"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, June 30, 2008

Siku ya Kwanza nitoke Vipi?

Wapo ambao siku ya kwanza ukitokea na maua basi umefungua mlango katika moyo wake. Fikiria wewe ni kijana wa kiume umepanga kukutana na binti ambaye unategemea awe mchumba wako, unawaza je, itakuwaje? Je, atanikubali kweli? Ataridhika jinsi nilivyo kweli? kiroho kinakutunda kweli maana hujazoea haya mambo!
Huhitaji kuwaza au kufanya mambo makubwa just relax fuata hizi tips bila shaka lazima utamvutia kiasi cha yeye kutaka kukutana na wewe tena na tena.

HAKIKISHA IDARA YA USAFI UMEKAMILIKA
Umeoga vizuri, umevaa nguo safi, unaweza kuvaa nguo za gharama na bado zikawa chafu so vaa nguo safi, piga mswaki na kuwa na meno safi.
Wapo akina dada akishajisikia unanuka basi bye bye, au akiona meno ni machafu na mboga za tangu juzi zimo kwenye meno anakata tamaa kabisa, au mdomo unaonuka.
Pia angalia kucha zako zipoje, kama ni chafu una balaa wewe!

JALI MUDA
Jitahidi kuwepo mahali mlikubaliana katika muda muafaka, kama ni mara ya kwanza na umemuweka dada wa watu akusubiri zaidi ya saa nzima huwa haipendezi pia ni dalili kwamba hupo makini. Hata kama umechelewa kuna dhalula karibu kumpigia simu na kumueleza sababu na utafika muda gani. Siyo kwenda kujieleza baada ya kufika huku umechelewa.

USIWE MTU WA KUJISIFIA NA KUONGEA TU
Usitumie muda wako wote kuongea habari zako mwenyewe na wewe kuongea tu bila yeye kumpa nafasi kuongea. Ni vizuri sana ukawa na hekima kuuliza maswali huku ukimpa nafasi kubwa yeye kuongea huku wewe unamsikiliza. Pia be fun, hakikisha anfurahi ila usizidishe maana inabidi usome saikolojia zake kujua ni dada wa aina gani.
Pia hata kama lugha yako ina maneno ya ajabu ajabu uwe makini kwani kuna akina dada wengi hujiuliza hivi kama anatukana, au analalamika, au analaani hivi leo siku ya kwanza je, tukioana?
Pia achana na habari za kuanza kuongelea mahusiano yako ya nyuma au habari za wanawake wengine unless either ni mama yako mzazi.

TABASAMU.
Kutabasamu ni ufunguo wa moyo wako ulivyo ndani, isijetokea dada aka smile na wewe ukawa umeweka tu ndita usoni na kuzima mdomo kama uso wa mtu anayekunywa gongo. Mwanamke anayehitaji mwanaume friendly, aliyetulia na uwe wewe kama ulivyo bila kujifanya ni mtu Fulani hivi.

TEMBEA NA PESA
Inatokana na sehemu ambayo umepanga kukutania na kama mwanaume ni vizuri kutembea na pesa ingawa kweli unaweza kuwa na dada ambaye ana pesa na anataka kulipa ni vizuri hiyo bill lipa wewe kwa mara ya kwanza kwani itaonesha huna uchungu na ngawira zako. Pia ukishapewa bill usiulize sana maswali yanayoonesha upo very concerned na hizo pesa just pay it tight away.
Siyo unaenda bila pesa na bill ikija unaanza kung’aa macho na kujihurumia.

ANGALIA TABIA ZAKO
Jitahidi kuwa gentle, fungua mlango kwa ajili yake, unapoongea mwangalie usoni siyo kifuani. Jiamini hata unapoongea ongea kama mwanaume ambaye ni source of woman’s happiness. Unaweza kumgusa wakati unaongea ila uwe makini kumsoma kama kweli anafurahia kwani this is your first time, kuna wanawake wanapenda kuwa touched.
Pia uwe makini usiwe mtu wa ku-force mambo kwa maana kwamba unataka kila kitu siku hiyo hiyo kieleweke.
Hapa unafungua mlango tu wa kukutania mara kwa mara na kufahamiana kwani akipendezwa na wewe leo basi kesho atataka mkutane tena na ndipo unaweza kuanza kuingiza topic zako maana sasa mmeanza kuzoeana.

2 comments:

Anonymous said...

Mheshimiwa ,nijambo jema kufikilia nini kinatokea siku ya kwanza unapo fanyiwa interview. nafikiri kwa swala la kzi ni kawaida mtu ajibidishe siku ya interview ili aweze kujiuza vyema.Lakini kwa swala la ndoa nafikiri ni tofauti kidogo kwani watu hujuana kwanza na kisha baadaye mambo hujileta kiurahisi. Mimi binafsi naamini uhusiano wa watu huanza bila wao kujitambua na kisha kila mmoja wao kujiona anahitaji mwingine na anahisi kitu cha tofauti kati yao. Nafikiri si rahisi kukutana na mtu mara moja na siku hiyo ukamwambia unataka kumwoa.Na kama hili swala ni kweli basi watu wanahitaji kuyatekeleza hayo uliyo yaeleza kila siku amabyo mungu amewapa. Na ninapinga wale wanao wadanganya hao wanataka kuwaona kwa kujisafisha nje eti waonekane wanawafaa , simu ya kuazima,suti ya kuazima,eti kwako mambo fresh wakati maskini ni mtu wa kawaida tuu.Maisha si pesa na pesa si maisha ,. Hayo uliyayaeleza na mambo ya muhimu na ni ya kila siku si kwa sababau unataka kumwona Atusunguche. Na wale wanao vizia kina Mlyabange kwa kuwa waana pesa wana takiwa kujua kuwa watanunua na maisha yao vilevile ili wayatumia kama watakavyo.
Tatu naomba kujua Age diefference katika ndoa ina faida gani na hasara gani na hiyo dfference isizidi kiasi gani na kwanini.
Ok Mungu awabariki.
www.sharuvembo.wordpress.com

Lazarus Mbilinyi said...

Ni kweli suala la ndoa na kazi ni tofauti kidogo, ni lazima ujuane naye kwanza na kujuana naye ni pamoja na kupata muda wa kukaa naye na kuongea naye ndo ile sumaku ya kuvuta itaendelea kuwa na makali zaidi, hao akina Atusunguche wanakataga tamaa sana kutokana na ninyi akina mulyabange kutokuwa makini na vitu vidogo na muhimu, unakutana naye upo ovyo na unaongea ovyo tu badala ya yeye kukuona unafaa unazidi kumpa wakati mgumu, pia fahamu ni ndoto za kila mwanamke kupata the best man, mwanaume ambaye anafaa na atampa kila anatarajia. Pia ni vizuri unapoongea naye uwe wewe na si vinginevyo, ukiazima suti ya mzee kihalali ndo utoke nayo hapo unajidanganya mwenyewe. Be you 100%