"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, June 19, 2008

Je, Chini Kunapwaya? (2)

Wapo wanawake akishazaa watoto wawili au watatu uke wake hulegea na kupelekea kutofurahia tendo la ndoa.
Hasa kama hakuwa mtu wa mazoezi tatizo linaweza kuwa kubwa, hata hivyo kufanya mazoezi ya Kegel ndiyo jibu kamili ya kurudisha uke kwenye mstari na kuanza kufurahia tendo la ndoa.
Mara nyingi wanawake huwacheka sana wanaume ambao visamaki vyao ni vidogo sana kwa kuwatania kwamba hata ukikohoa tu wakati wapo sita kwa sita kanachomoka, wakati huohuo wanaume nao huwacheka wanawake ambao huko chini kwenye machimbo ya dhahabu kuna pwaya mno kiasi kwamba mwanaume akiingiza mpini hasikii kitu chochote yaani hakuna ule mgusano au msuguano unaoleta raha ya tendo la ndoa.
Wengine wanaita ana uke kopo la kimbo.
Pia kuna wanawake uke umejaa maji kwelikweli hata uume ukiwa ndani ni kuteleza tu bila msuguano wowote wala kubana kokote matokeo yake hakuna ladha na utamu wa tendo lenyewe.

Dawa ipo tena bure na ipo ndani ya uwezo wako, kitu cha msingi ni kukubali mabadiliko na kuwa na hamu ya kutaka kubadilika.
Kuwe na uke tight unaokupa raha wewe na mume wako na zaidi afya yako ya uzazi kuwa imara.
Hata kwa wanaume zoezi hili ni simple wala halina gharama.

Ni kawaida wanaume wengi kuogopa kwenda kwa daktari kuongea masuala ya afya ya uzazi, hapa huhitaji kwenda kwa daktari, ni wewe mwenyewe kuwa serious kwani ukifanya vizuri utakuwa na uwezo wa kusimamisha mti wako kwa muda mrefu na pia unaweza kuhimili kubana kutofika kileleni mapema kabla ya mwandani wako.

Wanawake wengi baada ya kuzaa zaidi ya mara moja na kama hawakuwa watu wa mazoezi misuli ya uke hulegea na kupelekea kupoteza mnato na u-tight wa uke na pia kutojiamini wakati wa kufanya mapenzi kutokana na kupwaya kwa uke.
Kitaalamu hili zoezi huweza kurudisha hiyo hali ya kuwa tight baada ya miezi miwili kwa kufanya kila siku mfululizo na kwa kujitoa na kuwa serious.

Je, hili zoezi ni gumu?
Si gumu
Ni rahisi sana
Ni salama
Siyo zito na halichoshi
Linaweza kukupa matokeo baada ya wiki nane

Je, unaanzaje au nitajuaje huu ndo msuli wenyewe?
Kwanza ili kufanya hili zoezi anza kwa kutambua misuli ya uke au uume inayohusika kwa kuzuia mkojo unapotoka, then kojoa kwa kukata huku ukikaza misuli kwa kutoa mkojo kwa kuhesabu sekunde 4 hadi 10 au namba 1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9, 10 the unakojoa tena ujazo wa kijiko cha chai then unaanza upya kwa kukata na kuhesabu 1 – 10 kila unapoenda kukojoa muda wowote.

Hii inasaidia kutambua msuli unaohusika na kukaza uke au uume.
Msuli uliotumia kuzuia mkojo ni rahisi kuuhisi ndo huo unahusika.
Hii misuli husaidia kukaza matundu matatu huko chini kwa mwanamke ambayo ni uke, tundu la mkojo na tundu la kutolea haja kubwa.
Ndiyo maana watu wanaofanya upuuzi ule wa sodoma na gomora kuna wakati huhitaji kuvalishwa nepi maana misuli imelegea hauwezi kuzuia tena haja kubwa.

Ukishapatia kujua msuli upi unamtumia kuzuia mkojo, basi unaweza kuendelea na zoezi hata kama hukojoi au kutoa haja kubwa kwa kuendelea kukaza kama vile unakojoa au unatoa haja kubwa ingawa siyo.
Unaweza kurudia zoezi muda wowote hata kama hukojoi mahali popote, kwenye kiti ofisini, kwenye daladala nk.
Wakati unafanya Hakikisha kuna tofauti ya sekunde tatu hadi kumi.
Pia unaweza kuongeza kukaza hiyo misuli kila ukikojoa fanya zaidi ya 20 kwa siku
Fanya kwa wiki nane mfululizo.
Kumbuka!
Kama wewe ni mwanamke ambaye chini kunapwaya au mume wake amekuwa analalamika kwamba hapati ladha na utamu halisi basi hili zoezi la kubana misuli litakuwezesha kubana uume au kuuvuta kwa ndani, au kwa kuukamua hatimaye anapata raha kwa msuguano unaokuwepo na wewe kufika kileleni haraka.
Ukitaka kujua uke wako unakubali zoezi jaribu kuingiza kidole wakati unafanya hili zoezi then utahisi kidole kubana zaidi kuliko kawaida.


No comments: