"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, April 24, 2008

Honeymoon (Fungate) -3-

(Sasa safari imeiva kwenda honeymoon) Vitu Muhimu Kubeba unapoenda Honeymoon:
Kujua ni vitu gani utavibeba kwenda navyo honeymoon ni hatua muhimu sana na inabidi uwe makini ili ukifika huko usiwe na muda wa kulalamika kwamba, kuna kitu ulipaswa kuwa nacho lakini umekisahau.
Pia inabidi uwe makini, maana unaweza kubeba vitu ambavyo hata hutavitumia.
Kitu cha msingi ni kuangalia kwanza yale mambo utaenda kufanya ukiwa huko, aina ya hali ya hewa, je ni sehemu za baridi au sehemu za joto?
pia muda utakaotumia kukaa huko na huyo mpenzi wako.
Unaweza pia kufuatilia kuona je sehemu mtakayo tumia (hotel) kwa honeymoon yenu inatoa vitu gani kwenye huduma zao ili msije beba vitu ambavyo nao wanatoa pia.
Suala la nini kinafaa kuchukua, ni muhimu kujadiliana pamoja na mwenzi wako ili kupunguza vile vitu ambavyo mnaweza kuvibeba wote na kuongeza mzigo wa bure.
Ifuatayo ni Orodha ya vitu Muhimu Kuvibeba kwa Ajili ya Honeymoon.
Begi (Luggage)
Ni vizuri kubeba begi ambalo si kubwa sana hadi linachosha kubeba.
Usichukue begi kubwa au mizigo mikubwa sana, zingatia kwamba mnaenda kupumzika (relax) baada ya hekaheka nyingi za harusi na pia kuanza maisha mapya na yule anayetimiza ndoto zako hapa duniani.
Haina umuhimu kubeba nguo zote na kujaza kwenye begi, kitu cha msingi unaweza kubeba zile nguo za kawaida (casual wear) nguo za kuvaa mchana, nguo za kuvaa usiku, nguo za kuvaa chumbani na nguo za ndani (inner wear).
Nyaraka Muhimu (Documents)
Vitambulisho, ATM cards (pesa), orodha ya namba za simu muhimu, ticket, passport nk.
Pia inategemea umesafiri kwenda sehemu gani kwa ajili ya honeymoon, lolote linaweza kutokea, iwe ajali au dharura hivyo unahitaji kuwa na nyaraka muhimu ili kikitokea kitu chochote inakuwa rahisi kupata solution hata kuomba msaaada.
Nguo
Mwanaume
Mwanaume usisahau vitu vifuatavyo, Mkanda (hiari), Mashati, Viatu, Sandals, Kofia (fun), Jacket au koti (kama kuna baridi sana), Tshirts, bukta (shorts), Nguo za ndani za kutosha, socks na nguo za sports na vingine unavyooona wewe vitakufaa

Mwanamke
Mwanamke usisahau vitu vifuatavyo Bras, Kofia, Jacket au koti (kama kuna baridi), Vito kama herein nk, Nguo za ndani za kutosha na zenye style tofauti na rangi tofauti, Sandals, Skirts na tops pia nguo zingine ambazo wewe unaona zitakufaa.
Camera, CD player, Laptop, memory card, Simu (mobile)
Hakikisha kama umebeba simu unachukua na chaja yake.
Kupiga picha ni muhimu sana hasa kutokana na wakati muhimu kama huo wa ku-relax na mwenzi wako na kutengeneza kumbukumbu muhimu za maisha mapya na msingi wa maisha pia.
Pia mnaweza kusikiliza mziki mzuri mnaopenda wakati mnajipumzisha chumbani au wakati wa mambo fulani fulani hapo kitandani.
Kuna hotel zina wireless connection ya internet hivyo mnaweza kutumia laptop yenu kuweza kujua nini kinaendelea duniani.
Siyo lazima uwe na vitu vyote nimevitaja hapo juu ni uamuzi na pia kama mnavyo.
Pia ni muhimu kuwa na simu hasa ikitokea dharura.
Pia mnaweza kubeba dawa za kutulia maumivu kama kichwa nk, kalamu na karatasi na miwani .
Afya, usafi na kuoga (Bathroom)
Mwanaume
Ni muhimu kubeba vitu vifuatavyo, dawa ya kusukutua (mouthwash), dawa ya meno(toothpaste), mswaki, Shampoo, nyembe za kunyolea (razar) na shaving cream, kitana, Deodorant, na taulo la kuogea pia mints na vitu vingine unavyovifahamu.
Mwanamke
Ni muhimu kubeba vitu ambavyo mume wako havitumii kwani wewe na yeye ni kitu kimoja kwa hiyo unahitaji kubeba vitu vile ambavyo ni kwa ajili yako kama vile Pads and tampons, mswaki, tissue, taulo na vipodozi vyote unavyoona vinakufaa.
Mahaba (Romance)
Kwa kuwa mnaenda kufanya mapenzi kwa mara ya kwanza (kama ni mabikira) ni muhimu kujiandaa vizuri na kama ni mara ya kwanza kwa mwanamke kufanya tendo la ndoa hii ni kudhihirisha kwamba atahitaji lubricants kwa ajili ya kulainisha (njia) ili kupunguza maumivu kwa mara ya kwanza.
Na kama hamuhitaji kupata mtoto mapema, naamini inabidi mfikirie mtaenda na kifaa gani au njia gani ya birthcontrol (kuzuia mimba) au Njia ya asili (muwe mmepanga tarehe vizuri)
Pia ni muhimu kuwa na sabuni zinazozuia bacteria na fungus kwani tendo la ndoa kwa mara ya kwanza husababisha maambukizi ya fungus na bacteria kwenye viungo vya uzazi vya mwanamke.
(Tutaangalia kwa upana zaidi kwenye somo la Lubricants kwa ajili ya mwanamke bikira)
Tutaendelea na somo.............................................................
No comments: