"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, April 4, 2008

Mambo madogo madogo ni muhimu pia

Weekend ni wakati mzuri kwa ajili ya kuhakikisha unakuwa na muda mzuri mpenzi wako, mke wako, mume wako, mchumba wako, soul mate wako, partner wako, honey au sweetie wako nk.
Naaamini utasema kwamba dunia ya leo mambo muhimu ni uchumi, kazi zetu nk, kitu cha msingi bila amani, upendo na furaha ktk nyumba zetu bado hata kama tutakuwa na pesa nyingi.

Kama wewe ni mwana ndoa jitahidi hii weekend kufanya mambo tofauti kabisa na jinsi unavyofanya kila siku hasa weekdays.

Kitu cha msingi ni wewe kuwa mbunifu kufanya vitu vidogo vidogo (kama unaweza kufanya makubwa fanya) ambavyo vitasababisha mwenzi wako akuone unamjali na unawajibika mahusiano.
Kama ni mwanaume unaonaje hii weekend angalau unasaidia kazi ndogondogo pale home kama vile
kutandika kitanda,
kupika kama unaweza,
kuwaandaa watoto,
kufanya usafi, kusaidia kufua nguo nk
just do it romantically,
Na ukitoka leo kazini unaonaje pia kama utaenda kununua zawadi yoyote kwa ajili yake, ingawa hii weekend zawadi muhimu ni wewe mwenyewe kuwa na muda na yeye.

Na kama ni mwanamke naamini utakuwa mbunifu zaidi kufanya vitu vipya kwani wanaume siku zote wanataka kitu kipya katika mahusiano.
Unaonaje ukihakikisha chumbani kunakuwa tofauti kabisa kuanzia
Kitanda na mashuka yake nk
marashi mbalimbali chumbani
na pia wewe mwenye kuhakikisha una nukia vizuri kwani smell of your body affects emotions, jipambe sawaswa tofauti na siku za kawaida kwa ajili yake,
Tafuta time kuwa naye yeye tu na kama hukupika wewe mwenye wiki zima jaribu this weekend kumpikia mwenyewe kwa mikono yako chakula cha uhakika.
Pia usisahau kumuombea mkeo au mumeo maana (maombi) ndiyo yatawahakikishia kwamba kitanda chenu shetani hapati nafasi kulala maana akilala, kuangalia TV kunakuwa raha kuliko faragha ya chumbani kwenu.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Kama wewe ni single na ndo upo kwenye process za Uchumba najua hii weekend umepanga mkutane mkaongee mipango yenu, nahisi tangu mmekutana wiki iliyopita umeona kama siku haziende, Mungu ni mwema weekend ndo hiyo.
Jitahidi unapokuwa na mke/mume wako mtarajiwa unatumia jina lake vizuri kwani kuna raha yake mtu ukimtaja kwa jina lake mwenyewe kama vile Mungu anavyojitambulisha kwetu kwa jina lake na kututaja majina yetu.
vijana wa siku hizi Badala ya jina mnatumia maneno kama ‘
"Oya twende zetu!"
"Hey nikununulie nini!"
Tumia jina lake hiyo inakupa point kwamba ni presentable
Pia tumia huo muda kumfurahisha kwa maneno matamu, yanayotia moyo ili kumsahaulisha na yale amepitia wiki zima, kwani hapo ndo mnaanza kutoa picha ya nyumba yenu jinsi itakavyokuwa.
Pia ni muhimu unapokutana naye Ongea mambo muhimu; siyo mambo ya watu wengine au ku-discuss michezo ya kwenye TV, muda mnaotumia kukaa pamoja na kuongea ni muhimu sana mtakuja kuukumbuka mbele ya safari
Pia angalia usichome daraja!

Nawatakia weekend njema na Mungu awabariki sana


2 comments:

Hellen said...

Unajua mambo madogo madogo ndiyo yanayojenga sana mahusiano ila kuwa wanaume ambao wao hufikiri kuwa mwanamke amefuata hela zake au utajiri wake kama anao au hata kama hana akijua tu kuwa mwenzi wake anamtegemea basi hiyo ni ishu. Kuna makabila piga ua hawezi kumsaidia mwenzi wake, kupika, kufua, kufanya usafi hata kuwaandaa watoto anajua hizo ni kazi za kike. wengine hata kazi ambazo anapaswa kufanya mwanaume zile zinazotumia nguvu pia hawafanyi wanawaacha wake zao wafanye. Utashangaa kuwa mwanaume anafanya kazi na mwanamke anafanya kazi na wote wakarudi late hours lakini bado mwanaume hawezi msaidia mwenzi wake kwa kuwa tu anajua kuwa ni kazi za kike. Kinachohitajika ni watu kuwa na hofu na Mungu kwanza na waijue dini ipasavyo then ndoa zetu zitadumu sana maana watu watakuwa na upendo wa kweli na watasaidiana kwa kila jambo

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Hellen Nashukuru sana kwa mchango wako wa mawazo naamini kama kila mwanandoa angefahamu wajibu na nafasi yake iwe kwa jambo dogo au kubwa ndoa zetu zingekuwa nzuri sana na tusingesikia mambo ya kuchokana, Tuombe Mungu kila mwana ndoa aweze kujitahidi kuimarisha ndoa yake kila iitwapo leo