"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, May 16, 2008

MATITI

Huko kijijini kwetu zamani kama wewe ni mtoto wa mwisho basi utanyonya ziwa la mama hadi basi, maana ilikuwa unaenda hadi kuchunga mbuzi porini ukirudi mama anakukalisha kwenye kitu then unaanza kunyonya na kufaidi ziwa la mama hadi miaka zaidi ya 6.
Sijui hii sasa hivi imekaaje maana matiti yanapewa umuhimu zaidi kwenye sex kuliko chakula cha mtoto.Hata Senegal nako kifua wazi kwa kwenda mbele
Ni vizuri mwanamke kuhakikisha anakuwa hasa kwa habari ya matiti yake kwa ajili yake, mtoto na mpenzi wake pia.
1/3 ya titi ni tishu ambayo ni fat na sehemu inayobaki ni tishu ya titi lenyewe, hii ina maana kwamba kuongezeka kwa size ya titi wakati mwingine hutegemea pia vyakula unavyokula kama vina fat maana yake utaongeza size ya matiti pia kama tumbo, mapaja na nk.
Size ya matiti haina uhusiano na na kiwango cha maziwa yatakayotoka kwa maana kwamba hata kama una matiti makubwa sana unaweza kutoa kiwango sawa na matiti yenye size ndogo pia likija suala la kupata magonjwa kama cancer haijalishi una size gani ya matiti kama ni kupata au kutopata.

Matiti makubwa sana kwa size wakati mwingine husababisha mwanamke asijisikie comfortable hasa kama ni binti ambaye yupo shule kwani wengi humukodolea mimacho sana (hasa wavulana na kumpa majina ya utani kutokana na kuwa na maziwa makubwa wakati umri mdogo) na hupata usumbufu kiasi cha kufanya asishiriki hata katika michezo mbalimbali shuleni.

Pia matiti yenye umbo dogo sana kisaikolojia husababisha mwanamke asijisikie vizuri hasa kutokana na kifua chake kuwa kama mwanaume kitu ambacho hujisikia kama ni sexless na pia not attractive hasa kwa wanaume kwani matiti yanamvuto wake kwa wanaume.

Hata hivyo kitu cha msingi ni mwanamke kujiamini na kuikubali hali aliyonayo ingawa kwa nchi zilizoendelea kwa sasa vyumba vya kufanya surgery (implant) za matiti vipo busy kuliko wakati wowote katika historia ya dunia kwani akina dada wengi wapo busy wengine kuyapunguza size na wengine kuongeza size na wengine kuyaweka wanavyokata wao.

Katika titi sehemu iliyo sensitive sana ni kwenye chuchu na chuchu ina vitundu kuanzia 6 – 9 ambavyo vimeunganishwa kwa mfano ya mifereji (ducts) na kwa ajili ya kutoa maziwa wakati mtoto ananyonya.

Binadamu ni mamalia peke yake ambaye matiti huwa kamili kabla hata mtoto hajazaliwa tofauti na Mbwa au wanyama wengine ambao ili ziwa liwe kubwa na kamili ni hadi mimba na kuzaliwa mtoto, hiyo ni kuthibitisha kwamba matiti ya binadamu yanahusika moja kwa moja na suala la sexual pleasure hata wakati ambapo mwanamke hayupo fertile.

Mwanamke anayenyonyesha au mwenye mimba wakati wa tendo la ndoa anaweza kutoa maziwa hasa wakati akifika kileleni, hivyo mwanaume asione shida au mwanamke kujisikia vibaya, hiyo haina shida kwani ni maziwa tu yanatoka na mzee anaweza kunywa pia ila aangalie asije akazoea kisha kakawa kamchezo kake kila siku kunywa maziwa hatimaye akamaliza chakula cha mtoto.

Yapo mazoezi ambayo mwanamke akifanya huweza kumhakikishia size na shape nzuri (kusimama)
(Tutajifunza baadae aina ya mazoezi kwa ajili ya kuyapa size na shape nzuri).

Pia matiti kuvalishwa sidiria (bra) na ili mwanamke apendeze ni vizuri kujua size ya matiti yako ili uweze kununua bra ambayo ina size halisi ya matiti kuliko kuvaa bra yoyote unayoikuta inapendeza Kariakoo, kwani kuwa na sidiria halisi kwa matiti yako ni dhahiri kwamba hata ukivaa utatoka vizuri na pia utajiamini hata ukitembea mbele za watu.

IMANI POTOFU KUHUSU CANCER YA MATITI
Kuna fununu nyingi sana kuhusiana na nini husababisha cancer ya matiti, jinsi ya kufahamu kama umeambikizwa na jinsi ya kutibu.

UWONGO:
Ni wanawake peke yao wanaoweza kuambukizwa cancer ya matiti:
UKWELI:
Wanaume pia waweza kupata cancer ya matiti, ingawa ni asilimia moja tu (1%) ya wale wanaopatikana na cancer ya matiti ni wanaume.

UWONGO:
Kama katika familia yenu hakuna mwenye cancer ya matiti au aliyewahi kuugua cancer ya matiti basi huwezi kupata cancer.
UKWELI:
Kila mwanamke ana hatari ya kupata cancer ya matiti. Watu 9 kati ya 10 ambao wanaonekana kuwa na cancer hawana historia ya familia kuugua cancer, ingawa unavyozidi kuwa na ndugu wengi wanaoathirika kwa cancer kuna uwezekano mkubwa na wewe kuugua pia.

UWONGO:
Ukigundulika kuwa na cancer ni taarifa kwamba hutapona na kifo kinakusubiri.
UKWELI
Cancer ya matiti hutibika vizuri kama itagunduliwa mapema, wanawake wengi wamepona cancer ya matit baada ya kugundulika mapema na kupata matibabu.

UWONGO
Cancer ya matiti ina kinga
UKWELI
Cancer ya matiti haijapata kinga bado, kinga thabiti ya cancer ya matiti ni kujua (detection) mapema ili kupata tiba kabla jaijasambaa mwili mzima.

UWONGO
Ukiwa na uvimbe kwenye matiti maana yake una cancer ya matiti
UKWELI
Asilimia 80% ya uvimbe kwenye matiti huwa ni dalili ya mwanzo kabisa ya cancer ya matiti.
Pia uvimbe kwenye matiti wakati mwingine ni kitu cha kawaida hasa mwanamke anapokuwa kwenye siku zake ingawa uvimbe wowote usio wa kawaida lazima ufanyiwe checkup na dakatari kuweza kujua ni nini.

UWONGO
Maumivu kwenye matiti huweza kusababisha cancer ya matiti.
UKWELI
Hakuna uthibitisho wowote kwamba cancer ya matiti husababishwa na maumivu ya matiti, ingawa wakati mwingine kuuma kwa matiti huweza kusaidia kujua kama una cancer ya matiti.
UWONGO
Kuwa na mtoto au kutokuwa na mtoto hakuna uhusiano na Cancer.
UKWELI
Utafiti unaonesha kwamba mwanamke anayepata mtoto (zaa na kunyonyesha) akiwa chini ya miaka 30 hupunguza uwezekano wakupata cancer ya matiti na mwanamke ambaye hajazaa kabisa baada ya miaka 30 anauwezekano wa kupata cancer zaidi.

Ewe mwanamke hata kama una matiti makubwa sana au madogo sana au ya kawaida; matiti ambayo yamesimama kama embe au yamelala kabisa, yawe na chuchu zilizosimama na kuchongoka au yawe na chuchu zilizojikunja kinyume (inverted) na kuonekana kama kilema au kwa jinsi yoyote ile matiti yako yanavyoonekana,
Kitu cha msingi ni kwamba
Hayo ni matiti yako,
Ni mali yako,
Mungu amekupa kama zawadi
Hivyo yafurahie,
Na jisikia fahari kwa jinsi yalivyo.

No comments: