"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, June 2, 2008

Tabasamu

Kutabasamu ni zawadi ya upendo!Picha Ni Dada Lisa akiwa Malyasia
Tabasamu ni dirisha linalofunguka kuonesha mwonekano wako wa kwanza mbele za watu
Tabasamu ni muhimu sana katika maisha kwa sababu kubwa kabisa tatu ambazo ni kama ifuatavyo:

Kwanza:
Tabasamu ndiyo asset kubwa, ujumbe na signal ambazo tabasamu hutoa kwa watu wengine huonesha jinsi tulivyo, nini tunahitaji, na namna na jinsi tulivyo.
Tabasamu ni kama kipimo cha nje cha mood na jinsi tunavyoonekana.

Pili:
Tabasamu hueleza haraka na moja kwa moja kama mtu unaingilika (approachable), tabasamu huonesha nini tutataka kwa wengine na pia huonesha kwamba wanathamani.

Tatu;
Tabasamu ndiyo silaha kubwa na ya pekee ya kuweza kuunganishwa na watu/mtu mgeni kwako unapokutana naye kwa mara ya kwanza na unaweza kujenga urafiki kwa hilo tabasamu. Unapokuwa mgeni machoni pa watu huhitaji kuongea chochote bali kutabasamu tu na mtu unajiunganisha.
Tabasamu hupenya kwenye lugha zote na kutufanya tuwe very attractive.

Tabasamu ni muhimu likatumika kila wakati na si kusubiri hadi muda maalumu kwa sababu tabasamu huonesha haiba yako na aina ya mtu ulivyo.
Watu wasiotabasamu hawavutii siku zote matokeo yake watu hujitenga nao.
Mtu anayetabasamu ni kama mtu anayetoa jua na mwanga unaosababisha na wengine kuitikia kwa tabasamu na kufanya dunia iwe mahali salama kuishi.

Hivyo jiamini, mwangalie mtu na kumpa tabasamu kwa kutumia macho yako na meno na midomo ili kuonesha kwamba unaingilika.

Kama wewe ni kiongozi basi kutabasamu ni sehemu ya uongozi wako, kiongozi anayetabasamu hutengeneza bond na wale anaowaongoza na matokeo yake anakuwa approachable.
Tabasamu ni alama ya kwanza kabisa inayofanya watu waonekane attractive, hata uvae upendeze, hata ununue nguo za gharama bila tabasamu bado utaonekana hujapendeza kama tutalinganisha na mtu mwenye tabasamu.
Wengine wanasema tabasamu ni mkeka unaotandikwa ili kukukaribisha mkae ili muweze kuongea, watu wanaotabasamu ni kama vile wanatoa miale ya joto linalosababisha wengine wavutiwe na wao ghafla.

Kuna watu tumejaliwa kwa asili yetu kutabasamu na kuna wengine lazima mfanye kazi ili muwe mnatabasamu.
Kama unaogopa kutoa tabasamu kutokana labda kwa kuwa na meno ya mbele yaliyooza au kung’oka unaweza kutumia meno ya bandia (Dental crowns)

Kutabasamu ni silaha kubwa kabisa na haina gharama yoyote.
Kumbuka ni muhimu kuwa na furaha na kutabasamu kwani huwezi kujua utakutana na mtu wa aina gani, kwa tabasamu lako
unaweza kubadilisha maisha,
unaweza kupata mchumba,
unaweza kupata mume au mke,
unaweza kupata business ya uhakika,
unaweza kufungua mlango wa baraka za tofauti.
Sijazungumzia kutabsasamu tu kila unapotembea hata mahali ambapo hakuna watu wewe ni kukenua meno na kutabsamu tu hapo watu watakuona mwehu, utachanganya mambo, tumia tabasamu mahali panapotakiwa!
3 comments:

Subi said...

Lisa habari za masomo? Pole na mitihani. Ninakuombea mafanikio mema. Wafikishie salam rafiki zetu wa huko.
Upendo daima!

Mbilinyi Junior said...

Sina nyongeza kwa hili tabasamu

Mary said...

Tabasamu la Lisa linaonesha matumaini. Mungu akutunze