesha upendo wa kweli ni sawa na kuvamia mipaka ya mashamba ya watu, au ni sawa na kuingia kwenye nyumba za watu bila kukaribishwa.
Hivyo wanawake kwao ni ngumu kutenganisha love na sex
Wanapenda kuwa na ukaribu na mapenzi ya kweli ili kumruhusu mtu kuwa naye kitandani na kuingia kwenye nafasi yake ya siri kufanya mapenzi.
Ndiyo maana huwa wanajisikia kutumiwa na kuumizwa na mwanaume ambaye haoneshi upendo wa kweli.
Wanahitaji mwanaume anayewasililiza, anayewapenda, anayewajali, anayekuwa tayari wakati anamuhitaji, mwanaume anayebembelezam, mwanaume ambaye anajua kuwahudumia wao kama viumbe rasmi na maalumu Mungu ametoa zawadi kwa wanaume duniani.
Swali
Je Mumeo ni mwanaume anayepigilia misumari tu? au ni mwanaume anayeingia kwenye mipaka ya mashamba ya watu? au ni mwanaume anayeingia kwenye nyumba za watu bila kukaribishwa?
Jibu
Jibu unalo wewe kama ni mwanaume una kazi ya kufanya na kama ni mwanamke una kazi pia ya kufanya katika hili, Nawatakia weekend njema.
Thursday, April 17, 2008

Mkataba wa Ndoa Ukivunjika, Unahaki kudai Zawadi ulizotoa

Kitendo cha kuvalishwa pete kinaweza pia kuchukuliwa kuwa ni ushahidi wa kuwepo kwa ahadi ya kuoana
MKATABA wa kufunga ndoa ni mkataba kama mkataba mwingine wowote unaotambulika kisheria.
Mkataba wa kufunga ndoa unaweza kufanywa kwa njia ya mdomo, mmoja wa wanaokusudia kufunga ndoa kupendekeza kwa mwenzi wake kuwa wafunge ndoa.


Kwa habari zaidi Jiunge na Kaka Lusungu Hemed wa Gazeti la Tanzania Daima


Je ni Size ya Kiatu au Mchezaji Mwenyewe

Kwa wanaojua Mchezo Soccer; Kitu cha Msingi si Size ya Kiatu, Bali ni Skills za Mchezaji Mwenyewe ndiyo Zinawezesha Mchezo uwe mtamu na Kisha Magoli ya Kutosha.
Maswali ambayo huwasumbua sana Wanandoa wengi na yamefika mezani kwa madaktari wa mambo ya afya na mahusiano ni kuhusu wanawake kutofika kileleni (orgasm) na wanaume kumaliza haraka tendo la ndoa (ejaculation) na pia, je kuna uhusiano wowote kati ya mwanamke kufika kileleni na size ya kiungo nyeti (penis) cha mwanaume?

Ukiangalia haraka unaweza kusema hayo mambo mawili yanafanana; kwani kama mwanaume anaweza kumaliza haraka (kukojoa au kufika kieleleni), ina maana ni dhahiri mwanamke atakosa kufika kilele kwani mwanaume anakuwa alishamaliza zamani,
Lakini ukweli ni kwamba kama mwanaume atamuandaa mwanamke vizuri basi hata kama huwa anawahi kumaliza haraka (dakika 2) itakuwa haina shida.

Pia watu bado wanajiuliza, ni size gani na urefu gani unafaa kwa kiungo nyeti cha mwanaume kuhakikisha mwanamke anafika kileleni?
Je ni udogo kiasi gani unafaa kumwezesha mwanamke kufika kileleni?

Wapo wanaume kutokana na walivyoumwa kuwa na umbile dogo automatically hujasikia inferior au vibaya na kujiona kama vile hawana uwezo wa kuwapa wapenzi wao mapenzi halisi na kuwafikisha kule wanataka na matokeo yake wengi huwa hawapo wazi kujiachia kwa wake zao au wanaogopa hata wake zao kuona na kuwapa uhuru kukifurahia hicho kiungo nyeti na adimu wakati wa tendo la ndoa.

Kila mwanaume ana kiungo tofauti kama ilivyo kwa alama za vidole vilivyotofauti kwa kila binadamu.
Ukubwa au kimo cha kiungo si msingi wa ufanisi wa utendaji wa tendo la ndoa bali muhusika mwenyewe ndiyo msingi wa mafanikio katika tendo la ndoa.
Huhitaji kuwa mjinga kiasi hicho kudhani kwamba urefu au ufupi, unene au wembamba wa penis ndiyo unafanikisha mke wako wako au mpenzi wako kufikia kilele; badala yake unaweza kumsababishia maumivu na kumkosesha raha ya mapenzi.

Hata mwanaume mwenye penis ndogo anaweza kuwa mtaalamu wa kumfikisha mke wake katika furaha ya kweli katika tendo la ndoa.
Njia pekee ni kijifunza jinsi ya kufanya mapenzi vizuri, jinsi ya kuwa partner mzuri.

Huo ni mwili wako upende, jifunze kuutumia, jitahidi kuutumia kwa ubunifu na kwa kimahaba zaidi.
Mbusu na kumpa mgusu wa mwili mpenzi wako kwa muda mrefu hadi unahakikisha amenyegeka vizuri kwa kumchezea sehemu zote ambazo ukimgusa anapata raha inayomuwezesha kuwa hot kwa kuwa ni partner wako; mwili wake wote ni mali yako na ni wewe, hivyo safiri kila sehemu ya kiungo cha mapenzi kwa kadri unavyoweza kuliko kukimbilia kumwingilia wakati hata hajanyegeka.

Amini, usiamini kila mwanamke anapenda mwanaume au mume ambaye ana kipaji, talent, ana ubunifu, aliyemtaalamu anayeweza kumpa romance ya uhakika na si kuwa na penis kubwa tu bila ujuzi then baada ya dakika 2 upo pembeni unapiga usingizi wakati partner wako anaugulia kwa kuachwa kwenye mataaa.
Hapo ndipo utasikia mwanamke anasema hajisikii kama unampenda anaona kama vile unamtumia tu ili kutimiza matakwa yako ya mapenzi.

Kuwa na kiungo kidogo siyo kosa wala uhalifu bali umeumbwa hivyo na kuujua mwili wako na kujua majibu sahihi ya mahitaji ya kimahaba kwa mke wako hiyo ndiyo akili na unaonekana mwanaume Smart kwani wewe ndo unajua kupenda, unajua mapenzi.

Kuhusu mwanaume kumaliza haraka, pia si kosa wala uhalifu hata kukufanya ujione si lolote, badala yake elekeza jitihada katika kukabiliana na hilo tatizo na inawezekana kwa kupata ushauri wa daktari au kufanyiwa maombi au deliverance hahaha!.

Kitu cha msingi unatakiwa kujua kwamba kuna tofauti kubwa sana za kijinsia kati ya mwanaume na mwanamke.
Kwa asili mwanaume hupenda mara mwanamke akiwa uchi yeye mara moja aingize na kuendelea na mchezo wakati mwanamke yeye anahitaji maandalizi, jitahidi kuwa na muda wa kutosha wa foreplay kwa mke wako zaidi ya dakika 10-15 ili awe tayari kwa tendo la kuingiliwa na wewe.

Na kila mwanamke ana namna yake ya kufikishwa kwenye raha mwingine atapenda aina fulani ya mkao na mwingine atapenda aina nyingine ya mkao, mwingine atapenda achezewe kisimi na mwingine atapenda achezewe chuchu, na mwingine atapenda sehemu nyingine hivyo mwanaume anahitaji kuwa mvumilivu na sharp kumsoma mke na kujua ni kitu gani anahitaji na wapi anahitaji kuguswa zaidi ili afike huko kunako raha yenyewe.
Pia mawasiliano wakati wa faragha yenyewe ni muhimu; kwa maneno na vitendo wengine hawasemi bali wanakuelekeza kwa mkono.

Hebu tuangalie aina za Nne za wanaume wanamaliza haraka na sifa zao:
Aina A:

Huyu hajijui kama ni mtu wa kumaliza haraka (dakika 2), anapotaka mapenzi anamuita mke wake, then akishamvulia nguo ni kuingiza na fanya dakika 2 amemaliza, hajali lolote, hajui mwanamke ana kitu kinaitwa kufika kileleni, hajawahi kusikia na hana mpango wa kujua, anajua anachofanya ni sahihi.
Tendo la ndoa akijitahidi ni dakika 5

Aina B:
Anajua sana kwamba mwanamke anatakiwa afike kileleni ila anajifanya hajui. Tofauti na (Aina A) hapo juu, yeye akiona mwanamke anaugulia kwa kuachwa solemba yeye hujifanya ndo mwanamke amefika kileleni, na wala haulizi kwa mke wake kama hivyo ndo kufika kileleni ili apate ukweli.

Aina C:
Anajua tatizo lake, hafurahii kabisa hii hali na anataka kumuona Daktari ila anaona aibu na anasema hana muda wa kwenda kumuona Daktari au mshauri yeyote wa mambo ya Ndoa. Anajitahidi kwa kumuandaa mke wake kwa kubusu na kumpa migusu ya kimahaba ya kila aina, Ila yeye akiwa tayari tu anaacha kuendelea kumwandaa mke wake na badala yake anaingiza na kumalizia then imetoka, hafurahii ile hali ila ndo hivyo maisha yanaenda.

Aina D:
Huyu anajua tatizo lake na pia anajua umuhimu wa mke wake kufika kileleni;
hivyo anaanza kwa kumpa mke wake romance ya uhakika hadi anafika kileleni kabla hajamwingilia.
Akiona mke yupo katika hali inayoonesha ameridhrika na amefika kileleni kwa njia za stimulation ndipo na yeye anaanza kufanya mapenzi kisha anamaliza huku mke wake amefurahi kwani amefika kule kunatakiwa.

Hii ina maana kwamba kama mwanaume ni mjanja na ana akili ya kujua yeye ni mtu wa kuwahi kumaliza na anamwandaa mke wake hadi anaridhika, basi kwa ke kuwa mtu wa kumaliza mapema haina tatizo na anaweza kuwa na mahusiano mazuri na yenye furaha katika mapenzi na mke wake huku juhudi zingine za kumuona daktari na maombi zikiendelea.
Pia afahamu kwamba hahitaji kuwa mchoyo na mtu wa kujitanguliza yeye (selfish) na badala yake kumtanguliza mpenzi wake afike kileleni kwanza badala yake.

Kiukamilifu; kufanya mapenzi vizuri kwa mwanamke ni penis ya kawaida, kumuandaa vizuri na kwa muda wa kutosha, busu za kutosha sehemu anazopenda, kumpa mgusu wa mwili kwa mikono yako sehemu zote zinazompa raha ya mapenzi, kukaa ndani yake kwa muda mrefu huku akipata msuguano wa muda mrefu na kwa mwendo anaotaka yeye kutokana na anavyoitikia, kujua mikao yake ya mapenzi anayopenda ili kupata raha zaidi na zaidi kufahamu na kumpa kile anahitaji ili kufika kileleni.

Kumbuka kama amawahi kufika kileleni maana yake anajua vionjo muhimu vinavyoweza kumfikisha kileleni hivyo mwanaume mbunifu wa mapenzi lazima unamsikiliza yeye akuongoze kule anataka kwenda kwani kwa mwanume kufika kileleni kwako ni kitu ambacho kipo.

Na Mwisho,
Je mwanamke unawajibu gani katika kuleta usawa kuhakikisha utendaji wa mapenzi unakidhi haja yako?
Jibu;
Unahitaji kuwa wazi kuongea na kuelezea kile Unahitaji kufanyiwa tena kwa uwazi na uhuru. Usibaki kimya na kulala tu usingizi wakati wa tendo ndoa ukidhani kwamba utafika kileleni, ongea kwa mumeo mwambia kwa upendo kabisa nini Unahitaji, kwani ukipoteza hamu ya mapenzi basi hii raha ya mapenzi sahau kabisa kwani unakuwa umechimba shimo ambalo huwezi kutoka.

Wednesday, April 16, 2008

Pesa katika Ndoa

Pesa ni kuweka na kuchukua, je wewe ni mtu makini Kuweka au Kuchukua? Hakuna mtu ambaye huwa anaingia kwenye Ndoa huku anajua hiyo ndoa Haitafika mbali.
"Wahenga Walisema Kinga ni Bora kuliko Kuponya".
Jinsi Unavyokuwa na Ufahamu mkubwa wa nini kinaweza kutokea baada ya kuoana hiyo itakuwezesha Kuzuia na Kujiandaa kukabiliana na changamoto zitakazotokea mbele ya safari ya Ndoa.
Matatizo yanayohusiana na pesa yamekuwa chanzo kikubwa cha migogoro ya ndoa nyingi. Matatizo haya huhusika moja kwa moja na jinsi ya kusimiamia na uaminifu katika pesa.
Kama hujaoa/olewa bado unaweza kukaa partner wako mkaongea masuala ya pesa na pia ukapata ufahamu wake kuhusu suala zima la pesa ili mkiingia kwenye ndoa unajua kabisa mwenzangu ni mtu wa aina gani lipokuja suala la pesa na uchumi kwa ujumla.
Na kama upo kwenye ndoa naamini umemchunguza mwenzako na kujua ana tabia ipi likja suala la pesa.
Hapa chini kuna maswali ambayo kama mwongozo tu hasa pale ynapojibiwa kwa ukweli na uaminifu ambayo inaweza kukusaidia kujua mtazamo wa mwenzako kuhusu pesa.
1. Wakati unafanya shopping huwa unafikiria kitu gani hasa?
(a) Vitu unavyonunua.
(b) Pesa unayotumia kununua hivyo vitu

2. Ikitokea mwisho wa mwezi ukapungukiwa pesa hata kama una mahitaji muhimu?
(a) Nafikiria Kukopa
(b) Sinunue kitu chochote

3. Huna Fedha (cash) na unataka kununua vitu na upo mbali na Bank yako utatoa uamuzi gani?
a) Nitatumia ATM card niliyonayo kwenye ATM machine iliyojirani
b) Sitanunua kitu kwani sipendi kutumia ATM card kwani kuna gharama za kutumia kadi

4. Huwa unajisikia una uwezo kifedha pale ikiwa?
(a) Una nunua kile kitu umekuwa unahitaji.
(b) Unapoiweka fedha kama mali (save).

5. Kwa jinsi unvyowekeza sasa na kuweka akiba.
(a) Hujui kabisa ni kiasi gani utakuwa nacho siku ukistaafu kazi.
(b) Unajua kiwango halisi cha pesa utakuwa nayo utakapostaafu kazi.

6. Unapoweka pesa bank kwa ajili ya akiba.
(a) Unajisikia ni wajibu (inaumiza kidogo)
(b) Unajisikia ni raha sana

7. Ukiwa na rafiki zako, unapoongelea masuala ya pesa huwa hukosi kutaja kipi ?
(a) Punguzo la bei uliyopata
(b) Punguzo la mali uliyonunua

8. Kama umepandishwa cheo utasherehekea vipi?
(a) Kwa kununua kitu maalumu kwa ajili yako mwenyewe
(b) Utaruka hewani na kushangilia “waoooooo”

Kama Amejibu kwa kuchagua (a) nyingi basi ni Mtumiaji mzuri wa pesa (Spender) na kama amejibu kwa kuchagua (b) nyingi basi ni mweka akiba mzuri (Saver)

Kama kuna tofauti kubwa yaani mmoja ni mtumiaji na mwingine anapenda kuweka akiba basi uwezekano wa kuwa na migogoro inayotokana na fedha ni kubwa, lakini haina maana kwamba itakuwa migogoro bali changamoto kamili inayokukabili mbele ya safari na unabidi ujiweke sawa jinsi ya kushughulikia Tatizo la pesa ndani ya ndoa.

Na kama partners wote ni Watumiaji; maana yake hakuna atakayekuwa na break ya kuzuia matumizi na matokeo yake mwisho wa njia kunakuwa zogo na matatizo ya fedha kwani mnatumia bila kuwake akiba.
Madeni huumiza ndoa, uwe mwangalifu.
Na kama wote ni watu wa kuweka akiba; hiyo ni nzuri ila mnahitaji wakati mwingine kufurahi kwa kutumia pesa kwa ajili ya just for fun.
Maana mnaweza kujikuta ni mabahiri wa ajabu kiasi kwamba hata raha ya kutumia pesa hakuna.
Kitu cha msingi ni kuhakikisha kila mmoja anamsoma mwenzake kujua mwenzake ana mtazamo gani kuhusu suala la pesa.
na pia kujua ni jinsi gani mnaweza kuhakikisha mnafurahia maisha ya sasa na wakati huo huo mnawekeza fedha na miradi ambayo mbele ya safari mtakuwa na fedha kwa ajili ya kusomesha watoto na hata wakati mkiwa wazee.
Wakati ni sasa usisubiri ukiwa mzee ndo unapanga mipango mikubwa ya kuwekeza anza hata kabla hujaoa au kuolewa.
Kama umeolewa au umeoa; panga malengo, timiza ndoto zako.
Kuwa na ndoa imara yenye afya ni pamoja na kuwa na mafanikio katika Creation of Wealth kwa ajili ya maisha yenu miaka 5, 10, 20, 50 au 100 ijayo
.