"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, June 1, 2008

Malezi Ya Mtoto

Tabasamu lako nimelipenda, nani amekufundisha? Wakati mgumu katika malezi ya mtoto ni pale unapotakiwa kumfundisha tabia njema na adabu au nidhamu kwa ujumla.
Unahitaji kuwa na subira na uvumilivu wa hali ya juu ili usiishie kukata tamaa na kuharibu mambo kabisa.
Ni vizuri kuanza kumfundisha mtoto kitu kilicho chema na kilicho kibaya kila anapozidi kukua, hii ni kumhakikishia anakuwa mtu mwenye majukumu yake na uhakika wa maisha yake na jamii inayomzunguka.


Zifuatazo ni tips ambazo unaweza kuzitumia kumlea mtoto kuwa na tabia njema tangu mdogo.
Kawaida watoto huangalia wazazi kama mfano (role model). Usitegemee mtoto wako kuwa na tabia njema kama mzazi mwenyewe tabia yako ni ovyo. Hivyo basi jiweke mfano mzuri kwa watoto na onyesha tabia ile unataka na wao wawe nayo.
Si rahisi kumfundisha mtoto kila kitu kwa siku moja au kwa mwaka mmoja.


Anza kumfundisha mambo ya msingi kwa kadri anavyozidi kukua. Mtoto akifikia miaka 3 huanza kuelewa vitu hivyo anza kumfundisha tabia njema kama vile ukarimu, jinsi ya kula vizuri, nk
Ukitaka mtoto awe anaongea kwa heshima, anza mwenyewe kwa mfano kusema “asante” “samahani’ “nisamehe” nk unapofanya hivyo unawatia moyo na wao kufanya hivyo.
Uwe mwangalifu na lugha unayotumia kila siku kwani watoto hupenda kuiga (imitate) jinsi wakubwa wanavyoongea.
Ndiyo maana mtoto akishinda wiki moja tu na mtu mwenye maneno ya kihuni naye yeye ataanza kuyapepeta hayo maneno hadi ushangae.
Mfundishe mtoto wako kuongea na wenzake kwa heshima. Mfundishe jinsi ya kusalimia tena kwa mikono huku akitabasamu, pia mfundishe mtoto anavyotakiwa kuwa mbele za watu (public) au akiwa nyumbani au nyumbani kwa mtu.


Nakumbuka wakati wadogo tulifundishwa na mama yetu hakuna kula kwa watu hata njaa iume namna gani tulikuwa hatuli kwa watu isipokuwa kwa ndugu zetu tu kama shangazi, mjomba, bibi au babu, ingawa nilikuwa nashangaa sana watoto wengine wakija kwetu hata kabla hajakaribishwa nilikuwa najua kwa jinsi anavyokikodolea chakula hapa hata kabla hujakaribisha ataanza kunawa mikono

Kama mtoto anaonesha tabia mbaya, usiache, nenda naye chemba na mweleweshe na aelewe kosa lake na kumuonya, ukionesha tabia mbaya usichukue muda kumueleza kwamba alichofanya ni kosa au vibaya haraka iwezekanavyo.


Hakikisha pia kama unamuonya si mbele za wenzake, mwite peke yake na mwambie.
Usiwe unaimba wimbo wa kuwa na tabia njema kila siku kama unaona habadiliki na badala yake msifie kwa tabia ile njema kidogo anayoonesha.


Usimpe maneno ya jumla kwa mfano “ Kila siku wewe ni mzembe” badala ya kumsaidia hapo unamjengea hali ya kushuka moyo na hatajiamini.
Ila kama unamtia moyo hata kwa kile kidogo amefanya basi anaweza kutiwa moyo na kujitahidi kufanya vizuri zaidi.
Pia uwe makini na watoto kuangalia TV na Video kwani kuna program ambazo watoto huiga tabia za wahusika kwenye vipindi.

Usiwaonye watoto wakati wa kula, tafuta muda muafaka ndiyo uwafundishe au kuwaonya. Muda wa kula ni kwa ajili ya kula.
Wafundishe watoto kufanya kazi pamoja na wewe tangu wadogo hata siku wageni wakiwa wapo wape nafasi kusaidia kuwahudumia wageni.

Pia ni vizuri wazazi wote wawili kuwa na umoja hasa pale mtoto anapokosa, si suala la mama peke yake au baba peke yake kwani watoto wanaweza kudhani wanaonewa na mzazi mmoja kwa vile mmoja tu ndo anahusika na kurekebisha nidhamu ya watoto, katika kulea mtoto hakuna upendeleo.

Samaki Mkunje Angali Mbichi, ukiacha akakauka……
1 comment:

Anonymous said...

Umeandika, mbali ya mengi, "Pia uwe makini na watoto kuangalia TV na Video kwani kuna program ambazo watoto huiga tabia za wahusika kwenye vipindi."

Na tamati yako, “Samaki Mkunje Angali Mbichi, ukiacha akakauka……

Ukiangalia kwa makini picha ya kwanza ya tabasamu la mtoto pendeza, pozi lake, na mtindo wa kuvaa jua-miwani, wafikiri haya yote kayapata wapi?

Very interesting!

Anaonekana “a cool little guy”!