"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, April 21, 2008

Honeymoon (Fungate) - Utangulizi

Hicho kitanda kione tu! kama ulipitia hapo una hadithi ya kuongea na kama bado, kuna hadithi nzuri sana inakusubiri, utamu ni pale wote mkiwa zero (bikira) na hata siku moja hujawahi kuona nini sijui..... halafu unaambiwa twende tukaoge pamoja then mrudi hapo hapo kwenye hako kakitanda!
Honeymoon ni nini?
Ni wakati ambapo wanandoa wapya huenda sehemu mbali na mahali wanapoishi (holiday) baada ya siku ya harusi yao, kwa ajili ya kupata uzoefu mpya wa maisha mapya ya mahusiano ya kimapenzi katika ndoa.
Pia wanandoa wapya huenda sehemu ambayo ndugu na marafiki hawawezi kuwaingilia na shughuli yao hiyo yakufahamiana kimwili na kiroho na kupeana uzoefu mpya wa kuanza kuishi pamoja.
Pia ni wakati mzuri kwa wana ndoa kupumzika baada ya shughuli nzito ya harusi.
Pia ni mwezi mzima wa maisha ya ndoa tangu kuoana.

Kwa nini Honeymoon na si jina lingine?
Simulizi za kwanza kabisa kwenye karne ya 16 hasa huko kaskazini mwa Ulaya, kulikuwa na tabia ya kijana wa kiume kumteka binti (kidnap) anayetaka kumuoa na kuingia naye mitini hadi mwezi upite huku ndugu wa binti wakimtafuta.
Huo mwezi mzima ambayo kijana wa kiume alikuwa na binti a huku anaendelea na uhusuano wa mapenzi ulikuwa unaitwa ni honeymoon na haikuwa kesi.
Muhimu ilikuwa lazima ujitokeze baada ya mwezi na pia ndugu wa binti walikuwa wanakonyezwa na ndugu wa kijana kwamba binti yao ni salama so wasubiri mwezi.
(Pia kuna makabila ya kiafrika hii system ilikuwepo)

Pia simulizi nyingi za kale huko misri na baadhi ya nchi za Scandinavia zinaonesha kwamba wana ndoa wapya walikuwa wanapewa kinywaji kinachotokana na asali (Mead) kunywa kila siku kikombe kimoja kwa mwezi mzima.
Ndiyo wakaita honeymoon.
Na Pia ulikuwa ni mwezi wa kwanza kwao kwa ajili ya kuhakikisha wanafanya kweli ili kupata mtoto kwa sababu waliamini hiki kinywaji kilikuwa kinawapa viini muhimu kwa ajili ya kuhakikisha uzazi na afya njema kwa wanandoa wapya.

Pia kuna simulizi zinazofananisha maisha ya ndoa kama asali kwa maana kwamba mwezi wa kwanza tangu kuoana ni mtamu kama asali kuliko miezi mingine,hivyo kuitwa honeymoon.
Utamaduni wa honeymoon unahusiana sana na wanandoa ambao ni mabikira (mwanaume na mwanamke).
Kuna watu wanaenda honeymoon wakati wanajuana kimwili tayari (sex) na wengine walishaishi pamoja tayari, hiyo haitaitwa honeymoon bali vacation tu ya kawaida kama zingine.

Honeymoon ni mahali pa kujenga msingi wa nyumba
Honeymoon si tu kuwa mbali na marafiki na ndugu ni mahali ambapo unaenda kujenga msingi wa ndoa yako na huyo mume na mke mpya.
Ni wakati ambapo unaenda kuyafukia maisha yako ya zamani na kuanza maisha mapya ukiwa na mtu mwingine kabisa mpya.

Siku ya ndoa mnakuwa mmeunganisha physically tu, lakini mkiwa honeymoon mnaunganika katika mambo yote kimwili, kihisia, kiroho na kuhakikisha ndoa inakuwa ndoa kisheria.
Honeymoon ni wakati wa kujenga sura mpya ya maisha ya pamoja mtakayokuwa nayo hadi kifo kitakapowatenganisha.
Unapopanga jinsi harusi itakavyokuwa usiweke nguvu nyingi kwenye harusi ukasahau kwamba unahitaji muda mzuri wa kuwa honeymoon na mke/mume mpya kwa ajili ya kujenga msingi mpya.
Ndoa nyingi zogo huanzia kwenye honeymoon so unahitaji kuwa mwangalifu na makini zaidi kuhakikisha hii likizo yako ya honeymoon inakuwa honeymoon na si vinginevyo.
Tutaendelea na mambo ya msingi ya kuzingatia huko kwenye huo mwezi mtamu kama asali............

No comments: