"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, April 30, 2008

Maumivu wakati wa tendo la ndoa -3-

Katika utafiti uliofanywa na kituo cha kuthibiti magonjwa ya zinaa huko Chicago (CDC) Marekani na kutangazwa rasmi kwenye vyombo vya habari tarehe 11/03/2008, inakisiwa kwamba asilimia 26 ya mabinti wenye umri wa miaka 14-19 nchini Marekani wameambukizwa moja ya magonjwa ya zinaa.
Pia kwa mabinti wa kimarekani weusi hali ni mbaya zaidi.
Je, hii inakupa picha gani katika usalama wa afya ya uzazi?
Suala la kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa linasababishwa pia na magonjwa ya zinaa au kwa kimombo Sexual transimitted diseases or infections (STDs & STIs)

Haya ni magonjwa yanayoweza kuambukizwa kwa kufanya mapenzi na mtu ambaye ameathirika tayari na magonjwa ya zinaa.

Je nitajuaje nimeambukizwa magonjwa ya zinaa?
Kama ni mwanamke angalia dalili zifuatazo.
Majimaji ya ukeni ambayo yana harufu isiyo ya kawaida na yenye rangi tofauti na wingi kuliko ilivyo kawaida.
Maumivu au kusikia kama unachomeka au mwasho wakati wa kwenda haja ndogo.
Maumivu na mwasho katika maeneo ya uke.
Maumivu ya ukeni wakati wa tendo la ndoa
Vidonda na malengelenge katika eneo la uke.

Kama ni mwanaume dalili zifuatazo.
Majimaji kutoka uumeni ambayo yana harufu isiyo ya kawaida, au yakiwa mengi.
Kuhisi mwasho ndani ya uume, wakati na baada tu ya kwenda haja ndogo
Vijidonda na sugu ama malengelenge juu au katika sehemu za kiume.
Vipele au uvimbe katika sehemu za siri.
Je, kuna ukweli wowote mwingine kuhusu magonjwa ya zinaa?
Kuambukizwa magonjwa ya zinaa hakumaanishi una wapenzi wengi; ingawa kuwa na wapenzi wengi ndiyo chanzo cha magonjwa ya zinaa, hivyo wana ndoa inabidi kuwa makini kuhusu hilo.
Pia haya magonjwa hakiachwa kutibiwa si kwamba yataleta maumivu wakati wa tendo la ndoa tu, bali pia husababisha madhara ya kudumu kwa afya yako na wakati mwingine kusababisha ugumba au utasa.
Je ni magonjwa yapi ya zinaa ni ya kawaida ukiacha UKIMIWI?
Chlamydia
Husababishwa na viini vya bacteria na waweza kuathiri uke, mrija wa kupitisha mkojo, uume au sehemu ya kupitishia haja kubwa.

Dalili:
Kwa wanawake
Dalili hazionekani kwa urahisi.
Ubaya ni kuwa ugonjwa huo unaweza kuathiri fallopian tubes – yaani mirija ya kupitia mayai kutoka kwa ovari hadi kwenye nyumba ya uzazi hivyo basi kusababisha utasa.
Wakati mwengine dalili hii unaweza kuiona - kutokwa na majimaji ya ukeni yasiyo ya kawaida na kuhisi maumivu wakati wa kukojoa.

Kwa wanaume
Ugonjwa huu huathiri mrija wa kupitishia mkojo, uzuri ni kwamba dalili huonekana wazi, kama vile uume kutokwa na ute na kusikia maumivu wakati wa kukojoa.

Matibabu:
Ni pamoja na kufanyiwa uchunguzi wa mkojo au damu.
Unapotambuliwa daktari hupendekzeza dawa maalum ya kumeza.
Kama umefanya mapenzi hivi karibuni basi yafaa mke au mume wako naye aarifiwe ili nae atibiwe pia.

Kisonono (Gonorrhoea)

Dalili:
Wanawake
Hutokwa na ute mwingi wa njano au kijani kutoka ukeni na kusikia maumivu wakati wa kukojoa.

Kwa wanaume
Uume uliathirika hutoa ute wa njano au kijani, na kupata maumivu wakati wa kukojoa.
Pia kuna uwezekano wa kuwashwa ama kutokwa na maji maji katika sehemu ya kupitishia haja kubwa.
Ingawa baadhi ya watu huwa hawaoni dalili zozote kabisa lakini bado wanaweza kuwambukiza wanaofanya mapenzi nao.
Matibabu:
Iwapo matibabu hayatapatikana kwa haraka kuna hatari ya mirija ya kupitisha mayai (fallopian tubes) kuharibika na hivyo kusababisha utasa.
Kama una kisonono usifanye tena mapenzi hadi utakapofanyiwa uchunguzi na kupewa madawa ya kutibu ugonjwa.
Ni muhimu sana kumfahamisha mpenzio ili nae pia atibiwe.

Herpes
Huu husababishwa na aina fulani ya kirusi, kama kile kinachosababisha mafua na vidonda vya mdomoni.
Mbali na kusambazwa kupitia ngono pia husambazwa kupitia kufanya mapenzi ya kunyonyana sehemu za siri.

Dalili:
Ni Kupata vidonda ukeni au uumeni mfano wa vile vinavyotokea mdomoni wakati wa homa kali ya mafua.

Matibabu:
Sasa kuna dawa na krimu za kupambana na virusi hivi.
Lakini kumbuka hata unapotibiwa virusi vya herpes bado hubaki mwilini mwako na vinaweza kuzusha tena vindonda.
Pia kama umja mzito unaweza kumwambukiza mtoto wako, hivyo basi kama una vijidonda ni vyema kumjulisha mkunga wako ama daktari ili upate matibabu yafaayo.

NSU (Non-specific urethritis)
Ni herufi zinazotumiwa kuelezea magonjwa ya bacteria yanayoathiri mfereji wa kupitisha mkojo yaani urethra.
Magonjwa hayo husambazwa kwa kupitia kufanya mapenzi.
Dalili:
Kwa wanaume dalili kubwa ni kutokwa na ute, kutoka kwenye tundu ya uume na huenda akahisi maumivu wakati wa kukojoa.
Huenda ukasikia maumivu au kuwashwa-washwa.

Matibabu:
Majimaji yakitoka kwenye uume, isipokuwa mkojo au manii, ni lazima uchunguzwe na daktari, au nesi katika kliniki ya afya ya uzazi.
Unaweza kutibiwa kwa kutumia vidonge vya anti biotics

Kaswende (Syphilis)
Ugonjwa huu nao husababishwa na bacteria Treponema Pallidum
Dalili zake hazionekani kwa urahisi.
Huenda ukaanza kwa kijidonda au kipele kwenye uke au uume au sehemu ya kupitishia haja kubwa.
Kidonda hiki kinapopona usidhani ndio mwisho wa maambukizo la! Viini hivyo vinaweza kubaki mwilini kimya kimya kwa miaka mingi!

Matibabu:
Ni bora daktari kufanya uchunguzi wa damu kwani majimaji ya ukeni au uumeni huenda uchunguzi wake usionyeshe viini vya kaswende.
Kaswende ni hatari, kama haitibiwi, inaweza kusababisha utasa au ugumba, na hata kuathiri moyo, mishipa ya damu, ngozi ya mwili, mifupa na hata ubongo na kurukwa na akili.
Hata hivyo matibabu yake ni rahisi – Zipo dawa aina (antibiotics) zinazoweza kutibu kaswende kabisa.
Ili kuzuia kuenea kwa maradhi hayo ni vyema mpenzio nae pia atibiwe.
Tutaendelea na somo letu
WWWWWWWWWWWWWWWWWWWWWWWWWWWWWWW

No comments: