"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, June 14, 2008

Ktk Ndoa msikasirike wote

Hawa ni Bwana John na mke wake Betty Deep River Canada waliponikaribisha nyumbani kwao walinifundisha mambo mengi kuhusu ndoa.Ni jambo lisilopingika kwamba ndoa zina raha yake na utamu wake hasa kila mmoja akimtanguliza mwenzake na kufuata misingi sahihi ya kuimarisha upendo, furaha na amani katika ndoa.

Ni mafanikio ya ajabu sana kwa jamii za leo kuona watu wanasherehekea kufikisha miaka 5, 10, 15, 20, 45 na hata zaidi 50.


Unapoongea na watu ambao ndoa zao zimeweza kuvuka milima na mabonde hadi miaka 35 ni lazima usikiliza kwa makini kwani kuna maneno ya hekima na busara.


Wao wanasema siri kubwa ya ndoa yao kudumu kwa muda mrefu ni kama ifuatavyo:

Msikasirike wote kwa wakati mmoja.

Kama unataka kulaumu basi fanya kwa upendo wa hali ya juu sana.

Usikumbushie makosa ya nyuma.

Ni vizuri wakati mwingine kuachana na ulimwengu wote lakini si kuachana ninyi wawili.

Usiende kulala huku mmoja akiwa na donge moyoni.

Hakikisha umempa mwenzako sifa kwa kazi moja aliyofanya angalau kwa siku mara moja.

Kama umefanya makosa, kubali na omba msamaha.

Ili kugombana wanahitajika watu wawili tu, hivyo chunga sana.

Wakati umekosea kubali na wakati upo sahihi kaa kimya.

No comments: