"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, April 11, 2008

Ndoa na Nyumba -4-

Bwana Bao kutoka China (Mongolia) ambaye ndiye mwanaume mrefu duniani (2.3m, 7ft 8in) Akiwa na Mke wake Xia Siku ya Harusi Tarehe 26/03/2007 (Source: www.happynews.com)
Haijalishi ni mwanaume mrefu, mfupi, mnene, umesoma, hujasoma au vyovyote vile; kitu cha msingi ni kufuata kanuni ili ndoa yako iwe imara.
SIFA NJEMA ZA MWANAUMEMpole.
Asiwe mwepesi wa Hasira.
Mcheshi.
Anayeshaurika.
Anayewajali watu wa nyumbani mwake (mahitaji)
Aliye na shukurani na kusifu

(kwa lolote jema alilolitenda mkewe)

Anayeaga aondokapo kwenda matembezini au kazini au popote

(Mawasiliano)


ILI KUMPENDA MKE MWANAUME UNAPASWAKumheshimu mke wako kama mrithi pamoja na wewe katika neema ya uzima katika Kristo.
Mke wako ni mtu wa kwanza kwako siyo ndugu zako wala rafiki zako.

Mtaambatana na kuwa mwili mmoja.

Mara kwa mara utamwambia mke wako alivyo wa muhimu na thamani kwako
Utaendelea kumpenda kwa upendo ule wa kwanza wa wakati unampata.
Utakuwa kiongozi wa kusimamia nidhamu ya nyumba yako ukisaidiwa na mke wako.

Utakumbuka kutekeleza au kutimiza vile vitu vidogo ambavyo ulimwahidi mke wako kwamba utafanya.

Macho yako yataelekea kwa mke wako tu na sivinginevyo.
Utafanya juhudi kusikiliza yale yaliyosemwa na mke wako.
Utambusu kila siku asubuhi kwa upendo.
Hutakuwa mchungu likija swala la fedha.

(1Pet 3:7, Est 5:3, Wimb 8:1, Mwanz 21:12, Yer 5:8, Ay 31:1, Mith 5:15-20, Math 5:37, Efes 6:4,)


No comments: