"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, June 9, 2008

Silaha zingine mmmm!

Hii silaha si maarufu sana kwa wanawake, ipo silaha nyingine ambayo wapo wanawake wanaipenda sana kuitumia wakiwa kwenye ndoa.
Kwa nini baadhi ya wanawake hupenda kutumia silaha ya kuwanyima unyumba (sex) waume zao kama njia ya kuwaadhibu pindi akifanya makosa au akitaka amnunulie kitu na mume akawa hanunui au hatimizi ahadi?
Ndoa inapaswa kuwa ni taasisi ambayo watu wanapaswa kupendana, kushirikiana, kufanya mambo kwa pamoja na pia kufurahia maisha pamoja ambayo wamekubaliana kuishi.
Kitu kinachoshangaza ni kwamba likitokea tatizo basi kitu cha kwanza kuharibika ni chumbani. (No sex today)
Hivi kwa nini msinyimane chakula tu, mnanyimana unyumba au kama ni mume wako ni shabiki wa soka basi ficha angalau remote ili akose kuangalia Euro 2008 naamini hiyo ni adhabu tosha kuliko hiyo silaha ya kumnyima tendo la ndoa.
"Ingawa njia sahihi likitokea tatizo ni kuzungumza na kupata ufumbuzi"

Ni dhahiri kabisa ndoa nyingi (si zote) likitokea tatizo, basi silaha ya kwanza mwanamke kuitumia ni kunyimana sex kitandani, na kama ndo wale wenye hasira, ujue wiki au mwezi mtalala mzungu wa nne mpaka unyoke.
Nidhahiri pia kwamba tendo la ndoa ni kitu muhimu sana katika ndoa, linapokuja suala la wanandoa kuamua kuadhibiana kwa kunyimana basi wawili hawa huwa katika wakati mugumu na hasa kwa yule anayeadhibiwa.
Wengi wanapenda kutumia hii silaha kwa sababu ni kweli tendo la ndoa lina control maisha si jamii tu bali hata uchumi, na ndiyo maana watu wanaoana kwa sababu wanataka sex, ingawa wengi wanaweza kupinga hilo.
Pia wapo wanawake wenye wanaume wababe ambao hata ukiamua kumuadhibu kwa kumnyima sex bado utatoa tu, kitu ambacho unafanya unajitoa katika kushirikiana naye na anakuwa kama vile anafanya kile kitendo peke yake na wakati mwingine unaweza kuongea kwa kutaka amalize haraka ili uendelea na msimamo wako kwamba umemuadhubu.
Unamwambie mumeo
Fanya haraka mimi nilale zangu"
au
"Bado hujamaliza?",
Naamini mwanaume mwenye busara hawezi kulazimisha sana sana atatafuta solution ya kudumu na kama mwanaume ni mwaminifu basi mwanamke umepatia na kama si mwaminifu umejimaliza maana usijesikia kesho amepata nyumba ndogo ambayo inaweza kufanya maajabu.
Napinga kabisa nyumba ndogo kwa nguvu zote, ila naomba wanawake kutumia njia zingine kama unataka kumuadhibu mume wako ila si kumyima tendo la ndoa.
Pia wapo wanawake ambao kama anataka kitu na mwanaume hajampa au hajamnunulia basi anatumia silaha yake ya kukunyima sex hadi ununue au ampe.

"Kwa mwanaume mwaminifu ni kweli unamuumiza sana, ila kwa mwanaume ambaye si mwaminifu fahamu unajimaliza mwenyewe"

2 comments:

Fikirikwanza said...

Msitake nitumie busara zangu zote kwa kucheka hadi njaa inisumbue. Hivi imekuwa chumvi hadi watu mnyimane kana kwamba inakwisha?.
Kama ni hivi kweli nje ya ndo ni kwema kuliko huko ndani!

Lazarus Mbilinyi said...

Fikiri Kwanza,

Ukweli hakuna taasisi nzuri na tamu kama kuwa kwenye ndoa, kitu cha msingi ni kupata yule ambaye anakufaam ndiyo maana kama upo nje ya ndoa ni vizuri kutumia uwezo wako wote, akili zako zote na nguvu zako zote kiroho, kijamii, kimwili, kiuchumi kuhakikisha inaingia na mtu sahihi.
Maisha ya ndoa ni matamu sana mtu asikudanganye.