"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, May 20, 2008

Ni kitu Kidogo Lakini Muhimu Sana

Safi sana kaka Ndiaye kwani ukimbeba hivi mkeo angalau kwa wiki mara moja inasaidia sana kutopata kitu wanaita "skin hunger" kwa mkeo na mtoto naye anajua baba na mama wanapendana.

Ulioa au kuolewa kulikuwa na sababu na pia ulifanya commitment kuhakikisha unatumia muda wako wote wa maisha yako na yeye milele na milele au hadi kifo kitakapowatenganisha.


Kama unataka kuwa na mume mzuri anayehakikisha anakutunza wewe na watoto wako na ana ku-treat vizuri au kama unataka kuwa na mke ambaye siku zote mambo ni safi kila siku, basi unahitaji ku-invest vilivyo kwenye ndoa yako.
Jitahidi kumpa romantic life kila iitwapo leo, kufanya juhudi kukitunza kile ulichaonacho, kwani usione vinaelea vimeundwa na wewe pia unaweza kukiunda chako kikaelea, uwezo unao na muda ni sasa.
Ili ndoa iwe imara unahitaji kutumia muda wako na nguvu zako ili maisha yawe safi wewe na mpenzi wako.

Kuna vitu tunaviita vidogo sana ambayo ni muhimu sana katika kila ndoa yenye furaha na afya, hivi vitu havilengi kufanya mapenzi (tendo la ndoa) moja kwa moja

(nonsexual physical affections)


Hivi ni vitu muhimu na havitakiwi kuachwa kwa kila ndoa imara na yenye afya na ndoa imara na yenye afya huleta raha si kwa wahusika tu bali kwa familia nzima kwa jamii inayowazunguka na taifa pia.

Ni vitu gani hivyo vidogo Muhimu?
Kumpa mgusu wa kimwili mwenzako (touching),

Kumshika kwa mikono yote (holding),

Kumkumbatia (hugging)

Kuongea pamoja au kumsikiliza mwenzanko dakika 10 au 15 kila siku (quality time)

Kuongea na mwingine kumsikiliza mwenzake kila siku kunajenga ukaribu na kuaminiana, na kupeana mgusu wa kimwili kila usiku na asubuhi husaidia kila mmoja kujiona ni wa thamani kwa mwenzako.

Inakuwaje hapo?
Je, umewahi kusikia kitu kinaitwa "Njaa ya ngozi"

(skini hunger)
Basi, njaa ya ngozi ni mwitikio wa kihisia kutokana na kukosa kuguswa kimwili.
Binadamu huhitaji kiwango fulani cha kugusana ngozi kwa ngozi kila siku ili kuishi na kukosa hicho kitendo basi ngozi hupata njaa na matokeo yake mtu hudhoofika na kufa.

Njaa ya ngozi ndiyo inayosababisha sana wapenzi kutaka kufanya tendo la ndoa
Katika milango mitano ya fahamu, kugusa ndiyo mlango pekee wa fahamu unaojulikana kuwa ni muhimu kuliko yote, kitaalamu umuhimu wa kuguswa (touch) huzidi ule wa chakula.
Kuguswa ni mlango wa kwanza wa fahamu kujitokeza wakati wa mtu anazaliwa na huwa mlango wa mwisho wa fahamu wakati mtu anakufa.
Na kuna wana ndoa wengi sana wanapata njaa ya ngozi bila waokujijua hapa hatuzungumzii kufanya mapenzi bali tunazungumzia nonsexual touching kama vile kukumbatia, Mguso wa mtekenyo.

Kuguswa (touch) ni moja ya muhitaji muhimu ya Binadamu hivyo Hakikisha kila siku unampa mpenzi wako Mguso wa kimahaba iwe kumpa busu huku umemshika au umemkumbatia.


Kitu kingine kidogo muhimu ni nini?
Kitu kingine muhimu ni kwa mwanamke kuwa na vivazi vinavyoacha mwili wazi ukiwa chumbani.

Tafuta chupi ambazo zinavutia kwa mume wako kukuangalia mkiwa wawili tu hata kama hamjapanga kufanya mapenzi hiyo inampa hamu na kujiona anakuhitaji zaidi kila siku.
Kuna wanandoa ambao kwao kuwa mikao ya hasara hasara na uchi chumbani ni mwiko, hapo mnajinyima raha mwenyewe.


Tutaendelea ......................................................


No comments: