"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, May 10, 2008

Weekend Njema

Nawatakia weekend Njema.
Kabla hujaumbwa Mungu alikujua na bado ana mpango na maisha yako; haijalishi kwa sasa maisha yako yapoje.
Mungu alikuwa anajua wazazi watakaokuzaa,
Mungu alikuwa anajua sehemu utakayozaliwa kijiji, wilaya au mkoa,
Mungu alikuwa anajua Mume atakaye kuoa au mke utakayeoa,
Mungu anajua hata shidaulizonazo, matatizo unayokumbana nayo, upweke ulionao na
Kila aina ya maisha unayopitia.
Usikate tamaa, au kuzimia moyo na kuhisi kama vile Mungu amekuacha au kama vile ni wewe tu unayepitia kwenye shida na majaribu au matatizo kama uliyonayo.
Kitu cha msingi ni kwamba Mungu ana mpango na maisha yako!
(Yeremia 1:5)No comments: