"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, May 8, 2008

Watoto kama hawa wanategemea mipango thabiti ya kuanzia familia, jamii na viongozi wa taifa ili wapate huduma bora kama elimu na stadi za maisha.Watoto wa kijiji cha Wangama - Njombe
"Hatuendi mijini tutabanana hapahapa kijijini kwa kuanzisha mashamba ya misitu na baada ya miaka 20 msitushangae"
Nilimkuta huyu Bwana mdogo akipiga jemba bila masihala; utakumbuka homework kweli hapo!

Mara nyingi mawifi huwa hawaivi ila hawa nilikuta ni kitu kimoja

Ukipita Ilula kuelekea kitonga basi kutana na Mzee Bonge anakuuzia nyanya kwa bei poa kabisa.

Mambo ya mji kasoro bahari karibu, unaweza kujua ni hoteli gani hiyo?

Baada ya miaka 50 ijayo eneo la Manzese litakuwa limefunikwa na maghorofa kama Kariakoo, ingawa kwa sasa ghorofa zinahesabika

Manispaa ya Iringa ni moja ya miji misafi hapa Tanzania

Zamani ukiwa kijijini siku ya harusi jiandae kutembea kwa mguu na bibi harusi wako hadi uchoke; siku hizi poa sana hata chai maharage maharusi wanatumia.

Hapo tunapasua mbao then tunaziuza Dubai! je zinakidhi viwango ya soko la kimataifa?

Hapa ndipo safari yangu ya kutafuta elimu ilianzia.

Vijana wengi wa vijijini njia kuu ya usafiri ni baiskeli. Hapa ni Ramadhani Njombe

No comments: