"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, May 11, 2008

Mother's Day

Leo si siku maalumu ya "MAMA" hapa Canada.
kila mmoja anamshukuru mama kwa zawadi au kwa jitu chochote anachoona mama anastahili na anaweza kumpa kumbukumbu.
Najua mama yangu upo mbali sana na mimi ili tuweze kukaa pamoja nikakushukuru kwa jinsi ulivyonilea hadi nimeweza kufika hapa nilipo na jinsi nimekuwa nafaa kwa jamii bila wewe naamini dunia ingepata hasara kwa mimi kuwepo duniani.
Najua ulikuwa na wakati mgumu sana kuhakikisha naendana na malezi yako, Mungu akubariki sana pia ni maombi yangu kwamba Mungu akupe maisha marefu zaidi ili nizidi kujifunza zaidi kutoka kwako.Mama yangu mpenzi (Atwelukye) akiwa na wajukuu zake - April 2008
Njombe Tanzania

Ni nafasi ya pekee na pia ni baraka kubwa kuwa Mama. Mama ni upendo na furaha na pia ni kila kitu kwea mtoto. Mama ni kiumbe wa kwanza ambapo mtoto hupata mguso na kujisikia katika hisia zake. Mama ni kimbilio, mwamba na mwali na watoto hujisikia vizuri wakiwa na mama hasa linapokuja suala la hisia.
Kuwa mama pia ni kazi na ili uwe mama mzuri huna budi kuyaangalia yafuatayo kwa umakini zaidi.

Mama ni upendo kwa watoto.
Nyumbani panaweza kuwa ni mahali ambpo mpo busy sana muda wote na mizunguko mingi, kama mama tambua kwamba watoto wanahitaji kukua huku wakijua kwamba wanapendwa na wazazi wao na hili ni muhimu kwani na wao wanahitaji siku moja kutoa upendo kwa watu wengine hapa duniani.

Mama ni mfano wa watoto (role model)
Siku kwa siku, dakika kwa dakika saa kwa saa watoto wanakuangalia wewe mama, wanakupenda na wanapenda sana kuwa kama wewe katika maisha yao. Kutokana na jinsi unavyotenda, unavyofanya na unavyoongea ndivyo watoto wako wanatavyokuwa.

wafundidhe kuwa na nidhamu kwa upendo.
Malezi bora, nidhamu na adabu ni vitu muhimu sana katika kukua kwa mtoto. Watoto wanahitaji kuwa na mipanga katika mambo yanayofanya na tabia yao njema ni muhimu sana kitu cha msingi lazima unapowafundisha au kuwakanya au kuwaonya au kuwapa adhabu lazima iwe kwa upendo na kwa kiasi. Siyo kuwaumiza na kuwatendea unyama.

Wape sifa wanazostahili.
Mara nyingi mama huona mambo mabaya tu mtoto anafanya, ni vizuri kuona na yale mazuri mtoto anafanya na kumpa sifa anazostahili. Kama mama kila mara kazi yako ni kuwasahihisha tu makosa itawapa nafasi watoto kujiona wao ni watu wa kushindwa tu. Watie moyo kila hatua nzuri mtoto anafanya katika maendeleo ya kuwa na tabia njema. Ukiwaamini na wao watajiamini na kuwa imara zaidi.

Hakikisha ndoa yako ipo imara.
Kama umeolewa, watoto mara nyingi hujifunza jinsi ndoa zilivyo kwa kuwaangalia na hasa kuangalia wewe mama una treat vipi mume wako. Uimara wa ndoa za watoto wako unategemea sana upendo unaouonesha kwa mume wako na jinsi wanavyoona katika kukua kwao.

Kula pamoja nao.
Maisha ya sasa na mifumo yake imefanya kila mtu kuwa na ratiba yake inawezekana mama una shift yako kazini na baba naye ana shift yake kazini na mnakosa hata muda wa kula pamoja na watoto. Ni vizuri kula na watoto ili kuweza kupata muda wa kuwa pamoja na kujifunza kutoka kwao angalau mara nne au tatu kwa wiki.

Mama unahitaji kuonesha wema kwa watoto
Ukiwaonesha wema watoto wako basi na wao watakuwa wema kwa watu wengine. Mama ambaye ni mchoyo na watoto wake huwa wachoyo pia.

Mama unahitaji kuwa mwalimu
Kila mama unafanya fahamu au fanya kama mwalimu. Kila kazi unafanya ni nafasi ya kufundisha watoto wako. Kila nafasi iwe wakati wa shida au wakati wa raha wafundishe watoto kitu kipya.

Waambie watoto kuhusu Mungu
Kanisa linaweza kuwafundisha watoto wako habari za Mungu na mambo mengi yanayohusu Mungu. Lakini watoto huangalia na kusikiliza maana ya imani kupitia mama, watoto hujua ukweli wa mambo ya kanisani kwa kupitia mama hapo nyumbani jinsi unavyofanya na jinsi unavyoongea.

Wakati mwingine wape vichekesho na utani kidogo.
Maisha ni furaha na kuchangamshana hasa kwa watoto, basi ukipata muda cheza na mtoto mchezo anapenda, au kitu anfurahia kufanya. Siyo unakuwa serious hadi watoto wanakukimbia kila ukiingia nyumbani

Fahamu rafiki wa watoto wako
Mama mzuri lazima atakuwa anajua rafiki wa watoto wake na wakati mwingine huwaleta nyumbani ili wafurahi pamoja. Wape furaha watoto kwa kuwakaribisha rafiki zao kwako na wewe pamoja.

Jitunze mwenyewe:
Wewe ni mtu muhimu sana na kutokana na ukubwa wa majukumu ya kutunza watoto wakati mwingine mama hujisahau kujitunza mwenyewe.

Wewe mama ni mtu muhimu sana kwa maisha ya watoto wako, una nafasi nzuri sana ya kuwatengeneza weatoto wako kuwa unavyotaka kwa habari ya tabia njema na mafanikio.
Hivyo wapende watoto wako, walinde na wafurahie.

Wanawe huondoka na kumwita heri

Mithali 31:28


No comments: