"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, May 6, 2008

Kwa wenzetu mbwa ni sehemu ya familia, anatambulishwa kama mtu.
Nimeona kwenye kampeni za uchaguzi wa wawakilishi wa bunge (jimbo la Ontario) kwenye CV ya mgombea (candidate) mbwa hajasahaulika.
Kama ni mbwa jike anapewa "she" na kama ni dume "he"
Natumia muda wangu mwingi sana kuwa ndani ya hili Jengo.
Algonquin College (pembroke Campus)

Masomo hunoga pale ukiwa unafanya kwa vitendo si nadharia peke yake


Huyu Bibi ana miaka 95 lakini bado anadundaKwa wanafunzi wengi kabla ya mtihani mnakaa kujadili na kuweka mikakati mizito kuhakikisha mnafanya vizuri.
Nikiwa na hili jembe (tractor) kwa kweli mjini hamtaniona.
Hivi mfuko wa pembejeo Tanzania matractor huwa mnawakopesha akina nani?
Mbona vijijini hatuyaoni?
Nimkuta jamaa anatumia hili tractor kuchanja kuni kwa ajili ya ku-heat nyumba yake wakati wa winter

Rafiki yangu John Veen (85) fahari yake ni tai ya bendera ya taifa Tanzania


Ukiingia mji kama mlevi utajua bar ipo wapi; pia kama ni mtu wa ibada utajua kanisa lipo wapi.
Hali ya kanisa hapa ni Canada ni kusuasua.
Kwenye hili kanisa siku watu wakijaa ni watu kumi (10) tu, hakuna cha kijana utakutana ana vibibi na vibabu.
Watu wanatumia muda mwingi kwenye sehemu za kula chakula kama Tim Hortons, Wendy, Subway na McDonald kuliko kanisani, pia ukitaka watu wajae church andaa banguet au chakula hapo ndo utajua hawa jamaa wanajua kuabudu chakula.

No comments: