"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, April 9, 2008

Ndoa na Nyumba -2-

Ulla & Emmanuel
Kijiji cha Wangama - Njombe Tanzania
14/10/2006 Msingi ya Ndoa na Nyumba (mwendelezo.......)
Ndoa Lazima Ianze na Kuacha.Kuacha haina maana kutokujali bali ni kujitoa zaidi kwa Mkeo au Mumeo
Pamoja na huduma za Mungu bado unahitaji kuwa na ratiba ya kumpendezesha mkeo/mumeo
(1Kor 7:32 35)
Baadhi ya watu hujisahau hasa kutokana na majukumu yao
Kuacha kunawahusu wote mke/mume
Mwanamke kwenda kwao kila leo ni dalili kuwa huko aliko kuna shida
Mnatakiwa kuacha mambo yenu ya zamani mliyoyazoea kama vile, kutegemea tena wazazi.
Wazazi wa upande wowote wasiruhusiwe kuingilia maisha ya mmoja wenu
Ni makosa makubwa ya kiufundi katika ndoa kuwasikiliza wazazi wako kuliko mume wako au mke wako

ONYO AU TAHADHARI KUBWA!
Baba/mama mkwe huchonganisha na baadae hujifanya waamuzi hasa ikitokea labda walikuwa hawajaridhia kuoana kwenu,
hivyo inabidi wanandoa kuwa kitu kimoja
Katika jamii nyingi za Kiafrika bado kuna mfumo dume ambao mke huonekana ana thamani ndogo kuliko kaka au dada wa mwanaume
Kuendekeza ndugu (shemeji/wifi) kuachwe.
Mara nyingi nao hufanya pia wamemwoa, hivyo hutoa amri za kipuuzi na hata kutumia vitu bila kibali cha mke wa kaka yao na akifa wao hufurahia mali.

Mlinde mke wako kwa kila baya linalojitokeza.
Shughuli za kazi (ofisini, kanisani, rafiki nk) visiwe muhimu kuliko ndoa.
Hapa yatupasa kuwa na kiasi Kwani;
Asiye Wajali wa Kwao ni Mbaya Kuliko Asiyeamini.

NDOA INAHITAJI KUAMBATANA KATI YA MUME NA MKE
(Mwanzo 2:24)
Ndoa ni kuungana (kushikamana) kiasi kwamba kutenganisha kutaleta madhara
Mnaunganishwa katika nyanja zote za
Kiakili,
Kimwili
Na KufikiriaKatika kufanya mapenzi msiwe na mipaka mmoja akimtaka mwenzake basi pasiwepo na kikwazo.
(1Kor 7: 3-5)
Pia kushirikiana katika kucheka pamoja na kulia pamoja na kula pamoja kutembea pamoja.
Mila za makabila mengine haziruhusu wanawake kula na wanaume wala wanaume kukaa na wanawake katika maongezi sebuleni au mahali popote.
Lakini kwa mwanamke Christian;
Kula na mumeo,
Kuoga na mumeo,
Kuomba Mungu na mumeo tena mmeshikana mikono au mmekumbatiana, Kutembea na mumeo mmeshikana mikono
Ni sehemu ya maisha ya wanandoa.
Iwapo mnalala pamoja mkiwa uchi iweje mpeane zamu kwenda kuoga?
Mwendapo mahali usimtangulize au kumwacha mwenzako tembea bega kwa bega na mshikane mikono mkiongea
Kiroho mnaomba pamoja, mkiombeana na kutiana moyo
Kimapato mshirikiane na mawasiliano yawe mazuri,
mpatapo mshahara kaeni pamoja mtoe fungu la kumi kasha mworodheshe mahitaji yenu na kupangia matumizi.
Epuka kununu a vitu vya nje ya bajeti
Au kuwe na mfumo unaowezesha mke na mume kuwa na mawasiliano wazuri kuhusu mapato, miradi na matumizi


Imetokea mara nyingi katika jamii zetu; mwanaume anapokufa, mwanamke hajui hata Bank Account ya mumewe wala miradi aliyowekeza.

Mara nyingi anguko lolote katika ndoa hutokana na kutokuambatana

Mungu Hapendi Kuachana

(Malaki 2: 1 5)

KUMBUKA MKEO!

Ametokana na Ubavu – Ili awe Karibu na wewe

Ametoka Karibu na Moyo – Ili Apendwe na wewe
Ametoka Chini ya Mkono – Ili Apate Ulinzi wako
_____________WWWWWWWWWWW_____________


1 comment:

Anonymous said...

Safi sana Emanuely,japo 2006 lakini ni baraka kuona watu wakifanya maamuzi ya maana kama haya.Ni mfano wa kuiga.
Pia asante Mr mbilinyi kwa somo zuri ofcourse nimelipenda.
Mungu akubariki.
elly