"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, June 24, 2008

Je, Nitajuaje ni yeye?

Kumekuwa na maswali mengi sana naulizwa na vijana wengi wa kike na wakiume ambao wanataka kujua ni yupi anaweza kuwa mchumba halisi ambaye atakuwa mke au mume wangu.
Ukizingatia kwamba ukioa au kuolewa tu ni uamuzi ambao unaweza kupelekea kuwa mtu wa furaha katika maisha yako au mtu huzuni na kujuta siku zote katika maisha yako.
Kutokana na uzoefu wangu wa kawaida (mimo siyo expert wa mambo ya ndoa au mahusiano) kujua huyu ndiye; kwangu ulikuwa uamuzi rahisi mno kuliko maamuzi mengi ambayo hunipa shida kuchagua.

MAHUSIANO HUWA RAHISI TANGU SIKU YA KWANZA
Tangu siku ya kwanza nilipojikuta naonana uso kwa uso upendo uliokuwa kati yangu na yeye ulikuwa natural, nilijihisi nimemuona mwanamke ambaye namfurahia kila kitu, namkubali kama alivyo, nilihisi kama tulizaliwa tuishi pamoja na sasa nimempata mtu ambaye nimekuwa namtafuta, nilijiona ananitosheleza kimwili na kiroho ninapoongea naye na mvuto ninaoupata.
Kila kitu katika mahusiano na urafiki wetu kilikuwa natural na hisia mpya kabisa hapa duniani.
Wapo ambao katika safari ya uchumba hadi ndoa huzipiga na kugombana mara nyingi sana, leo wanazipiga au kununiana au hugombana na kesho wanapatana tena na kurudiana.
Wanaendelea na kasheshe hizo hizo mara kwa mara hadi wanaoana.
Isiji kuwa unarudiana naye hata kama kuna ugumu katika mahusiano yaliyapo labda kwa kuogopa ukiachana naye hutapata mtu mwingine wa kuoana naye, ni busara kuachana wakati wa uchumba kuliko kuachana ikiwa ndoa.

UHUSIANO MZURI NA FAMILIA, NDUGU NA MARAFIKI
Inaweza kuwa tofauti kidogo hasa linapokuja suala la dini, kabila, nk kwani mara nyingi wazazi na familia nyingi huwa na lao kuhusu kabila au dini. Ikitokea kwamba mchumba wako ni kabila moja, dini moja na bado ndugu zako, familia yako au marafiki zako hawaelewani naye ni vizuri kufikiria upya.
Wewe umelelewa na familia na kutokana na hayo malezi ndivyo ulivyo na umempata huyo mchumba kutokana na tabia yako uliyokulia au kulelewa na hiyo familia na kama bado hakubaliki maana yake hapo kuna bendera nyekundu inawaka na inaashiria kuna kitu hakipo sawasawa.
Kawaida ukishaingia kwenye mapenzi (fall in love) huweza kupunguza uwezo wako wa kuamua na kuona kasoro ndiyo maana wanasema love is blind.
Hii haina maana kwamba unatakiwa kuvunja mahusiano eti kwa sababu ndugu, familia au marafiki hawakubaliani na huyo mchumba wako ila ni kawaida kwamba inawezekana kuna kitu ndugu zako na familia yako wanakiona na wewe hukioni ambacho mbele ya safari unaweza kukilipia gharama kubwa na utaenda kwa nani kuomba ushauri, maana umekuwa kichwa ngumu.
Jaribu kuchunguza kile ambacho ndugu zako au familia au marafiki wanasema vibaya kuhusu huyo mtu wako inawezekana ni kweli.
Ni kawaida kama umepata mtu wa kufanana na wewe basi huweza kujichanganya kirahisi sana na ndugu zako, familia yako na marafiki zako.

HUTAONA KITU KIKUBWA CHA KUMBADILISHA
Kawaida, hata kama mnapendana kuliko binadamu yeyote chini ya jua, bado tofauti zitakuwepo hata migogoro itajitokeza pia, kama kuna jambo kubwa sana unaona ni muhimu sana yeye abadilike basi hiyo ni ishara kwamba fikiria kwa makini.
Tatizo ukishashambuliwa na chemical za love unaweza kujikuta unadhania kwamba haina shida kwa tatizo au kasoro alizonazo na utavumilia.
Ukiingia kwenye ndoa chemistry ya mapenzi hushuka na kupanda kutokana na jinsi mnavyojitahidi kuimarisha ndoa yenu; hapo ndipo sasa utagundua kwamba ulichemka and too late.
Usiingie kwenye ndoa ukidhania utambadilisha mtu sana sana wewe ndo utabadilishwa na ndoa na kuwa kitu kingine.
Kama umegundua kuna kitu ambacho ni tatizo kubwa sana mbele ya safari na hutaweza kuishi nacho ni vizuri ku move out kuliko kupoteza muda wako na kujifariji na baada ya miaka 3 ya ndoa ujikute upo kwenye jehanamu yako mwenyewe.
Watu hupata upweke lakini upweke wa kwenye ndoa ni mbaya kuliko upweke mwinghine wowote.

NI RAFIKI
Mvuto wake ni kitu muhimu sana katika mahusiano.
Ndani ya mahusiano lazima kuwa na mzizi mkuu wa urafiki ambao hata mkiwa wawili sehemu yoyote duniani bado mnajiona hajapungukiwa na pia bado mnajiona ndiyo marafiki bora duaniani.
Je, unajiona unahitaji kutumia muda na yeye tu, je unajisikia raha kuwa na yeye wawili tu.
Je, unahisi yeye ndiye anastahili wewe kumwambia siri zako na kwamba ni yeye tu anakufahamu kuliko mtu yeyote duniani, kama ni NDIYO, basi mshike vizuri.
Kuwa best friends hata baada ya kuoana ni raha sana, na ndoa hudumu, maana hakuna anaye bore mwenzako.

UNAPOFIKIRIA KUOANA NAYE HAIKUPI SHIDA
Kama unajikuta unapofikira kuoana naye huna wazo lingine la kuhisi ndoa inaweza kuwa na matatizo na unajisikia amani ya kweli moyoni na kwamba future yako na yeye itakuwa sawa basi umepatia.

“Marriage is not about finding a person you can live with, it’s about finding the person you can’t live without.”

No comments: