"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, June 16, 2008

Wana cheat na hawakamatwi, why?

Wao hawatumii simu kuwasiliana.

Msingi mkubwa wa wanaume wa aina hii wanatunza siri kuhusu wao wenyewe na familia zao, kazi zao hata majina yao wakati mwingine

HAWATUMII SABABU YA KUWA KAZINI
Mara nyingi mtu anaye cheat hutumia style moja ya kuwa kazi zinamfanya kuwa busy kumbe anatumia muda na hawala yake, hivyo basi wadanganyifu wa kiwango cha juu hawatumii sababu ya kuwa kazini kwani wanajua akianza kushtukiwa jambo la kwanza ni kuangalia muda anaotumia kazini.

HUHAKIKISHA MKE ANA FURAHA MARA ZOTE
Kwa kuwa atafanya kila njia kuhakikisha mwanamke anakuwa na furaha, hii ina maana kwamba mwanamke mwenyewe atajisahau na kujiona kuna amani kumbe ndani yake kuna udanganyifu mkubwa. Anaweza kukupa zawadi kila mara hasa akisafiri, anafanya kila kitu kuonesha anakujali kumbe anakuzunguka na inakuwa ngumu sana mwanamke kujua kwa sababu kila kitu anachohitaji anapata.

HAWATUMII SIMU
Wanaume wa aina hii si kawaida yao kuwapa mawahala namba za simu za mkononi, nyumbani au kazini. Wanajua kupitia simu za mkononi text message tu inaweza kuharibu mambo, acha kupigiwa simu kabisa. Pia wanajua wanawake ni rahisi sana likitokea jambo lolote ambalo hajaridhika au kukorofishana mara nyingi hupiga simu kwa wake wa hawa wanaume ili kuvuruga zaidi. Ndiyo maana hawatumii simu.

WANALIPA CASH BILA RISITI
Kawaida hawatumii credit card kulipia huduma zao kwani kuna bank huonesha matumizi ya pesa yako kwenye bank statement (hasa nchi zilizoendelea). Wanaogopa kwani kwenye account kunaweza kuonesha hotel na sehemu alienda na jinsi alivyotumia pesa.
Pia hawataki risiti kwani anaweza kujisahau akiwa nyumbani risiti ikakutwa kwenye mfuko wa suruali au wallet.

WANABANA MATUMIZI
Kawaida cheater mzuri hakopi pesa kwa ajili ya kustarehe na huyo mwanamke na pia anahakikisha matumizi yana balance na kuwa kama kawaida, hawana mambo ya ku-impress mwanamke kwa kutumia fedha nyingi hadi kukopa kwani wanajua matatizo ya kifedha yakitokea lazima atiliwe mashaka na kushikwa so mambo ya pesa wapo makini sana.

HAWADANGANYI OVYO
Hawana tabia ya kudanganya sana na mara kwa mara, kwani wanajua ipo siku data zitagoma bali wao huelezea uwongo unaofanana sana na ukweli ambao anayeambiwa anadhani ni ukweli kumbe ndani kuna uwongo.
Pia hawezi kueleza kitu hadi aulizwe pia anakuwa na majibu mafupi yasiyo na maelezo mengi ili kuficha data zaidi.

HAWATUMII MARAFIKI
Kawaida hawatumii marafiki au marafiki kuwasaidia kuficha siri zao. Wanajua marafiki kwa kuchemka au kwa makusudi wanaweza kufikisha habari kwa familia. Hujitunzia siri wao wenyewe na yeye tu ndo anajua kila kitu. Hata mwanamke ataambiwa asimwambie mtu na akimwambia mtu urafiki unakufa kwani anajua jinsi watu wengi wanavyojua issue basi uwezekano wa habari kuzunguka ni mkubwa.

WANAENDA MBALI
Kawaida cheaters wa aina hii si kawaida yao kutembea na majirani, marafiki, wasichana wa kazi au wafanyakazi wenzao au mtu yeyote ambaye yupo connected na mke wake, wao huenda mbali kabisa ambako hakuna mtu anawajua. Wanatumia ile principle kwamba ukiona mwizi anaimba jirani ndo kukamatwa kumekaribia, hivyo hawathubutu kuwa na wanawake wa karibu ambao jamii anaishi wanamfahamu.

KUMBUKA
Kuwa mwaminifu katika ndoa yako ndiyo jambo la misingi na muhimu si maisha yako tu bali hata familia, ukoo wako na jamii nzima.
Kumbuka kila mwizi ana siku yake ya arobaini hivyo basi hata kama hujagundulika ni vizuri kuacha hiyo tabia mapema ili uanze kujenga familia bora na yenye mafanikio pasipo wewe mwenyewe kuishi ndani ya guilt.

SWALI
Mume wangu nahisi si mwaminifu na ana cheat je ni njia ipi rahisi niweke kufanikiwa kumkamata?
JIBU
Tumia siku nzima unamfuatilia wapi anaenda na kuwa na nani, ila Hakikisha ni siku ambayo tangu mapema umemwambia utakuwa busy sana ili ajue hutamfuatilia, hivyo kwa kuwa upo busy ataamua kwenda kujirusha kama kawaida yake.


No comments: