"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, April 15, 2008

Ndoa na Nyumba -6- (Mwisho)

Oa/Olewa na Yule Umempenda na Yeye Amekupenda Pasipo Shaka.
Uwe na Uhakika Mia kwa Mia Kwamba Unampenda;
Bila kushawishiwa na Mtu au Hali Bali wewe Mwenyewe.
Na Ukioa/Kuolewa Mpende na Kumtunza Kwa Uwezo Wote Maana ni Wewe
Uliyeamua Kumpenda na Kuoa/Kuolewa Naye. MAMBO AMBAYO MARA NYINGI HUWA ADUI WA NDOA
UTAJIRI
Kuwa tajiri si viabaya kwani kila mtu anawaza siku moja awe tajiri pia utajiri unatofautiana kutokana na maendeleo ya jamii anayotoka mtu.
Mwanume tajiri hupendwa na wanawake/wasichana na pia huwa na tamaa ya kutafuta fedha kiasi cha kukosa muda na mke wake.
Hivyo mke hujikutana akiwa mlinzi wa nyumba na hukosa huduma muhimu za kuwa na muda na mume wake.
Kama wewe ni mwanaume tajiri hasa kutokana na mtazamo wa jamii yako ni muhimu sana kuweka muda maalumu kuwa na mke wako na pia kuwa makini na wanawake/wasichana wanaokuzunguka katika shughuli zako za kila siku.

UMASKINI
Jamii nyingi za kiafrika bado kazi ya kutafuta lishe/mahitaji ni ya baba, hivyo hushughulika sana na kujikuta amekuwa baba zaidi kuliko kuwa mume.
Unahitaji kuhakikisha unakuwa na muda na mke wako wako.
Pia kuwa mvivu wa kutafuta maendeleo na mafanikio husababisha familia kuwa masikini na kukosa mahitaji muhimu kama chakula, mavazi na nyumba; matokeo yake hata suala la mapenzi linakuwa halina hisia kwani uchungu wa maisha hutawala akili na fikra.
Pia wapo wanawake ambao kwao kuolewa ni sifa, sherehe, kuvaa bila kujitoa kufanya kazi kuchangia kuongeza kipato cha familia matokeo yake umaskini hutawala na kuzikalia baadhi ya familia hadi kuhatarissha maisha ya ndoa ya wahusika
MADARAKA
Wapo wana ndoa ambao madaraka ya ofisini huyaleta hadi nyumbani.
Hiyo ni tabia hatari kwa afaya ya ndoa na chukuzo kwa mume/mke.
Maafisa hawana muda na wake/waume zao kwa sababu ya makongamano/semina/ziara mbalimbali.Hivyo wake zao wengi hutumia madereva kukidhi haja zao za kimwili
Mke ambaye ni ofisa humwachia house girl kazi za kupika, kufagia chumbani, kupeleka maji bafuni na hata kutandika kitanda, hivyo kusababisha mke kupinduliwa na house girl.

MAMBO AMBAYO WANAUME WAKIFANYA
HUWAKERA WAKE ZAOWababa wenye madaraka kuyapeleka madaraka nyumbani.
Wababa kutotenga muda wa kutosha kukaa na wake zao ili kuongea yanayowahusu mke na mume.
Mume kumwachia mke kulea watoto hasa wakati wa usiku.
Mume kutomtia moyo mke wakati wa ujauzito.
Mume kumchanganya mama na watoto wa kike wanapokosa.
Mume kutokuwa na maandalizi mazuri wakati wa kukutana kimwili na mkeoMume kujijali mwenyewe.
Mume kusaidia ndugu zake bila mke wake kujua.
Mume kubagua watoto na kuwapendelea baadhi yao.
Mume kuwa na upendo na ukaribu au kucheka na binti waishio nao huku yupo mke wake, inategemea pia aina ya ndoa na aina ya mke unayeishi naye kama ana wivu hapo mnaweza kuumizana.
Mume kutomshirikisha mkewe katika huduma, miradi au kazi zake ili aweze kumwombea na kujua pia mwenendo wa hiyo huduma au kazi au mradi.
Kutoonesha shukrani wala kutokuwa na msamaha.
Mume kutomtazama mkeo usoni mkiwa chumbani.

NB: Sijaweza kumalizia ya jinsi ya kumwandaa mke au mume chumbani kwa ajili ya tendo la ndoa, kama unahitaji unaweza kunitumia email lazarusmbilinyi@gmail.com nitakutumia


No comments: