"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, April 14, 2008

Ndoa na Nyumba -5-

Kwa Wakristo Suala la Mafanikio ya Ndoa si Kubahatisha;
Bali ni Suala la Kufahamu Maandiko na Kujua Wajibu wa Kuwa Mume au Mke. Kubadilika kwa Style ya Maisha Kutoka Traditional na Kuwa Modern Hakujabadilisha Wajibu wa Mume au Mke Katika Kufanikisha Ndoa Kuwa Imara.
WAJIBU WA WA MUME KWA MKEWE
KUPENDA
Kwa kiwango cha Kristo kwa kanisa
Kupenda ni matendo (actions) siyo tu kujisikia au kuhisi ni kufanya vitu vizuri kama vile kutoa, kutabasamu, kusamehe nk
(Efeso 5:25, Yohana 3:16)
KIONGOZI (KICHWA) MTAWALA
Mume ni kichwa cha mke
Naye atakutawala
Amri hii hairekebiki kwa kelele za Beijing kudai usawa; ila utekelezapo maagizo ya Kristo amri ya kutawaliwa inakufa
(Efeso 5:23, Mwanzo 3:16c)
MLINZI WA MKEWE –
Kama chombo kisicho na nguvu
Mwanaume ni mwokozi wa mwili wa mke
Mke hujiona salama awapo na mumewe
Hivyo mume mlinde mkeo na maadui wa ndani na nje kama vile baba na mama, mashemeji/mawifi na marafiki
(1Petro 3:7, Efeso 5:23, Isaya 4:1)
KUTUNZA FAMILIA.
Kuhakikisha familia inapata chakula cha kutosha, malazi, mavazi na elimu kwa watoto
(Mwanzo 3: 17)
KUMPAMBA MKEWE
Mume sharti ampambe mkewe apendeze ili aweze kuvutia
(Amnunulie vipodozi, nguo nk)
WAJIBU WA MKE KWA MUMEWE
KUTII
Kumtii mume kama kumtii Kristo.
Watu huchanganya sana neno kutii na kuheshimu.
Kutii kunakosemwa hapa ni kuwa endapo wawili mume na mke mmeshindwa kufikia uamuzi wa pamoja, basi, mke atatii uamuzi wa mumewe kama vile wamekubaliana awali.
(Efeso 5:22)
KULEA WATOTO (FAMILIA)
Kuhakikisha afya ya mumeo na watoto
Kuhakikisha kuwa chakula kinaliwa kwa wakati na kizuri
Kuhakikisha usafi wa malazi, mavazi na miili yao
Kufundisha watoto maneno ya Mungu
Kuchunguza nyendo na tabia za watoto na mumeo na kuchukua tahadhari mapema.
KUMSHAURI MUMEMke mwenye busara ni mshauri mwema kwa mumewe.
Hatatoa ushauri wa kuleta maangamizi.
Ushauri unafaa lakini ushauri mwingine upimwe kabla ya kufanyia kazi.
Ona mashauri mabaya ya wanawake kwa waume zao:-Hawa kwa Adamu – Kula tunda
Sara kwa Ibrahimu Kulala na mjakazi
Mkewe Ayubu kwa ayubu mumewe – Ayubu aliukataa ushauri wa mkewe
Naona Mke wangu ananiita; naamini ananihitaji mara moja, Tafadhari tutaendelea na somo letu;

No comments: