"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, April 9, 2008

Ndoa na Nyumba -3-

Siku ya Harusi ni Siku ya Tofauti Kwa Kila Aliyeipitia na Wale Wanaotarajia.
Sherehe za Harusi Zilikuwepo na Zitakuwepo Bila Kujali Kabila, Taifa au Dini.SABABU YA KUOA NA KUOLEWA
Kuondoa Upweke au Umimi.
Kupata Raha. (kufurahishana)
Kupata Moto (joto) Kuinuana na Kusaaidiana.
Kupata Uzao – Kuijaza dunia (Watoto ni Baraka na Zawadi kwa Wazazi)
(Ruth 1:9, Kumb 24:5, 1Fal 1:1-4, Muh 4:9-11, Mwanzo 4: 1, 9: 1, 1: 28)
SIFA NJEMA ZA MWANAMKEAwe mwema
Mwenye hekima
Mwenye adabu
Mwenye busara
Awe mkarimu
Msafi (mwili na nyumba)
Mpole
Mwenye huruma
Mdadisi
Mvumilivu
Mcheshi
(Mith 15:1, Mith 22:9, Mith 19:14, Mith 14:16, Mith 16:5,24, Mith 12:4, 31:10 –30)
ILI KUMHESHIMU MUME; MKE UNAPASWAMuombee kila siku
(Yeye alivyo hekima, busara, ulinzi, baraka, ujuzi,
kuelewa, kiroho, mafanikio, kushinda majaribu nk)
Mshukuru Mungu kwa kazi anayofanya kwa ajili familia yenu.
Mshukuru Mungu kwa ajili ya Mume wako umepewa na Bwana.
Kumbuka Mungu amemuweka mume wako kuwa kiongozi wa nyumba yako pamoja na wewe.
Angalia Sifa za Mumeo na Uzikubali na Ongeza mara kwa mara
Mwambie Mumeo ni Namna gani Unamfurahia na Kumpenda
Usitoe sifa zake Mbaya Mbele za Watu au Kubishana
Mtie moyo na kuwa msaaada wakati wa jambo gumu
Jihadhari na jinsi unavyomuuliza maswali
Changamkia Pale Anapoonesha Upendo
Fikiria mambo Mazuri juu ya Mumeo
Thamini vitu Anavyovipenda na Asivyovipenda
KAWAIDA MWANAMKE!Usitegemee starehe nyingi kama zile ulizokuwa unapata kwa wazazi wako au ndugu zako.
Utakuwa na juhudi katika kujenga nyumba ya mume wako uliye naye.
Hutakuwa mgomvi na mchokozi wala kumpiga mumeo kwa mwiko.
Utampa mume wako haki yake
Thamani ya mumeo ni zaidi ya wanaume wote.
Umtii mumeo kwa Roho ya upole na unyenyekevu
Usimuruhusu mtu yeyote atambue kwamba unao wakati mgumu
( siri za ndani zisitoke nje)
Utahaakikisha macho yako yanamwangalia mumeo wakati amevaa kabla ya kutoka kwenda kazini au kutembea
Utajitoa na kumtii mumeo kwa moyo wote na kumruhusu kuwa kichwa cha nyumba Utahakikisha mumeo ni bora kuliko watu wengine
Mwanaume ni dereva wa gari la ndoa na mwanamke anaweza akashauri na kupendekeza njia ya kupita na siyo kunyang’anya usukani.
Mith 14: 1, Filp 2:3, Wimb 5: 9-16, Kol 3:18, 1Pet 3:6, Ef 5: 33
1Pet 5:9, 1Pet 3:1-4, Ez 16:32, 1Kor 7:3-5, Mith 21:19
Tutaendelea na sifa njema za Mwanaume!.................................

No comments: