"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, May 31, 2008

Ukimpenda, Hutampiga Utamkumbatia na Kumbusu

Bado tunaendelea kulaani vitendo vya wanaume au wanawake kudundana kwenye ndoa kama suluhisho la kutatua matatizo au migogoro inapojitokeza ndani ya ndoa.
Unaweza kusoma shairi hili hapa chini na kupata ujumbe.
Asante Born again pagan kwa shairi lako.
DOMESTIC VIOLENCE
My Memory Shoe Pinches With Indelible Hurts!
©Born Again Pagan -
New York, 2008

Recovery happens
But this one is delayed
If not arrested;
Basic confidence lacking
Mirage competence
Invisible connection
Vacuous caring spirit
Arid character
Anger mismanaging brewer
Or just selfish motives,
Jealousy progenitor!

When scale-weighed,
Leaves much to be desired:
Vivid is the picture
My Rata (Father) laid a stick
On my Mai (Mother)
On three occasions
When still a tender-age boy;
Recovery has not come about
From that traumatic memories
My dear Mai suffering
Due to my dear Rata’s battering!

My memory a shadoof
Tears still irrigates my cheeks,
Like the waters of the mighty Nile
Over Egyptian dry Sahara Desert,
To pinch my conscience
Never to any woman!

The three incidents
My Rata battered my Mai,
Mine has become stunted growth
Under nutrient deficient
Forcing a reverse gear
Back to the future;
Give me the necessary nutrients
Of growth out of this back to future!

Empower my mind fragility
To totally forget it
When my younger brother,
Older sister and I woke up
To witness our so battered Mai
And asked why our beloved Mai
Had black marks on her eyes!
Emwe muchali okwera ameso!
(You are too young to comprehend
The reality of life!)
Mai consoled us;
My sister doubted!

Was it plausible,
My unconvinced sister inquired,
On a retreat to go
Three tender siblings
Nyumbani kwa mjomba
(To the home of Mai’s brother)
Away from our Rata?
Mbenawe emisango ejijokubha kisi;
Nichali nemwe anhu
(But things will be okay;
For here with you I am)
Mai consoled us again!

In her arms our Mai held
My younger brother,
Who promised Mai
That he would bite Rata
The next moment Rata
Laid a blow to Mai!

Empower me to forget
That vulnerability and scare,
Which tied the essence of survival
To our Mai by following her
All days long,
Like little ducklings at a pond
Of hostility and insecurity!

Into a bitter enemy
Rata had turned
Forcing parental abandonment
Of the non-aligned position
Always upheld
During cold war moments
Between Rata and Mai;
Into an open hostility
The social environment so turned!

My Mai,
To all chores you attended
With anchored determination
And forgiving resilience,
Without remorse,
Without compunction,
Without complaints,
Without holiday,
Without weekends
For the brood’s sake!

A new pair of fitting shoes
Who will buy me
For my memory shoe pinches?
A knee-wounded soldier,
My walking is but a limp
Awesomely long trudging distance
This life-journey to cover out there
In this world without end!

From my past bruised
And hurt memories,
Who will liberate me
And eradicate my scars
That crap the style
Of my philistine streets
Of my mega city,
The center of life control
Of this human body machine?

Who will volunteer
To come out to street clean
With the brooms
Of forgiveness
Of forgetfulness
On behalf of my dear Rata
So departed and resting
In their permanent dwellings?
Who will sieve out
Of my haunted spirit
All the wrought about
Three-incident dirties
When Rata inflicted beatings
On my Mai;
Who will fill the emptiness
Of my heart
With repentance
Of never again?

Who will sharpen
That pair of scissors
To cut the ribbon
Of love re-conquered
Between a husband and wife,
As partners in life?

None but you all,
Bha rata na bha mai bhone
(All men and women)
Of my beloved Earth!
So your gumption gather
For Rata and Mai
A pair of sharp scissors to remain
And cut the ribbon
Of love re-conquered
And live where domestic violence
Is never blissfully condoned
In our one world;
Different cultures!

Bha mai na bha rata bh'Echaro
(Earthly women and men all),
Give me napkins of forgiveness;
Give me napkins of forgetfulness
To wipe off the last tear-drop
Now trickling and drenching
The keyboard of this computer!

Rata wani,
(My dad),
In your new permanent residence,
Vindicated you are of any wrongs
Then rifting you to
Kicks and fists;
Mai wani,
(My mom),
Accept repentance
On behalf of your husband,
Rata wani!

Ukimpenda, hutampiga, utamkumbatia, utambusu!

Mambo ya kudundana hadi kutoana ngeu kati ya wanandoa yamepitwa na wakati na si njia sahihi ya kutatua matatizo.
Soma makala ifuatayo kama ilivyoandikwa na kaka Maggid Mjengwa wa gazeti la Raia mwema pia unaweza kupitia blog yake.
JUMA la jana tulishuhudia uzinduzi wa kampeni ya kupambana na vitendo viovu dhidi ya wanawake. Kwenye moja ya safu za magazeti yetu ilipambwa picha inayomwonyesha mwanamke aliyepofuliwa jicho na mumewe akisimulia kisa chake mbele ya Rais Jakaya Kikwete.
Hakika, ilikuwa ni picha ya kusikitisha yenye kutoa mfano mmoja tu kati ya mingi juu ya vitendo viovu na vya kikatili dhidi ya wanawake vinavyofanywa na wanaume.
Uzinduzi wa kampeni ile unatutaka tuzidi kukumbushana wajibu wetu katika jamii. Hususan wajibu wa wanaume na zaidi mitazamo yetu kwa mwanamke.
Nimepata kuhadithia kisa cha bwana mmoja aliyepata kuwa tajiri na mwenye mali nyingi. Alikutana na mwanammke, wakapendana sana. Wakaamua kuoana. Siku ya harusi yao, bwana yule alimpa mkewe sharti moja. Sharti gumu sana. Akamwambia: "Ukitaka ndoa yetu idumu hakikisha huniingilii kwa jambo lolote nitakalofikiri na kuamua. Ukikiuka sharti hilo, basi, nitakufukuza mara moja nyumbani kwangu. Siku ya kuondoka nitakuruhusu uchukue kitu kimoja tu katika mali zote nilizonazo. Ukichague kitu hicho na ukichukue wende nacho kwenu.
Ikatokea jioni moja, katikati ya mazungumzo, Bibi yule alitamka: "Hapana sikubaliani nawe!" Hivyo, alikiuka sharti lile. Bwana yule alikasirika sana. Akatamka kwa hasira: " Unakumbuka sharti langu, ufikiri sasa kitu kimoja cha kuchagua kilichomo ndani ya nyumba yangu, alfajiri ikifika uanze safari ya kwenda kwa wazazi wako. Baada ya kuyasema hayo bwana yule hakutaka tena kuzungumza na mkewe, akachukua pombe zake, alianza kunywa, chupa moja baada ya nyingine. Alilewa chakari, alisahau hata kwenda chumbani, akalala kitini.
Mkewe akaomba msaada wa vijana nyumba ya jirani. Kwa pamoja wakambeba bwana yule hadi nyumbani kwa wazazi wa mke. Asubuhi ikafika, bwana yule alikurupuka usingizini, akajikuta yumo kitandani nyumbani kwa wakwe zake. Nimefikaje hapa?! Aliuliza kwa upole na kwa mshangao. Mkewe akamkumbatia na kumwambia: "Uliniambia siku ya kuondoka nyumbani kwako nichukue kitu kimoja tu, nami nimekuchukua wewe mpenzi wangu. Bwana yule alitabasamu na kumpiga busu mkewe. Kisha wakaongozana kurudi nyumbani kwao!
Katika malezi tunaona hali ya wazazi kutumia nguvu zaidi hata kufikia kuwapiga watoto wao pale wanapofanya makosa. Jambo hili linaonekana kuwa ni la kawaida kabisa. Jamii inalikubali, haioni kuwa mzazi anayetumia mkono au bakora kumwadhibu mtoto wake badala ya kutumia kauli, kuwa mzazi huyo ameshindwa kuikabili changamoto ya kulea. Kuwa mzazi huyo ana mapungufu.
Hali hiyo inaendelea hadi kwenye shule za chekechekea, msingi na sekondari. Mtoto anaachwa kuadhibiwa kwa bakora mara ile anapoanza masomo ya chuoni. Na ndipo hapa tunaposhuhudia, kuwa baadhi ya watoto hawa waliozoea kuelekezwa kwa bakora hupata taabu sana kujiongoza wenyewe kama watu wazima.
Tukirudi kwenye mahusiano kati ya mke na mume, si kweli kuwa, katika karne hii bado tuna wanawake wenye kuamini kwa dhati ya moyoni, kuwa kama waume zao hawawapigi na kuwatoa ngeu, basi wanaume hao hawawapendi. Hii ni dhana potofu ambayo kuna baadhi yetu, hususan wanaume wanataka kuiendeleza ili kuhalalisha maovu yao.
Ni upumbavu kumpiga na kumpofua jicho au kumtoa nundu mkeo halafu umwambie eti ni kwa sababu unampenda! Unayempenda kwa dhati hutathubutu kumpiga, utaongea nae, utamkumbatia, utambusu. Hayo ndio mapenzi.
Katika hili la kubadili mitazamo hasi kwa wanaume dhidi ya wanawake ni vema tukawekeza zaidi katika malezi ya watoto wetu. Tufanye hivyo majumbani na mashuleni. Ni vigumu kuwabadilisha kitabia wanaume, kuwa wasiwapige wake zao huku tangu utotoni mtoto wa kiume anaona jinsi baba anavyomgeuza mama yake kuwa mfuko wa kufanyia mazoezi ya ngumi.
Ni vigumu kuwabadili tabia hiyo wavulana walio mashuleni ilihali tuna sheria ya viboko ya mwaka 1975 yenye kuruhusu mwanafunzi kuchapwa bakora tatu. Idadi hiyo ya bakora hakuna anayeizingatia katika shule zetu. Bakora hupigwa wakati mwingine bila hata ya anayepigwa kujua idadi yake kwa jinsi zilivyo nyingi. Baadhi ya walimu wanaamini kuwa mwanafunzi hawezi kumwelewa mwalimu bila viboko. Wanawajengea hofu kubwa wanafunzi kiasi cha wengi kuchukia shule.
Bila shaka, wanawake ndio waathirika wakubwa wa maovu haya ya kupigwa na wanaume majumbani. Kuna haja ya kumsaidia mtoto wa kike. Tumpe nguvu mtoto wa kike kuanzia nyumbani hadi shuleni.
Mitazamo hii hasi ya wanaume inachangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa vitendo hivi vya ukatili dhidi ya mwanammke. Hatuna takwimu sahihi, lakini inasemekana kuna idadi kubwa ya wanawake wanaopoteza maisha yao kila mwaka kutokana na vipigo vya waume zao. Vingi ya vipigo hivi vinatokea ndani ya kuta nne za vyumba vya wanandoa.
Tuondokane na mitazamo potofu ya kimila na kitamaduni yenye kuhalalisha maovu na vitendo vya ukatili kwa mwananmke. Tumpe mwanamke na hususan mtoto wa kike nafasi yake katika jamii na hata katika masuala ya mapenzi na kujamiana. Mathalan, bado tuna makabila yenye mila za kurithishana wake katika zama hizi UKIMWI.
Ni ukweli pia, kuwa katika jamii yetu asilimia kubwa ya wanawake hawana nafasi ya kuamua kwa ridhaa yao juu ya suala zima la mahusiano kati ya mwanamke na mwanamme achilia mbali kushiriki kwenye tendo la ndoa.
Kwamba wanawake wanabakwa si vichochoroni tu, bali asilimia kubwa ya wanawake wanabakwa ndani ya kuta nne za vyumba vyao, na mara nyingi hubakwa na waume zao waliowaoa; kwamba kwa vile mwanamume ndiye aliyeoa, basi, anaona kuwa anayo mamlaka ya mwisho ya kuamua ni wakati gani atafanya tendo la ndoa hata bila ya ridhaa ya mkewe.
Wengi wetu tu mashahidi wa tunavyoziona hatua zenye kupelekea mtazamo hasi kwa nafasi ya mwanamke katika jamii zinavyoanzia. Zinaanzia nyumbani. Katika nyumba nyingi binti wa kike hana thamani sawa na mtoto wa kiume. Binti huyu wa kike anakua katika mazingira ya kutojiamini.
Mara nyingi binti wa kike huwa na elimu ya chini mno kama amepata bahati ya walau kwenda shule. Malezi ya mtoto wa kike ni ya kumwandaa ili siku moja akipata bahati aje "bwana" afunge ndoa naye, na hata kama si ndoa basi amchukue tu "akamfadhili".
Binti huyu wa kike analelewa katika mazingira yenye kumfanya awe na hofu kwa mwanamme. Tushiriki kuibadili mitazamo hii.
0754 678 252

Friday, May 30, 2008

Ahh kumbe!

A HUSBAND COMES FROM CHURCH;
HE GREETED HIS WIFE AND LIFTED HER UP.
HE CARRIED HER AROUND THE HOUSE.

THE WIFE WAS SO SURPRISED AND SHE ASKED 'DID THE PASTOR PREACH ABOUT BEING ROMANTIC'?
THE HUSBAND SAID, 'NO, HE SAID WE MUST CARRY OUR BURDENS AND SORROWS'.

Wataalamu wa Ndoa wanasema hivi!


As for Me and My House we will serve the Lord
(Joshua 24:15)
Kuna wataalamu 600 wa masuala ya ndoa (marriage experts) walikaa pamoja kujadili misingi (fundamentals) muhimu ya ndoa ambayo wanandoa wakiifuata ndoa zao zitakuwa imara na zenye afya hadi kifo kitakapowatenganisha.
Misingi hiyo ili imeinamia zaidi kwenye imani ya Kikristo, ingawa mtu yeyote bila kufuata dini yake anaweza kuifuata na bila shaka ndoa yake itakuwa ya tofauti.

Kuna mambo mengi sana muhimu ya kufanya katika ndoa ili ndoa iwe imara na yenye mafanikio, hawa wataalamu walichambua yale ya mambo msingi tu ambayo yakifuatwa basi vitu vingine muhimu katika ndoa inakuwa ndani yake.
Tumeshayaongea sana haya mambo hapa kwenye blog hii inaweza kuonekana kama kurudia, hata hivyo kuna kitu muhimu na kipya unaweza kukipata hapa leo.

Je, ni Misingi ipi hiyo?

Kwanza - Kristo kuwa Kiongozi wa Ndoa
Ndoa ambayo inaendeleza, ongeza, imarisha na kufurahia mahusiano na Yesu Kristo itakuwa na picha kamili ya Yesu na kanisa.
Kila mwanandoa atakuwa na uhusiano mzuri na Kristo na atajitahidi kufanana na Kristo na matokeo yake dhambi itakaa mbali na dhambi kukaa mbali basi upendo wa kweli wa kimungu huongoza ndoa.

Ndoa yenye msingi wa Kristo huwa na maombi na maombi ni mawasiliano ya wanandoa na Mungu, hivyo kwa kuwa na connection kati ya Mungu na wanandoa, Mungu atakuwa anaipa stabilization ndoa yao kila wanapokutana na tatizo, shida au jaribu.

Unajua kuna siku shetani huwa anaamua kupaka matope (mavi) mmoja ya wanandoa ili asipendwe (unajisikia kutovutiwa na mwenzako), ni kwa maombi tu unaweza kuharibu kazi za aina hii za shetani si pesa, wala elimu wala ujanja.

Kwenye ndoa kuna good times na bad times na Kristo huweza kuwapitisha wanandoa vizuri kama wanamtegemea yeye, hilo halina ubishi ni amini na kweli.

Pili - Upendo wa Kujitoa
Maisha ya binadamu ni safari ndefu, si sahihi kwamba siku zote ndoa itakuwa na mapenzi yaleyale ya motomoto, au kupendana kule kule kama mwanzo, kiwango cha mahaba kupanda tu graph kila iitwapo leo; si kweli, kutokana na kuwa na malezi tofauti na mambo mengine inawezekana ndoa kupita kwenye wakati mugumu sana, kuna stress, kuna kukata tamaa, kuna business kufilisika, na kuwa wakati tu inatokea mume na mke kila mmoja hampendi mwenzake bila sababu, hivi vyote vinahitaji watu wenye Upendo wa kujitoa ili kurudi kwenye mstari.
Katika ndoa conflict na disagreement hutokea bila upendo wa kujitoa basi ndoa haiwezi kufika popote.
Kwenye ndoa hakuna mtu perfect wote bado tuna tumia Learner driving license kwa maana kwamba tunaendelea kujifunza na kutoa efforts za kuhakikisha ndoa inakuwa na afya na inaendelea kudumu na kudumu na kudumu.

"A house divided against itself can not stand"


Kuna utafiti ulifanywa kwa wanandoa waliopata talaka, asilimia 40 walisema wanatamani kurudi kwenye uhusiano wao wa kwanza, hii ni kuthibitisha kwamba wangekuwa na upendo wa kujitoa basi wasingeamua kuomba talaka zao kwani kuna watu ambao conflict kidogo tu, tuachane!

Hawana dogo na wengine sasa kuoa na kuolewa ni kama shopping!

Tatu - Mawasiliano
Utafiti unaonesha kwamba watoto wadogo wa kike wamebarikiwa sana (talented) na uwezo wa kuongea na lugha kwa ujumla (linguistic), huweza kuongea haraka na mapema kuliko watoto wadogo wa kiume.
Hiyo tabia huendelea hadi wanapokuwa watu wazima na kwa maana hiyo wanawake na wanaume lipokuja suala la kuongea na mawasiliano kwa ujumla kuna tofauti kubwa.
Inajulikana kwamba wanawake huongea maneno kati 40,000 hadi 50,000 kwa siku wakati wenzao wanaume huongea maneno 15,000 hadi 25,000 kwa siku.
Hivyo basi wanawake ni viumbe wanaohitaji mwanaume kuuongea ili na yeye aongee hayo maneno yake, ndiyo maana kwa mfano kama umetoka kazini basi mwanamke anapenda sana umwambie mambo mbalimbali kama vile unafikiri kitu gani, nini kilitokea kazini, watoto wameshindaje, unajisikiaje kuhusu yeye mwanamke nk.
Wakati huohuo wanaume hujisikia sawa tu hata asipoongea chochote akifika nyumbani kutoka kazini matokeo yake mke anakuwa bored na hayo ni mawasiliano mabovu.
Wanaume kushindwa kuelezea hisia zao kwa wake zao ni kitu kinachowaumiza sana.

“Show me a quiet reserved husband, I will show you a frustrated bored wife”


Panga muda maalumu kwa ajili ya maongezi ya maana na mke wako hata kwa kuwa na matembezi au outing.
Hata hivyo wanawake wanapaswa kufahamu kwamba kuna wanaume ambao hawawezi kuwa kama wanavyotaka wao kwani ndivyo walivyo.
Mume wako hataweza kukutimizia mahitaji yako yote kwani hakuna mwanaume duniani ambaye anaweza kumpa mwanamke vyote anavyohitaji, ndiyo maana hata wewe mwanamke mwenyewe hupo perfect mia kwa mia.

Kumbuka

Unapowasiliana na mume au mke;
Badilisha kile ambacho kinaweza kubadilishwa
Elezea kile ambacho anaweza kukielewa
Fundisha kila ambacho anaweza kujifunza
Patanisha kile ambacho anaweza kukubaliana
Rudia kile ambacho anaweza kukiimarisha.Thursday, May 29, 2008

Mwanamke Mjamzito na Tendo la Ndoa

Wakati wa ujauzito wanawake wengi hukosa hamu ya tendo la ndoa hivyo mwanaume unahitaji kuwa na mawasiliano mazuri ili mambo yaende vizuri.
(Picha kwa hisani ya inmagine) Je, Mwanamke mwenye mimba anaweza kuendelea na tendo la ndoa?
Hakuna ushahidi wa kisayansi unaothibitisha kwamba tendo la ndoa kwa mwanamke mwenye mimba ya hatua yoyote ya ujauzito inaweza kumuathiri mwanamke mwenyewe au mtoto tumboni (fetus)
Hata kama kunatokea miscarriage bado sayansi inathibitisha kwamba chanzo huwa si sababu ya tendo la ndoa wakati mwanamke ana mimba, bali sababu zingine kabisa.
Tafiti nyingi zimefanywa kwa kufuatilia wanawake ambao waliendelea na tendo la ndoa huku wakifika kileleni (orgasm) na wale ambao hawakuwa wanafika kileleni wakati wa tendo la ndoa, na wale ambao hawakufanya kabisa tendo la ndoa muda wote wa ujauzito.
Matokeo yalionesha kwamba wanawake wote walizaa watoto ambao hawana tofauti yoyote kiafya.
Hivyo tendo la ndoa ni salama kabisa muda wote wa ujauzito.

Je, ni wakati gani huruhusiwi tendo la ndoa wakati wa ujauzito?

Ni pale tu mwanamke anapojisikia kuwa na bleeding au maumivu yoyote au leakage ya majimaji yajulikanayo kitaalamu amniotic fluid.
Mwanamke mwenye mimba haruhusiwi kuingiza upepo (by forcing) kwenye uke wako kwani husababisha kitu kinaitwa Air bubble kitendo ambacho kinaweza kusababisha kifo kwa mwanamke mwenyewe au mtoto tumboni kwani hu-block mishipa ya damu. Wapo wanaume huwa na mchezo wa kubusu huku wanapuliza huko bondeni (afrika ya kusini) kabla ya kuanza kuchima dhahabu.
Pia kama mmoja ya wanandoa ana magonjwa ya zinaa (STD) haruhusiwi tendo la ndoa hadi daktari athibitishe kwamba amepona ama sivyo anaweza kusababisha mtoto tumboni aambukizwe.
Pia kama una historia ya tatizo la cervix
Kumbuka!
Pia ifahamike kwamba si wanawake wote wakiwa na mimba hupenda tendo la ndoa wengine huwa hawapendi kabisa.
Utafiti unaonesha pia kwamba mwanamke mwenye mimba hukosa hamu ya tendo la ndoa miezi mitatu (3) ya kwanza, then hupenda sana tendo la ndoa miezi mitatu inayofuata na Pia miezi mitatu ya mwisho hukosa tena hamu ya tendo la ndoa kwa sababu ya saikolojia ya kusubiri mtoto kuzaliwa.
Ingawa uzoefu unaonesha kwamba mwanamke mwenye mimba husisimka haraka na kufika kileleni mapema sana kwa sababu damu huwa nyingi sana kuzunguka uke na hivyo kuwa sensitive zaidi kuliko akiwa hana mimba, pia ni dhahiri kwamba mwanamke anayefurahia tendo la ndoa wakati ana mimba hupata utamu wa uhakika.

Kitu cha msingi pia ni kuzingatia mikao au milalo wakati wa tendo la ndoa kwani mwanamke mwenye mimba anahitaji mikao au milalo ambayo haikandamizi tumbo lake.
Hakikisha mnakuwa na communication nzuri kuhusiana na suala la tendo la ndoa ili kila mmoja aweze kuwa msaada kwa mwenzake.
Hawa ni akina mama wa kichina wakijimwaga mitaani kwenye mashindano ya kupaka rangi matumbo maalumu kwa wanawake wenye mimba tu.

Wednesday, May 28, 2008

Kuna Ndoa Batili na Batilifu????

Kumekuwa na mkanganyiko katika kutambua maana na tofauti ya ndoa batili na ile batilifu.
Kimsingi hizi ni ndoa mbili zenye hadhi ya tofauti miongoni mwa wanandoa husika na mbele ya macho ya sheria. Kila moja ina sifa za kipekee zinazoifanya iwe na stahili ya kuitwa au kutambulika kama ndoa batili au batilifu. Hapa tatizo si sheria, bali ni elimu ya lugha ya Kiswahili katika matumizi, hasa kwa upande wa taaluma ya sheria.
Ndoa Batili
Hii ni ndoa ambayo kimsingi tangu asili yake ilishakosa sifa za kuwa ndoa kwa sababu ya kukosa moja au jumla ya vigezo vinavyohitajika kuifanya kuwa ndoa kamili.
Hii ni pamoja na vigezo vyote vinavyosimama kama mhimili wa ndoa kisheria. Hii hujumuisha vitu kama hiari katika kuingia mkataba wa ndoa kati ya wanandoa husika, jinsia za wahusika na hata mahari.
Hivi ni baadhi tu ya vitu au vigezo ambavyo ni kitovu cha mahusiano ya wawili kuwa katika hadhi ya kutambulika kama wanandoa halali. Sasa basi, endapo moja au jumla ya vigezo hivi vyote vitakosekana katika ndoa husika, basi moja kwa moja itakuwa ndoa batili, yaani isiyotambulika kisheria.
Msingi mkubwa wa ndoa hizi ni kwamba, haziwezi kusuluhishwa kwa namna yoyote kwani kwa kukosa sifa hizo za msingi zinakuwa zimepoteza hata uwezo wa kufikiriwa kisheria, yaani kuwekewa katazo na sheria ya nchi.
Mfano mzuri ni wa ndoa za watu wa jinsia moja ambazo kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, ni batili bila ya kujali kama katika ndoa hiyo wahusika waliridhiana na walifuata taratibu zote hitajika kisheria.
Ndoa Batilifu
Hizi ni zile ambazo zinachukuliwa kisheria kama ndoa halali mpaka hapo itakapotolewa amri ya kuivunja kutoka katika chombo chenye mamlaka ya kufanya hivyo, ambacho ni mahakama.
Lakini mahakama haiwezi kuamua tu kwamba ndoa fulani ni batilifu kuanzia sasa, bali huzingatia sababu na hoja zinazokubaliwa na sheria ambazo tunaweza kusema kuwa haziharamishi ndoa bali zinaiweka katika hatihati ya kuwa haramu.
Kwa mfano, endapo itatokea mmoja kati ya wanandoa akashambuliwa na maradhi ya zinaa, ndoa hii huwa ni batilifu, kwani hali hiyo inaweza kuwa sababu tosha ya kuvunjika kwake kwa ajili ya usalama wa mwenzi wake.
Hata kama wakati wa kufunga ndoa mmoja alikuwa na maradhi hayo na mwingine alikuwa hajui hilo, baada ya kujua anaweza kulalamika na mahakama ikaridhia na kutangaza kuvunjika kwa ndoa husika.
Kukataa kwa makusudi au kwa sababu za kimaumbile kushindwa kutimiliza ndoa pia kunaweza kuwa sababu ya kufanya ndoa husika kuwa batilifu, yaani baada tu ya kufunga ndoa wahusika hutakiwa kutimiliza ndoa kuashiria kuhalalisha maingiliano kati yao.
Sasa endapo mmoja wao atakataa kwa makusudi na bila sababu za msingi kutimiliza hilo, anayekataliwa anaweza kuiomba mahakama kuivunja ndoa husika baada ya jitihada za makusudi kushindwa kumshawishi kufanya hivyo.
Mahakama pia inaweza kuruhusu kuvunjika kwa ndoa husika kama baada ya ndoa kufungwa, mume anagundua kwamba mke wake ana ujauzito wa mwanamume mwingine. Mahakama italisikiliza hilo kama tu itathibika kuwa wakati wa kufunga ndoa husika mwanamume hakuwa na taarifa hiyo. Lakini endapo itathibitika kuwa alikuwa na taarifa kabla ya ndoa, lalamiko na maombi yake hayatasikilizwa.
Sababu nyingine ambayo mahakama inaikubali katika kuivunja ndoa batilifu ni kama itatokea mmoja wa wanandoa kuugua kifafa au wazimu. Kama maradhi haya yatakuwa ni ya kujirudia rudia na mwenzi wake hakulijua tatizo hili kabla, basi mahakama inatoa haki ya kutangaza kuvunja ndoa hiyo endapo itaombwa kufanya hivyo.
Lakini ikumbukwe na kuzingatiwa kuwa mahakama itahitaji kujiridhisha kuwa ugonjwa huo ni wakujirudia rudia na wala si kama aliwahi kuugua au huwa anaugua baada ya muda mrefu.
Aidha, haimaanishi kuwa pindi ikigundulika hivyo basi huwa ni sababu tosha au ni lazima ndoa husika ivunjwe, la hasa. Kama mume au mke wamekubaliana na hali hiyo, ndoa hiyo itakuwa na hadhi kama zilivyo ndoa nyingine.

Hii habari ni kwa hisani ya gazeti la Mwananchi
http://mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=5874
Simu 0786 809798 almajah2000@yahoo.com

Maandalizi ya tendo la ndoa (Foreplay)

Kabla ya hili tunda kuliwa kuna umuhimu wa kuhakikisha linaandaliwa kwa uhakika na wewe unayetaka kulila ili uweze kulifaidi vizuri, si suala na kukurupuka na kulivamia bila maandalizi mazuri na ya kutosha. Kuna tofauti kubwa sana kati ya mwanaume na mwanamke linapokuja suala la tendo la ndoa au kufanya mapenzi au sex.
Je, maandalizi ya tendo la ndoa (foreplay) ni nini?
Ni kitu kinachofanyika kati ya wakati mmetoa nguo zote na kabla ya mwanaume kuingiza uume kwenye uke.
Ni kubusiana, kugusana, na kuchezeana hadi mnakuwa mmesisimka vya kutosha kwa ajili ya tendo la ndoa.
Ni kuuungana kihisia, kiroho na kimwili kwa muda wa kutosha kabla ya tendo la ndoa
Ni msingi na kitu muhimu kwa ajili ya kuhakikisha unapata tendo la ndoa lenye kuridhisha.
Ni sanaa ya kuelezea upendo na kukaribishana kwa ajili ya tendo la ndoa.
Ni muhimu kwa ajili ya kumwandaa mwanamke kwa ajili ya tendo la ndoa.
Ni kumhusisha partner wako vizuri zaidi kupata hisia za upendo na ukaribu kimahaba yeye kujiona mtu maalumu kwako
Ni aina ya meditation (kutafakari) ambapo hukusahaulisha na mambo ya dunia (ulimwengu wa nje) na kuondoa strees na kukuwezesha ku-focus kwenye mapenzi moja kwa moja (connection)na yule umpendaye.
Pia kusoma maandishi yanayosisimua, kuangalia video na picha zinazosisimua na maongezi yanayoosisimua kimapenzi ni foreplay pia.
Je, tofauti ya kuwahi kusisimka kwa mwanaume inaweza kuleta tatizo?
Wanaume wana mzunguko mfupi sana kuamshwa kimapenzi (arousal), wakati wanawake wanamzunguko mrefu sana katika kuamshwa kimapenzi.
Ingawa pia uwezo wa kusisimka na kuamshwa kimapenzi unategemaa sana mambo yafuatayo:-
Umri - unavyozidi kuzeeka homoni hupungua hivyo kutumia muda zaidi.
Afya - kama unaumwa na dhaifu unahitaji muda zaidi.
Uzoefu na malezi - kama umelelewa na kuelezwa kama sex ni mbaya kazi ipo
Kuna matatizo mengi hujitokeza hasa kutokana na tofauti kubwa ya mzunguko wa kusisimuana na kuamshwa kimapenzi kati ya mwanaume na mwanamke na hii hupelekea hata baadhi ya wanandoa kujisikia vibaya na kutokupenda kabisa tendo la ndoa.
Kwa kuwa wanaume ndiyo husisimka haraka na kumaliza tendo la ndoa mapema kuliko wanawake ambao wakati mwingine kwanza ndo wanakuwa waanaanza kusisimka na kupata raha ya tendo.
Suala la msingi ili kuondoa matatizo ni wahusika kuwa na elimu au sayansi ya mwili na tendo la ndoa linavyokuwa.
Kama wote ni vilaza (mbumbumbu) na hawajui sayansi ya miili yao basi, mwanaume anaweza kudhani kwamba mwanamke anashindwa kuitikia msisimko anaompa, wakati huohuo mwanamke naye anaweza kudhani ana matatizo kwa kushindwa kusisimka haraka sawa na mwanaume anavyosisimka hivyo kukata tamaa na kujiona wote wana kasoro kumbe ni mzima na tatizo ni ufahamu wa miili yao wenyewe.
Hii tofauti ya kusisimka kimapenzi wakati wa tendo la ndoa wakati mwingine hupelekea kuathiri kabisa maisha ya mahaba kwenye ndoa hadi pale wote watakapofahamu vizuri mwitikio wa miili yao linapokuja suala la sex.

Je, unamchukua mwanaume dakika ngapi kufika kileleni?
Kawaida mwanaume inamchukua dakika 3 tu kuweza kufika kileleni tangu asisimke kimapenzi, wakati mwanamke humchukua zaidi ya dakika 15 kufika kileleni tangu asisimke, hii ina maana kwamba bila maandalizi mazuri ya kusisimuana mwanaume huweza kufika kileleni hata kabla mwanamke hajaanza kusisimka na muda ambao mwanamke alitakiwa kufika kileleni mwanaume anakuwa tayari alishamaliza kazi zamani.
Utafiti unaonesha ni asilimia 20 au 30 tu ya wanawake hufika kileleni na tatizo kubwa ni kutokuandaliwa vizuri na wapenzi wao (wanaume) na maandalizi mazuri ndiyo siri pekee ya mwanamke kufika kileleni na hatimaye kufaidi utamu wa tendo la ndoa.
Mahusiano mazuri maana yake ni wawili ambao wanatimiziana mahitaji muhimu na hitaji muhimu katika ndoa ni pamoja na tendo la ndoa.
Suala la tendo la ndoa lina umuhimu sawa na maeneo mengine katika ndoa kama kazi, chakula nk.
Ni muhimu kuwa na maarifa kuhusu mwili na tendo la ndoa kwani waingereza wanasema
Knowledge is Power

Je, ni makosa gani (deadly) ambayo wanaume hufanya katika kumuandaa mwanamke?
(i) Kuwa na haraka
Wanaume wengi huwa na haraka ya tendo la ndoa bila kuzingatia umuhimu wa kumuandaa muhusika kwanza.
Wanawake hutumia muda mrefu ili kusisimka ndiyo maana unahitaji kutumia muda bila kuwa na haraka ili uweze kumsisimua na zaidi kuwa na sex nzuri na yenye kuridhishana.
Ni vizuri kutumia muda wa kutosha kumuaandaa na kama unaweza hata kumfikisha kileleni hata kabla ya kumwingilia.

(ii) Kukosa kujua sehemu muhimu za kuchezea
Zaidi ya matiti, shingo na midomo (lips) na kisimi wanaume wengi hawajui ni sehemu zingine zipi ambazo wanawake huwasisimua zaidi.
Kuna sehemu zingine ambazo mwanamke akuguswa anaweza kusisimka haraka zaidi.
Tumbo, matako, mapaja, nyuma ya shingo, mabega, mgongo, sehemu iliyopo kati ya uke na nyuma
(kutumia mtandao wa Vodacom au tigo ni dhambi kubwa kabisa tena ukome kama una hayo mawazo, mwenye hekima na afahamu naongea nini)
Hizi sehemu ni muhimu sana kwake kuguswa wakati wa kumuandaa.
Pia lazima uwe mtundu kuweza kusoma lugha yake na jinsi nini anakifurahia na nini hafurahii wakati wa maandalizi.

(iii) Kuwa bubu bila kuongea maneno matamu na kumsifia
Wakati wa tendo zima la kufanya mapenzi wanawake wanategema mwanaume awe anaongea si kuwa bubu na kuongea huanzia kwenye maandalizi na kama wewe ni fundi wa kuongea basi hutachukua muda mrefu kuhakikisha moto umewaka.
Kuna maneno matamu, kwenye mapenzi maneno matamu yapo ya aina mbili, kwanza ni dirty words (mfano uke kwa jina jingine unaitaje vile au uume kwa jina jingine unaitaje vile) na pili maneno ya kumsifia juhudi yake au alivyo na umbo zuri. Dirty words husaidia kumsisimua na kupa nyege zaidi na maneno ya sifa husababisha atoe juice zaidi.

(iv) Kubusu kwa kinyaa au bila Ustaarabu
Wakati unambusu usiache mimate kila mahali uwe mstaarabu pia usioneshe kwamba una kinyaa katika kubusu baadhi ya sehemu ambazo yeye anapenda umbusu, huyo ni mke wako na yeye wewe ni mwili mmoja, yeye ni wewe na wewe ni yeye, hivyo unaruhusiwa kubusu sehemu yoyote ndiyo maana usafi ni jambo la kwanza kabisa katika mapenzi.
Kumbuka kuna msema ambao husema
CLEANNESS IS SECOND TO GODLINESS

Tuesday, May 27, 2008

Je, Upoje Kitandani

Nazima Tv, halafu nakwambia kitu!! Picha kwa hisani ya inmagine

Je unadhani wewe ni mwanaume mzuri kitandani? Hapa kuna maswali kwa ajili yako.
Je ni mara nyingi mke wako huwa anakuhitaji kwa ajili ya tendo la ndoa?
Je, kila unapofanya mapenzi yeye hufika kileleni? Je unauhakika jinsi ulivyo mzuri kitandani
Basi jibu maswali yafuatayo kwa uangalifu na uhakika bila kudanganya na angalia mapendekezo ya majibu ambayo yapo kila baada ya swali.

Kama ni mwanamke basi unaweza kumuonesha mume wako haya maswali ili ajibu ajipime yupo wapi katika kukuhakikishia unapata raha inayotakiwa kitandani siku zote.

Je, ni mara ngapi huwa unajisifu sana kwamba wewe ni mzuri kitandani?
(a) Kamwe sijisifu
(b) Mara chache
(c) Kila wakati
Watu ambao hujisifu kwamba ni wazuri kitandani mara nyingi hawajiamini. Suala la tendo la ndoa ni maada sensitive sana kwa wanaume, hivyo kujisifu inawezekana ni kujaribu kufunika ukweli.

Je, nini mtazamo wako kuhusu usafi?
(a) Nipo kawaida, naoga, najinyoa ndevu na kutumia vipodozi vya wanaume na kuvaa nguo safi
(b) Kuna siku siogi, pia naweza kuvaa nguo moja hata mara mbili
(c) Nipo makini mno, naosha mikono kila wakati na sipendi kabisa kugusana na mtu mwingine asije nichafua
Kuwa msafi siku zote ni kitu kizuri sana. Wanawake wapo sensitive sana na kile wananusa kuliko wanaume.
Hii ina maana kwamba harufu mbaya huweza kumuathiri mwanamke kuliko mwanaume. Ni muhimu kuoga kila mara na kuvaa nguo safi, ingawa kuwa msafi kupitiliza kunaweza kuzima hamu ya mapenzi kwa mpenzi wako kwani huwezi kubusu kila sehemu kwa kuogopa kuchafuka.

Je, mwonekano wako upoje? Umepinda au umenyoka?
(a) Imara na mara zote mgongo umenyooka
(b) Imara sana labda niwe nimechoka basi mgongo huinama
(c) Kila wakati natembea nimeinama na kupinda mgongo
Mwonekano (posture) ovyo siku zote unahusiana na Uvivu. Na kama ni mvivu maana yake wewe si mzuri kitandani pia.
Wanaume wenye posture nzuri siku zote huwa wanasimama wima na mabega yakiwa sawa bila kuinama na pia ni wanaume ambao hupenda ku-improve vitu vingi katika maisha mojawapo ni suala la kitandani. Wanaume wenye mwonekano (posture) nzuri ni wazuri kitandani pia.

Je, ni mara ngapi unaongea na mikono
(a) Sifanyi kabisa
(b) Nafanya kila ninapoongea
(c) Mara moja au mbili kila ninapoongea
Wanaume wanaongea huku mikono nayo ikisaidia mara nyingi ni wabunifu na wafikiriaji wazuri. Hujitahidi sana kuhakikisha wanapofanya mapenzi kunakuwa na matokeo mazuri. Kama una mwanaume wa jinsi hii basi utafurahia kitandani maisha yako yote hadi uzeeni.

Je, wewe ni mbunifu kiasi gani kitandani?
(a) Nafanya kwa utaratibu uleule kila siku miaka Nenda miaka rudi
(b) Ninafanya tofauti kidogo angalau baada ya muda
( c) Najitahidi kuwa na kitu kipya angalau kila ninapofanya mapenzi
Kuwa bored ndiyo sababu kubwa ya uhusiano wa mapenzi kuwa ovyo na hata hamu kwisha kabisa. Kujaribu kitu kipya pamoja na mikao tofauti wakati wa kufanya mapenzi husaidia kitanda kuwa cha moto kila mara.
Wapo wanandoa ambao wapo kwenye ndoa zaidi ya miaka 60 na bado wana enjoy mapenzi.

Je, kuna umuhimu wowote kwako kwa mke kufika kileleni?
(a) Huwa sijali afike au asifike, ni kama hainihusu
(b) Ni vizuri akifika kileleni
(c) Nahusika sana na napenda afike kileleni na pia namsaidia kwa kiasi kikubwa kuhakikisha anafika kileleni
Kufanya mapenzi kuzuri kunategemea sana jinsi ya kutoa na kupokea kati ya wahusika. Wanaume wengi wao ni rahisi sana kufika kileleni kuliko wanawake wakati wapo kitandani. Wanawake ni viumbe wa hisia hivyo huhitaji muda zaidi ili kuweza kufika kileleni. Ingawa wanawake wengi hawapowazi kuongelea hili, bado kufika kileleni ni kitendo kinachowapa kuridhika vizuri na tendo la ndoa.
Hivyo kama huwa unahakikisha anafika kileleni basi wewe ni mwanaume mzuri kitandani.

Je, ni mahali gani unamtumia kwa ajili ya tendo la ndoa?
(a) siku zote ni kitandani kwetu chumbani
(b) Chumbani sehemu yoyote, chini au kitandani
(c) Mahali popote ambapo tunaweza
Kama kunakitu kinatakiwa kuepukwa kwa nguvu zote basi ni ile kuwa na mazoea ya kuwa na sehemu au utaratibu mmoja wa kufanya mapenzi miaka Nenda rudi. Jaribu kuwa na sehemu tofauti za kufanya mapenzi, mnaweza kusafiri au kwenda camping au sehemu yoyote.
Hawezi kusahau kumbukumbu za hizo sehemu.

Je, unapokuwa kwenye tendo la ndoa huwa unasimamamisha kwa muda gani?
(a) Dakika mbili au pungufu
(b) Kama dakika 15 hivi
(c) Hadi saa nzima kama kuna umuhimu
Hakuna ubishi uume uliodinda husaidia kumsisimua mwanamke wakati wa kufanya mapenzi. Wakati mwingine mwanamke hukata tamaa kama akijisikia wewe husisimki na matokeo yake wote mnaambulia sifuri.
Ni ukweli pia uume uliosimama na kudinda vizuri huwezi kumpa mwanamke msisimko ambao huwezesha kumfikisha kileleni.

Je, ni muda kiasi gani huwa unatumia kumuandaa mpenzi wako
(a) Sina huo muda
(b) Dakika tano hivi
(c) Hadi nihakikishe yupo tayari au amesisimka vya kutosha kiasi cha yeye kutaka.
Kama wote tunavyojua maandalizi (foreplay) ni muhimu mno kwa ajili ya tendo la ndoa.
Bila maandalizi tendo la ndoa halina ladha yoyote zaidi ya kuumizana.
Kama huwa hufanyi maandalizi yoyote hapo ni dhahiri kwamba haitawezekana kwa mkeo kufika kileleni na hatafurahia inapofika muda wa kwenda kitandani.

Na kama unatoa muda wa kutosha kwa wajili ya foreplay basi atakuwa anasubiri kwa hamu kubwa kusikia muda wa kitandani umefika.
Pia ni vizuri kufahamu kwamba mwanaume mzuri ni yule ambaye hata baada ya kumaliza tendo la ndoa si mtu wa kukurupuka na kutoa uume wakati mke hajamruhusu kwani utamu wa tendo la ndoa kwa mwanamke ni wa muda mrefu zaidi hivyo ni vizuri kubaki ndani zaidi ya dakika 10.


Je, ni mara ngapi unafanya mapenzi kwa kushtukiza?
(a) Si rahisi na kawaida
(b) Mara moja kwa mwaka
(c) Mara kwa mara tunapotaka kufanya mapenzi
Kuna raha yake kwa mwanamke kufanya mapenzi kwa kushtukiza. Utaratibu wakati mwingine huwa una bore, ni kama mazoea. Sex ya kushtukiza wakati mwingine huleta kumbukumbu nzuri zaidi na kuwa enjoyable.
Wanawake huwafurahia wanaume ambao huwapa kile wanatarajia linapokuja suala la kitandani.
Ukiwa mbunifu na mwanaume mwenye utundu kitandani basi mkeo atakushukuru na kukupenda zaidi kwa sababu unampa raha kamili.

Intimacy

INTIMACY

THERE ARE STAGES FOR PERMENENT COMMITMENT OF PHYSICAL INTIMACY

Eye to body
Reveals about person sex, size, shape, age, personality and status
Eye to Eye
When woman and man who are strangers to each other exchange glance, they may smile to be better acquainted
Voice to Voice
Initial conversation, what is ur name, what do you do for living, people learn much more about each other like opinions, activities, habits, hobbies, likes and dislikes and may become friends
Hand to Hand
First instance of physical contact it is non-romantic
Hand to Shoulder
Affectionate embrace is still non-committal. Man and woman are side by side, this is more than close friendship and probably not real love
Hand to waist
This is not common for people of opposite sex can do, it is clearly romantic. They share secrets or intimate language with each other
Face to face
Gazing into another’s eyes. Hugging and kissing.
Sexual desire becomes very important factor
Hand to head
Touch the head when kissing, this is emotional closeness
Hand to body
Sexual and private
Mouth to breast
Touching below the waist
Intercourse

Monday, May 26, 2008

Ulivyo Ndivyo Unavyotakiwa Kuwa

Anayekupenda anakupenda kwa sababu ya jinsi ulivyoNajiamini kwa jinsi nilivyo
Picha kwa hisani ya morioM

Wanawake wengi hasa katika jamii za leo wengi wanaukataa mwonekano wao na kuhisi size au shape walizonazo bado hazijafikia kiwango kinachotakiwa na wapenzi wao.

Tafiti nyingi zinaonesha kwamba asilimia 80 ya wanawake wenye umri miaka 18 hadi 35 hawaridhiki na size na shape za miili yao.
Wengine wanajiona ni wembamba sana na wengine wanajiona ni wanene sana, wengine wanajiona matiti ni madogo mno, wengine wanajiona matiti ni makubwa mno, wengine wanaona ngozi zao si laini kwa kiwango kinachotakiwa na wengine wanajiona ni wazee mno kuliko umri wao.
wengine wanajiona ngozi zao ni nyeusi mno hivyo wanahitaji kubadilisha kuwa nyeupe zaidi.
Wakati mwingine unashangaa kumuona mwanamke au binti aliyekuwa na size na shape nzuri amejibadilisha na kuwa na shape nyingine kabisa, hata unaweza kumsahau na kudhani ni mtu mwingine kabisa.
Anajiona amejitahidi kufikia viwango anavyodhani ndo anapependeza.
Wanawake wengi sasa wanapigana kufa na kupona linapokuja suala la mapaja, vifua, tumbo, unene na wembamba hata rangi.
Wengine wamejiingiza kwenye dieting ambazo matokeo yake wamekuwa wanaishi katika njaa na hatimaye kupoteza kinga ya mwili na kushambuliwa na magonjwa ovyo.
Sikatai upunguze uzito au kuwa mrembo!

Kuwa na negative image ya mwili wako husababisha kutojiamini na kutojiamini husababisha kuuchukia mwili wako na matokeo yake unaweza kuathiri maisha na uhusiano wa mapenzi ya yule umpendaye.
Kwa kuwa huupendi mwili wako, umeuchukia, hujiamini imekuwa vigumu hata kuwa uchi mbele za mume wako kwani unaogopa eti mwili hauvutii
"The body is not looking good"
Nikuulize swali!
Je, ni mumeo aliyekwambia mwili wako hauvutii au ni mawazo yako na mtazamo wako?

Kitu cha msingi ni kufahamu kwamba mume wako anakupenda kwa sababu ya jinsi ulivyo na anakupenda zaidi ya hilo umbo ulilonalo.
Jiamini na kujipa raha na mume wako kwa amekupenda wewe kwa sababu duniani upo wewe tu hata kama mpo mapacha bado yeye amekupenda wewe.
Ni kweli kuna wanawake kwenye TV na kwenye magazeti ambao kwa jinsi walivyo unaweza kuvutiwa uwe kama wao hata hivyo kila mtu duniani aliumbwa tofauti na hiyo tofauti ndiyo imefanya tuwe na mtu ambaye ni wewe.

Ukiona mume anakulaumu sana kwa sababu ya umbo lako, lazima kuna sababu nyingine nyuma yake ipo, otherwise atasaidiana na wewe kuhakikisha unakuwa anavyotaka yeye na si kukulaumu sana.
Ukiona kelele ni nyingi sana kwamba siku hizi huvutii inaweza kuwa ni kweli umejiachia na kutojipenda na kuwa mrembo na sexy ingawa pia uwe makini inawezekana hiyo ni sababu tu nyuma yake ana lake jambo.

Mume wako anakupenda si kwa sababu ya umbo lako tu kuna vitu vingi vinavyomvutia inawezekana ni:-
Unavyotabasumu
Unavyomkubali yeye kama alivyo
Unavyotembea
Matiti yako
Matako yako
Shingo yako
Macho yako
Nywele zako au
Jinsi unavyoongea nk
Ni vizuri pia ukaongea na mpenzi wako kwamba unataka kufanya kitu fulani kabla ya kubadilika na kuwa mtu mwingine na baadae ikawa masheshe, inawezekana akawa anavutiwa sana na weusi wako na wewe ukaamua kujipiga mkorogo na kuwa tofauti ikawa balaa.

Elekeza mawazo yako katika maeneo ya mwili ambao unaona kwako ni mazuri zaidi kuliko kuelekeza kwenye maeneo ambayo unadhani hayapendezi.
Kutumia uzuri wa mtu mwingine kuwa kipimo chako husababisha kujiona inferior zaidi kuhusiana na mwonekano wa mwili wako kuliko ungeamua kujiamini na kuukubali mwili wako kama ulivyo.
Usitamani kuwa na matiti makubwa kama fulani, au kuwa na nywele ndefu kama fulani matokeo yake kwa kuwa haiwezekani utajikuta huufurahii mwili wako.
Mungu hahitaji kuwa na watu ambao wote wananafanana ndiyo maana kila mtu alimuumba kuwa tofauti na hii tofauti ni pamoja na muonekano wa mwili wako na ndiyo inayofanya mtu upendwe na ufurahie mahusiano.

wewe ni mwanamke wa tofauti, upende mwili wako na jiamini kwani jinsi ulivyo ndivyo ulivyo hakuna mtu aliyekama wewe duniani ni wewe tu.

Saturday, May 24, 2008

Siri zingine

Kati ya wanawake na wanaume nani mabingwa wa kutunza
siri hatari wakati wa kuanza mahusiano?
Wanawake wengi ni innocent sana!
Wapo watu ambao wanapoanza mahusiano (urafiki wa kuelekea mke au mume) huficha siri zao za kwa kuogopa kwamba wakiziweka juu ya meza na kuwaambia wale wanaanza nao uhusiano mpya wanaweza kuwakataa na uhusiano kufa.

Ukweli ni kwamba siri zako kabla ya mahusiano mapya ni vizuri kumwambia mpenzi wako kwani ipo siku siri zako zitagundulika na kama zikigundulika basi hapo ujue utakuwa umepoteza trust na ukipoteza trust ni kama barafu linalowekwa kwenye jua likiyeyuka huweze kulirudisha kwenye hali yake ya kawaida.

Kuna msemo wa kingereza ambao husema
‘If you do not deal with your past, your past will deal with you”

Ni vizuri kujiuliza mwenyewe hivi ni kweli mpenzi huyo uliyenaye anakuona wewe kama ulivyo mtu halisi au kuna siri fulani ambazo umezificha?
Je, kweli ni wewe mwenyewe uliye halisi ?

Wengi huficha kwamba huko nyuma walikuwa na watoto, wengine huficha huko nyuma walishawahi kuwa na mahusiano na kwa sababu ya tabia yake mahusiano hayakudumu.
Wengine huficha hata ukweli kuhusu familia zao
Wengine huficha hata kiwango cha elimu zao, kazi zao, dini zao nk

Haina haja kuficha siri ambazo unajua ni siri kubwa kwani ipo siku mambo yatawekwa sebuleni then hiyo kashesha hapata tosha maana kuna swali utauzwa
"Kama umeweza kuficha siri kubwa kama hii kwa miaka yote hii je, nitakuamini kweli?"

Friday, May 23, 2008

Kutafuta mchumba kwa Internet

“I will never date a lady through the internet” Watu wengi hutumia mitandao (internet)
(hata zile zinaitwa christian dating sites) kwa ajili ya kujipatia mchumba na hatimaye mke au mume.
Je, ni njia sahihi? kuna hatari yoyote?
Basi Dr Christopher Eric anaapa kwamba hadi kifo hatarudia tena kutafuta mchumba au mke kwa kutumia mitandao.
Nini kimempata?
unaweza kupitia kwenye link ifuatayo

Thursday, May 22, 2008

Faida za Kukumbatiana

Binadamu ana muhitaji sita muhimu katika maisha nayo ni:-
Hewa
Chakula
Maji
Mavazi
Malazi
Kukumbatiwa (hug)

Hugging ni natural, ni kitendo kinachotupa afya, hakina pesticide, wala preservatives zozote.
Kukumbatiana ni sayansi, njia rahisi ya Kusaidiana, kuponya, kukua na ina kipimo cha ajabu katika matokeo yake.
Pia kukumbatiana ni sana, kuguswa si tu ni vizuri bali pia ni hitaji, sayansi inathibitisha kwamba kuguswa ni muhimu kwa maisha yetu kihisia na maisha kwa ujumla
Pia imethibitika kwamba hugging husaidia maendeleo ya mtoto katika kujua lugha na IQ.
Hugs ni tamu, huondoa upweke, huondoa hofu, hufungua milango kwa ajili ya feelings, hujenga mtu kuwa jasiri, hupunguza kuzeeka, kuongeza hamu ya chakula, husaidia kuweka mikono, mabega katika ubora zaidi pamoja na misuli yake, kama wewe mfupi basi hugs zinakufanya kazi nzuri kukunyosha (kunyumbulika) vizuri na kama wewe ni mrefu basi hugs hukuwezesha kukupa zoezi la kujikunja na kujinyosha.

Kidemokrasia hugs zinamfaa mtu yeyote bila kufuata chama kama ni chama tawala au chama cha upinzani, zinawafaa maskini na matajiri, watu weupe au weusi, wanene au wafupi, wenye dini na wasio na dini wote zinawafaa
(ingawa baadhi ya dini zinazuia vijana ambao hawajaoana kupeana hugs au mwanamke na mwanaume ambao si mke na mume, hapa sizungumzii wokovu nazungumzia dini)

Hugging hazina caffeine, nicotine wala calories na artificial ingredients yoyote, asilimia mia moja ni pure safi kabisa.
Hugging ni halisi, kitu timamu ambacho hakina kitu chochote hatari haihitaji battery wala checkups ya kila siku, hata wakati wa hugging huhitaji nguvu bali ukipata hugging unapata nguvu maradufu.

Hugs kiuchumi ni sound, hazina impact katika mazingira yetu ni environmental friendly, hakuna global warming kwa kukumbatiana, hugs hazihitaji vifaa maalumu ni rahisi, huwezesha siku za furaha kuwa za furaha zaidi, hufanya siku ambazo mambo hayawezekana ziwe siku ambazo mambo yanawezekana.

Huwezi kulipishwa kodi kwa hugging, huwezi kupata unene kwa hugging, huwezi kupata pollution kwa hugging, hakuna bills za kutoa hugging, wala hakuna inflation kwa hugging.
Hugging ni afya kwa mwili na roho, huponya msongo wa mawazo, kupunguza mawazo, huongeza uwezo wa kupata usingizi.

Huwezesha mwili kuwa na immunity ya kutosha kwa kupambana na magonjwa, huhuisha maisha ya mtu bila side effects kama medications zingine

Hugging ni dawa yenye miujiza!
Hugs ni free ndiyo maana wengi wanachukulia ni for granted, kama hugs zingekuwa zinauzwa kwenye maduka au stores au supermarkets, genge, kilabuni, sokoni, minada, stock exchange au grocery basi kwanza bei yake ingekuwa haishikiki na pia kila mtu angekimbilia kununua angalau japo apate moja kwa siku.

Hata kama hugs ni bure zisipotumika hazina thamani yoyote.
Hugs zisizotumika hupotea milele ni kama maji hazizoleki.

Wanasayansi wamethibitisha kwamba:
Hugs 4 kwa siku ni hitaji la kawaida kwa Binadamu kwa siku ili aishi.
Hugs 8 kwa siku huhitajika kwa ajili ya kuimarisha kiwango cha emotions kwa binadamu
Hugs 12 kwa siku ni muhimu kwa ajili ya kukua na kuwa mtu mwema na bora katika idara zote kiroho na kimwili.

Kama hugs kwako zinakufanya usijisikie vizuri (uncomfortable) basi jaribu angalau kufanya mambo yafuatayo:-
Tamka maneno mazuri yenye baraka na mema
Mguse mtu unaposalimia au unapoongea
Tabasamu
Sema asante
Samehe
Unapoweza saidia
Ukikosea tamka nisamehe


KUMBUKA!
Hakuna kitu kinaitwa hugs mbaya, hugs zote ni nzuri.
Lazima ukumbatiane na mtu angalau kwa siku mara moja na kama kuna mvua angalau mara mbili kwa siku.
Pia kumbuka kukumbatiana huku unatabasamu, kufumba macho si lazima
Kukumbatiana wakati mnaenda kulala hufukuza ndoto mbaya
Usikumbatie kesho kama leo mnaweza kukumbatiana!

Hug - Hug - Hug - Hug - Hug - Hug -Hug

Kumatiana Kumbatiana Kumbatiana

Kila siku usiache !


Wednesday, May 21, 2008

Huyu Mtoto Huyu!

SON: Dad, I want to marry.
DAD: Who do you have in mind?
SON: GrandMa.
DAD: Oh boy, that's my mum?
SON: But you married mine?
Asante sana Dada Subi kwa kutuhabarisha na kutuchekesha!

Kukumbatiana


Ni Muhimu ukafahamu kwamba mume wako au mke wako anahitaji kukumbatiwa mara kwa mara kwa ajili ya afya yake kisaikolojia na kimwili pia.
(Picha kwa hisani ya flickr) Dada Emmi anasema kwamba amemkumbuka sana mume wake ambaye yupo mbali kwa miezi zaidi ya sita sasa, anakiri kabisa kwamba kitu mojawapo kinachomfanya amumiss sana huyo mahabuba wake ni jinsi anavyojua kukumbatia (hug) anaendelea kukiri kwamba mpenzi wake huyo ni mchawi wa hugs na kwamba yupo huggable ile mbaya yaani acha, na dada Emmi hujisikia raha sana kwa Mguso ambao huwa anaupata, analikumbuka sana lile joto la mwili wake hasa wanapokuwa umeshikana kwa hug la uhakika, anamuona ni dawa, hujihisi yeye ni mali yake na hujisikia furaha isiyo ajabu Kuanzia mwilini hadi kwenye moyo.
Hayo ni maelezo ya dada ambaye anajua utamu wa kukumbatiwa na kukumbatia kitu ambacho ni hitaji kubwa muhimu kwa watu wanaopendana.

KUKUMBATIANA NI NINI?
Neno kukumbatia (hug) linatokana na neno hugga lenye maana kufariji.
Kukumbatiana kuna faida kubwa kuliko mtu anavyofikiria.
Utafiti unaonesha kwamba kukumbatiana husaidia watu kisaikolojia na kimwili pia.
Pia utafiti umeonesha kwamba kwenye mwili wa Binadamu (nervous system) kuna kemikali inayoitwa endorphins ambayo inapatikana kwenye damu iliyomo katika mfumo wa fahamu na husaidia kupunguza maumivu na hutuwezesha kujisikia salama, ahueni, kutiwa moyo, raha na utamu (euphoric).
Utafiti unaonesha kwamba watu wanapokumbatiana hizi kemikali huongezeka mwilini na hivyo kukumbatiana ni dawa tosha kabisa ya kumaliza maumivu mwilini kisaikolojia na kimwili (painkillers)
Pia Utafiti umeonesha kwamba kukumbatiana huongeza kinga ya mwili (immune), imethibitika kwamba kwenye ubongo kuna sehemu inayohusika kuitikia wakati watu wanakumbatiana.
Mfano:
Mtoto asipokumbatiwa (touch) kwa muda unaotakiwa sehemu ya ubongo hupoteza seli za misuli (atrophies) na kinga ya mwili hupungua.
Tunapokumbatiwa tangu watoto tunajenga uwezo wa kuwa na
Upendo,
Kupenda na
Kupendwa,
watoto ambao wamekulia mazingira ya kutokumbatiwa huwa wagumu sana kuwapenda wenzao.
Utafiti wa jamii katika tamaduni mbalimbali unaonesha kwamba jamii ambazo watu hawakumbatiani ni violent na wauaji.


JE BARA GANI MAARUFU KWA WATU KUKUMBATIANA?
Mwanasaikolojia Bwana Sidney Jourard alisafiri mabara yote na kugundua kwamba bara la Ulaya ndiyo linaongoza kwa watu wengi wanaopenda kukumbatiana likifuatiwa na Amerika na mengine yakifuatia


Wanaume na wanawake wote wanapenda kukumbatiana kwa maana kwamba wote wanahitaji kulisikia joto la upendo wa kukumbatiwa.
Wakati wanawake wengi walipoulizwa kwa nini wanapenda kukumbatiwa wengi walikiri kwamba sababu kuuu ni Kujisikia wanapendwa, kwa upande wa wanaume wengi wanakiri kwamba hupenda kukubatiana na wanawake kwa sababu hupenda kusikia Mguso wa matiti
(hapa hatuzungumzii mama au dada au ndugu)

SABABU ZINAZOFANYA WANAUME WAWE WANAPENDA KUKUMBATIWA NA WAPENZI WAO WANAWAKE
Raha ya mguso wa matiti
Wanaume hujisikia salama
Husaidia kushuka chini wakiwa na hasira
Hujisikia ana rafiki wa kweli
Hujisikia kupendwa
Naweza kumnusa mpenzi wangu na kupata harufu nzuri aliyonayo
Kufurahia kuamshwa kimapenzi
Hujisikia ni mali yake
Ni nafasi na kutoa na kupokea upendo
Kusikia joto la upendo
SABABU ZINAZOFANYA WANAWAKE WAWE WANAPENDA KUKUMBATIWA NA WAPENZI WAO WA KIUME
Inawafanya kujisikia kupendwa
Hujisikia wameunganishwa na kuwa karibu zaidi
Najisikia salama
Ni dawa kisaikolojia
Najisikia joto la upendo
Najisikia kulindwa
Hufarijika na kujiona mwanaume anamjali
Hujisikia vizuri miili kugusana na kujisia mtu muhimu

Mata Amritanandamyahi kiongozi wa kiroho wa Guru kutoka India yeye hujulikana kama Hugging saint na huzunguka dunia nzima kukumbatiana na watu, inaaminika kwamba akikukumbatia unaponya magonjwa pia.

Tutaendelea na somo kuangalia aina za kukumbatiana

Nawatakia utazamaji mwema wa mechi ya soka Champions League

Chelsea VS Man united

Tuesday, May 20, 2008

Ni kitu Kidogo Lakini Muhimu Sana

Safi sana kaka Ndiaye kwani ukimbeba hivi mkeo angalau kwa wiki mara moja inasaidia sana kutopata kitu wanaita "skin hunger" kwa mkeo na mtoto naye anajua baba na mama wanapendana.

Ulioa au kuolewa kulikuwa na sababu na pia ulifanya commitment kuhakikisha unatumia muda wako wote wa maisha yako na yeye milele na milele au hadi kifo kitakapowatenganisha.


Kama unataka kuwa na mume mzuri anayehakikisha anakutunza wewe na watoto wako na ana ku-treat vizuri au kama unataka kuwa na mke ambaye siku zote mambo ni safi kila siku, basi unahitaji ku-invest vilivyo kwenye ndoa yako.
Jitahidi kumpa romantic life kila iitwapo leo, kufanya juhudi kukitunza kile ulichaonacho, kwani usione vinaelea vimeundwa na wewe pia unaweza kukiunda chako kikaelea, uwezo unao na muda ni sasa.
Ili ndoa iwe imara unahitaji kutumia muda wako na nguvu zako ili maisha yawe safi wewe na mpenzi wako.

Kuna vitu tunaviita vidogo sana ambayo ni muhimu sana katika kila ndoa yenye furaha na afya, hivi vitu havilengi kufanya mapenzi (tendo la ndoa) moja kwa moja

(nonsexual physical affections)


Hivi ni vitu muhimu na havitakiwi kuachwa kwa kila ndoa imara na yenye afya na ndoa imara na yenye afya huleta raha si kwa wahusika tu bali kwa familia nzima kwa jamii inayowazunguka na taifa pia.

Ni vitu gani hivyo vidogo Muhimu?
Kumpa mgusu wa kimwili mwenzako (touching),

Kumshika kwa mikono yote (holding),

Kumkumbatia (hugging)

Kuongea pamoja au kumsikiliza mwenzanko dakika 10 au 15 kila siku (quality time)

Kuongea na mwingine kumsikiliza mwenzake kila siku kunajenga ukaribu na kuaminiana, na kupeana mgusu wa kimwili kila usiku na asubuhi husaidia kila mmoja kujiona ni wa thamani kwa mwenzako.

Inakuwaje hapo?
Je, umewahi kusikia kitu kinaitwa "Njaa ya ngozi"

(skini hunger)
Basi, njaa ya ngozi ni mwitikio wa kihisia kutokana na kukosa kuguswa kimwili.
Binadamu huhitaji kiwango fulani cha kugusana ngozi kwa ngozi kila siku ili kuishi na kukosa hicho kitendo basi ngozi hupata njaa na matokeo yake mtu hudhoofika na kufa.

Njaa ya ngozi ndiyo inayosababisha sana wapenzi kutaka kufanya tendo la ndoa
Katika milango mitano ya fahamu, kugusa ndiyo mlango pekee wa fahamu unaojulikana kuwa ni muhimu kuliko yote, kitaalamu umuhimu wa kuguswa (touch) huzidi ule wa chakula.
Kuguswa ni mlango wa kwanza wa fahamu kujitokeza wakati wa mtu anazaliwa na huwa mlango wa mwisho wa fahamu wakati mtu anakufa.
Na kuna wana ndoa wengi sana wanapata njaa ya ngozi bila waokujijua hapa hatuzungumzii kufanya mapenzi bali tunazungumzia nonsexual touching kama vile kukumbatia, Mguso wa mtekenyo.

Kuguswa (touch) ni moja ya muhitaji muhimu ya Binadamu hivyo Hakikisha kila siku unampa mpenzi wako Mguso wa kimahaba iwe kumpa busu huku umemshika au umemkumbatia.


Kitu kingine kidogo muhimu ni nini?
Kitu kingine muhimu ni kwa mwanamke kuwa na vivazi vinavyoacha mwili wazi ukiwa chumbani.

Tafuta chupi ambazo zinavutia kwa mume wako kukuangalia mkiwa wawili tu hata kama hamjapanga kufanya mapenzi hiyo inampa hamu na kujiona anakuhitaji zaidi kila siku.
Kuna wanandoa ambao kwao kuwa mikao ya hasara hasara na uchi chumbani ni mwiko, hapo mnajinyima raha mwenyewe.


Tutaendelea ......................................................


Monday, May 19, 2008

MAMA MKWE

Kuna mabinti wengine wanapoolewa wanakuwa na busara na hekima jinsi ya kuishi na mama mkwe.
Huyo dada Kwenye picha ni mfano wa kuigwa jinsi alivyo na hekima na busara kuishi na si mama mkwe tu bali hata ndugu wote wa mumewe. JINSI YA KUWEKA MIPAKA NA MAMA MKWE
Kila binti ambaye anatarajia kuolewa au ambaye ameolewa mara nyingi likitajwa neno “Mama Mkwe” hupata mshituko kidogo hasa jamii zetu za kiafrika ambazo bado mtoto wa kiume mara nyingi humsikiliza sana mama yake katika maamuzi mengi ya kwenye ndoa yake kuliko mke wake anayeishi naye.
Wanawake wengi walio katika ndoa mpya hupata wakati mgumu sana pale wanapoona mama mkwe anakuwa na uwezo wa kum-control mume wake na matokeo yake utani wa jadi unaanza (vita) kati ya mama mkwe na binti na wakati mwingine huleta mvurugano mkubwa kabisa wa ndoa.
Wakati mwngine matatizo ya mama mkwe huanzia tangu kijana wa kiume anapotoa taarifa kwamba amepata mchumba kwani wazazi nao wakati mwingine huwa wanataka uoe mke wanaotaka wao na kitendo cha wewe kuoa mke wa aina nyingine tayari vita huanza.

Pia wakati mwingine matatizo kuanza wakati wa maandalizi ya harusi kwa mama mkwe kutaka wanandoa wafanye anavyotaka yeye.

Kitu cha msingi ni kwamba wewe binti siku ya harusi ni siku yako na siku maalumu kwako si siku yake hivyo akuache wewe na mume mpange jinsi mnavyotaka siku yenu iwe.


Kwa kila mahusiano iwe urafiki, iwe ndugu, iwe mashemeji ni muhimu kuwekwa mipaka ambayo haipaswi kuingiliwa ili mahusiano yawe mazuri na yenye mafanikio.

Kila mafanikio huwa na siri basi hata kuishi vizuri na mama mkwe kuna siri zake muhimu ambazo ni kama ifuatavyo.

UPENDO NA KUCHUKULIANA
Mama mkwe ni mama ambaye bila yeye huyo mume uliyenaye usingempata, hata kama ungeolewa na mwanamke mwingine bado hata huko ungepata mama mkwe ingawa asingekuwa yeye.

Na pia kama unahitaji mahusiano bora na familia imara basi mahusino mazuri na mama mkwe ni muhimu sana.
Hata kama hapa mwanzoni mama mkwe unaona anasumbua au haeleweki, jitahidi kuwa naye karibu kwa upendo na upole na kuchukuliana wakati unamsoma tabia zake.

ONGEA NA MUMEO
Wapo wanawake ambao baada ya kuolewa tu kasheshe zinaanza na mama mkwe, Kitu cha msingi ongea na mumeo kama unahisi mama mkwe anaingilia ndoa yako, maana umeolewa na mwanae siyo ukoo, hata kama mumeo alichangisha michango kwa ukoo mzima ili kulipa mahari kwani hiyo wewe haikuhusu, muhimu yeye ni mumoe na ni wako peke yako.
Kuwa na mawasiliano na mumeo ni jambo la kwanza au hatua ya kwanza kabisa kupambana na matatizo ya mama mkwe.

Likitokea tatizo usibaki nalo moyoni eti kuogopa mumeo asijue, ndoa nzuri ni ile ambayo mwanamke unakuwa huru kueleza hisia zako kwa mumeo bila woga wala kuogopa hata kama zitaleta maumivi muhimu usitunze siri moyoni.

MUME MWENYEWE
Kama limejitokeza tatizo kati ya mke na mama mkwe basi mume anatakiwa kuchukua hatua kama kweli anajali mke au anajali ndoa yake.
Kuna wanaume ambao husikiliza zaidi mama zao hata kama waongo na hawasikilizi chochote kutoka kwa mke wake.
Kuna wanaume ambayo mama zao huongoza ndoa zao kwa remote.
Katika maamuzi mengi mke akitaka kujua utasikia mume anasema
"Mama amesema"
Hiyo ni mbaya sana na huwaumiza sana wanawake wengi kwenye ndoa. Yaani mwanaume unashindwa kuwa na maamuzi hadi mama aseme kwani wewe bado mtoto mdogo wa shule?
Mwanaume ndiye unatakiwa kumtetea mke wako na kuwa mstari wa mbele kuhakikisha ndoa inakuwa na amani na mwanaume ndo mtu wa kuchukua hatua kuongea na mama yako kuweka mambo sawa.

UMOJA
Wakati mumeo anaongea na mama mkwe ahakikishe ana present issue kwa umoja yaani aongee kwa maana kwamba ni wewe na yeye na kwamba kama kuna tatizo mama mkwe analeta, basi mnaumizwa wote wewe na mume na si wewe peke yako.
Kwa mfano badala ya kusema
Mke wangu anatatizo
anatakiwa kusema
sisi tunatatizo
au
"mimi na mke wangu tunatatizo

UWE WAZI NA MKWELI
Uwe muwazi na mkweli jinsi unavyojisikia kwa mama mkwe wako kwani kama unajisikia unahitaji kuwa na muda zaidi na mume wako, basi mwambia mama mkwe kwamba unahitaji muda na mumeo. Pia unapoongea na mama mkwa unahitaji kuongea kwa hekima na busara ili usimkwaze. Unaweza kumwambia jinsi unavyofurahi kuwa katika familia yake na jinsi unavyofurahia kuwa naye ingawa pia unahitaji muda na mumeo peke yenu.
WEKA MUDA
Kama unaishi na mama mkwe nyumba moja unaweza kupanga muda maalumu kila siku hasa kama unafanya kazi na hushindi hapo nyumbani. Weka muda ili wewe na yeye muongee pamoja ili msiingiliane muda wa wewe na mumeo na yeye na mtoto wake (mumeo)
MFANO
Kabla ya kuoa binafsi nilikaa na wazazi wangu kuwaeleza kwamba wazitegemee kwamba nitaoa mke wanayetaka wao badala yake nitaoa mke ninayetaka mimi mahali popote duniani, wazazi wangu walikubaliana nami na pia wakatoa baraka kwamba kitu cha msingi muishi kwa amani na upendo.
Pia mke wangu kwangu comes first, the wazazi, ndugu zangu tuliozaliwa tumbo moja, ndugu na rafiki zangu.
Usipomheshimu mke wangu maana yake hujaniheshimu mimi. Ukimuheshimu mke wangu maana yake umeniheshimu mimi.

Friday, May 16, 2008

Uwongo na Ukweli

Ni kawaida watu kudhani kwamba kama zawadi imefungwa kwa kabrasha au mfuko au package nzuri sana basi kilichomo ndani kitakuwa ni kitu chenye thamani kubwa sana na kizuri sana.

Ukweli ni kwamba ufungaji wa zawadi au uzuri wa material yanayotumika kufunga zawadi haviwezi kukwambia uhakika wa uzuri wa kitu kilichomo ndani, badala yake unahitaji kufikiria zaidi, au kufanya utafiti zaidi ya hayo makabrasha ya kufungia zawadi ili kujua kilichomo ndani.

Linapokuja suala la mahusiano, hasa mahusiano mapya, watu wengi huwaangalia partners wao kwa nje bila kuangalia undani wa mtu mwenywe ili kujua ndani kuna kitu gani.
Wengi huvutiwa na uzuri wa nje au sifa za nje badala ya kuangalia na kuchunguza kile kilichomo ndani ya huo uzuri.
Watu hawaoni sababu ya kunguza au kutumia muda kupata ukweli na matokeo yake ni kujuta mbele ya safari.

Siku hizi si ajabu ukakuta mtu ameshakubaliana na mtu hadi kufika hatua ya mbali sana katika mahusiano bila hata kujua majina yote mawili ya mtu ambaye anasema anampenda na kwamba bila yeye anaona maisha hayana maana.
Watu wanafahamiana na baada ya mwezi tayari wanakubaliana kuoana na kuwa mke na mume.

Kuna mfano wa rafiki yangu aliyekuwa anajiandaa na harusi, siku moja baada ya kupata pesa akaamua kwenda Kariakoo kujipatia kiatu murua kabisa kwa ajili ya siku yake maalumu yaani siku ya harusi.
Alipofika dukani alipata viatu anavyohitaji na akawapa ruhusa wanaomuuzia wamfungie kwenye mifuko safi kabisa, wale vijana kwa jinsi walivyokuwa sharp walimfungashia viatu vyake kwenye mifuko (packing material) nzuri sana na kwa jinsi kabrasha zima la viatu lilivyokuwa linaonekana basi akaamini viatu vyake viko ndani.
Alikaa wiki nzima bila kufungua hivyo viatu huko nyumbani kwani aliamini kilichomo ni viatu vyake vizuri wacha visubiri siku ya harusi, lakini kuna siku aliamua kupima upya isije ikawa labda vyote ni vya kulia au kushoto, ile kufungua huku ametabasamu alishtuka kuona ndani ya ule mfuko mzuri na unaopendeza jamaa walimbadilishia na kumfungia matambara na makaratasi mfano wa viatu.
Nilisikitika sana kwani hii ni mfano wa mahusiano mengi ambayo huanza bila watu kuwa waangalifu.
Unahitaji ku-dig deeper linapokuja suala la mahusiano,
Utajiri, Kujulikana, Cheo, Urembo, Uzuri wa ngozi,
Familia yenye uwezo, Vipaji, Usomi, Umaskini au
kitu chochote cha nje ni sawa na kabrasha ambalo linatumika kuibeba zawadi yenyewe.

Inaweza kuwa zawadi ni makaratasi na matambala tu yamewekwa humo na utakapokuja kugundua unakuwa umeshachelewa kabisa na matokeo yake kujuta.
Umeuziwa mbuzi kwenye gunia shauri yako!
wakati unao fikiria kwa makini

Kawaida kama unatafuta uhusiano wa kudumu ni vizuri uka-invest muda mwingi kuhakikisha unamfahamu mtu vizuri, moyo wake
(marry the soul not the skin).

Maisha tunapoishi hupelekea mabadiliko ya sifa za nje, watu hufirisika, watu hunyonyoka nywele, watu huzeeka, watu hupata stress, watu huwa vilema, watu hunenepeana, watu huugua, watu hubadilika, watu hukonda hata wakawa tofauti na walivyo labda wakati wa kuanza urafiki wenu muwe mmekubaliana kwamba yakitokea mabadiliko tu kila mtu aanze mbele au achukue chake, ndo maana leo ndoa ni kama watu wanaoenda shopping.

Kama upo kwenye process za kuanza mahusino naomba jiulize hivyo ni kweli unavyomuona huyo unayemwita mpenzi wako alivyo nje ni sawa alivyo ndani?
Pia uwe makini usije ukaanza kujua baadae,
Jieulize, kama anaku-control wakati hamjaoana, je, akikuoa au mkioana ndo ataacha au kubadilika?
Kama sasa hivi hamjaoana hataki kazi; Je, unauhakika mkioana atafanya kazi?
Je, kama leo hamjaoana ni mlevi, anavuta sigara, mvuvi na mzembe, je mkioana ataacha?
Je una imani kubwa ya kuhakikisha kama leo hana mguu, mkioana atakuwa na mguu?
Uwe makini Na angalia ndani siyo nje.

Maana unaweza baadae kujitetea, unajua nilikuwa mdogo, so sikuwa makini.
Sikiliza tunakushauri mapema
Be very careful.


MATITI

Huko kijijini kwetu zamani kama wewe ni mtoto wa mwisho basi utanyonya ziwa la mama hadi basi, maana ilikuwa unaenda hadi kuchunga mbuzi porini ukirudi mama anakukalisha kwenye kitu then unaanza kunyonya na kufaidi ziwa la mama hadi miaka zaidi ya 6.
Sijui hii sasa hivi imekaaje maana matiti yanapewa umuhimu zaidi kwenye sex kuliko chakula cha mtoto.Hata Senegal nako kifua wazi kwa kwenda mbele
Ni vizuri mwanamke kuhakikisha anakuwa hasa kwa habari ya matiti yake kwa ajili yake, mtoto na mpenzi wake pia.
1/3 ya titi ni tishu ambayo ni fat na sehemu inayobaki ni tishu ya titi lenyewe, hii ina maana kwamba kuongezeka kwa size ya titi wakati mwingine hutegemea pia vyakula unavyokula kama vina fat maana yake utaongeza size ya matiti pia kama tumbo, mapaja na nk.
Size ya matiti haina uhusiano na na kiwango cha maziwa yatakayotoka kwa maana kwamba hata kama una matiti makubwa sana unaweza kutoa kiwango sawa na matiti yenye size ndogo pia likija suala la kupata magonjwa kama cancer haijalishi una size gani ya matiti kama ni kupata au kutopata.

Matiti makubwa sana kwa size wakati mwingine husababisha mwanamke asijisikie comfortable hasa kama ni binti ambaye yupo shule kwani wengi humukodolea mimacho sana (hasa wavulana na kumpa majina ya utani kutokana na kuwa na maziwa makubwa wakati umri mdogo) na hupata usumbufu kiasi cha kufanya asishiriki hata katika michezo mbalimbali shuleni.

Pia matiti yenye umbo dogo sana kisaikolojia husababisha mwanamke asijisikie vizuri hasa kutokana na kifua chake kuwa kama mwanaume kitu ambacho hujisikia kama ni sexless na pia not attractive hasa kwa wanaume kwani matiti yanamvuto wake kwa wanaume.

Hata hivyo kitu cha msingi ni mwanamke kujiamini na kuikubali hali aliyonayo ingawa kwa nchi zilizoendelea kwa sasa vyumba vya kufanya surgery (implant) za matiti vipo busy kuliko wakati wowote katika historia ya dunia kwani akina dada wengi wapo busy wengine kuyapunguza size na wengine kuongeza size na wengine kuyaweka wanavyokata wao.

Katika titi sehemu iliyo sensitive sana ni kwenye chuchu na chuchu ina vitundu kuanzia 6 – 9 ambavyo vimeunganishwa kwa mfano ya mifereji (ducts) na kwa ajili ya kutoa maziwa wakati mtoto ananyonya.

Binadamu ni mamalia peke yake ambaye matiti huwa kamili kabla hata mtoto hajazaliwa tofauti na Mbwa au wanyama wengine ambao ili ziwa liwe kubwa na kamili ni hadi mimba na kuzaliwa mtoto, hiyo ni kuthibitisha kwamba matiti ya binadamu yanahusika moja kwa moja na suala la sexual pleasure hata wakati ambapo mwanamke hayupo fertile.

Mwanamke anayenyonyesha au mwenye mimba wakati wa tendo la ndoa anaweza kutoa maziwa hasa wakati akifika kileleni, hivyo mwanaume asione shida au mwanamke kujisikia vibaya, hiyo haina shida kwani ni maziwa tu yanatoka na mzee anaweza kunywa pia ila aangalie asije akazoea kisha kakawa kamchezo kake kila siku kunywa maziwa hatimaye akamaliza chakula cha mtoto.

Yapo mazoezi ambayo mwanamke akifanya huweza kumhakikishia size na shape nzuri (kusimama)
(Tutajifunza baadae aina ya mazoezi kwa ajili ya kuyapa size na shape nzuri).

Pia matiti kuvalishwa sidiria (bra) na ili mwanamke apendeze ni vizuri kujua size ya matiti yako ili uweze kununua bra ambayo ina size halisi ya matiti kuliko kuvaa bra yoyote unayoikuta inapendeza Kariakoo, kwani kuwa na sidiria halisi kwa matiti yako ni dhahiri kwamba hata ukivaa utatoka vizuri na pia utajiamini hata ukitembea mbele za watu.

IMANI POTOFU KUHUSU CANCER YA MATITI
Kuna fununu nyingi sana kuhusiana na nini husababisha cancer ya matiti, jinsi ya kufahamu kama umeambikizwa na jinsi ya kutibu.

UWONGO:
Ni wanawake peke yao wanaoweza kuambukizwa cancer ya matiti:
UKWELI:
Wanaume pia waweza kupata cancer ya matiti, ingawa ni asilimia moja tu (1%) ya wale wanaopatikana na cancer ya matiti ni wanaume.

UWONGO:
Kama katika familia yenu hakuna mwenye cancer ya matiti au aliyewahi kuugua cancer ya matiti basi huwezi kupata cancer.
UKWELI:
Kila mwanamke ana hatari ya kupata cancer ya matiti. Watu 9 kati ya 10 ambao wanaonekana kuwa na cancer hawana historia ya familia kuugua cancer, ingawa unavyozidi kuwa na ndugu wengi wanaoathirika kwa cancer kuna uwezekano mkubwa na wewe kuugua pia.

UWONGO:
Ukigundulika kuwa na cancer ni taarifa kwamba hutapona na kifo kinakusubiri.
UKWELI
Cancer ya matiti hutibika vizuri kama itagunduliwa mapema, wanawake wengi wamepona cancer ya matit baada ya kugundulika mapema na kupata matibabu.

UWONGO
Cancer ya matiti ina kinga
UKWELI
Cancer ya matiti haijapata kinga bado, kinga thabiti ya cancer ya matiti ni kujua (detection) mapema ili kupata tiba kabla jaijasambaa mwili mzima.

UWONGO
Ukiwa na uvimbe kwenye matiti maana yake una cancer ya matiti
UKWELI
Asilimia 80% ya uvimbe kwenye matiti huwa ni dalili ya mwanzo kabisa ya cancer ya matiti.
Pia uvimbe kwenye matiti wakati mwingine ni kitu cha kawaida hasa mwanamke anapokuwa kwenye siku zake ingawa uvimbe wowote usio wa kawaida lazima ufanyiwe checkup na dakatari kuweza kujua ni nini.

UWONGO
Maumivu kwenye matiti huweza kusababisha cancer ya matiti.
UKWELI
Hakuna uthibitisho wowote kwamba cancer ya matiti husababishwa na maumivu ya matiti, ingawa wakati mwingine kuuma kwa matiti huweza kusaidia kujua kama una cancer ya matiti.
UWONGO
Kuwa na mtoto au kutokuwa na mtoto hakuna uhusiano na Cancer.
UKWELI
Utafiti unaonesha kwamba mwanamke anayepata mtoto (zaa na kunyonyesha) akiwa chini ya miaka 30 hupunguza uwezekano wakupata cancer ya matiti na mwanamke ambaye hajazaa kabisa baada ya miaka 30 anauwezekano wa kupata cancer zaidi.

Ewe mwanamke hata kama una matiti makubwa sana au madogo sana au ya kawaida; matiti ambayo yamesimama kama embe au yamelala kabisa, yawe na chuchu zilizosimama na kuchongoka au yawe na chuchu zilizojikunja kinyume (inverted) na kuonekana kama kilema au kwa jinsi yoyote ile matiti yako yanavyoonekana,
Kitu cha msingi ni kwamba
Hayo ni matiti yako,
Ni mali yako,
Mungu amekupa kama zawadi
Hivyo yafurahie,
Na jisikia fahari kwa jinsi yalivyo.

Thursday, May 15, 2008

Kazi ya matiti

Kwa mwanamke matiti yana makusudi na hayo makusudi ndiyo sababu ya mwanamke kuwa na matiti.

Matiti ni tissue hakuna mfupa ndani yake hivyo yanahitaji kutunzwa ili kuwa na size na shape ambayo mwanamke ameumbwa nayo si suala ya kuyaacha tu bali lazima yatunzwe.


Je, matiti huanza kukua lini?
Matiti huanza kukua kwa msichana hasa anapofikisha miaka 8 – 13 wapo wasichana ambao huchelewa sana kuwa na matiti hadi wanapofikisha miaka 14.
Kuanzia miaka 8 - 13 wakati huu mwili wa msichana huanza kutoa homoni ya estrogen, inayohusika na uzazi wa mwanamke
Matiti huendelea kukua hadi miaka 20 pia hutegemea kiwango cha homoni kwenye mwili wa msichana
Kabla ya matiti kujitokeza kabisa kwanza chuchu na ngozi inayozunguka hujitokeza mahali ambapo titi linatakiwa kuwa kwenye kifua cha mwanamke, chuchu huanza kuwa nyeusi pamoja na ngozi inayozunguka kuwa na aina fulani ya vipele na hatimaye titi hujitokeza na kuwa size inayotakiwa.

Ukubwa wa titi hutegemea sana kiwango cha homoni pamoja na genetics za mwanamke mwenyewe kutokana na wazazi.
Wapo wanawake wenye matiti makubwa na wapo wanawake wenye matiti madogo na kila mmoja ana raha yake kutokana na ukubwa au udogo.
Ni kawaida titi la kushoto huwa dogo kuliko lile la kulia na mwanamke hahitaji kuogopa au kujiona ni kilema, pia wapo wanawake ambao chuchu zao zimegeuka badala ya kufunga zenyewe huwa zimefunguka na hupelekea mwanamke kutojiamini na kutojisikia huru na matiti yake hasa kuonekana kwa mpenzi wake.

Uzuri wa mwanamke si matiti tu kuwa madogo au kuwa makubwa uzuri wa mwanamke ni pamoja na maeneo mwengine ya mwili wake.
Wanawake wanahitaji kufahamu kwamba wanaume huvutiwa sana na wanawake kutokana na jinsi wanavyowatazama (wanavyoona) na kwamba wanaume hupenda kwa vipande (packages) yaani mwanaume anaweza kuvutiwa na mwanamke kwa
miguu yake,
mapaja yake,
matako,
kiuno,
matiti (makubwa au madogo),
sura,
nywele,
shingo,
anavyocheka,
macho,
midomo,
, urefu,
ufupi nk.

Hivyo mwanamke kuwa na matiti madogo sana au makubwa sana lisiwe tatizo la kujisikia vibaya badala yake inabidi ujiamini na size na shape ya matiti yako na kuwa huru kuyatumia kwa kadri unavyotaka kuyafurahia wewe na umpendaye.

Kazi ya matiti:

Kutoa maziwa
Matiti hutoa maziwa ambayo ni chakula bora kwa mtoto.
Hii hupelekea matiti kuongezeka size kila anapokuwa kwenye hedhi na wapo wanawake ambao hujisikia maumivu wakiwa kwenye siku zao na pia wapo ambao huwa hawapendi kabisa hata kuguswa, hivyo kama wewe ni mwanaume na unapenda sana matiti ya mke wako au mpenzi wako ni vizuri ukafahamu kwamba si kila siku na si kila mwanamke hufurahia kushikwa matiti kila siku, zipo siku atakwambia akishikwa matiti anapata maumivu badala ya raha.

Mapenzi.
Matiti huhusika moja kwa moja na tabia ya mambo ya mapenzi kwa binadamu kwanza kwa kuvutia mwanaume na pia kwa ajili ya utamu wa mwanamke mwenyewe (pleasure) anaposisimuliwa wakati wa tendo la ndoa.

Katika utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Vienna imedhihirika kwamba matiti yenye umbo kubwa sana yana upungufu wa msisimko wakati wa kusisimuliwa kimapenzi kwa asilimia 24 ukilinganisha na matiti yenye umbo dogo.
Kwa hiyo wanawake wenye matiti madogo hufaidi zaidi linapokuja suala la mapenzi.

Pia chuchu ndiyo sehemu sensitive kuliko zote kwenye titi hivyo mwanamke akipata mwanaume anayejua kulihudumia vizuri titi basi mwanamke anaweza kufika kileleni, ingawa utafiti unaonesha kwamba ni wanawake wachache sana hufika kileleni (1 kwa 100) kwa kuchezewa matiti badala yake husaidia kupata msisimko na kupelekea sehemu zingine kujibu kama vile uke na kisimi.
Wataalamu bado wanapendekeza kwamba matiti si kwa ajili ya chakula cha mtoto tu, bali ni kwa ajili ya suala la kufanya mapenzi kwani binadamu ni mamalia peke yake ambaye wakati wa mapenzi wanaweza kufanya wakiwa uso kwa uso hivyo kunahitajika organ nyingine ya kuwapa raha wakati wa tendo la ndoa ambayo ni matiti.
Tutaendelea na kazi za matiti...................................

Wednesday, May 14, 2008

MATITI YA MWANAMKE

Kila utamaduni una mtazamo wake kuhusu mwanamke kutembea kifua wazi huku matiti yakining'ia au kufunikwa kabisa.
Kwa wazungu kuonesha matiti ni kuwa uchi na baadhi ya jamii za Kiafrika kama Swaziland kuonesha matiti ni ruksa.
UTANGULIZI
Zaidi ya kuwa matiti ni kiungo katika mwili wa mwanamke, pia matiti ni alama au kitambulisho cha mwanamke kuonesha yeye ni mama, huonesha mapenzi/upendo, ulinzi, nguvu, upendo, kukomaa kwa mwanamke na afya.

Kama wewe ni mwanamke sijui unajisikiaje ukikumbuka siku ya kwanza ulipovaa sidiria (bra) na sijui ilikuwaje?
Na sijui hii imekaaje maana unaweza kukuta mwanaume anaongea na mwanamke lakini mwanaume badala ya kumwangalia mwanamke usoni yeye anamkodolea kwenye kifua chake au matiti yake kitu kinachoonesha kuna kitu kisicho cha kawaida kinamvutia mno.

Kuna mambo mengi sana yanayoongelewa kuhusiana na suala la matiti katika kona zote za dunia, kwenye magazeti, kwenye TV kwenye radio nk.
Huku Brazil wasichana wanakiri kabisa kwamba wapo tayari kukosa kununuliwa gari lakini wapo tayari kupewa offer ya kubadilisha matiti kuwa katika size na shape wanayotaka kwani kwao matiti ni muhimu sana kuliko gari likija suala la mahusiano na wanaume

Je, ni kweli style ya mwanamke anayotumia wakati wa kulala huathiri size na shape ya matiti yake?
Je, kwa nini zaidi ya wanawake milioni 2 hapa Amerika wameamue kufanya upasuaji kwa ajili ya kubadilisha size na shape ya matiti?
Je, mwanamke mwenye matiti size ndogo au Size kubwa hupata msisimko (arousal) sawa wa kimapenzi linapokuja suala la foreplay?
Je, ni kweli kuna mazoezi yanayofanya matiti kuwa na size nzuri na shape nzuri bila kulala (kuwa malapa)?
Je, ni kweli titi la kushoto kwa ni dogo kuliko lile la kulia?

Je, matiti yana nafasi kubwa sana kwa wanaume kuvutiwa na mwanamke linapokuja suala la mahusiano?

Basi usichoke kupitia hapa ili tuchambue swali moja baada ya lingine kuhusiano na kiungo hiki muhimu tangu mtu anazaliwa na pia kuangalia jinsi ya kutunza na hatimaye mwanamke kuwa na uelewa na kuhusiana na matiti pamoja na magonjwa kama Cancer ya matiti