"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, May 13, 2008

VYAKULA VINAVYOONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOA

Vyakula tunavyokula vinachangia sana chemistry ya miili yetu kuhusiana na suala la hamu ya mapenzi (libido) PILIPILI
Kama tunavyojua wote mara nyingi chakula ambacho kimeungwa pilipili hufanya hata mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati mwingine hata jasho kutoka au kamasi kutoka.
Kwenye pilipili kuna kitu kinaitwa capsaicin ambacho hufanya pilipili iwe na hali ya ukali ambao huwezesha ubongo kutoa homoni ya endorphins ambayo katika hali ya juu huleta mgusu wa hisia za raha.
Pia pilipili husisimua mfumo wa ufahamu (nerves) wa ubongo na katika kufanya hivyo huwezesha kumshwa haraka kimapenzi (kunyegeka) na pia ili ukiguswa au kubusiwa au kunyonywa au kupapaswa uweze kupata hisia kila sehemu

MATUNDA NA MBOGA ZA MAJANI.
Mlo wenye matunda na mboga za majani una matokeo makubwa sana katika hamu ya tendo la ndoa kwa njia nyingi.
Kwanza matunda na mboga za majani hupunguza kiwango cha mafuta na unene (cholesterol), kuongezeka kwa mafuta mwilini huzuia mzunguko wa damu kwa kubana mishipa ya damu.
Pia kula matunda na mboga za majani huhakikisha balance ya uzito kwani unene (obesity) kwa wanaume kuna matokeo mabaya katika kuzalisha homeni za testoeterone na hatimaye jogoo kushindwa kuwika na kuwa na libido kidogo.
Na pia wanandoa wanapozidi kunenepeana ndipo na hali ya kufurahia au kutaka au hamu ya tendo la ndoa huzidi kupungua.

NAFAKA
Nafaka zina nyuzinyuzi (fibre) na sukari ngumu (complex sugar) ambazo kusaidia kutunza uzito wa mwili.
Nafaka husaidia katika kuzalisha homoni za testosterone kwenye damu.
Na pia nafaka huwezesha mtu kuwa na nguvu hatimaye kwenda masafa marefu wakati wa tendo.
Kula nafaka nzima kama vile brown bread badala ya white bread, pia kula nafaka halisi badala ya cornflakes ni jambo zuri linalokuhakikisha afya nejama na mahusiano mazuri ya ndoa yako
TANGAWIZI
Tangawizi ni chakula ambacho husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini, na tangawizi zinajulikana sana kwa kusukuma damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi yaani uke na uume.
Inaweza kuliwa mbichi, au kupikwa au kuanikwa na kuwa kama unga.ASALI
Asali ina madini yanayoitwa boron, ambayo husaidia mwili kutumia homoni ya estrogen ambayo ni homoni inayohusika na viungo ya uzazi na mapenzi kwa mwanamke.
Pia kuna utafiti unaoonesha kwamba asali huongeza nguvu, kitendo ambacho kitapelekea mwanamke kuwa uwezo na hamu ya tendo la ndoa au libido.
KARANGA
Karanga huhusika moja kwa moja na kutunza mfumo wa mzunguko wa damu kuwa na afya (vascular system).
Pia mfumo wenye afya (mzunguko wa damu) katika uke na uume huwezesha mwanaume na mwanamke kupata msisimko wa mapenzi haraka hatimaye tendo la ndoa kuwa zuri.
Pia karanga zina madini muhimu kama vile magnesium, asidi ya folic na zinc ambayo ni muhimu sana katika usalishaji wa mbegu za mwanaume.OYSTERS
Huwa na kiasi kikubwa sana cha madini ya zinc na haya madini ndiyo huhusika zaidi na uzalishaji wa homoni ya testosterone kwa wanaume.
Pia imethibitika kwamba wanaume wenye ukosefu wa madini ya zinc huwa na matatizo ya nguvu za kiume na wakati huohuo kuwa na madini mengi ya zinc mwilini huongeza kiwango cha shahawa.SOYA
Pamoja na kuwa na kiwango kidogo sana cha fat na pia kuwa na kiwango kizuri cha protein, soya zina phytoestrogens ambayo husaidia sana wanawake ambao wamefikia menopause kutengeneza homoni estrogen ya ziada.
Husaidia uke kuwa laini (wet, lubricated) mwanamke akisisimliwa wakati wa tendo la ndoa.CHOCOLATE
Chocolate ina phenylethylamine, kemikali ambayo husababisha hisia (feelings) za furaha wakati wa mwanamke au mwanaume kufika kileleni (orgasm)


16 comments:

Subi said...

Basi kwa wenye kujali afya ya tendo la ndoa, imeshafahamika wakati wa kwenda sokoni vyakula gani vinunuliwe na mtoto asivichezee vikiwamo kwenye jokofu, 'ni chakula ya baba'. Asante kwa darasa!

Lazarus said...

Wajina,

vipi je kuhusu vinywaji (siyo ulevi) nasikia kuna vinywaji mtu ukipata basi unajisikia kunyegeka na kuwa sexy, najaribu kuuliza wazoefu wanasemaje hasa huko Tanzania.

Subi said...

Natoka kapa hapo, binafsi sifahamu vinywaji vinavyosaidia kuamsha ashki.

Lazarus Mbilinyi said...

Wajina,
Basi itabidi nikuandalie somo kabisa, nafahamu baadhi kwa kuwa vinywaji vinatofautiana kati ya nchi na nchi najaribu kufanya utafiti kujua ni vinywaji gani huku Afrika na huko Ulaya, au Amerika hata Australia na Asia. Kuna vinywaji visivyo na kileo na ukipata tu basi unajisikia kunyegeka kwelikweli, shoka moja mbuyu......

Anonymous said...

Jamani kama kweli mbona mimi mwenzenu wala huwaga sifiki mshindo kwa ile mashine kuwa ndani labda wakati wa roma ya nguvu alafu nikifika sijisikii tena kuendelea. hii imekaaje

Lazarus Mbilinyi said...

Samahani hujaeleza wewe ni mwanaume au ni mwanamke ili tuweze kupata sehemu ya kuanzia.

Haiwezekani usipate mshindo ndiyo maana romance ni kitu cha msingi ilikuwa na tendo la ndoa linaloridhisha.


Upendo daima

Anonymous said...

tatizo watu wanataka nguvu za kiume ili wafanye mapenzi kila siku au wafanye mapenzi na wanawake wengi kwa siku moja. lakini mkijiwekea ratiba mbona miguvu kibao.

Anonymous said...

Natafuta mchumba ...mimi ni boy wa miaka 26...mawasiliano 0764839091...sms zote zitajibiwa ..its serious

Anonymous said...

Nataka mwanamke wa ukweli wa kudumuu nae mm Niko Arusha nipigie 0684114147

MartinMologa.com said...

Kuna vitu mtu anazaliwa navyo,kama nguv za kiume hizi hazpo kwa mangi wala kwa masai

Anonymous said...

Hili darasa zuri muuendelee kutupa vitu.

Anonymous said...

wadau hlo xomo limeniguxa mimi kwa sababu nina tatizo la kupiga bao 4 na kuendelea..mie nataka bao 7 kwa siku

TIBA NA USHAURI said...

Kwa ushauri na njia za kupunguza na hatimaye kuacha kabisa kuangalia picha za porngraphy na kupiga punyeto au masterbation kwa vijana wenzangu na pia namna ya kurudisha nguvu za uume zilizopungua kwa tiba ya vyakula, please tuwasiline #usharinasaha18@gmail.com

TIBA NA USHAURI said...

Kwa ushauri na njia za kupunguza na hatimaye kuacha kabisa kuangalia picha za porngraphy na kupiga punyeto au masterbation kwa vijana wenzangu na pia namna ya kurudisha nguvu za uume zilizopungua kwa tiba ya vyakula, please tuwasiline #usharinasaha18@gmail.com

TIBA NA USHAURI said...

Kwa ushauri na njia za kupunguza na hatimaye kuacha kabisa kuangalia picha za porngraphy na kupiga punyeto au masterbation kwa vijana wenzangu na pia namna ya kurudisha nguvu za uume zilizopungua kwa tiba ya vyakula, please tuwasiline #usharinasaha18@gmail.com

FESTO SHINE said...

Asante sana kwa ushauri mzuri .chakula ya baba isipungue ndani jamani akina mama mmeelewa hapo. Msidharau hili jamani liheshimike