"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, May 5, 2008

MAMBO AMBAYO MWANAMKE ANAHITAJI KUTOKA KWA MWANAUME

Wapo wanaume hugongwa na magari hivihivi!(Picha kwa hisani ya Buzzle)
Ni mara nyingi sana tunasikia wanaume wakisema
“mke wangu wala huwa simuelewi”
Ni kweli wanaume tunahitaji kujua baadhi ya vitu kuhusu wanawake ili tuweze kuwafahamu zaidi.
Je ni mambo gani wanawake huhitaji kutoka kwa mwanaume?

Wanawake huhitaji mwanaume anayesikiliza zaidi kuliko kutoa jibu tu.
Wanaume ni watu wa kutia majibu (problem solvers).
Pia wanaume hujitahidi kuhakikisha mambo yanakuwa sawa kwa kila mmoja bila kusahau masuala ya mahusiano hata hivyo kuna wakati na muda wa kutoa suluhisho na pia kuna wakati ambao mwanaume anatakiwa kusikiliza tu kwa mwanamke.
Kama mke moja kwa moja amekuomba usaidie kutoa sukluhish la jambo Fulani hapo haina tatizo moja kwa moja toa jibu an fanyia kwazi.
Ila kama mke anakueleza kitu ambacho amekutana nacho iwe kazini au akiwa na watoto usitoe suluhisho kabla ya kumsikiliza kwanza.
Wanawake wanahitaji kubwa la kutaka kusikilizwa na hii ndiyo tofauti kati ya mwanaume na mwanamke, wanaume hutumia ubongo tu hata bila kuongea kuhakikisha anapata tatizo la issue zake wakati mwanamke hulazimika kuzungumza na kusikilizwa ili kupata jibu la issue yake.
Kama mwanaume hutumii muda ku-discuss mambo na mke wako hiyo siyo nzuri ndiyo maana anaweza kutumia muda wake kuongea na rafiki zake kwenye simu kwa sababu hujafanikisha hitaji lake la kusikilizwa.
Mwanaume unapoongea na mwanamke hakikisha:-
Unapoongea naye kwanza unamwangalia usoni (eye contact) ili ajue unamsikiliza
Anapomaliza kuongea hakikisha unaonesha ulikuwa unamsikiliza hasa kwa kurudia yale ameongea kwa mfano unaweza kusema, “kwa hiyo ulikuwa unaniambia ………”
Then muulize yeye alikuwa anafikiriaje kupata jibu la hiyo issue yake kabla wewe kutoa jibu.
Kufanya hivyo kutaonesha unajali sana hisia zake hasa suala zima la kusikilizwa na pia itamsaidia yeye mwenyewe kuangalia ni jinsi gani anaweza kuhusika kupata jawabu la issue aliyokuwa anakueleza.
Wataalamu wanasema mwanamke kawaida huongea maneno 45,000 kwa siku na mwanaume maneno 15,000 kwa siku hivyo ukiwa unamkatisha kuongea na kudakia kwa kutoa jibu bila kumsikiliza kisaokolojia una muumiza na itabidi atafuta mtu mwingine wa kuongea naye.

Wanawake wanahitaji mwanaume anayemuhitaji
Wanawake wanapenda kuona wanahitajiwa na mwanaume.
Siyo tu wanapenda kujisikia wapo sexy au beautiful pia wanapenda kufahamu kwamba mwanaume ambaye anatumia muda wake mwingi pamoja anavutiwa naye kila siku.
Hapa ni suala ka mwanaume kuwa na busara kuhakikisha unamtia moyo kwani kutokana na jinsi wanwake walivyo pamoja na majukumu yao wengi wakishazaa watoto miili yao inabadilika maumbo hata wao hujisikia wapo tofauti na kupoteza ujasiri, hivyo mwanaume unahitaji kumtia moyo hata kwa kumwambia kwa sasa nakuona wamo kuliko zamani.
Na kumwambia anavutia hivyo atajitahidi zaidi kujiweka kwenye form na kuwa sexy siku zote
Kama unaweza wakati anaandaa dinner unaweza kumbusu shingo yake na kumsifia jinsi ngozi yake ilivyo nyororo, na ukamnong’oneza maneno matamu jinsi alivyo mrembo hiyo itamjengea kitu kipya kwenye mind na moyo wake hivyo atakuamini na kujiskia vizuri zaidi.
Hata wakati mkiwa faragha jitahidi kwenda na mahaba kama vile zile ziku za kwanza mlipokuwa ndo mnaoana unaweza kumueleza
jinsi ngozi yake ilivyo nzuri,
hips zake zilivyo bomba,
miguu yake ilivyo ya uhakika,
shingo yake ilivyo kiboko,
na hapo chini palivyo patamu,
fahamu kwamba maongezi yako yanajaza kitu muhimu sana kwenye kichwa chake na atajisihia unamuhitaji na unampa usalama zaidi.

Mwanamke anahitaji mwanaume ambaye si rafiki wa watoto tu bali ni mtu anayelinda nidhamu ya watoto.
Likija suala la kuwapa nidhamu watoto wanaume wengi hujiweka pembeni na kuwaachia wanawake peke yao, wanawake hujisikia vizuri pale mwanaume anaposhirikiana na mke wake katika kuwalea watoto kuwa na nidhamu nzuri hasa pale wanapokosea.
Huwa inaumiza sana wanawake pale anapomwambia mtoto asifanye kitu fulani au anampowakataza kabisa kufanya kitu, then wakienda kwa baba yeye anawakubalia na kuwambia fanyeni.
Mwanaume huonekana kama yeye ndiye mzazi rahisi sana kwa watoto na hivyo kutengeneza mazingira ya mama kuonekana mnoko.
Hiyo huweka hasira kwa mwanamke na pia mwanaume unakuwa unarutubisha bomu ambalo siku yoyote linaweza kukulipukia wewe mwenyewe, pia kuna kitu unakijenga ndani ya mke ambacho hafurahii.

Wanawake wanahitaji mwanaume anayewaamini hata kama ana wivu.
Mara nyingi mwanaume unapoondoka nyumbani unaweza kuuliza
“unaenda wapi?
“na utarudi saa ngapi?”
Haya ni maswali mwanamke akikuuliza anapenda umpe jibu bila tatizo kwani anataka kujua wewe mpenzi wake unaenda wapi na utarudi saa ngapi, kuna wanaume hapo huwa inakuwa ugomvi kisa unaulizwa unaenda wapi na utarudi saa ngapi.
Moja ya msingi wa mahusiano yoyote ni kuaminiana (trust)
Pia mke wako anaweza kupita sehemu na wanaume wakamsifia kwa jinsi alivyo mrembo, sasa kwa mwanaume isiwe hasira na kuanzisha zogo eti kisa wanaume wengine wamemwambia mke wako anapendeza.
Wanawake wanajisikia vizuri kuambiwa wanapendeza hata na wanaume na wanajisikia kweli mimi wamo kama hata fulani amenisifia nimependeza.
Mimi nakubaliana na najisikia vizuri kama hata wanaume wenzangu watamsifia mke wangu kwamba anavutia na nitamwambia kabisa kwamba fulani kasema unavutia sana naamini nitakuwa nimemtia moyo zaidi na atajisikia vizuri zaidi na pia atazidi kujiamini zaidi.

Wanawake wanahitaji mwanaume anayewapa uhuru.
Wanawake wanapenda sana kuwa huru na hii inafanya baadhi ya wanaume wasijisikie vizuri.
Kutokana na mabadiliko ya maisha ya ,wanawake wanafanya kila ambacho kipo kwenye akili zao kwa ajili ya kuendeleza na kuimarisha familia,
wanafanya kazi,
wanafanya business,
wanasafiri na
pia wanafanya miradi yenye lengo la kuimarisha uwezo wa familia kiuchumi.
Wapo wanaume huona haiwezekana mwanamke kufanya kazi za ofisini eti atakuwa huru mno kiasi kwambaatachukuliwa na wanaume wengine.
Hayo ni mawazo ya kizamani na hayana nafasi kwa karne ya leo.
Unamzuia mke hata kwenda shule eti atachukuliwa na wanaume wengine.
Mimi naamini ni vizuri kumtia moyo kwanza awe anajiamini na kwamba anaweza kufanya jambo lolote akitaka kwani uwezo anao.
Asipotiwa moyo na mume ni nani ataweza kumtia moyo ili ajiamini na kufanya mambo makubwa kwa ajili ya familia.
Maisha ya sasa hivi yanahitaji wana ndoa ambao wanachakarika kwelikweli hivyo ni suala la kumpa mke wako uhuru ili muweze kusaidiana kuendeleza familia na maisha kwa ujumla.

Wanawake wanahitaji mwanaume anayetambua mambo muhimu madogo anayofanya.
Usione nguo zako zimenyoshwa vizuri, watoto wanasafishwa na vizuri, nguo zinafuliwa na kunukia vizuri au chakula kinapikwa vizuri, hapo mwanamke amefanya kazi kubwa na anapenda sana umpe credit kwa kazi kama hizo na kama siku ukipata nafasi unaweza kumsaidia na mkafanya pamoja hiyo inatia moyo sana.
Kuliko wewe ni kuvaa tu au kula tu na kuona ni wajibu wake, ni kweli ni wajibu wake lakini hizo kazi si mchezo zinachukua muda na nguvu.
Kama mwanaume huwa husaidii kazi za nyumbani ni vizuri ukaanza sasa, huna excuse kama unataka kuwa na mwanamke ambaye anataka kujisikia ana mume anayemjali.
Hivi vitu vidogovidogo vinawafanya wanawake wajisikia raha sana mkifanya pamoja.
Pia unakuwa umempunguzia muda wake wa kufanya hiyo kazi moja na kumpa muda wa ziada hata wa kuwa na wewe mwenyewe pia.
Wapo wanaume hulaumu tu mke wangu kila wakati yeye na kazi mchana na usiku na hata akiingia chumbani anakuwa amechoka, kumbe wewe mwenywe husaidii kazi ili mke apumzike.
Mwanamke huhitaji mwanaume anayefanya vitu anavyovipenda
Kama anaenda shopping unaweza kwenda naye na mkawa na muda mzuri pamoja huko kwenye shopping, kama anapenda kwenda kwenye matamasha ya miziki na michezo unaweza kwenda naye pia mkawa na muda mzuri, kama anapenda kuhudhuria semina za ndoa au neno la Mungu nenda naye pamoja.
Hii ni kuonesha kwamba na wewe wamo katika yale anapenda hiyo itaonesha kwamba unamjali sana na ina maana kubwa sana kwake.
Siyo mwaka unaisha hujaenda na mke mahali yeye anapenda then unasema ninamjali sana mke wangu.

Mwanamke anahitaji mwenzi siyo Baba.
Huwa inasikitisha sana kwamba mwanamke hawezi kufanya kitu chochote hata kile ambacho kipo logical mpaka apate ruhusa kwa mume.
Hiyo siyo ndoa bali ni uhusianoa wa mtoto na mzazi.
Kuna mambo ya msingi kama yale yanayohusu pesa hayo ni kweli yanahitaji kuwasiliana kwanza ndo mtu ufanye mfanye.
Lakini hata kama anataka kwenda kula lunch na rafiki zake wa kike lazima aombe ruhusa kwa mume hiyo kali.
Mwanaume pia inabidi ujiulize je, wewe huwa unamuomba ruhusa mambo yote unayofanya?
Ka sivyo kwa nini yeye akuombe ruhusa kila kitu?

Mwanamke anahitaji mwanaume ambaye hamlinganishi na mama yake.
Utakuta mwanaume analalamika kwamba mama yake ndiye
aliyekuwa anapika chakula kizuri,
au mama yangu alikuwa anafua nguo kwa sabuni fulani nzuri zaidi
au mama yake alikuwa anafanya hiki na kile.
Fahamu kwamba mke ni mtu tofauti sana na mama yako aliyekuzaa.
Ni kweli watu huwa tunakuwa na kumbukumbu nzuri sana za mambo mazuri ambayo mama zetu walikuwa wanatufanyia ila kama umeoa na unataka kila kitu kama mama yako ni vizuri ukahama na kwenda kwa mama yako mapema.
Wanawake ni watu ambao siku zote hujitahidi sana kuhakikisha mambo yanaenda na kama mwanaume hujaridhika na jinsi anavyopika, au anavyofua nguo au kulea watoto ni vizuri ukamsaidia kufanya vile unataka kuliko kumsema kwa kulinganisha jinsi mama yako alivyokuwa anafanya.
Hapo una mambo ya mawili ya kufanya
kwanza kumsaidia
au pili fanya mwenyewe.

Mwanamke anahitaji mwanaume hot kwenye sex pia
Wanawake pia wanahitaji tendo la ndoa linalowaridhisha na kuwafikisha pale wanahitaji. Anahitaji mwanaume anaye mtimizia ndoto zake za mahaba, anafurahia na kujisikia raha jinsi Mume anavyompa mgusu wa kimwili wenye msisimko wa raha,
Anajisikia vizuri kupata busu tamu,
Anajisikia vizuri kukumbatiwa
Anapenda kusikia maneno matamu ya kimapenzi kwenye masikio yake
pia wanapenda kusikia na kuona mambo mapya kitandani siyo mazoezi ya kila mwaka mambo yaleyale, anajisikia vizuri kuwa na mwanaume mbunifu na dereva mzuri.
Hahitaji mwanaume anayempeleka kitandani na baada ya dakika mbili amemaliza.
Hapo unaweza kumpotezea hamu ya tendo la ndoa ambayo ni zawadi kuu Mungu ametupa viumbe wake.
Mwanamke anahitaji mwanaume anayejua kumuandaa kabla ya tendo lenyewe na pia anahitaji mume anayejua kumaliza kwa mtindo ambao anaridhika.
Mwanaume unahitaji kuhakikisha tendo la ndoa linakidhi kiu yake, anaridhika na linakuwa na maana kwako na kwake na kila siku hamu inazidi kukua zaidi.


No comments: