"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, June 4, 2008

Mahitaji ya Msingi Ktk Mahusiano

Je, kumnunulia mwanamke gari ni hitaji muhimu?
(picha kwa hisani ya morio M) Ni dhahiri unafahamu kwamba Mahitaji muhimu ni lazima yatimizwe ili mtu uwe na furaha katika maisha.
Kama mahitaji yako ya msingi hayatekelezwi, basi utajisikia hujaridhishwa inavyotakiwa na utatumia muda mwingi ili utimiziwe moja kwa moja au kwa kuzunguka.
Na wakati mwingine wapo watu ambao akiona mahitaji muhimu hayapatikani katika mahusiano yaliyopo unaanza kutafuta kutimiziwa hayo mahitaji nje ya ndoa au nje ya mahusiano yaliyopo.
Kama mpenzi wako anakupa mahitaji muhimu kwenye mahusiano basi hapo utaridhika na mtakuwa mnajenga mahusiano yaliyo imara na yenye afya.

Ni jambo la busara kama unaona mpenzi wako hakupi mahitaji yako muhimu ukamwambia kwa hekima na busara ili akutimizie kwani hawezi kusoma mind yako kwa kubaki kimya na kujua unahitaji kitu gani.
Mahitaji muhimu katika mahusiano ya ndoa au uchumba yamegawanyika katika sehemu kuu tano nazo ni
1. Mahitaji ya kihisia (emotional)
2. Mahitaji ya Kimwili (physical)
3. Muhitaji ya kijamii (social)
4. Mahitaji ya kiroho (spiritual)
5. Mahitaji ya kiusalama (security)

MIFANO
Mahitaji ya kihisia
Hitaji la kusikia na kuambiwa unapendwa, una thamani kwa mpenzi wako, kujisikia wewe ni muhimu katika maisha yake, kujisikia wewe ni mali yake, hitaji la kujisikia unaheshimiwa wewe binafsi na yeye, hitaji la kujisikia mpenzi wako anakuhitaji zaidi ya kazi zingine unazofanya kama kulea watoto nk, hitaji la kujisikia wewe ni mtu wa kwanza kwake kwa kila kitu, kujisikia wewe ni mtu maalumu kwake, hitaji la kujisikia unaaminiwa, unakubalika na pia anakupenda na kukuhitaji, hitaji la kujisikia ana appreciate kwa jinsi ulivyo na unavyofanya nk

Mahitaji ya kimwili
Hitaji la kuguswa (touched and caressed), kupata busu, kukumbatiwa, na kushikwa hata kubebwa akiweza, hitaji la kujiona unaruhusiwa kuwa naye katika faragha yake, kujisikia huru kuwa naye kimwili pale unamuhitaji, kujisikia wewe ni sehemu yake pale mnapowasiliana na watu wengine, kutiwa moyo, kuwa na tendo la ndoa linalokuridhisha kama upo kwenye ndoa nk.

Mahitaji ya kiroho
Hitaji la kuheshimiwa na kusaidiwa mambo yako ya kiroho, kuheshimiwa kwa tofauti za kiroho zilizopo nk.

Mahitaji ya kijamii
Hitaji la kukumbukwa kwa simu, email au aina yoyote ya mawasiliano ukiwa mbali, hitaji la mpenzi wako kupanga ratiba shughuli zake na kukuhusisha au kukujulisha, hitaji la kuwa pamoja katika shughuli za jamii kwa pamoja, kukujali na kuwa mpole mbele za watu mkiwa pamoja, kukutia moyo na kukusaidia kimwili na kihisia mbele kwenye public, kuambiwa vitu vizuri kwenye mazingira ya public, kuwa treated vizuri mbele za watu, kufurahia pamoja katika majukumu ya kijamii, kujisikia wewe ni mtu muhimu na maalumu kwake mbele za watu hata kama mpo busy.

Mahitaji ya kiusalama
Hitaji la kutetewa, kusaidiwa, kutiwa moyo, kushirikiana wakati wa matatizo, shida au mgogoro wowote unapokupata. Hitaji la mpenzi wako kukukimbilia kukupa msaada unapotakiwa, hitaji ka kuona mpenzi wako yupo committed na yupo loyal kwako na yupo hivyo permanently. Hitaji la kujiona hata ukiangukia mikononi mwake unakuwa umeangukia sehemu ambayo ni soft nk.

KUMBUKA
Usipomtimizia mke wako au mume wako mahitaji muhimu anaweza kupata hayo mahitaji kwa mtu anayeshinda naye kazini au mahali popote.
Inawezekana humpi kile anahitaji kihisia, au kimwili au kijamii au kiusalama au inawezekana humpi busu la uhakika au humkumbatii au humsifii kwa yale mazuri anafanya na mtu mwingine nje ya ndoa yako au uhusiano anafanya kazi nzuri ya kumpa hayo mahitaji, bila kujua wanaweza kuanza mahusiano hatari yasiyo rasmi na wakafika mbali na hatimaye kuharibu ndoa yako au mahusiano yenu.

Mpe Mpenzi Wako Mahitaji muhimu

No comments: