"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, May 16, 2008

Uwongo na Ukweli

Ni kawaida watu kudhani kwamba kama zawadi imefungwa kwa kabrasha au mfuko au package nzuri sana basi kilichomo ndani kitakuwa ni kitu chenye thamani kubwa sana na kizuri sana.

Ukweli ni kwamba ufungaji wa zawadi au uzuri wa material yanayotumika kufunga zawadi haviwezi kukwambia uhakika wa uzuri wa kitu kilichomo ndani, badala yake unahitaji kufikiria zaidi, au kufanya utafiti zaidi ya hayo makabrasha ya kufungia zawadi ili kujua kilichomo ndani.

Linapokuja suala la mahusiano, hasa mahusiano mapya, watu wengi huwaangalia partners wao kwa nje bila kuangalia undani wa mtu mwenywe ili kujua ndani kuna kitu gani.
Wengi huvutiwa na uzuri wa nje au sifa za nje badala ya kuangalia na kuchunguza kile kilichomo ndani ya huo uzuri.
Watu hawaoni sababu ya kunguza au kutumia muda kupata ukweli na matokeo yake ni kujuta mbele ya safari.

Siku hizi si ajabu ukakuta mtu ameshakubaliana na mtu hadi kufika hatua ya mbali sana katika mahusiano bila hata kujua majina yote mawili ya mtu ambaye anasema anampenda na kwamba bila yeye anaona maisha hayana maana.
Watu wanafahamiana na baada ya mwezi tayari wanakubaliana kuoana na kuwa mke na mume.

Kuna mfano wa rafiki yangu aliyekuwa anajiandaa na harusi, siku moja baada ya kupata pesa akaamua kwenda Kariakoo kujipatia kiatu murua kabisa kwa ajili ya siku yake maalumu yaani siku ya harusi.
Alipofika dukani alipata viatu anavyohitaji na akawapa ruhusa wanaomuuzia wamfungie kwenye mifuko safi kabisa, wale vijana kwa jinsi walivyokuwa sharp walimfungashia viatu vyake kwenye mifuko (packing material) nzuri sana na kwa jinsi kabrasha zima la viatu lilivyokuwa linaonekana basi akaamini viatu vyake viko ndani.
Alikaa wiki nzima bila kufungua hivyo viatu huko nyumbani kwani aliamini kilichomo ni viatu vyake vizuri wacha visubiri siku ya harusi, lakini kuna siku aliamua kupima upya isije ikawa labda vyote ni vya kulia au kushoto, ile kufungua huku ametabasamu alishtuka kuona ndani ya ule mfuko mzuri na unaopendeza jamaa walimbadilishia na kumfungia matambara na makaratasi mfano wa viatu.
Nilisikitika sana kwani hii ni mfano wa mahusiano mengi ambayo huanza bila watu kuwa waangalifu.
Unahitaji ku-dig deeper linapokuja suala la mahusiano,
Utajiri, Kujulikana, Cheo, Urembo, Uzuri wa ngozi,
Familia yenye uwezo, Vipaji, Usomi, Umaskini au
kitu chochote cha nje ni sawa na kabrasha ambalo linatumika kuibeba zawadi yenyewe.

Inaweza kuwa zawadi ni makaratasi na matambala tu yamewekwa humo na utakapokuja kugundua unakuwa umeshachelewa kabisa na matokeo yake kujuta.
Umeuziwa mbuzi kwenye gunia shauri yako!
wakati unao fikiria kwa makini

Kawaida kama unatafuta uhusiano wa kudumu ni vizuri uka-invest muda mwingi kuhakikisha unamfahamu mtu vizuri, moyo wake
(marry the soul not the skin).

Maisha tunapoishi hupelekea mabadiliko ya sifa za nje, watu hufirisika, watu hunyonyoka nywele, watu huzeeka, watu hupata stress, watu huwa vilema, watu hunenepeana, watu huugua, watu hubadilika, watu hukonda hata wakawa tofauti na walivyo labda wakati wa kuanza urafiki wenu muwe mmekubaliana kwamba yakitokea mabadiliko tu kila mtu aanze mbele au achukue chake, ndo maana leo ndoa ni kama watu wanaoenda shopping.

Kama upo kwenye process za kuanza mahusino naomba jiulize hivyo ni kweli unavyomuona huyo unayemwita mpenzi wako alivyo nje ni sawa alivyo ndani?
Pia uwe makini usije ukaanza kujua baadae,
Jieulize, kama anaku-control wakati hamjaoana, je, akikuoa au mkioana ndo ataacha au kubadilika?
Kama sasa hivi hamjaoana hataki kazi; Je, unauhakika mkioana atafanya kazi?
Je, kama leo hamjaoana ni mlevi, anavuta sigara, mvuvi na mzembe, je mkioana ataacha?
Je una imani kubwa ya kuhakikisha kama leo hana mguu, mkioana atakuwa na mguu?
Uwe makini Na angalia ndani siyo nje.

Maana unaweza baadae kujitetea, unajua nilikuwa mdogo, so sikuwa makini.
Sikiliza tunakushauri mapema
Be very careful.


No comments: