"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, June 11, 2008

Kutoka Nje

Aliyekuwa Gavana wa Jimbo la New York Elliot Spitzer akiwa na mke wake Silda, akiongea mbele ya waandishi wa habari baada ya kukumbwa na scandal ya kutoka nje ya ndoa kwa kupata huduma ya Malaya March 12, 2008.
Je, huyo mwanamke alijisikiaje?
Je unahisi Mumeo ana cheat?
Wanawake wengi (siyo wote) wana hisi kwamba waume zao wanamahusiano ya mapenzi na wanawake wa nje ya ndoa zao lakini wanashindwa kufahamu namana gani au ni dalili zipi zinaweza kupelekea kupata ukweli na kuujua na hatimaye kumkamata au kuwabamba.

Wapo wanaume ambao hutumia ujanja wa hali ya juu sana ili asiweze kugundulika kwamba anafanya cheating (tutaangalia baadae), hata hivyo zipo dalili za kawaida ambazo wanaume wengi ambao wana cheat unaweza kuwajua.
Kitu cha msingi si kwamba ukiona dalili moja basi unafikia uamuzi kwamba ana cheat, unaweza kuharibu mambo au kuishia kudundwa bure.
Hizi ni dalili za kukusaidia wewe kuweza kuchukua hatua zaidi kuchunguza hasa kutokana na wewe mwenye kuhisi kitu kisicho cha kawaida.
Nakumbuka kuna mama mmoja aliniomba ushauri kutokana na yaliyompata ya mume wake kumpa mimba haouse girl wao ambaye yeye mwanamke ni shangazi, hata hivyo baada ya kumuuliza niligundua kwamba kulikuwa na dalili nyingi sana ambazo zilikuwepo ila yeye mwanamke hakujali wala hakuchukua hatua zozote na alipoanza kuchukua hatua binti (house girl) tayari alikuwa ana mimba miezi 6.
Mumeo amempa mimba house girl ambaye ni ndugu yako na umemchukua kijijini kwenu, wametiana mimba ndani ya nyumba yako mwenyewe, kwenye kitanda chako mwenyewe bila wewe kujua hadi mimba ina miezi 6 na mnaishi pamoja.
Zifuatazo ni dalili zinazoweza kupelekea kupata data kugundua kwamba hapa mwanaume ana cheat au anaanza ku-cheat.

MABADILIKO YA GHAFLA YA MWONEKANO WAKE
Mwanaume ambaye ana cheat au anayeanza cheating atajitahidi kuonekana smart na attractive, anaanza kuwa na aina mpya ya mwonekano wake hasa kutokana na yule nayetaka kuwa naye, kumpendezesha hawala yake, anaweza kuwa alikuwa si tabia yake kunyoa ndefu na sasa ghafla kila siku kipara kwenye kidevu bila maelezo,
Pia angalia tofauti na mazoea yake je, anapofika nyumbani anakimbilia kuoga au hataki usimguse akiogopa utamnusa na kupata harufu ya manukato ya hawala yake?
Ukihisi chunguza!

JINSI ANAVYOSHIRIKIANA NA WEWE
Jinsi mwanaume anavyo ku-treat unaweza kujua kuna kitu zaidi ya jinsi anavyo react.
Yeye kujihusisha na mwanamke mwingine lazima kutaleta mabadiliko na jinsi anavyoku-treat wewe.
Anaweza kuwa anakuchukia bila sababu au anaweza kuwa mpole kuliko kawaida hadi ukashangaa nini kimemtokea. Hata kama alikuwa hakupi zawadi unaweza kuona unapewa zawadi bila kutegemea.
Kumbuka sababu moja haitoshelezi kujua kwamba anafanya cheating, lazima uchunguze na upate ukweli.

MAONGEZI
Ikiwa kuna mambo anakataa kuyaongelea au anachagua au anakuwa na majibu mafupi kuliko zamani basi inabidi uwe makini, hasa story zinazohusu watu kuwa na nyumba ndogo, watu kutoka nje ya ndoa, watu kufumaniwa nk.
Pia ukiona anataja majina ya watu ambao huwafahamu vizuri hasa wanawake, anataja sehemu ambazo ni ngeni na si kawaida yake kuongelea unatakiwa kuwa makini inawezekana ni dalili kwamba ameanza kuvutwa shati.
Kumbuka si kweli kwamba kila mwanamke ambaye anamtaja basi unachukulia ni hawala yake.
Chunguza!

KAZINI
Mara nyingi wanaume wengi hujitetea kwamba walikuwa kazini au wanaenda kazini hata siku za weekend ili kupata muda wa kutoka nyumbani, siku nyingine mwambie tunaenda wote, ukiona anatapatapa ujue hiyo safari si ya kazini bali ya Sinza Madukani.
Pia wanaume wasiowaaminifu hutumia cover ya kazini kwa cheating zao na kama huwa anafanya kazi za shift wewe ndo unatakiwa kuwa makini zaidi kwani kuna shift za usiku na kama akipatia kwamba ameenda kazini usiku kumbe kaenda kwa hawala basi huko ni sherehe.
Kitu cha msingi chunguza mabadiliko ya ghafla ya ratiba yake ya kazini na kuwa tofauti na kawaida yake, pia ni vizuri kujua bosi wake au rafiki zake wa kazini ili kama amekwambia ameenda kazini unaweza kuongea na bosi wake kuhakikisha ila uwe na hekima na busara. Unaweza kukuta kazini hayupo wiki!

RATIBA
Binadamu ni mtu wa tabia, kila mtu ana ratiba ambayo baada ya muda huwa kama tabia yake. Chunguza mabadiliko ya tabia yake na ratiba zake kama zimebadilika ghafla.
Kama amebadilisha ratiba zake ghafla chunguza nini kimesababisha, kama alikuwa hana mazoea ya kusafiri kikazi na sasa kila siku anasafiri, chunguza.
Inaweza kuwa kweli anaenda kufanya kazi lakini wakati mwingine mmm anasafiri naye. Pia kama alikuwa hana time na nyumbani sasa mmemleta house girl na anapenda kubaki nyumbani wewe ukiondoka.
Chunguza! anaweza kuwa ameanza kukafuatilia hako katoto maana watoto wa siku hizi nao kazi kwelikweli!

MATUMIZI YA PESA
Kuwa na Affairs ni gharama.
Kama ana hawala lazima atatakiwa kumburudisha kwa vyakula, vinywaji, mapochopocho, kitimoto, chips kuku , hela za saloon, usafiri tena anataka tax, zawadi na kama amepata limbukeni basi kifedha ataumia hata kama ni makini namna gani lazima kutatokea matatizo ya kifedha katika familia kwani matumizi yataongezeka.
Na wanaume kwa kujidai wao ni Bill gates lazima uchumi utayumba tu.
Hivyo uwe makini na ku-track mabadiliko ya fedha au bajeti hasa ukiona pesa hakuna na pia hakuna mnachofanya.
Chunguza!

KUSAFIRI
Wanaume wengi wasiowaaminifu huambatanisha safari zao za kikazi na mambo ya cheating, wengine husafiri kikazi na mahawala hadi nje za nchi na unaambiwa mwanamke si lazima kwenda airport au hataki kuzindikizwa.
Chunguza kwa nini?
Unahitaji kuwa makini na hizo safari zake wakati mwingine anaweza kwambia ameenda kwenye semina Morogoro kumbe yupo Kimara, Au ameenda Arusha kumbe yupo Bagamoyo.
Ni vizuri mwanamke kujua kazini kwa mumeo pamoja na wafanyakazi wenzake ili akisema amesafiri basi waweza kuwasiliana na wenzake ili ujue kweli amesafiri au ndo amesafiri kwenda kwa hawala.
Tumia hekima na busara usikurupuke!

KUTOKUPATIKANA
Kwa mwanaume kuwa na wanawake wawili na kuwaridhisha na kila mmoja akaridhika anahitaji muda mwingi, kwa kuwa tuna masaa 24 tu kwa siku kama ana mtu lazima kupatikana kwake kutapungua maana anatakiwa kwenda kazini, kwenda kwa hawala na pia familia, hapo lazima hata kama atakuwa mjanja kutakuwa na mabadiliko ya yeye kupatikana nyumbani kama kawaida yake.
Ukiona ameanza kurudi nyumbani zaidi ya saa nne usiku bila sababu ya msingi anza kuchunguza hata kama anasema alikuwa na rafiki zake kwa ajili ya mambo ya business, familia ni zaidi ya business, hivyo mwanaume anayejali huwa ana balance muda wa familia na business.

SIMU
Hapa patamu kweli, wengine wamewekeana mipaka kwenye ndoa kila mmoja hakuna kugusa simu ya mwenzake, kwa nini? kuna siri gani?
Cheating nyingi zinahitaji mawasiliano na mawasiliano mengi ni kwa njia ya simu tena za mobile. Wapo wanaume hujiamini sana hadi kuruhusu kupigiwa simu hata nyumbani, hivyo uwe makini na simu za wanawake anazopigiwa na pia mwangalie usoni na jinsi anavyo react anapopigiwa simu za aina hiyo au kama akipigiwa simu anaenda mbali kuongelea wakati mpo wawili tu wewe na yeye.
Au hata kabla ya kuongea anakata na kusema atampigia.
Pia wapo wanawake (mahawala) wao ni- beep tu ili mwanaume ampige hivyo basi uwe makini na hao beeers kwa simu ya mumeo.
Pia chunguza kama simu yake ya mkononi anaibania sana yaani hata akienda kuoga anaenda nayo, lazima itakuwa ina mabomu mazito inayo.
Chunguza si mara moja ila kwa hekima na busara.

GARI
Kama mna gari wakati mwingine wengine husahau vitu bila kutegemea, hivyo uwe makini na kuangalia kwenye gari kuna kitu gani kimewekwa kwani kuna wanaume wasiowaaminifu hawathubutu kabisa kuacha au kuweka vitu vya mahawala wao nyumbani bali kwenye magari kwani wanajua wanawake hawawezi kuchunguza na kuanza kukagua, unaweka kukuta vitu vya ajabu ikawa go ahead kwa ajili ya kufanya u FBI.

TENDO LA NDOA
Uwe makini na mabadiliko ya kufanya mapenzi, wengi baada ya kuchoshwa na hawala akifika nyumbani amechoka au anaanza kukulaumu kwamba upo baridi au humpi mapenzi ya kweli ingawa unajitahidi kutoa utaalamu wako wote.
Pia anaweza kukosa hamu ya mapenzi na wewe, hivyo uwe makini kuchunguza kama kweli hakuna mtu wa tatu anayeingilia hapo.
Kuna wengine akifika kileleni anaweza kutamka jina la hawala yake hivyo uwe makini na maneno yake huko chumbani.

CHAKULA
Inabidi uwe makini na mabadiliko ya tabia yake ya kula chakula, mahawala wengi huweza kubadilisha tabia ya ulaji wa mumeo, anaweza kuanza ghafla kupenda chakula aina nyingine pia anaweza kuanza kupenda chakula cha hotel fulani ghafla.
Pia inaweza kutokea akawa kila ukimuandalia chakula hali kama kawaida yake, inawezekana kampitia sehemu na huyo mwanamke wakala so ameshiba, kwani wanaume wengi wa kiafrika tumelelewa mazingira ya kwenda kula chakula alichopika mke sasa inakuwaje leo hataki au kila mara ameshiba wakati huohuo amechelewa kurudi si ndo njaa ingeuma zaidi.
Chunguza!

HARUFU
Kila mtu ana harufu yake ya mwili ya asili. Inabidi uwe makini na harufu inayotofauti na kawaida yake.
Mnuse anaporudi kazini hasa anapokupa hug na pia kwenye gari lake. Unaweza kugundua harufu ambayo itakupa hints za kuanza kumchunguza zaidi

KAMA UMESAFIRI
Si kawaida kwa mwanaume asiyemwaminifu kumleta kimada wake nyumbani kwenu wakati hupo, lakini wapo ambao hudiriki kumleta kimada ndani ya chumba chenu na ni kawaida sana mwanamke mgeni akiingia kujisahau na kusahau vitu alivyokuja navyo kama chupi, leso, vito nk so siku ukirudi uwe makini kuangalia vitu ndani ya chumba chako, bafuni na sehemu zingine na ukikuta kitu kigeni tena hutumiwa na wanawake basi anza kuchunguza.

ZAWADI
Uwe makini sana na sikukuu zilizopo kwa mwaka kama vile Christmass au Valentine’s Day unaweza kukuta kadi au zawadi zimefichwa kwenye gari au ndani ya nyumba na pia risiti za manunuzi ya hizo zawadi unaweza kuzibamba mahali popote.
Chunguza upate ukweli.

MATUMIZI YA INTERNET
Ingawa hii si kawaida kwa nchi zetu za Afrika, kwa nchi zilizoendelea ambako kila familia nyumbani kuna internet, inabidi uwe makini na muda anaotumia kuchat au mawasiliano ya email zake zipo wazi au ni siri, anaweza kuanza kwa internet hadi akaja kukutana na huyo mwanamke kimwili.

USHAHIDI
Kama mtu anafanya cheating kuna wakati huwa inatokea bingo data zinakuja zenyewe by nature. Baada ya kuzoea anaweza kujisahau na kuacha kitu muhimu na kikakutwa, angalia wallet yake, nguo zake za ndani, kwenye mifuko ya suruali, drawer, shelves, kwenye begi lake, hata kule ofisini kwake nk.
Unaweza kupata ushahidi wa uhakika.

TABIA YAKE MBELE YA WANAWAKE WENGINE
Utafiti unaonesha kwamba mwanaume anaweza kufanya cheating mara nyingi na mwanamke ambaye anafahamiana naye iwe kazini, jirani, rafiki wa familia, house girl, watu anaofanya nao business, au watu aliosoma nao nk.
Kama wewe ni mtafiti unaweza kufahamu au kung’amua kitu hasa akiwa na mwanamke ambaye anatembea (sex) naye, kwani wanawake wenyewe akitembea na mwanaume mara nyingi humuona mwenye mume si lolote na pia kuna aina fulani ya aibu huwepo wakiwa pamoja na wewe.
Kama ni house girl unaweza kuona kaanza kiburi na kukuringia ambako ni tofauti kabisa na kawaida yake, maana anajua mzee tunakula wote.
Tutaendelea!

No comments: