"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, June 17, 2008

Usingizi

Usingizi hauna adabu ukiukopa ujue utaulipa mahali ambapo hukutegemea.
Jamaa wanauchapa usingizi bila kujali mahali walipo.Usingizi ni hitaji kuu la kimwili (physical) na pia ni hitaji kubwa kuliko chakula na mazoezi.
Chakula ni muhimu lakini unaweza kuishi siku 30 – 50 bila kula. Pia mazoezi ya mwili ni muhimu lakini watu wanaishi miaka Nenda rudi bila mazoezi na wanadunda tu.

Kama utaenda masaa 36 bila kulala usingizi automatically utapoteza uwezo wa ku-concentrate na hatimaye kuwa unstable.

Kutokulala muda au masaa ya kutosha husababisha deni la usingizi ambalo matokeo yake ndo mtu kushindwa kufanya kazi, kufikiria, kuwa na mood ovyo hata wakati mwingine kulala katika eneo hatari bila kusudia. Utafiti unaonesha pia ajali nyingi barabarani hutokea si kwa sababu madereva wameutwika bali usingizi

Pia Utafiti unaonesha kwamba wafanyakazi wa shift ya usiku ndio wanaoongoza kuchapa usingizi kazini au muda wa kazi.

Wakati wa kulala baadhi ya viungo huendelea kutwanga mzigo kama kawaida wakati mtu mwenyewe wala hajitambui na pia kuna baadhi ya sehemu kwenye ubongo hufanyi kazi zaidi kuliko ukiwa hujalala.

Mwili wa Binadamu unatumia saa ya asili ambayo katika kuzunguka kwake hutumia mwanga na kukishakuwa giza basi usingizi huja wenyewe.


Utafiti unaonesha kwamba watu ambao hawapati usingizi vizuri wanaweza kukumbwa na:-

Msongo wa mawazo

Matatizo ya afya

Kisukari

Kupoteza control za emotion

Kupoteza kumbukumbu

Kuwa na mood mbaya

Kusababisha ajali

Kazi za usingizi katika mwili ni pamoja na

Kuupa mwili nguvu mpya

Kushusha chini mawazo na kila masumbufu kiakili

Refresh mtazamo wa mambo

Husaidia kustimulate mtu kuwa mbunifu

Kawaida mtu mzima anahitaji kawaida ya masaa 7 hadi 8 kwa siku ili kupata usingizi

Na watoto wanahitaji masaa zaidi ya 9 kwa siku kwa ajili ya usingizi.


Kumbuka

Huwezi kuudanganya usingizi kwani unaweza kupata madhara makubwa kuliko uanvyotegemea.

Huwezi kuwa mfanyakazi bora kama hupati uzingizi na pia huwezi kuwa mpenzi mzuri kama huwa hupati usingizi wa kutosha.

Kuna baadhi ya vitu husababisha mtu kukosa kupata usingizi mnono akilala

Kulala eneo ambalo lina kelele

Kuumwa (kama kuumwa jino vile)

Medications

Kuwa na hofu na mashaka

Kazi za shift

Kabla ya kulala Hakikisha

Unaachana na vinywaji vyenye caffeine kama kahawa

Unamsikiliza music (relaxing soft unaokubembeleza)

Soma kitu ambacho kinakupa comfort

Fanya maombi


No comments: