"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, April 2, 2008

Love Bank Account


Ndoa au Mahusiano Yoyote ya Kimapenzi
ni
Mfano wa Bank Account Tulizonazo.
Unapopata mwenzi wako ni kama vile umefungua Bank Account na katika kuendelea na maisha au relationship kila siku unafanya transaction ambazo ni either Kuweka pesa (Deposits) au Kutoa pesa (Withdraw)
Pia ni muhimu sana kujua hali ya Account yako bank ipoje; kwani unaweza kwenda kuchukua pesa ukakuta hakuna kitu, kumbe ume-overwithdraw zaidi kuliko unavyotakiwa.
Hakikisha kila Wakati Account Yako Ina Pesa.

Katika mahusiano (relations) iwe ndoa, uchumba au vyovyote vile; kila siku uanhitaji kujua kama umeweka pesa (deposits) au umetoa pesa (withdraw)
Na pia ni muhimu sana kujua mwenendo wa Bank Account yako ili ujue kama unaweza kufunga kabisa accocunt au kuendelea nayo.
Love Bank Account ni muhimu sana katika maisha ya kila siku ya mahusiano na kama vile mti au mmea wowote unahitaji kutunzwa ili uweze kustawi na Love bank Account pia inahitaji kuwa na Pesa muda wote ili iweze kudumu.

Unapomkubali mtu kuwa mwenzi wako (Soulmate) maana yake umefunguwa Love Bank Account kwake.
Ni jukumu lako kuhakikisha kila siku Kuna Balance ya pesa za kutosha ili inapotokea unahitaji kufanya manunuzi yoyote basi kuna akiba ya kutosha.

Unapompa feeling (hisia) nzuri za kukuhitaji wewe zaidi maana yake unafanya deposits, unaweza pesa za kutosha.
Kuna mambo mengine katika mahusiano watu hudhani ni vitu vidogo sana lakini ni muhimu sana na vina maana kubwa,
Unapo mwamini (trust),
unapompa zawadi haijalisha ni nini,
unapompa muda, unapo mpa busu,
unampa maneno ya ya sifa na kutia moyo,
unampomsikiliza,
na kumjali hapo
unafanya Deposit na Account yako kwake inajaa.

Lakini unapokuwa
humjali,
unampa maneno mazito na magumu yanayoumiza (criticism),
Ignore,
hutunzi ahadi zako
wala kumlinda na kumpa kile anahitaji
hapo una withdraw kwa kiasi kikubwa na inawezekana unafanya over withdraw ya hiyo Account
na siku mambo yakiwa mambo kuna kuwa hakuna balance, na zogo linaanza.

Please Hakikisha Love Bank Account ya Mkeo, Mumeo, Mchumba Wako, Mpenzi Wako Umeifanyia Deposits za Uhakika then Tutajua wewe Unajua Kupenda.

Ubarikiwe na Bwana

1 comment:

Hellen said...

Kwa topic hii mpendwa nina mfano mmoja ambao ni hai. Kuna rafiki yangu ambaye amebahatika kubata mume mzuri sana. Mume anayemsaidia kazi zote za ndani, kupiga deki, kufanya usafi wa choo na bafu, kufua, kuchota maji. Ila la ajabu huyo rafiki yangu sasa anamuona mume wake kama vile ni mjinga au sijui niseme kuwa yy anajiona ni kichwa sasa, badala ya kumshukuru mungu kwa kumpa mume mwema mume anayemtimizia mahitaji yote, kuanzia mavazi, mapambo, kusaidia usafi wa nyumba na kuhakikisha kuwa maji hayakosekani ndani ya nyumba na kuwa chakula kipo stoo cha kutosha. Sasa ubaya ni kuwa yule mume amevumilia kwa muda wa miaka minne na kuchoka, sasa amebaki na kovu moyoni mwake kwa kuona kuwa mwenzake hataki kubadilika. Akimtajia mapungufu yake ili abadilike na wawe na furaha ndani ya nyumba yao yeye mke anasema kuwa "mimi ndivyo nilivyo" lakini anataka mume abadilike mfano aachane na marafiki wake, ndugu za mume wakija nyumbani ni matatizo ila nduguze wakija ni sawa. Anabagua wazazi wa mumewe ila wazazi wake wanapokelewa vizuri tu sasa vitu kama hivi mara nyingi vinavunja nyumba nyingi na kusababisha makovu na maumivu katika nyumba. Na kama mtu hajasimama katika Mungu na kuuelekea msalaba wa KRISTU ni wazi kuwa nyumba ndogo hazitapungua. Sisi kama wakristu na wana wa Mungu tunapaswa kuwa na hofu ya Mungu ili tuenende katika mwenendo mwema.