"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, May 14, 2008

MATITI YA MWANAMKE

Kila utamaduni una mtazamo wake kuhusu mwanamke kutembea kifua wazi huku matiti yakining'ia au kufunikwa kabisa.
Kwa wazungu kuonesha matiti ni kuwa uchi na baadhi ya jamii za Kiafrika kama Swaziland kuonesha matiti ni ruksa.
UTANGULIZI
Zaidi ya kuwa matiti ni kiungo katika mwili wa mwanamke, pia matiti ni alama au kitambulisho cha mwanamke kuonesha yeye ni mama, huonesha mapenzi/upendo, ulinzi, nguvu, upendo, kukomaa kwa mwanamke na afya.

Kama wewe ni mwanamke sijui unajisikiaje ukikumbuka siku ya kwanza ulipovaa sidiria (bra) na sijui ilikuwaje?
Na sijui hii imekaaje maana unaweza kukuta mwanaume anaongea na mwanamke lakini mwanaume badala ya kumwangalia mwanamke usoni yeye anamkodolea kwenye kifua chake au matiti yake kitu kinachoonesha kuna kitu kisicho cha kawaida kinamvutia mno.

Kuna mambo mengi sana yanayoongelewa kuhusiana na suala la matiti katika kona zote za dunia, kwenye magazeti, kwenye TV kwenye radio nk.
Huku Brazil wasichana wanakiri kabisa kwamba wapo tayari kukosa kununuliwa gari lakini wapo tayari kupewa offer ya kubadilisha matiti kuwa katika size na shape wanayotaka kwani kwao matiti ni muhimu sana kuliko gari likija suala la mahusiano na wanaume

Je, ni kweli style ya mwanamke anayotumia wakati wa kulala huathiri size na shape ya matiti yake?
Je, kwa nini zaidi ya wanawake milioni 2 hapa Amerika wameamue kufanya upasuaji kwa ajili ya kubadilisha size na shape ya matiti?
Je, mwanamke mwenye matiti size ndogo au Size kubwa hupata msisimko (arousal) sawa wa kimapenzi linapokuja suala la foreplay?
Je, ni kweli kuna mazoezi yanayofanya matiti kuwa na size nzuri na shape nzuri bila kulala (kuwa malapa)?
Je, ni kweli titi la kushoto kwa ni dogo kuliko lile la kulia?

Je, matiti yana nafasi kubwa sana kwa wanaume kuvutiwa na mwanamke linapokuja suala la mahusiano?

Basi usichoke kupitia hapa ili tuchambue swali moja baada ya lingine kuhusiano na kiungo hiki muhimu tangu mtu anazaliwa na pia kuangalia jinsi ya kutunza na hatimaye mwanamke kuwa na uelewa na kuhusiana na matiti pamoja na magonjwa kama Cancer ya matiti

4 comments:

kamala J Lutatinisibwa said...

mzee unaafanya utafiti! endelea kutuelimisha mkuu. safi sana bonge la uelimishaji, sijui da'Subi anasemaje?

Subi said...

Hapa sina la kusema Kamala, mi namsikiliza mtafiti wetu Lazarus. Mwelimishaji wa masuala ya ndoa, mahusiano kwa ujumla na afya ya uzazi.

Masuala ya mapenzi, mihemuko ya mwili, ukuaji wa via za uzazi nk. kila mtu ana uzoefu na uelewa wake kulingana na jamii na mazingira aliyokulia, hivi ni vizuri kusikia toka kwa wengine na kisha mtu akachambua kile kinachoendana na anavyojiona/jihisi yeye! Elimu haina mwisho wala haifai kuihodhi, wacha tu tujuzane!

calvin lekule said...

NAOMBA KUFAHAMU VITU VINAVYOSABABISHA MATITI YAWE MAKUBWA NA VYAKULA VINAVYO PUNGUZA UKUBWA WA MATITI PAMOJA NA MAZOEZI,PIA JE NI KWELI STAILI YA KULALA PIA INATAKIWA KUZINGATIWA?

calvin lekule said...

napenda kuelewa zaidi kuhusu matiti rafiki,