"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, April 29, 2008

Maumivu wakati wa tendo la ndoa - 2-

Kichwani (brain & mind) ndiyo kiungo kikubwa cha tendo la ndoa, jinsi unavyojiweka kwenye akili zako inaweza kusababisha raha au maumivu ya tendo la ndoa(Picha kwa hisani ya clearingfiles)

Kwa nini ujisikie maumivu.

Maumivu wakati wa tendo la ndoa husababishwa au hutokana na sababu za kihisia na za pia (physical and emotional)
Ili kujua kwa nini maumivu kutokea ni vizuri kujua nini hutokea kwa mwili wa mwanamke wakati wa tendo la ndoa (sex)
Mwili wa mwanamke hupitia hatua nne (4) muhimu kukamilisha tendo la ndoa.

HAMU (dedire)
Hapa mwanamke hujisikia anataka kufanya tendo la ndoa


KUSISIMKA (arousal)
Hapa mwili husisimka kwa sehemu zake za siri (vagina) hutanuka urefu na upana pia hutoa majimaji yanayorahisisha mwanaume kuingia (penis penetration), kisimi hudinda na kuongezeka ukubwa, chuchu husimama na kusisimka, uterus hupanda juu nk


KUFIKA KILELENI (orgasm)
Hapa ni kilele cha mwitikio wa tendo la ndoa, misuli hujikusanya (contradict) na kumpa hisia kubwa za raha na utamu wa tendo lenyewe.


SULUHISHO (resolution)
Viungo vyote vinavyohusika na tendo la ndoa hurudi kwenye hali ya kawaida

Aina za maumivu na sehemu wakati wa tendo la ndoa kwa mwanamke zinaweza kutokea kwenye katika sehemu zifuatazo

Sehemu ya nje ya vagina, yaani vulva na huumia wakati inaguswa au kuwasha hata unapotumia baadhi ya sabuni na wakati mwingine kusababisha makovu au utando unaonesha kuna cheese.

sehemu ya tundu la kuingia kwenye vagina na sehemu ya ndani ya Vagina unayoungan na uterus.

Je ni kawaida mwanamke kupata maumivu hata kama hajaambukizwa magonjwa ya zinaa?
Kawaida kila mwanamke ana aina ya chachu au hamila (yeast) kwenye sehemu za siri zake za siri, na hii yeast ikiongezeka sana inaweza kusababisha kuwasha au maumivu wakati wa kukojoa mkojo wa kawaida na pia husababisha kutoa majimaji meupe mithili ya maziwa na hii hutokea kama mwanamke anatumia antibiotics au medication inayosababisha kuua bacteria wanaofanya hiyo yeast kutoleta madhala yoyote.

Hivyo ni jambo la kawaida kwa mwanamke kujisikia maumivu mara chache wakati wa tendo la ndoa ingawa maumivu yakizidi inabidi uchukue hatua inayotakiwa ili kupata tiba kamili.

Vitu gani vinavyosababisha kuumia wakati wa tendo la ndoa?


Kukaza kwa misuli ya vagina (Vaginismus)

(tamka vaj-uh-niz-muh s)

Ni kukaza kwa misuli ya vagina bila hiari (involuntary) na kusababisha tendo la ndoa kuwa gumu au kutofanyika kabisa.

Mwanamke mwenyewe anaweza asijue kwamba misuli inayozunguka vagina umekaza na kusababisha maumivu wakati mwanaume anaingiza penis.
Hii hali hutokana na hofu na mashaka aliyonayo mwanamke kuhusiana na suala la tendo la ndoa kwamba anaweza kuumia (kisaikolojia).
Pia wanawake wengi wenye vaginismus hawajawahi pata furaha ya tendo la ndoa maishani mwao na wengi ni waoga sana hata kwenda kwa madaktari kuhofia daktari anaweza kuchokonoa vagina zao hivyo kuongeza tatizo zaidi.

Ni nini husababisha hiyo hofu na mashaka?
Malezi aliyofundishwa kwamba tendo la ndoa ni chafu na baya na dhambia na hata akiolewa anafahamu kwamba tendo la ndoa ni chafu na baya.
Malezi aliyolelewa kwa kuambiwa kwamba vagina ni nyembamba sana na hivyo tendo la ndoa husababisha mwanamke kuumia.
Kama amewahi kudhalilishwa kimapenzi kama kubakwa anaweza kuwa na hofu na tendo la ndoa kwa sababu aliumizwa.
Kama amewahi kupata magonjwa ya zinaa yaliyokuwa yanamuumiza sana na kumpa shida pia anaweza kuwa anahisia za kuumia wakati wa tendo la ndoa.
Wanawake wengi wa aina hii hupata raha sana wakati wa foreplay na utamu wa mahaba huwaisha pale tu penetration ikianza.

Kitu cha msingi ni kwamba ili tendo la ndoa liwe tamu na zuri hali ya akili na ubongo ni muhimu sana kwani hisia zote za utamu wa tendo hutafsiriwa kwenye ubongo na ubongo ukipata pollution ya mawazo mabaya basi kila kitu kitaenda kombo.

Tutaendelea na somo kuangalia vitu vingine vinavyosababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa.......

2 comments:

miriam said...

VIPI KAMA NIMESHA WAHI KUCHANWA WAKATI WA KUJIFUNGUA, NAKISHA MPAKA LEO SIHISI RAHA YEYOTE WAKATI WA TENDO LA NDOA?

Lazarus Mbilinyi said...

Dada asante kwa swali zuri, niutajitahidi kujibu kwa ujumla hata hivyo naomba unitumie swali lako kwa email lazarusmbilinyi@gmail.com