"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, April 8, 2008

Ndoa Na Nyumba -1-

Olive & Joseph Kabila KWANINI KUJIFUNZA NDOA NA NYUMBANyumba iwe mahali pazuri pa kuishi.
Tujue kwamba Mungu ndiye mwanzilishi na mtawala wa Ndoa na Nyumba.
Kuondoa hofu na miiko ya kikabila/tamaduni na jadi ambazo zimekuwa moja wapo ya vikwazo vya ndoa.
Kurekebisha hitilafu katika ndoa.
Tuweze kuwafundisha wengine (walioana au wanaotarajia) kuhusu wajibu ulio mbele yao.
Vijana wawe na Uhakika siyo Kubahatisha.

Ndoa Ni Nini?
Ni mtu mume na mtu mke walioamua kuishi pamoja kama mtu na mkewe wakiwa na kibali cha wazazi na Kanisa.
Ni Muungano wa kudumu wa mwanaume na mwanamke kuwa mwili mmoja.
Hivyo ndoa ni Agano na Fungamano kati ya mwanaume na mwanamke walioamua kuishi pamoja.
Mathayo 19: 4-6 Marko 10: 6-9 Mwanzo 2:24
Hamkusoma ya Kwamba yeye Aliyewaumba Mwanzo, aliwaumba Mtu Mume na mtu Mke, kwa sababu hiyo mtu atamwacha Baba Yake na Mama yake na hao wawili watakuwa mwili mmoja.
Nyumba Ni Nini?
Si jengo la kuishi bali,
Ni mahali ambapo mke na mume wataishi kwa Kupendana, Kuheshimiana na Kuaminiana
Ni mahali pa pumziko na kimbilio la amani unapokuwa umekata tamaa.
Ni mahali ambapo joto La moto wa Upendo, Mwangaza wa macho ya Furaha, Huruma na Utii vinatawala.
Ni kanisa na shule za kwanza kwa watoto kujifunza.
Ni mahali ambapo ulimwengu huangalia uhusiano wa kanisa na Kristo.
Mithali 14:1
Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake, Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake.
Joshua 24:15
Mimi na Nyumba yangu tutamtumikia Bwana.
MSINGI WA NDOA NA NYUMBA.Mungu ndiye mwanzilishi wa Ndoa na Nyumba
Zaburi 127:1
Bwana asipojenga nyumba, waijengao wafanya kazi bure, Bwana asipoulinda mji yeye aulindaye akesha bure.
Mungu ndiye aliyeweka utashi (tamaa) wa kuoana ndani yetu
Wazo la mke na mume ni wazo la Mungu; Uumbaji haukukamilika mpaka mwanamke alipoumbwa.
Na Aliwaumba kwa Tofauti Ambazo Ndiyo Kivutio Kati Yao.
Mungu alitengeneza ndoa ili atatue tatizo la kwanza la mtu kuwa na UPWEKE.
Mwanamke hakuumbwa awe mtumwa bali msaidizi
(Mwanzo 2:18)
Ndoa ilipangwa na Mungu kuleta Furaha sio Huzuni.
Aliweka raha zote ndani ya watu ili pawepo na Upendo Msisimuko na Utoshelevu.
Adamu alishangilia alipomuona Eva (mwanamke)
Mwanz0 2:23
Adamu akasema, "Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu na nyama katika nyama yangu," basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanaume.
Mith 18:22
Apataye Mke apata kitu chema; naye ajipatia kibali kwa Bwana.
______&&&&&&&&&&&&______________


No comments: