"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, June 3, 2008

Kupelekeshwa

Mwanamke akiwa controlled hawezi kujiamini; kutojiamini kunamfanya kila anachofanya asiwe na uhakika,
Na kutokufanya vitu kwa uhakika matokeo yake ni kuishi maisha ya upweke Wengi wanaamini kwamba kuolewa au kuoa ni kuondoa upweke, ukweli ni kwamba unaweza kuolewa au kuoa na ukaishi ndani ya upweke uliokithiri.
Wapo wanandoa wengi wanaishi katika upweke mbaya zaidi kuliko wale ambao hawajaoa wala kuolewa.
Tabia ya kupelekeshwa (controlled) imekuwa ni tabia ambayo wanaume wengi (si wote) katika jamii za kiafrika umedumu kwa muda mrefu na bado ipo.
Tabia ya kupelekesha hujionesha kupitia hisia za manano, matendo na ishara na watu wenye tabia ya kupelekesha.
Wapo ambao huanza tabia ya kupelekesha tangu kuanza kwa mahusiano na kwa kuwa wengi hudhani tabia kama hizo zitakuja kubadilika huchukulia ni suala dogo sana.
Huanza kwa kukupelekesha na vitu anavyokupa kama zawadi, muda wako, wakati mwingine hata kama hujafanya kosa anakwambia wewe kwamba ndiye muhusika na umesababisha.

Mwanandoa anayepelekesha mwenzake kawaida haridhiki na kazi na mambo anayofanya mwenzake na huonekana kama vile mwenzake hajafikia viwango vinavyotakiwa kuishi pamoja. Mwenzake haruhusiwi kununua kitu, haruhusiwi kuleta rafiki, haruhusiwi kutumia pesa hata kidogo bila yeye kujua, haruhusiwi kuwa na marafiki, haruhusiwi kufanya chochote bila ruhusa.
Na wengi ya watu wanaopelekesha wenzao huwa na masauti makubwa, ukimbishia anatoa sauti kubwa hadi unanyamaza mwenyewe.

Bahati mbaya ni kwamba wengi ya wanao wapelekesha wenzao huwa hawajui kama wanachofanya ni kuwapelekesha bali ni kuwapenda na kuwalinda.
Wapo wanawake au wanaume ambao wapo katika mahusiano na wanajitahidi sana kuhakikisha kila kitu kinaenda vizuri, hata hivyo kwa kuwa waume zao au wake zao ni watu ambao ni controlling, juhudi zao za kuimarisha ndoa na maisha kwa ujumla huishia katika kujuta na kujiona wapweke.
Ni muhimu kujadili na mume wako au mke wako kama mmoja anahisi anapelekeshwa.
Na kama ni ndiyo basi fanya mabadiliko badilika.
Wapo wanandoa akisikia mwenzake anasafiri au hatakuwepo basi anajiona raha sana, sababu kubwa ni kwa kuwa anayeondoka ni controling, anampelekesha, anamnyima uhuru, demanding, msumbufu, dikiteta.
Je, ukisikia mke wako au mume wako anasafiri utajisikiaje, huru au mpweke?
Jibu unalo na jibu linaonesha unapelekeshwa au la.


No comments: