"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, June 10, 2008

Kuvuka Mipaka

Utafiti unaonesha wanawake wengi ni innocent linapokuja suala la nani zaidi katika kucheat ndani ya ndoa.
(Picha kwa hisani ya L. H Tanzania) Hivi unawezaje kujua umevuka mpaka wa urafiki wa kawaida kwa mtu ambaye ni nje ya ndoa yako?
Kuna alama tatu ambazo huweza kuonesha kwamba umevuka mpaka na kufahamu kuwa hapo kuna zaidi ya urafiki wa kawaida kwa mwanaume au mwanamke ambaye ni nje ya ndoa yako.
1. TUKUTO LA NDANI
(emotional intimacy)
Je, unajiona mnashirikiana zaidi kihisia na kimawazo mambo ya ndani na huyo mwanamke au mwanaume kuliko mke wako au mume wako?
Kama kuna hali hiyo ambayo inafanya kujikuta hisia zako za ndani zinashikiriana (share) na huyo mtu basi unavuka mpaka.

2. HISIA ZA KIMAPENZI
Je, unapokuwa naye karibu au pamoja unapata hisia za kimapenzi na kutamani kama ungepata nafasi ya kuwa naye kimapenzi? hasa kutokana na kutumia muda mwingi katika mazungumzo na yeye peke yenu mara kwa mara.
Cheating nyingi hutokea makazini, au mahali popote ambapo watu huwa wanashinda kwa ajili ya kazi zao na ikiwa mmoja wapo kati ya wafanyakazi anachukua nafasi ya mke au mume wako na kujikuta unavutwa naye katika hisia za mapenzi basi upo kwenye mstari mwekundu kwani unavuka mpaka

3. SIRI
Je, huwa unajikanyaga ukipigiwa simu na mwanamke au mwanaume mwingine zaidi ya mumeo au mkea, hasa simu ikipigwa kwenye mobile yako wakati mwanandoa mwenzako yupo?
Je, text messages zikiingia kwenye simu yako wakati mumeo au mkeo yupo huwa unababaika nazo?
Je, kama unasoma email zako unajitahidi kuficha mumeo au mkeo asijue unatumiwa na nani hizo email?
Pia una email address ambazo ni siri yako mkeo au mumeo hajui?
kwa nini unaficha na zaidi kwa nini unatumia hizo emails kuwasiliana na huyo mwanaume au mwanamke tu?
Maana yake hapo kuna kitu zaidi ya urafiki wa kawaida na unavuka mipaka.

Kama kuna sign mojawapo ya hizo hapo juu, basi huna budi kuufikiria upya huo urafiki.
Je, katika uhalisia wa asilimia mia kwa mia, mumeo au mkeo anajua wewe ni wewe?
kwa maana kwamba jinsi anavyokufahamu ndivyo ulivyo huna siri zingine.

Ni njia zipi zinafaa kuondokana na hiyo hali?
Kukutana kwa kikundi zaidi ya mmoja.
Ili kuepuka kuvuka mipaka zaidi ya urafiki wa kawaida basi unapokutana naye uwe zaidi ya mtu mmoja.
Usikubali kukutana naye mkiwa wawili tu.

Acha kuzungumzia mambo yako ya ndani ya maisha yako.
Cheating nyingi hutokea hasa pale mmoja ya wanandoa akianza kumsirikisha mwanaume au mwanamke nje ya ndoa kuzungumzia matatizo ya ndani si kwa lengo la kupata ushauri bali kuongea tu ili kujuana vizuri.
Matokeo yake hujikuta wakifahamiana zaidi na kuwa karibu na kuanza kutumia muda pamoja na hatimaye kujikuta huyo wa nje anamjali kuliko aliyenaye kwenye ndoa na matokeo yake wanaweza kufikia hatua ya kuangushana.
Wapo wanandoa ambao ni wepesi sana kuanza kuongea mambo ya ndani anayofanya na mume au mke na wakati mwingine hupelekea mazungumzo yao kunoga na kudhani wao sasa ndo wanafaa kuwa pamoja kuliko wale walionao kwenye ndoa zao.
Ingawa si mara zote inatokea, lakini kwa nini u risk maisha kiasi hicho.

FIKIRIA MATOKEO/HASARA YA KUTOKUWA MWAMINIFU KATIKA NDOA
Kutokuwa mwaminifu katika ndoa ni kibarua kigumu sana ambacho kinahitaji kazi ya ziada.
Utahitaji kunusa kila sign inayoonesha hushtukiwi, itabidi ufiche simu yako ya mkononi na sms zake, kila wakati ni hofu na mashaka kwani unaweza kukamatwa, pia itabidi uwe unapata muda kuhakikisha unapata time ya ku-share na huyo kimada wakati huohuo mke wako au mume wako naye anakuhitaji.
Je, utatumikia mabwana wawili bila kushitukiwa?
Ni kazi kwelikweli.
Wakati ukiwa mwaminifu hakuna kazi ni kufurahia uhuru wako na yule umpendaye, mpenzi, mahabuba, mwandani na asali wako.

Kitu kigumu zaidi ni pale ukibambwa na huo udanganyifu, data zikigoma, mambo yakiwa hadharani,
je, uta-deal vipi na hiyo aibu?
Fikiria baada ya kujulikana kwamba umekuwa si mwaminifu na watoto wako wakajua na wakafahamu kwambakumbe baba humpendi mama, au mama humpendi baba.
Fikiria historia ambayo utakuwa umeitengeneza?
rekodi mbaya kwamba hukuwa mwaminifu kwa mke au mume wako

Jaribu kufikiria kwa makini sura na uso huruma na wa aibu na kuumizwa wa huyo mwanamke au mwanaume ambaye siku ulipooana naye uliahidi kwamba mtaishi milele hadi kifo kitakapotutenganisha na leo umemsaliti kiasi hicho?

Je, ndugu zako, wazazi wako, watakaposikia aibu uliyoiweka juu ya jamii?

KUMBUKA
Mke au mume wako pamoja na watoto wako ni vitu vya thamani sana na kitendo chochote cha kukosa uaminifu kinaweza kupekelea maafa na maangamizi ya familia yako.
Tutaendelea na dalili za mwanaume anaye cheat!

No comments: