"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, June 13, 2008

Wanaume Nao mmm!

Wanaume wa vijijini wao hawana noma, nasikia kisu kina kata kila siku.
Hawana pressure wala stress za kulipa bills au kupanda kwa nauli za daladala.
Pichani ni wanaume wa kijiji cha Wangama huko Njombe wakishiriki katika harakati za kupanda miti kwenye vyanzo vya maji mwezi March 2008


Ukichunguza kwa makini aina (species) zote za wanyama wa kiume wote wanatabia moja ya kuwa na hamu kubwa ya kufanya mapenzi (high sex drive), chunguza jogoo tangu anaamka asubuhi kazi yake ni nini, chunguza beberu tangu asubuhi kazi yake nini, chunguza simba, nk. Halafu uje ulinganisha na Binadamu, kiumbe mwanaume kuhusiana na suala la sex.

Mwanaume siku zote ni mtu wa kulianza linapokuja suala la sex na wataalamu wanasema kwamba kila baada ya dakika 15 mwanaume huwaza kuhusu sex, yaani wazo la kufanya mapenzi huingia akilini mwake kila mara hata kama hajamuona mwanamke na akimuona basi ni balaa.

Pia wanasayansi wanasema kwamba kila drop moja la majimaji ya mbegu za kiume (seminal fluid) huwa kunakuwa na zaidi ya mbegu za kiume milioni 300 na mwanaume ana uwezo wa kutoa hizo mbegu kupitia sex (ejaculation) mara 2 au 3 kwa siku. Na kitendo hiki cha kutokutoa hizo mbegu huweza kumuathiri (frustration) akili yake na hali yake ya kimwili.

Mwanaume huweza kutengeneza mbegu (semen) kila baada ya masaa 42 hadi 72 na hiki kitendo husababisha mgandamizo wa kimwili wa kutaka kuzitoa kwa njia ya sex.

Pia wanaume wanaoishi vijijini Utafiti unaonesha kwamba wao hushiriki tendo la ndoa mara nyingi zaidi kuliko wanaume wa mijini, hii ni kutokana na wanaume wa mijini kukumbana na misukosuko ya maisha na kuathirika kisaikolojia hivyo kuathiri mwili kutaka sex.

Wanaume huwa frustrated sana na wanawake kwa sababu wanawake mara nyingi hawapendi sex.
Wanawake nao huwa frustrated sana na wanaume kwa sababu wanaume kila wakati wao wanataka sex.
Wanawake wanawalaumu wanaume kwa sababu hawajui kupenda.
Wanaume nao wanawalaumu sana wanawake kwa sababu wanaongelea sana upendo lakini hawataki kuweka katika vitendo (sex)
Binadamu hufanyi mapenzi kwa sababu ya homoni ya testosterone ambayo kwa kiasi kikubwa ni kwa wanaume.
Mwanaume wa kawaida huzalisha hii homoni mara 20 kuliko mwanamke, ndiyo maana mwanaume anakuwa na drive kubwa ya sex.
Hii ina maana kwamba jinsi mwanaume anavyojisikia kukosa sex kwa siku moja ni sawa na mwanamke anavyojisikia kukosa sex kwa siku 20.

Kujua hili basi unaweza kujua kwa nini ukimnyima mume wako sex unakuwa umemuumiza kiasi gani. Sina maana uwe unalazimishwa kutoa sex hata kama hujisikia kitu cha msingi ni mawasiliano mazuri na upendo kwanza.

Siyo wanaume wamejisababishia hili bali ni genes, wameumbwa hivyo na ndiyo maana wanaitwa wanaume.

Mwanaume anaweza kuzalisha mtoto kila anapofanya mapenzi wakati mwanamke anaweza kuzaa watoto kwa kila baada ya miaka miwili, hii ina maana kwamba mwanamke anatakiwa kuchagua nani anatakiwa kuwa baba wa mtoto.
Wanaume siku zote wanatafuta quantity wakati wanawake siku zote wao ni kutafuta quality.

Ndiyo maana wanaume hutafuta sex kwenye mahusiano na wanawake hutafuta upendo.
Kwa mwanamke upendo ni proof kwamba mwanaume atabaki kwake na kuwa naye wakati wanaume wao baada ya sex ndiyo hujisikia mwanamke anampenda.

Men fall in love through sex; women fall in sex through love.

Hivyo basi kwa mwanaume kuwa na mke kwa ajili ya kuwa naye kimapenzi ni jambo la msingi na muhimu kwa sababu humuhakikishia yafuatayo:-
Kujisikia ni mwanaume.
Kuimarisha upendo kupitia mke wake.
Husaidia kuondoa migogoro (conflict) ndani ya nyumba yake.
Kujisikia maisha ni kitu kizuri na kinachompa raha zaidi (exciting)

KUMBUKA
Hii ni sayansi linapokuja suala la maadili ya Kimungu hakuna lisilowezekana kwani yasiyowezekana kwa mwanadamu kwa Mungu yote yanawezekana.

Mwanaume anaweza kuishi bila sex kwa muda wowote anaohitaji na asipate matatizo yoyote.
Hapa najaribu kutoa mwanga wa kuweza kujua tofauti ya mwanamke na mwanaume.
Mafundisho ya dini yako yana nguvu kuliko hizi facts.

Ubarikiwe na Bwana!

Nkosi isikeleli Tanzania


No comments: