"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, June 29, 2008

Akili - Mazingira

Enzi zetu wakati wadogo midoli tulikuwa tunatengeneza wenyewe, kama magari, ng,ombe, mbuzi nk na tulikuwa tunatumia material yale yalikuwa yanapatikana katika mazingira yetu kama vile udongo, mabati, mabua n.k na hata kuiba ndala na kukatakata kuwa matairi.
Kasheshe ilikuwa pale tunapopoteza visu ambavyo wazazi walikuwa wanatumia jikoni, hata hivyo naamini tulikuwa wabunifu.
Watoto wa siku hizi wao ni kuchezea tu midoli hata hawajui imetengenezwa vipi, hata hivyo mazingira ni kitu muhimu sana katika kukua kwa akili ya mtoto.
Posted by Picasa

2 comments:

ruhuwiko said...

Nakuunga mkono enzi zetu ni kweli tulikuwa tunajitengenezea wadoli na magari wenywe. nakumbuka nilipokuwa mdogo nilikuwa nageuza kigunzi cha muhindi mdoli.Najua tunatumia peasa nyingi sana kununua vifaa vya kuchea kwa watoto, tembele katika blog yangu angalia hilo gari kijana wangu alitengenezewa na wajomba zake mwaka jana alifurahi sana.

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Yasinta,

Nimeona bonge la Scania (Made in Sweden)nimeliona kiboko kweli.

Enzi zetu hapo hilo gari halilali nitazunguka nalo nyumba nzima huku naendesha na mimi mwenyewe ndo injini kuunguruma.

Hata hivyo zikuhizi kuna makampuni yame specialize kutengeneza midoli ya watoto na midoli unakuwa na program zinazawawezesha kupata skilss za vile vipo katika ulimwengu na vinawapa akili zaidi. Ingawa tofauti ipo sisi tulikuwa innovative zaidi.
Mimi nakumbuka nilitengeneza na barabara yangu ya lami kwa ajili ya gari langu kupita.

Asante sana jirani tuzidi kuwasiliana na nashukuru sana kwa kunitembelea leo kwenye hiki kilima cha utajiri kwenye eneo la mahusiano, ndoa, mapenzi na familia.

Ubarikiwe na Bwana

Lazarus Mbilinyi
Ontario - Canada